NDUGU MICHUZI ZA WADAU,
POLE NA SHUGHULI ZA KUJENGA (NA KULILA) TAIFA
HIVI SIKU MOJA JK AAMUE ISOMWE DUA NA WOTE WALIONUFAIKA AMA WALIOGUSA HEL ILIYOTOKANA NA UFISADI WA EPA, TWIN TAWA ZA BOT, KAGODA, RICHMOND NA KADHALIKA NANI ATAPONA???
Mdau Njombe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. hawatapona wale walio katika system iliyopitia iyo mihela katika hayo mashirika,asa wale decision makers!!!
    watu wengine wako safi bwanae,sio wote sheitwani kama hao

    ReplyDelete
  2. Kweli swali la kizushi lool watakuja kudondoka wakubwa kibao mbona.huyo JK mwenyewe akisimama atakua labda kajizindika kwanza kabla ajawaruhusu kufanya hio dua.ha ha ha ha .
    mdau 'cha mtu mavi'.

    ReplyDelete
  3. Mi nafiri mdau swali lako ungeuliza ni kina nani watadhurika?. Hilo la nani atapo pona liko general sana katika watanzania takriban 40 Million watakao dhurika hapo hawazidi hata 2,000 na watakiisha dhurika itabidi nchi ifanye uchaguzi mkuu tena na katika uchaguzi huo tunaomba dua tena atakayepindisha matokeo tu naye adhurike. Nchi itakuwa lainii kama tunanawa vile, wauza mafuta, wauza gongo, wenye madaladala, majambazi, waua albino, vinaka, wafanyabiashara wanaobambikia, abadhirifu wa mali za umma, wazinzi, wadanganyifu wote wawe wa elimu etc, walarushwa Yaani wote tuanwasomea dua wakirudia tu wadhurike. Nakwambia katika mwaka mmoja tu Bongo itakuwa Dubai, miaka mitano itakuwa NY. Yaani haki tu, kazi nje nje unachagua ufanye ipi. "YAANI KAMA HIYO DUA IPO NI MKOMBOZI PEKEE WA BONGO"

    ReplyDelete
  4. tatondoka wachache ,kwani swala hizo huwashika wale waliokula au kutumoa wakijua zimetoka wapi, lakini naamini akbiza mkuu wa wilaya ya nanihii hawezi kupona ,kwani kwa njia moja au myingine akijua kabisa ,lazima ameshakutananazo.

    ReplyDelete
  5. Hakika wangekufa ama kudhurika wengi isipokuwa wafuatao ambao BAADHI TU, KATI YA WENGI):
    1. Balali, Marehemu(?)
    2. Zakhia, WF aliyepita
    3. Andrew Chenge, aliyekuwa
    mwanasheria wa serikali
    4. Basil Mramba, WF aliyepita
    5. Baadhi ya maofisi waandamizi wa
    BoT
    6. Wazee wa miundombinu
    7. Watembeza vimemo na
    8. Wote walio karibu na kushikana
    mikono

    Hata hivyo, siamini kama JK mwenyewe angeruhusu hiyo dua isomwe pamoja na kwamba hao hapo juu wangesalimika.

    Ambao wangedhurika ni wale waliopokea bahasha zisizo na anuani. Yaani, we acha tu! Wangesalimika wale ambao hawakupokea bahasha na badala yake walitumia mifumo iitwayo "electronic a.k.a automatic" i.e banking! Hajalishi bank ya wapi, hata kama ni ya huko New Jersey

    ReplyDelete
  6. Lo! Ama kweli wewe mdau wa Njombe ni MZUSHI! Ungetakiwa kuachia hapo kwenye akina Richmond na EPA na nanihiino...sasa umeongezea NA KADHALIKA...hiyo n.k. ina mambo mengi mno! Kwa hiyo kwa kweli hakuna atakayebaki! Maana BONGO imekuwa kila mtu anatumia ubongo kumFISADI mwenzie..

    ReplyDelete
  7. Mimi naona zaidi ya asilimia 50 ya watanzania watadhurika kwani hiyo mihela ilikuwa pia kwenye uchaguzi ambapo tulikula mipilau.
    Unakumbuka baadhi ya vinara waliokuwa wanapiga kelele juu ya EPA, maskini hawakujua kuwa EPA itawakumba jamaa zao, wengine walionekana kuhangaika kutafuta mipesa ya kuwawekea dhamana.
    Sasa hapa nafikiri hata mdau wa Njombe anaweza na yeye akadhurika na hiyo dua akabaki ameduwaaa

    ReplyDelete
  8. we kweli mzushi, unaleta habari za dua hapa! hata msome mpka kitabu kiishe hatudhuriki ng'o.... na mihela tumechota!

    ReplyDelete
  9. Ikiwa dua ya albadili ya kukaanga mtama na isomwe na watoto ambao ni malaika wale wallahi habaki mtu. Jamani acheni mchezo wa masihara. Nawaambieni hatabaki mtu wala kitu. Maanake hata kama fedha ilinunulia chakula cha mbwa au kuku nao watakufa. Na gari lililobeba hiyo mihela na hao waliosafiri na hilo gari wote watapukutika pamoja na gari.

    ReplyDelete
  10. Ikiwa dua ya albadili ya kukaanga mtama na isomwe na watoto ambao ni malaika wale wallahi habaki mtu. Jamani acheni mchezo wa masihara. Nawaambieni hatabaki mtu wala kitu. Maanake hata kama fedha ilinunulia chakula cha mbwa au kuku nao watakufa. Na gari lililobeba hiyo mihela na hao waliosafiri na hilo gari wote watapukutika pamoja na gari.

    ReplyDelete
  11. Ikiwa dua ya albadili ya kukaanga mtama na isomwe na watoto ambao ni malaika wale wallahi habaki mtu. Jamani acheni mchezo wa masihara. Nawaambieni hatabaki mtu wala kitu. Maanake hata kama fedha ilinunulia chakula cha mbwa au kuku nao watakufa. Na gari lililobeba hiyo mihela na hao waliosafiri na hilo gari wote watapukutika pamoja na gari.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...