Bro Michu Salama?
Nilikuwa najaribu kutafuta habari kuhusu fani ya PROJECT MANAGEMENT kwa hapoTanzania, jinsi inavyoendeshwa na jinsi inavytumika katika project mbali mbali nchini na kwenye makampuni.
Je kuna software maalum wanatumia ama la? Ntashukuru iwapo wadau watanisaidia maana ninajaribu kuandika paper kuhusu fani ya project management kwa hapo Tanzania. Pia kama kuna website yenye habari zaidi kuhusu hii fani kwa hapo Tanzania nitashukuru.
Heshima Mbele,
Mdau USA.
E mail yangu ni: zipompa@yahoo.com
Shukrani!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Fani (profession) na software ni vitu viwili tofauti. Mathalani madaktari hutumia software km EPI info, STATA, SPSS ku-analyze data za kiutafiti lkn si wote watumiao hizo software ni madaktari. Ndiyo kuna software ya Project Management lakini si ya Tanzania tu, hata ukiwa USA, Japan, Europe, Kenya etc unawekuitumia. Unachohitaji tu ni kununua licence yake.

    ReplyDelete
  2. Project management is a complete profession of dealing with overall aspects of planning,managing, controlling projects activities.

    Kuna software huwa inahusika kufannya hayo mambo especially Microsoft Office Project(its a product of microsoft), hii software can do everything for you ila you have to insert paramenters km List of activities and their sequences, resources innvolved and theiri corresponding costs per each activities e.t.c

    I thus advice you kusoma some project management knowlegde areas such as time management, scope mngt, risk mngmt,human resources mngmt, procurement mangmt, etc so as to be capaple of making strategic decisions in planing through to the project completionn stage.

    For more info, nenda google andika project management....then utaona kila kitu.

    ReplyDelete
  3. Duh Ndugu zangu hapo juu woote mmelikurupukia swali,sijui mlilisoma kwa kituo.
    Jamaa yeye anajua nini project management,infact anaandika paper kuhusu hiyo hiyo project management,alichotaka kujua ni je fani hii ipo tanzania,na je inaendeshwaje na kama kuna mifano labda alitaka kujua,like kampuni, websites na vitu ka hivyo na je kuna software yeyote wanatumia huko na kama ipo ni ipi.

    Sasa nyie ndugu zangu hapo juu (the first two)naona mnamsimulia mshikaji hadithi azijuazo.

    ReplyDelete
  4. Do you all actually think that all the projects in TZ are not being Managed? What is the question again?

    ReplyDelete
  5. wewe hapo juu (anon 3.09 pm) ndo umekurupuka.

    ukiangalia swali halijibiki, project mgt ni project mgt tu haiko customized kwa nchi.

    hebu msaidie wewe basi, naona unakadya wenzio halafu hutoi jibu.

    ndo usenene huo....

    ReplyDelete
  6. hivi kweli huyu jamaa anataka kuandika karatasi juu ya project management? je mwenyewe anajua au ana taaluma ya project management? maana masuali yake hayaonyeshi ujuzi wake juu ya project management.

    ReplyDelete
  7. Mdau USA,
    Chuo Kikuu Cha Dar-Es-Salaam, kitivo cha Biashara na Uongozi kinafundisha kozi ya "Management Science", pia Chuo-Kishiriki cha Uhandisi na Teknolojia kinafundisha "Industrial Engineering and Management".
    Pia Chuo Kikuu cha Mzumbe kupitia kitivo cha Sayansi na Teknolojia kinafundisha kozi ya "Production and Operations Management".
    Ukiweza kuwasiliana na wahadhiri katika vyuo hivi, inaweza kuwa manali pazuri pa kuanzia; kwani wao ndio wataalamu katika fani hii, na baadhi yao hujihusisha na kutoa Ushauri wa Kitaalamu.
    Natumai ushauri huu itakusaidia. Kila la heri katika utafiti wako

    ReplyDelete
  8. Jamani jamani ndio mambo ya kusoma haraka bila kutafakari, mwenzenu anaataka kujua kama kuna taasisi inayofundisha somo la Project management kama unavyofundishwa uhasibu, uhandisi compute science na vingenevyo. na Kama zipo ni zipi. Vile vile kuuliza software gani imekubalika na inatumika zaidi Tanzania kama kuna makampuni yanatumia taaluma hiyo kisasa zaidi kwasababu unaweza kuwa na project ndio ukatumia microsoft lakini kuna software packages zimetengenezwa maalum kwa Project management ambazo ziko za aina mbali mbali kwa hiyo kama Tanzania wanatumia ni ipi? Ni sawa sawa ana accounting system ambazo marekani wao wanatumia GAAP na Tanzania wanapendelea ile ya uingereza kwa hiyo jamani hii blog ni ya kuelimishana sio kujifanya wajuvi na kujibu visivyoo na hata kama mimi nimekosea kuelezea nielekezwe makosa yangu kwa njia yakistaarabu sio ya kuosha kinywa OK?

