Mtoto Peaceglory Mahimbo akionekana mwenye furaha katika kukumbuka siku yake ya kuzaliwa akiwa na wenzake watoto yatima wa kituo cha msimbazi centre ambapo ndio walipomuamulia wazazi wake akasherehekee nao siku hiyo ya tarehe 01.01.2009 alipotimiza mwaka mmoja katika kumuandaa na maisha ya kuwakumbuka na kuwajali wenye shida.
Mtoto Peaceglory akiwa na wazazi wake Mr & Mrs Mahimbo katika kituo hicho siku hiyo ya mwaka mpya wakifurahia siku ambayo Mungu aliwapa zawadi ya mtoto huyu ambaye walimsubiri kwa muda mrefu.
----------------------------
Hongera Peaceglory, hongera wazazi kwa kufikiria walio na shida katika siku ya furaha ya mtoto wenu. Huu ni mfano wa kuigwa.
-Michuzi



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. OOOOh jamani, mama na baba hongereni sana, Lucy me ni mshkaji wako wa CBE tulikuwa class moja tukila nondo na katumbo ka Peace tulikalea wote mana ulikuwa unatusumbua kweli class, ntakuambia mimi ni nani..ha ha ha ha haaa....nimefurahi sana kukuona...vibuti oyeeeeee!!!!!!

    ReplyDelete
  2. HUYU DADA MZURI JAMANI. WANAWAKE WASIOTUMIA MKOROGO WANAPENDEZA KWA STYLE YAKE. HUWEZI KUFANANISHA NA WANAOFANYA SURA ZAO ZIWE KAMA ZA KUCHORWA. MFANO HUU UIGWE.

    Mdau,
    Zimbabwe.

    ReplyDelete
  3. Anayefurahi na Yatima. Mungu atafurahi naye. Mungu awaongezee Wazazi hawa pamoja na Pieceglory mwenyewe. Happy Birth day to youuu.
    From Maganga Feruzi Ushirombo.

    ReplyDelete
  4. HONGERENI SANA TENA SANAAA...!!! KWAKWELI NI MFANO WA KUIGWA KABISA. NAWATAKIENI KILA LAKHERI NYINGI SANA NA MTOTO HUYU.

    ReplyDelete
  5. Hongereni sana wazazi wa Peaceglory!! Lakini pia jamaa alijitwalia kifaa safi kabisa kama anny wa January 03, 2009 12:36 PM alivyocomment hapo juu. Mwanamke huyu ana upana wa uso, size ya pua, midomo, kidevu na tabasamu lake kwa mbalii viko kweli proportional. Hapo Mungu aliumba na hakukosea hata kidogo. Halafu na yeye anajikeeep natural. Sio kama mabinti wengine unakuta mzuri lakini anajipaka mkorogo na angelface na hatimaye anakuwa kama kinyago. Hongera sana bwana Mahimbo kwa kuoa mke mzuri.
    Mdau

    ReplyDelete
  6. Jamani tusiparamie uzungu kama vile hatuna vyetu. Sasa jina la Peaceglory ndio nini? Wangemuita mtoto wao Furaha, Amani, Bahati, Baraka n.k. ingekuwaje?? Wake up people, mtoto akija huku UK au hata kwenda US watamcheka au kumdharau.

    ReplyDelete
  7. Hongereni sana kwa kupata mtoto mzuri, hivi nyie siyo akina Mr& Mrs Mahimbo wa TPB.Please naomba contact zenu mimi ni Kundi M.Iam so happy for you guys. Mmependeza sana na Mungu atawazidishia kwa kuwakumbuka yatima.Happy birthday to you Peaceglory.

    MDAU U.K

    ReplyDelete
  8. child abuse mbona mnamnyima mtoto starehe? mnamtumia kukidhi matakwa yenu?

    ReplyDelete
  9. picha inaoinyesha kweli hao watoto yatima yaani hawana furaha kabisa, ni hako tu kenye wazazi ndo jino lote nje, inatia huruma sana.

    ReplyDelete
  10. Hongera wazazi na Mungu awajalie muweze kumtunza mtoto wenu akue na maadili kama yenu.

