dear michuzi,
tumeongea jana mchana kwa simu, kwamba kuna zoezi la kuharibu mazingira,i.e kukata miti katika ufukwe wa ferry,(mbele ya Ikulu)mpaka ocean road.

nilipouliza watu waliokuwepo jibu ni kuwa panafanyika maandalizi ya ujio wa raisi wa china, na wengine wakasema kuwa panawekwa car park.

ila JE serikali juzi tu imetumia pesa nyingi kupanda miti along kilwa Road,minazi katika 3km from Bandari bendera Tatu mpaka junction ya kilwa road na mandela Rd (uhasibu) both sides of the road,3km mara 2= 6km,imepandwa minazi.

miti ya pale ocean road,iligharimu pesa kuipanda,hakukuwa na sababu ya kuing'oa.

naomba uziweke hizi picha ili tupate maoni ya wadau and if possible tuelezwe kwa nini amepitisha hili zoezi.

mdau wa Mazingira

Na Mdauzzz
niaje tena?




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. "CONFUSED" City Fathers!!

    ReplyDelete
  2. Acha kufuatilia kazi za watu wewe, hujui kwamba hapo kuna ujenzi unafanyika na kuna asilimia kumi ya gharama zitaenda kwa wenyenchi? kwani hayo mamiti yanawaingizia kitu gani kwasababu zile asilimia kumi zilizogawiwa kwa mkataba wa kupanda hiyo miti hujui kwamba zimekwisha? acha mambo yako lazima ukumbuke na maslahi ya wenzako. Mazingila, mazingila watakula mazingila hayo?

    ReplyDelete
  3. Unajua ili upate kazi lazima ufanye kazi. Sasa wanachokifanya hao ni kwamba kuna pesa ilitolewa ya kupanda hiyo miti (kazi ilifanyika), kuna pesa imetolewa ya kung'oa hiyo miti(kazi inafanyika) na baadae pesa itatolewa ya kupanda mingine(kazi itafanyika). Hivi ndivyo kazi inavyofanya upate kazi nyingine nina uhakika mdau wa mazingira huenda zamu itayofuata itakuwa ni kazi yako utapewa tenda ya kupanda kwa sasa ni zamu ya mwenye tingatinga. Ila ukumbuke mkono...., Hii ndiyo bongo bwana tambarareee mwanawane ila yote hiyo ni "wizi mtupu"

    ReplyDelete
  4. Je unafahamu umuhimu wa miti katika maisha ya bindanamu,Hasa sisi tunaoishi mijini where polution everywhere!!
    Juzi tu JK kapanda miti ktk uzinduzi,
    alafu leo watu wanakata miti,tena imepandwa na utawala uliopita,yeye anakata tuu.
    Huu ni Wizi MTupu!! na kutojali afya za Wananchi wapiga kura :(

    ReplyDelete
  5. wewe Anoymous wa pili hasira za nini umueleweshe tu mwenzio????? watu wanuchungu na nchi yao nenda na wakati bwana.

    ReplyDelete
  6. Hii ya kukata miti mbele ya Ofisi za Ikulu ni mpya, ni hivi majuzi tu tulikuwa tunaadhimisha siku ya upandaji miti.
    Eneo hili lilitakiwa kuwa mfano wa kuigwa.

    Mdau
    http://drfaustine.blogspot.com/

    ReplyDelete
  7. Jamani mbona mambo ya ajabu? Kwanini wanang'oa hio miti? Kweli tumekwisha, yani watu wanafikiria ulaji wao wa sasa na kuto kujali kitu chochote kingine.

    ReplyDelete
  8. Jambo hili tulifanyie utani kama si wakazi wa Dar kuikoromea serikali kwa kwenda mitaani kuandamana! basi mjue miaka michache tu Jiji litapandwa miti ya bandia(Plastiki)kutoka china.

