SINA KAWAIDA YA KUINGILIA MJADALA AMA MIJADALA, KWANI NIKIWA MTUMISHI WA GLOBU YA JAMII, SINA UBAVU WA KUFANYA ZAIDI YA KUBANDIKA KILA KINACHOKUJA MRADI HAKICHAFUI HALI YA HEWA.
NIMEULIZA USENENE UTAISHA LINI KWANI AGHALABU MFANO WA MDUDU HUYO HUWA NAUAMBATANISHA NA TABIA YA BAADHI YA WADAU KUPONDA KILA KILICHO MBELE YAO, NA KUTOA TASWIRA KWAMBA BAADHI YA WABONGO HAWANA LA KUFANYA ZAIDI YA KUKATISHA WENZAO TAMAA. YAANI BONGO HATUNA ZURI? HATUNA JEMA? KILA MTU ANA KASORO?
SIPENDI KUSEMA MENGI, ILA NATAKA IELEWEKE KWAMBA NIMEGUSWA NA KUSUMBULIWA SANA NA MJADALA UNAOENDELEA WA MH. SOFIA SIMBA NA PIA MAONI YA BAADHI YA WADAU (WACHACHE, SIO WENGI AMA WOTE, TENA WANAKERA KWELI!) AMBAO SIJUI WANAMUONAJE MDAU JOHN MASHAKA KIASI CHA KUTAKA KUMWEKA KWENYE KUNDI LA UADUI WA JAMII BADALA YA KINYUME CHAKE. UKIWAULIZA KAWAKOSEA NINI, HAKUNA. ILA TU NI SABABU ANATHUBUTU. JAMANI, TATIZO LIKO WAPI??
TUKIJA KWENYE KUTHUBUTU, HASA UKIMSIKILIZA MWANAKIJIJI, UTAKUTA ANASEMA NENO HILO HILO, JAPO HAJALITAMKA. WABONGO KATU HATUTOENDELEA KWA KUOGOPA KUTHUBUTU, ETI KWA KUWA UTAITWA MJUAJI, MTAKA SIFA N.K.
WADAU, NAOMBA KWA UNYENYEKEVU MKUBWA KWAMBA IKO HAJA YA KUBADILIKA NA KILA MMOJA WETU 'ATHUBUTU' KUFANYA KILE MUNGU AMEMJAALIA. NINA MAANA KWAMBA KUKOSOA (KWA KUJENGA, SIO KUBOMOA NA KUKATISHA TAMA) NI MUHIMU KATIKA KARNE HII. ZAMA ZA UJIMA ZIMESHAPITA. HAKIKA TUTAPIGA HATUA HARAKA SANA, TUKIWEZA KUPATA MBADALA WA KUKALIA USENENE.
ACHA MTU ANAYETHUBUTU AFANYE HIVYO. WEWE KAMA HUTAKI KUTHUBUTU USIKATISHE WENZIO TAMAA.
INANIUMA SANA TABIA HII YA USENENE. MIFANO NI MINGI MOJAWAPO NI KAMA HUO HAPO CHINI KWENYE KUBOFYA AMBAO UTAUKUTA NA KUONA MAONI YANGU JUU YA 'USENENE'.
HAKIKA BAADHI YA WADAU MNAUDHI KWELI NA KUKATISHA TAMAA WENZENU . SIJUI NI SIFA AMA NI ROHO MBAYA DHIDI YA MWANAJAMII MWENZIO. YAANI INAKERA SANA NA HATA WATANI WETU WA JADI WANATUCHEKA NA KUTUWEKA KWENYE FUNGU LA AINA GANI SIJUI.
NI AIBU KWELI JAMANI WADAU. TUACHE HIZO TABIA ZA KISENENE.
HAZISAIDII KITU AMA MTU. TUMEROGWA AMA NISEME NINI?? KWA NINI KILA KITU NA KILA MTU (KWENU NYIE BADHI) SIO SAWA??? NA KWA NINI KILA MTU KAKOSEA??? NA WEWE MWENYE 'USENENE' UNA UKAMILIFU GANI HAPO ULIPO??? ANGALIA KIDOLE KIMOJA KINACHOMUONESHA UNAYEMKANDIA, VITATU VINARUDI KWAKO. TAFAKARI
-MICHUZI
KUPATA MFANO WA 'USENENE'