    Ila ni kweli namuunga mkono @ 10:51 pm hivi haya majina ya watoto wetu tunawapaje siku hizi? Halafu kuna majina mengine yana make sense mtu akiwa Tanzania. Mtoto akikua na akajaliwa kuja nchi za wenye kidhungu chao hilo jina linakua halina maana au halieleweki kabisa. Na watoto hao huwa wanakosa raha sana shuleni na kulaumu kwanini wamepewa hilo jina. Kuna wengi nimewaona hapa USA it is tough. Mfano jina la Upendo ni heri umuite mtoto wako Ukundi etc kama hutaki kutumia jina la Upendo kwa maanakiswahili maana kwa kidhungu marekani halimake sense kabisa na wanazania ni nickname ya mastripper. Na lingine ni Precious zuri sana lakini jina hilo ni source ya kutaniwa kwa watoto wa elementary school.

    Kweli majina yetu ni mazuri sana na jinsi ninavyoishi huku ndio jinsi ninavyo yaappreciate zaidi.

    ReplyDelete
  11. Eh jamani i cannot believe my eyes,i though i was running blind for a minute eeh...dude(Mahimbo)where have you been long time jooh na Lucy wow hongereni sana when did glory came into this world eeh?...haya hebu email me please maana we have a lot to catch up...my email is Tyrapereira@hotmail.com

    Wee Miss Kundy hapo juu upo wapi jamani eeh my long lost buddy...yeah that is Mahimbo nakwambia na Lcy i see mahimbo had changed a lot from skinny dude to eeh!....

    ReplyDelete
  12. Hongera sana wazazi was Peaceglory. May God bless your family in 2009.

    ReplyDelete
  13. wewe mdau unayesema kuwa wazazi wamemnyima starehe mtoto wao kwa kumchagulia mahali pa kusherehekea birthday yake umekosea. toka lini mtoto mdogo kama huyo akachagua mahali pa kwenda siku ya birthday yake. wazazi ndio huchagua. kuna ubaya gani mtoto wako kusherehekea birthday yake na watoto yatima? mimi ninakuona unadharau watoto yatima. kwakweli nina wapa hongera kubwa hawa wazazi kwa kufanya hivyo. MUNGU AWABARIKI HAWA WAZAZI NA BINTI YAO.

    ReplyDelete
  14. @anon 10:51pm

    We mtu uko dunia gani? kwanza kumkosoa mtoto wa mwaka mmoja kuwa jina lake si sawa, ni verbal child abuse, what's wrong with the name Peaceglory? it's a very beautiful name!, I know someone by the name Glory in USA and people just adore her name!, there's nothing wrong with calling your child a beautiful name like Peaceglory, it's very Unique!, why use common names like the ones you mentioned all the time? why not go different sometimes? watch out usije kuwa child abuser, you can get yourself in trouble just by saying something against a child especially if you're in North America or Europe, where I guess that's were you are. Omba Mungu akusaidia uwe CIVILIZED!

    ReplyDelete
  15. Mr. and Mrs. Mahimbo.

    You guys Rock!, Very smart of you kwa kumfanyia mtoto birthday na watoto yatima. Mungu Awabariki. You gave me a great Idea. I'll probably do the same thing. I like you guys without even knowing you. You seem to be very nice people.

    GOD BLESS YOU AND YOUR FAMILY!

    ReplyDelete
  16. Good idea! Lakini siku nyingine mjitahidi mnunue na nguo kwa hao watoto wengine basi jamani. Maana hapo mtoto wenu tu ndo aonekana na kivazi chake cha kanisani, wengine wako tu na nguo zao za kushindia.

    ReplyDelete
  17. @anon wa 10:51
    Acha ushamba, hivi unafikiri uko nje ya nchi peke yako!!
    Nani ulisikia anachekwa kwa ajili ya jina lake!!!

    Ndugu yangu oni lako linatisha, na linaonyesha jinsi gani wakati unakuputa...jina ni chaguo la mtu la kidemokrasia, unamwita mtoto wako kwa jinsi unavyojisikia, na kwa wale wenzangu na mimi ukikua unajiongezea na jina lingine la kwako kwa raha zako na kwa jinsi unavyopenda...hakuna dhambi au jinai katika kuitwa au kujiita jina na hakuna mtu mwenye akili atakayecheka jina lako, kwani halimhusu na siyo chaguo lake.
    Ndugu yangu yawezekana hiyo sehemu unayoishi pengine wengine hawafiki.