    ReplyDelete
  9. Mr.Ndori asante kwa mchango wako,nina idea kidogo.Hao 'watu' uliowauliza na akina nani?Je wanahusika na huo ung'oaji wa hiyo miti.Ungechukua muda kidogo kwenda kwenye ofisi za jiji,idara zinazoshughulikia mazingira halafu ukatuletea info za uhakika kutoka huko ingekuwa vizuri zaidi.Siyo kitu cha ajabu sana kukata miti na kuweka kitu kingine ili mradi tu taratibu zote zikiwemo za mazingira zinafuatwa.Siyo vizuri kulaumu bila kuwa na data za kutosha.Ni hayo tu.

    ReplyDelete
  10. Watanzania sisi ni watu wa ajabu kabisa!!!

    ReplyDelete
  11. ndo manake annon apo juu
    ni "kula kwa kwenda mbele" haturudi nyuma wee ushaona mto wapanda mlima??
    zimeisha za miti now zingine ndo izoooooooo
    "*'@~## nanihii zao sana awa!!!

    ReplyDelete
  12. Bro Michu nafikiri inaweza kuwa kitu cha busara kumrushia hii thread mtaalam mwenzio mheshimiwa Salva ili aingie huku atuambie nini kinachoendelea hapo kwenye ufukwe. Maana vinginevyo tutakuwa tunaongelea kitu tusichokijua.Nafikiri tunaweza kuwa na nafasi nzuri zaidi ya ku argue baada ya kupata maelezo yake

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  13. Hehehe anon wa 13th jan 1201 umenifurahisha sana maana ndio ukweli wa mambo hiyo miti itapandwa na kukatwa mara mia hata to mantain livelihood za wenye nchi lol

    ReplyDelete
  14. wewe anonymous hapo juu siyo mazingila ni mazingira,waswahili bwana kiswahili kinawashinda kazi kuwakosoa watu wakiandika english.

    ReplyDelete
  15. MICHUZI HEBU PIGA SIMU IKULU TAFADHALI SANA. MITI WANAYOKATA IMEKUWAPO HAPO TANGU NYERERE YUKO IKULU, NA PENGINE KABLA YA HAPO. MITI HIYO INALETA MANDHARI NZURI SANA YA ENEO LA IKULU.

    WANAWEZA KUPUNGUZA MATAWI YALIYOOZA, LAKINI SIYO KUKATA/KUNG'OA MTI WOTE.

    MICHUZI TAFADHALI WASILIANA NA IKULU WAELEZE KILIO CHETU.

    ReplyDelete
  16. naungana na wadau wanaosema miti isikatwe ovyo na pasi kuwa na sababu; kwani zaidi ya kupendezesha, ni vizuri kwa mazingira na afya.

    Lakini kabla hatujaanza kulaumu tungejua ukweli wa kinachoendela hapa. Pengine kuna sababu ya maana kabisa na yenye faida kubwa (iwe ya kifedha au vinginevyo) ya kukata miti hii.

    ReplyDelete
  17. Mimi nahisi wataalam wetu wa mazingira hawajui ni kiasi gani cha gesi ya carbon dioxide (CO2) kinachozaliswa hapo Dar kwa siku na ni njia gani bora za kupunguza hiyo gesi. Inaonekana wanajua umuhimu wa miti lakini hawajui kiasi cha uchafuzi wa hewa ambacho kingepunguzwa na miti. Mimi nashauri sasa wataalam wetu wawe watu wa kwenda na takwimu na siyo kusema maneno kijumla jumla kwani athari zake ndiyo kama hizo. Bongo magari mabovu ni mengi sana, hivyo uchafuzi wa hewa nao ni mkubwa sana, athari zake kwa viumbe ni kubwa na ni nyingi. Tubadilike

    ReplyDelete
  18. Jamani si mnajua mambo ya bongo? Hiyo itakuwa ni amri tu ya mkubwa fulani kwamba hiyo miti yote ikatwe na kweli inakatwa. Sioni cha ajabu pale. Si kuna kampeni za upandaji miti kila mwaka na kuna kasma yake kabisa. Sasa tatizo liko wapi? Waache tu waikate itapandwa mingine. Bongo tambarale

    ReplyDelete
  19. Akili ni nywele.

