Home
Unlabelled
simba aunguruma dar
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
sasa wakuu huyu mama atafanya kazi ngapi? ubunge, uwaziri au uwenyekiti wa UWT? kweli kutakuwa na tija hapo au ni uroho wa madaraka tu? Ninamshauri JK atafute waziri mwingine badala yake maana inaoneka Sofia yeye mwenyewe ameshajiona kuwa anafiti zaidi kwenye UWT kuliko uwaziri
ReplyDeleteSio uroho wa madaraka ni watunga sehria wabadili sheria zao. How comes watu wengi wanaelimu na ujuzi lakini mtu mmoja analundikiwa mavyeo yote haya? Atawajibika kweli au ndi atakua mtia signature bila kusoma chochote.
ReplyDeleteHalafu UWT ni wa watanzania au wa wanaccm? Vyama vingi vimeanza siku nyingi lakini mpaka leoa hawajaweza kutenganisha kipi ni cha serikali na kipi ni cha chama.
TOO SAD
Mkutano wa Lowassa wazua balaa Monduli
ReplyDelete2009-01-10 12:13:37
Na Mwandishi Wetu
Mkutano wa viongozi wa jadi wa kabila la Kimasai ulioitishwa na kiongozi wake aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, umezua balaa, baada ya mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Mkoa wa Arusha, James Milya, kurushiana makonde mazito hadharani.
Tukio hilo lilitokea jana baada ya mkutano huo wa viongozi wa jadi wa Kimasai kuahirishwa kwa muda kwa ajili ya chakula cha mchana.
Mkutano huo uliokuwa wa siku mbili ulimalizika jana, lakini kwa mujibu wa Ole Sendeka, Lowassa hakuwepo wakati tukio la purukushani hiyo lilipotokea.
Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, Ole Sendeka alisema aliamua kujitetea baada ya Milya kumrushia konde ambalo alilikwepa.
Alisema kutokana na hali hiyo, aliamua kujitetea kwa kumrushia konde moja ambalo lilimpata hadi kuanguka chini.
Akizungumzia zaidi juu ya mkutano huo, Ole Sendeka alisema kwa ujumla haukuwa wa kisiasa na haukupangwa kwa lengo la kumhujumu.
Alisema wakati akichangia mada, katika mkutano huo uliokuwa na ajenda mbili, ya kuzungumzia elimu ya mtoto wa kike kwa jamii ya wafugaji na nyingine ya matatizo ya ardhi, baadaye Milya alichangia hoja hiyo akiwashutumu wanasiasa na hasa katika jimbo la Simanjiro kwamba ni mafisadi na wanafiki.
``Huyu bwana mdogo alinishambulia akidai kuwa sisi wanasiasa na hasa wa Simanjiro ni wanafiki na kwa nini hatuchukuliwi hatua.
Alitamka wazi ingawa hakutaja jina langu, lakini alisema `kama mchangiaji huyo aliyemaliza kuzungumza sasa hivi` akimaanisha jina lake (Sendeka),`` alisema.
Alisema baada ya kuahirishwa kwa muda kwa ajili ya kupata chakula, alimuuliza Milya kwa nini alimshambulia kiasi hicho naye akamjibu kwamba sasa ameanza vita.
Alisema bila kutegemea alirushiwa ngumi, ambayo hata hivyo, alifanikiwa kuikwepa.
``Katika kujitetea niliamua kumrushia ngumi moja ambayo ilimpata na akaanguka chini, nilichofanya ni kujitetea tu katika mazingira kama yale...`` alisema.
Lakini kwa upande wake Milya alisema hakumrushia ngumi, isipokuwa Ole Sendeka ndiye aliyempiga hadi akaanguka chini.
Alisema baada ya kuanguka Ole Sendeka alitaka kuendelea kumpiga, lakini wajumbe wa mkutano huo walimnusuru.
Hata hivyo alisema aliripoti tukio hilo katika kituo cha polisi cha Monduli na kufungua jalada namba Monduli/RB/35/09.
SOURCE: Nipashe
Hongera Mama Sophia Simba. Ukiwa kama Mwanasheria ulibobea katika masuala ya sheria za akina mama nadhani utakuwa chachu ya ukombozi wa mwanamke wa Tanzania. Sisi akina mama wote tunakuangalia na tutakuwa daima mstari wa mbele kukuunga mkono katika juhudi zako.
ReplyDeleteHongera sana mwenyekiti wetu na tumia sasa taaluma yako ya sheria katika kutukomboa akina mama.
Ni mimi mama Gatrude wa Mji Kasoro Bahari.
he huyo wa pembeni si yule lucy mayenga nasikia siku hizi amekuwa mbunge naona ukipata cheo na unatumia cream kujichubua, huyu dada niliishi naye jirani kule mikocheni uswahilini mvua ikinyesha tulikuwa hatuwezi kwenda shule na nyumbani kwao ukipitisha furniture inabidi ziingie kupitia kwenye bati kutokana na mlango wa nyumba yao kuwa mdogo sana nashangaa leo amekuwa mweupe hivi. hongera dada nakushauri sasa umhamishe mama yako umeshapata pesa haifai kuishi tena uswahilini vile kwenye choo cha uani ukijisaidia maji yanakurukia.
ReplyDeleteacha kumnanga mwenzio, hata kama hajamsaidia mama yake au kamsaidia we una shida, gani mkorogo kwa raha zake
ReplyDeletena wewe unayesema mama simba kabobea katika sheria unaelewa maana yake?? amewahi kumrepresent mtu ktk hilo ni advocate ??
she just did a law degree thats all !!