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 47 mpaka sasa

  1. MICHUZI UNATUCHANGANYA

    ReplyDelete
  2. Ni ugonjwa wa kuchukia. Inatokana na kozi fulani inayofundishwa seminari ya kuona watu fulani hawana sifa au haki kwa msingi ya kibaguzi. Kozi hii wamepewa pia waandishi wa habari katika semina zilizokuwa zikiendeshwa pale Morogoro za kutengeneza hoja dhidi ya watu wenye imani tofauti na yao.

    Wamejenga mtandao na ndio huwachafua watu wengine au kwa watu wa imani ayo wanaoona kuwa wanawaunga mkono watu wenye imani hiyo. Siku zote akichaguliwa mtu (balozi, waziri, PS au mkurugenzi wa shirika kama sio wao, tarajia usenene mwingi utakuwepo.

    Kinachonishangaza eti wewe hulijui hili.

    ReplyDelete
  3. Nakubaliana na wewe kaka. Hii hali haitatufikisha popote zaidi ya kuturudisha nyuma. Wenye fikra pevu husikia na kutenda yaipendezayo jamii. Ni wito wangu kwa wahusika kuacha vitendo vya namna hiyo kwani tuna kazi kubwa sana mbele yetu ili tuweze kuendelea. Katu majungu hayatatufikisha popote. Nikishasema hivyo napenda kumsihi hata mwenzetu mwenye website ya UTAMU ambayo huweka picha za watu kwa kuwadhalilisha, Anachokifanya hakitamsaidia chochote kwani wanadamu ndiyo hatumjui wala kumuona lakini Mungu anamuona na akumbuke kwamba anachokifanya kinaumiza ndoa za watu wengi na vilevile kinaumiza sana moyo wa Mungu aliyezibariki hizo ndoa. Hivyo kumbuka ndugu yangu unaweza kufurahia unayoya post katika webpage yako kwa kuwa haujulikani lakini Mungu anakuona, fikiri mara mbilimbili ni ndoa ngapi zimeumia kwa sababu yako? Utakuwa haujachelewa ukiacha sasa kwani unachokifanya si kizuri kamwe!

    ReplyDelete
  4. Ahsante sana Michuzi kwa ujumbe wako huu mzuri. Jamani WaTanzania tuhamasishane na tusaidiane badala ya kukejeliana na kutoana kasoro na kasumba zisizo na faida yoyote. Our kids and the whole nation need INSPIRATION and DREAMS.