    Hongera sana Baba na Mama Peace glory, kwa kufanya sherehe na hao ndugu zetu na Mungu akubariki kwa upendo wako na hata faraja uliyowapa na uliyotupa sisi tunaoona upendo wako huo. Kwa nia hiyo uliyoonyesha nawaombe wewe na familia yako Mungu awabariki.

    ReplyDelete
  18. Masikini watoto yatima wanatia huruma sana, yaani nimejisikia huzuni sana, yaani all of them are not even smilling except the birthday baby! Mungu awasaidie!

    ReplyDelete
  19. Msije mkanipakacha kama hao hapo juu but honesty naomba maana ya Peaceglory kwa kiswahili ni nini? Sioni maana yake kwa kingereza sasa ninaomba maana ya hilo jina kwa kiswahili. Naelewa maana ya peace na pia naelewa maana ya glory lakini peaceglory nimeangalia kwenye Webster dictionary lakini sioni. Is it a noun?

    ReplyDelete
  20. hii ni sawa na kusema mjimwema. ukizitenganisha unapata mji then mwema so look up for mji kwenye dictionary then look for mwema. usitubabaishe kwamba hujui maana ya peaceglory. hakuna tofauti ya wewe na huyo aliesema hilo jina la mtoto ni la kuchekwa.

    ReplyDelete
  21. jaman nyie mnamkomalia "mke wa mtu" sijui pua,lips,shavu,sijui nini khaaaaaaaaa HAMJATULIA kbs
    mtoto umefanya la maana kushiriki na yatima,,,yan mtabarikiwa
    they need love &care

    ReplyDelete
  22. Isn't it sad on how people come up with odd comments, The guy from America seems to be so ignorant.Natoa mfano wa hao wadhungu mnaowaona ndio wa kuigwa unajua kuwa watoto wa macelebrity wengi wana majina yenye maana kwao ambayo kwa wengine ni ya ajabu kama vile apple, savannah, Brooklyn, princess Tiaami etc sasa hao utasemaje, acha kudharau uafrika na utanzania sisi wazawa tunaona sawa kabisa hayo ni majina yetu tulipewa na wazazi na tutaendelea kuwapa wanetu.
    Mdau U.K

    ReplyDelete
  23. Katika yote mmesahau, LUCY ana black spot chini ya pua, kwa akweli kaumbika, halafu natural, halafu kasoma, halafu ana upendo. Duuu ebwane duu, duu uuuuuuu.Najivunia dada yangu mtanzania. TUKO juu

    ReplyDelete
  24. jamani nimefurahi sana kuona mnawakumbuka watoto yatima ,niwazazi wachache sana wenye uwezo wakufanya haya mliyo yafanya nyinyi mungu awabariki sana.

    ReplyDelete
  25. hahhahaha yaani kuna mdau kanichekesha kweli hapo juu. Glory maana yake ni mji na peace ni mwema haaaaahhhhhaaa wewe hapo juu umenichekesha sana

    Happy birthday baby gal

    ReplyDelete
  26. hongera mtoto mzuri peace glory na hongera kwa wazazi wako pia ila jamani huyu aliyeuliza maana ya peace glory hajakose ni sawa hata mimi nimebobea kwenye swala la lugha ni muadhiri wa chuo kikuu najaribu kupata maana ya hili jina sipati naomba mnieleweshe nitashukuru pia inawezekana hata wazai wamemuita tu kwa kulipenda bila kujua maana yake kamili. hongereni sana wazazi wa mtoto na mtoto pia

    ReplyDelete
  27. Conguratulaion mr. and mrs. Mahimbo.

    Kundi M, nimekufuma hapa unanitafuta na mimi nakutafuta ila sina Email yako wala simu yako ningekuwa nimesha kupigia. Please my contact ndeale@hotmail.com

    MDAU ZANAKI´S

    ReplyDelete
  28. Matatizo ya English za dictionary. Hizi lugha za watu tuaachie wenyewe.

    ReplyDelete
  29. Huyu nani tena anayeongea nonsense,na kukosoa wenzake, amekosa cha kuongea ama kilicho mpeleka kwenye webside ya michu nini? mbona comment yako haina point, omba kazi basi kwa Michu ya spelling check kabla hajazirusha hewani. Na wa bongo wanaokosea kiswahili wakiandika typing error,inamaana ni lugha ya watu ama wanaangalia kamusi acha ushamba una nyimbo kama nyimbo makwizi ama zilipendwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...