    ReplyDelete
  20. Akili ni nywele kila mtu ana zake na WATANZANIA I AM AFRAID HATUNA. Don't give me any lame excuse as to why hiyo miti inakatwa. NO REASONS WHAT"S SO EVER! Kama panatakiwa kujengwa kitu basi hiyo miti ihamishwe na sio kukatwa! kama wengine walivyosema hiyo ni amri tu ya mkubwa mwenye hayo magari kanunua sasa anatafuta tenda zisizo kuwa na kichwa ama miguu. Au utakuja kusikia hiyo sehemu imeuziwa mkubwa fulani anaanza kuleta vitu vyake visivyokuwa na mbele wala nyuma. YAANI TANZANIA KUSEMA KWELI INANICHOSHA SANA! BUSTANI ZA KUPUMZIKIA HATUNA BASI HATA HIYO MITI INAYOWAPA WATU VIMVULI WAKITEMBEA BARABARANI TUNAIKATA, KWELI TUTAFIKA SISI. YAANI VIONGOZI WETU WALIKUWA WANASUBIRI BABA WA TAIFA AFE TU WAGAWANE NCHI, NAKUTUFANYA WANANCHI WAJINGA. BUT I HAVE NEWS FOR YOU MAFISADI, FOOL US ONCE SHAME ON YOU, FOOL US TWICE SHAME ON US. NA HATUTAKUBALI MMUENDELEE KUTUFANYA WAJINGA SIKU NENDA SIKU RUDI. NO!!! NO!!MMEIBA HELA SASA HATA MITI MNATUKATIA WHAT NEXT?

    ReplyDelete
  21. MAALIM ISSA HABARI ZA SHUGHULI, NAONA WAHESHIMIWA WANAISHI NA KUFUATA TARATIBU ZA UONGOZI KWA "MISEMO/METHALI N.K" NA INASEMEKANA UNASEMA KUNA "PANDA MTI KATA MTI" KAMA SIO "PANDA MTI KATA MITI".

    ReplyDelete
  22. Shame shame shame!!!!!Think about the next generation....what happened to sustainable development???
    Tunazaa watoto promising them the world....Is this what we have in mind???
    Conserve the environment and protect mother earth from global warming....think green and stop being selfish.

    ReplyDelete
  23. WENYE NCHI HAO BWANA. KAONDOKA MKOLONI MZUNGU SASA TUNA MKOLONI MTANZANIA, KAKA ZETU, DADA ZETU, NDUGU ZETU, MARAFIKI NA MAJIRANI ZETU WAO NDIO WANATUFANYA HIVYO. ANGALAU WAKOLONI WALITUTAWALA KIZUNGU NA KUJENGA NCHI. HAWA NDUGU ZETU VIONGOZI WA SASA WAO WANAHARIBU KILA KITU. WANASAHAU HELA ZINA MWISHO! HELA ZINA MWISHO NDUGU ZETU!

    ReplyDelete
  24. hivi viongozi wetu wanafikiri kwanza kabla hawajafanya jambo au wanakurupuka tu. ni mtu gani aliye na akili nzuri atakata miti. hivi hawajui faida ya miti. wakoloni walipokua wanaitawala hii nchi walipanda miti mingi sana. walijua faida yake. toka wakati wa uhuru watu wamekua wakijikatia miti hovyo na serikali imekua ikinyamaza. hata ile misitu ilikua imetengwa karibu na miji watu wameiaribu kwa kujenga nyumba kwenye hiyo misitu. no wonder joto linaongezeka na ukame unaongezeka. jamani tuige mifano ya nchi zilizoendelea wanavyo tenga sehemu nyingi kwenye nchi na miji yao kwa ajili ya kupanda miti. tusijenge nyumba kila mahali bila ya kuacha sehemu za miti na mimea.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...