    ReplyDelete
  5. BWANA MICHUZI,
    AHSANTE KWA KUWA UMENENA.WAKATI MWINGINE NAJIULIZA HIVI HAWA WATU WANAOTUKANA NA WANAOSEMA MANENO MABOVU AMBAYO SIYO YA KUJENGA KAMA WANA AKILI TIMAMU? WAKATI MWINGINE NAFIKIRI KAMA VILE WANAVUTA BANGI KWA MASAA 24 NDIO UWEZO WAO WA KUFIKIRI UNAKUWA MDOGO NA KUFIKIA UKOMO KIRAHISI.NIMEKUWA NIKISOMA BLOG YAKO NA NYINGINEZO LAKINI NASHANGAZWA SANA KWA SABABU WENGI WA WATU WANATUKANA WAZIWAZI AU KUTOA MANENO YA OVYO YENYE KUKERA.KIMOJA AMBACHO KINANIKERA ZAIDI NI KASHFA NA MATUSI AMBAYO HAYATUSAIDII.MIMI NAISHI MASSACHUSETS NILIPOKUJA NYUMBANI MIAKA MITATU ILIYOPITA NIKIWA NA FAMILIA YANGU WAKIWEMO WAZAZI WANGU WAKATI TUKITARAJIA KUSAFIRI KWENYE STENDI MOJA YA BUS NILISHANGAA KUSIKIA WATU(SIJUI WAPIGA DEBE)WAKITUKANA MATUSI MAKUBWA OVYO, HAKIKA ILIKUWA NI FEDHEHA KWA FAMILIA YANGU NA WATU WOTE WALIOKUWA WAKITARAJIA KUSAFIRI NI AIBU TUPU.WENGINE NA POLISI WALIOKUWEPO WALIKUWA WANAONA KUWA NI KAWAIDA HAKUNA HATUA YOYOTE ILIYOCHUKULIWA,NASHINDWA KUELEWA KAMA HUU NI UTAMADUNI WA KISWAHILI KUTUKANA MATUSI YA NGUONI SEHEMU YA ABIRIA.NILIISHI KENYA NIKIWA NAFANYA KAZI UNDP MWAKA 2001 NILIONA USTAARABU MKUBWA SANA HAWA JIRANI ZETU WANAOONYESHA NA NILIVUTIWA NA HAWA JAMAA WANAVYOMAINDI MAMBO YAO.KILA MTU YUKO BUSY NA MAMBO YAKE HAKUNA MIKUSANYIKO YA OVYO(HANG UPS)NDIO MAANA NIKASEMA HUENDA MATUSI,KASHFA NA UVIVU(KUZUBAZUBAA MITAANI) NI MOJA YA UTAMADUNI WA KISWAHILI.AMINI USIAMINI TAIFA LETU LIMESHINDWA KUNYANYUKA KWA MIAKA 47 TANGU TUPATE UHURU KWA SABABU YA HIZI MENTALITY MBOVU MBOVU TUNATAKIWA PRODUCTIVE BADALA YAKE NGUVU KAZI KUBWA INATEMBEA TEMBEA MCHANA KUTWA BURE,BASI TUWE CREATIVE WENGI WETU HAWAJALI TUNAWEZA KUKOSOA TU MAMBO WALIOANZISHA WATU WENGINE YA KWETU KUANZISHA HATUWEZI.LAZIMA TUBADILISHE MINDSET ZETU AMA SIVYO TUTAENDELEA KUCHEKWA NA MAJIRANI ZETU.

    ReplyDelete
  6. Mkubwa hiyo inatokana na tabia ya wivu wengi wetu tumejaa wivu hatupendi kuona wenzetu wanjaribu kufanya vitu vya maendeleo.

    Naugana mkona na mdau mmoja aliyesema wengi wanaotukana au kukashifu wako nje ya nchi.

    Nasema hivyo sababu tangu nimekuja hapa ukerewe nimeona more than 60% ya wabongo niliokutna nao hukuwanaponda watu wanaojaribu au wanaofanya vitu vya maendeleo.

    Inauma sana

    ReplyDelete
  7. We michuzi nini maana ya usenene? usije anzisha balaa hapa

    ReplyDelete
  8. Michuzi,tatizo hilo la "Usenene" lipo sana kwa wale wasioona mbele.yani wale wanaoelekea kukata tamaa kimaisha ama kuridhika na walipofikia kwa kuamini kwamba hata wafanye jitihada gani,wataendelea kupia HATUA 2 MBELE,then HATUA 16 NYUMA.
    wengi wa hao "BIMBIRISA KIMBA",huwa hawana tena matarajio,ubunifu mpya wa maisha na wala kanuni yoyote ya maendeleo.nimeona hiyo kwa waTZ wa hapa nyumbani na hata walio Overseas for more than 20 yrs.same old same old.
    they're who/what they're n nothing can be done abt it.
    cha muhimu ni kwenda mbele 2 bila kufikiria hao wazee wa "DEAD ZONE" watapayuka kipi kipya.teh teh

    ReplyDelete
  9. Mkuu wa wilaya ya nanihii hapo kidogo unaumiza kichwa bure!!! moja ya kazi ya blog ya jamii nikupokea mawazo kutoka kila kona, yawe mabaya mazuri au yako neutral!!! hii age ya mtandawazi inakuja na faida na hasara zake. haiwekekani kila kitu kikawa maziwa na asali peke yake, sometime kuna mchunga kwa pembeni.kumbuka tu kuwa huu ni mjadala and dont try by any means ku- oppress sauti za wenye mawazo ambayo huyakubali au unayaona yanatolewa katika fikra ndogo. katika kila jamii kuna mchanganyiko wa watu tofauti hivyo basi mijadala lazima iliflect jamii yetu. kama jamii nzima ingekuwa na only positive people taifa letu lisingekuwa hapa!!