    ReplyDelete
  9. Well project Management field kama walivyosema jamaa kadhaa ni kubwa. Katika taasisi za Tanzania kama sikosei hakuna hata moja ambayo inatoa masomo ya field hiyo kama specialization pekee. wanachofanya huwa moja ya module/subjects ndani ya degree kadhaa. Mfano hutolewa kwa watu wanaosomea uchumi, biashara, ICT na engineering ingawa kunaspecific emphasise kwenye specific area. Mfano kwa wale wa ICT wanasoma IT project management wakilenga kusimamia masuala yote ya IT project as project managers etc..
    Kuhusu inatumikaje nadhani kama fields zingine, watu ambao wanakuwa na skill kwenye project management hupewa chance as project managers, facilitators nk.
    Kuhusu software, hakuna software ambayo itakufundisha project management. Software zilizopo zote zinaleng kumsaidia project manager katika process za kumanage project.. mfano planning, bugeting, resource organization etc.

    Lastly sasa hukuwa muwazi unaomba ushauri kama inalipa or ??/ but it is a good field.

    Regards,
    G7

    ReplyDelete
  10. Ni mimi mdau nilioweka hili swali. Nashukuru kwa wachache wenu mlio nielewa. Hii fani ninaifahamu vema. Ninachotaka kujua ni kama kwa Tanzania inatumika ipasavyo ama la? Na kama inatumika je kuna miongozo yeyote inayofuatwa katika fani katika ku run hizo project? Kuhusu software zitumikazo ziko nyingi mahsusi kwa ajili ya hii fani, ninachouliza mie ni kuwa ipi ndo inatumika zaidi huko?
    Kuhusu paper ninayotaka kuandika ni kuhusu fani ya Project management as a whole, mafanikio, makosa, je ni mpya (ina miaka mingapi kutumika TZ), je kuna vitu gani vya kuifanya iwe sanifu zaidi. Hivyo ninayomaanisha na kama nilikosea kusema mwanzo samahani..ila hii ni fani ninayoijua ila sio kwa jinsi inavyo tumika Tanzania.
    Natanguliza shukrani,
    Mdau USA

    ReplyDelete
  11. Mdau US nilikupata vyema; nilikuwa sina majibu ya uhakika ndio maana nikakuelekeza kwa wataalamu UDSM na MU wakusaidie. Kwa kuongezea tu hapo juu... kama ulikuwa unataka kujua kama kuna Chama/Jumuia ya wanataalumu hii, nasikitika kukuambia sidhani kama ipo. Kwa kawaida katika nchi nyingi, wanaohusika na fani hii ni watu wa "Operations Research". Hakuna chama cha "OR" Bongo, ila kinachikaribia kwa mbali ni
    1. Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Ugavi (Nat'l Board of Materials Manegement, NBMM). Ingawa hawa wanajihusisha na upande mmooja tu ambao ni "Supply Chain Manegement".
    2. Bodi yausajili a wahandisi na Body ya usajili wakandrasi (Engineering registration board; Contractors registration board). Hawa wanahusika na usimamizi wa mipango ya ujenzi/ukandarasi zaidi. Ila wanaweza kusaidia kujua pa kuanzia kama unataka kufanya utafiti juu ya fani kiujumla!!

    ReplyDelete
  12. Ng. Nalitolela P.S nimekupata. Shukrani sana. Kwa hio inaonyesha kwa ulivyoniambia hii fani ya project management kwa sasa Tanzania inamezwa na fani nyingine..kuna umuhimu wa wana PM kuungana na kuanzisha jumuia ya wana PM kwa Tanzania. Nashukuru Sana..nina jamaa yangu pale UDSM nitawasiliana nae ASAP..

    ReplyDelete
  13. Mimi nasoma project management arusha kuna tasisi inayoitwa Ticd inahusika sana so ivi vikozi vingine kama human resources, interpreneur, public administration, account, procurement na nyinginezo tunaziheuza module

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...