KIJANA MBAROUK MASSOUD ALIYETOWEKA TOKA KWAO HUKO TANGA
Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Mkwakwani, Tanga MBAROUK MASSOUD ametoweka nyumbani kwao huko Mikanjuni, Tanga tokea jumatatu tarehe 26/1/2009 na hajulikani alipo mpaka wakati huu na kusababisha huzuni na simanzi kubwa kwenye familia yake.Jitihada za kumtafuta sehemu mbalimbali hazijazaa matunda hadi sasa, hivyo tunaomba msaada kwa yeyote atakaypata taarifa za kijana huyu awasiliane nasi kwenye namba za simu zifuatazo:
1. 0717 998 082 - Mrs.Massoud
2. +1 614 584 2321 Mr. H. massoud( massoudhmj@hotmail.com)
3. 0754 336 128 Abdallah Massoud - Baba Mdogo
4. 0732 302 591 Moh'd Massoud - Baba dogo
5. 0713 770 191 Halima Abdallah - Mama mdogo
6.0713 475 155 WP Mwanaidi - Mama mdogo wa Iringa
7.0774 600 700 Uncle Kimolo wa Arusha
8.0715 260 377 Uncle Arch
9.0754 378 519 Uncle Japhet Makau
10. 0714 648 666 Muddy Massoud - Kaka wa Mbarouk
11. Mkuu wa shule Mkwakwani -0784 947 284
Pia taarifa inaweza kutolewa katika kituo
chochote cha polisi ambacho kipo karibu.
Familia inatanguliza shukrani za
dhati kwa ushirikiano utakaotolewa.


atakua wisconsin huyo, maana t-shirt inaonyesha anependa sana huko.
ReplyDeleteDogo nimekutana nae maeneo ya Malmö hapa sweden, msimtafute dogo anakula maisha huku ulaya!
ReplyDeleteNinyi hapo juu wewe "mzushi" na "annoy" acheni ujinga, kuweni watu wazima kidogo, kuwa nje ya nchi si swala la kujitangaza katika wakati mgumu kama huu wa kumtafuta mtu, acheni upuuzi kama hamna ya kuandika kaeni kimya!!! watu wanahangaika ninyi mnaleta ujinga.
ReplyDeletePoleni sana ndugu na jamaa wote mnaomtafuta huyo kijana, bado mdogo kwa kweli, hatujui alipo, but insh Mungu atamlinda mtampata, akiwa na afaya nzuri insh. ila Michuzi sijui kama unakujua huko Mikanjuni-Tanga, hii taarifa kuitoa humu kwenye blog sijui kama walengo haswa wa maeneo hayo wanajua hata maana ya blog ni nini, achilia mbali kuwa na uwezo wa kuingia na kuona hii taarifa, kwa hiyo ni naona njia nzuri ni ile ambayo inaweza kutumika na watu wengi haswa wa maeneo hayo wakapata taarifa zaidi,mfano kuweka hizi picha kwenye maeneo ya watu huko huko mikanjuni, kwenye baraza za kahawa nk kuliko huku kwenye blog, wengi wanaoangalia hizi blog ni wa daraja tofauti na sidhani kama huko mikanjuni wako wengi.
Mungu awape ngumu na uwezo wa kumpata insh. mdau
Mdau namba moja nimeipenda hiyo, ...umenichekesha sana.
ReplyDelete---
Wahanga msimaindi sana hata kwenye msiba tu watu huwa wanataniana. Nawaombeeni ndugu yenu apatikane haraka... maaana Tanga siku hizi usipime ushirikina umeshamiri sana na wanapenda kukafara watoto.
jamani yani watu wamepotelewa mtoto , wengine mnaleta mzaha?
ReplyDeletehivi umefikira kamai ingekuwa ni wewe unaomba msaada afu unajibiwa pumba kama hizo za ''mzushi'' na anon wa kwanza mngejisikiaje?
tumieni akili saingine. Mungu awasaidie wazazi na ndugu wa mtoto wampate mtoto wao.
Asante anonymous wa Jan, 29 pamoja na waliotangulia kutoa maoni yao kabla yako. Naamini wametumia fikra zao kwa kiwango cha juu kabisa wakati huu sisi wazazi tunapohangaika kumtafuta mtoto wetu mpendwa Mbarouk.
ReplyDeleteKuhusu kuleta tangazo hili kwenye blog hii ya michuzi na nyinginezo , hii imetokana na ukweli kuwa mtoto na wazazi wake pamoja na ndugu wengine ni watu wa kiwango hiki pia na tumeanza kupokea ushauri mbalimbali ya hatua za kufanya katika tatizo hili.
Aidha katika utoaji wa matangazo hatukuisahau jamii ya kiwango ulichoshauri kama vijiwe vya kahawa, bao,karata na taarabu.
Hatua nyingine tulizochukua ni pamoja na matangazo ya Tanga TV, Mwambao radio, wanafunzi na walimu wake wa Mkwakwani Sekondari, Kituo cha Polisi cha Mabawa kilichopo maeneo ya karibu.
Pia tumepata nafasi katika gazeti la Mwananchi la ijumaa January, 30 na ITV saa 12 jioni kwa saa za huko nyumbani.
Bila ya kuchoka, tunaendelea kuwasiliana na vyombo vingine vya habari na usalama katika kumtafuta mtoto wetu.
jamani poleni sana watu naona hawajui kiasi gani unauma kupotelewa na mtoto.im sure wote wanaoongea huo upuuzi hawana bahati ya kujaliwa watoto.sidhani kama wangeongea hayo.
ReplyDeletenaimboea familia mungu awape nguvu katika wakati huu mgumu.Na nawaombea mungu aweze kumrudisha mtoto huyo salama.
maskini pole sana mr massoud yaani nakuombea wewe na familia yako mungu awajalie nguvu katika wakati huu ngumu ambayo unaupitia sasa.Namuombea pia mtoto huyo mungu amuonyeshe njia ya kurudi nyumbani na kumuepusha na mabalaa yote ya huko nje alipo na amrudishe mtoto huyo nyumbani salama.
ReplyDeletepoleni sana