Steve Nyerere akimuigiza JK
Steve Nyerere, msanii maarufu mwenye uwezo mkubwa wa kuigiza sauti mbalimbali za viongozi wa nchi mbali mbali akiwemo JK, Makamba, Tibaigana, Mwl Nyerere,Osama Bina Laden,George Bush na wengineo maarufu.

Steve Nyerere anatarajia kuibuka na kipindi chake cha uchekeshaji kitakachoitwa Steve Nyerere talk show kitakachokuwa kinarushwa na Televisheni ya Taifa ya TBC.

Steve amesema kuwa kipindi hicho kitakuwa na cha kuwaalika watu mbalimbali na kuzungumza mada mbalimbali zitakazohusu maisha halisi ya kibongo yanayoizunguka jamii.

"Kipindi hicho kitakuwa kinarushwa moja kwa moja mimi nikiwa kiongozi wa kipindi hicho,katika kipindi hicho baadhi ya watu mbalimbali watakuwa wanaalikwa kuchangia mada ili kukifanya kipindi hicho kiwa tofauti na bora zaidi"amebainisha Steve.

Amesema kuwa kipindi hicho kitaanza kurushwa hewani mwezi ujao kikiwa chini maandalizi makubwa ya kampuni ya Hatman Productions.
Steve ameongeza kuwa kwa yeyote yule atakayemuhitaji katika shughuli yake ya aina yoyote ile basi awasiliane nae kwa no 0773 782424

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Habari yako Steve,

    Mimi nahitaji CD au DVD yako kama umeshawahi kurekodi. Nitakupigia simu baadaye tuongee zaidi.

    ReplyDelete
  2. Hongera na hivi vipindi ndio tunavyohitaji. Vipindi vya kuzungumzia mambo ya jamii na raia wake wa kawaida

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...