
Bado hatujajua sababu za mtoto wetu kuondoka bila kuaga na hilo tunalifanyia kazi kifamilia. Tunashukuru kwa msaada mkubwa tulioupata kutoka kwa ndugu,wadau, marafiki,jamaa na taasisi mbalimbali walioshiriki katika kumtafuta mtoto wetu bila kuchoka hadi alipopatikana.
Kwa ujumla wenu nyote tunawashukuru na kuwatakia mafanikio makubwa katika maisha yenu ya kila siku. Shukrani za pekee kwa wanablog na vyombo vya habari vifuatavyo:
Issa Michuzi
Maggid Mjengwa
Michuzi Jr
Haki Ngowi
Tanga TV ITV
Mwambao Radio
Asanteni sana.
Massoud Hamim,
Mzazi wa Mbarouk
Dogo unastahili bakora kwa kuwasumbua wazazi wako ni sisi wanablog kukutafuta!
ReplyDeleteHuyu anastahili adhabu kali sana ili abadili tabia yake hata kama kaudhika na kitu sio sababu kuwaweka wazazi roho juu watu hata hawalali kwaajili yake
ReplyDeleteDuh Afadhali kapatikana ,akiwa salama, maana siku hizi mtu akipotea kama si mwenye ilemavu wa ngozi, mnaanza kujiuliza ..hivi kiganja chake kina herufi "M" ? Poleni Wazazi na wanandugu wote kwa msukosuko huo mkubwa wa siku tatu.
ReplyDeleteMdau
Poleni wazazi na ndugu kwa kupata presha. Ila naona ya kuwa viboko na adhabu siyo tija, muelewesheni tu aone ni namna gani amewasumbua kama kweli aliondoka bila kuaga, na mujaribu kumwelezea juu ya hatari zilizopo kwa sasa. Akitambua hayo sidhani kama atarudia tena.Au yawezekana hata sio kosa lake, watu siku hizi wanatumia madawa ya kulevya kulewesha watu, kwani wangapi yamewakuta haya?! Na pia Tanga na Dar sio mbali, masaa matatu tu kwa gari ndogo umefika. Poleni sana
ReplyDeleteni kweli kabisa anabidi akanywe vizuri huyu maana umewaweka wazazi wako roho juu na haswa huyo aliye mbali na wewe inaelekea baba yake yuko njeya nchi.pia mkupati mama yako matatizo amabye najitahidi kukulea pekee yake.
ReplyDeleteMaoni ya wadau hapo juu yatazingatiwa kwa kiwango cha juu zaidi. Pia nasaha zinazoambatana na kujua kiini cha tatizo lililomuondoa nyumbani zitapewa kipaumbele ili tatizo hili lisijirudie kwake na ndugu zake.
ReplyDeleteKwa kumpata tu...tena salama ni jambo la kumshukuru mungu.Inabidi aadhibiwe mtoto mdogo hatakiwi kuondoka nyumbani bila kuaga....hata watu wazima na nyumba zao huaga wanapoondoka...mkunjeni angali mbichi otherwise goodluck with raising up trouble.
ReplyDelete