    ReplyDelete
  10. Mdau mkuu hapo umenena, watanzania hawaamini chochote kizuri, lakini sio kosa lao,fuatiria makala za jenerali ulimwengu,Makala ilikuwa na jina NCHI YA WABEUZI, KAMA makala za mwezi wa kumi.inasikitisha kuwa hivyo,na sio hali hiyo unayoiona ktk blog, hata vijijini huko nilikokuwa kabla ya kuja ulaya hali ni hiyohiyo,hakuna anayefanya jema,kama lipo, anakitu anatafuta na sio uzalendo.NDO IMANI ZA WATU.
    Hata hivyo mwenyekiti nawe unamakosa, umekuwa mpole mno, unapokea chochote, hata kama wadau hawatakiona wewe utakiona na hutaki kukijibu kama sio kizuri, nakumbuka nimekukosoa mara nyingi lakini hupost,dawa ni kwamba anayeandika vibaya mpe chance,kuna siku atajiona mjinga kama alichosema hakina akili.
    WATANZANIA hawatabadirika kwa sasa kwa sababu ya nchi kuwa na wabeuzi wengi,hawaamini chochote,soma RAIA MWEMA , maoni ni hayo hayo,wanaudhi sana,
    tusikate tamaa ,tuendelee kusema .USENENE utabadirika tu.

    ReplyDelete
  11. Ndugu Michuzi (pengine ni siku nyingi hujasikia mtu akikuita ndugu) ninakupa pongezi kwa busara unazojaribu kuzitoa hapa. Lakini nina mtazamo tofauti kidogo. Utamu wa uandishi wa blogu ni kupashana habari na kuelimishana, kubadilishana mawazo juu ya masuala mbalimbali, na wakati huo huo washiriki wakiburudishana kwa kutupiana utani (ambao ni pamoja na kinachoweza kuonekana kama kuchafua hewa-inategemea unaliangalia kutoka pembe gani!!) na kutupiana changamoto (kubwa na ndogo) kiutani!!! Kwa mfano malumbano juu ya kwa nini mtu fulani kajieleza hivi au vile, ni changamoto, ni utani, ni burudani, ni mwendelezo wa utamu wa kijiwe!!! sioni 'usenene' kama nasaha zako zilivyojiweka wazi!!! ninaomba kutoa hoja na shukrani kwa kuendeleza libeneke.

    ReplyDelete
  12. baada ya watanzania kuweza kusoma na kuandika no one will be immune for anything. as long umeweka issue yako mbele ya wananchi. the well wishers will praise you and hater will chants in hates rhythm.
    kuna ubaya gani wa kuwa hater, inaruhusiwa.acha watu wawe na mawazo tofauti, huo ndio uhuru wa kujieleza, maadamu umesema wako wachache nini tatizo. mawazo KAKAMAVU achia serikali za africa, their citizens they can't even scratch their butt.kwa kuongopa kushitakiwa.

    ReplyDelete
  13. usenene usisumbue lkn nawashuri wale wote wanahitaji uchumba wanaweza kupeleka picha zao blog huru ya jirani wazee wa kujiramba..

    Benzy

    ReplyDelete
  14. Mwalimu Nyerere alisema, namnukuu, " kama unampenda sana mualike unywe nae chai", wakati akitoa maoini yake juu ya mh John Malecela.
    Hii ni uthibitisho kuwa kama mwanahabari pindi unapomhoji mtu hauna majibu na matokeo ya majadiliano yenu.
    Mwanakijiji kama kweli wewe ni mwanahabari kweli hili jambo lisikusumbue kwani mh Simba aliyoyasema ndio kinyaa kwa jamii.
    Swali kwa mh Simba. Je mtu wa kwanza kumtunuku digrii mwenzie alikuwa na digrii?

    ReplyDelete
  15. najua utabania hii lakini its ok as long as utaipata wewe.
    Nyie wabongo mnataka hata mtu akimtia mwenzie kidole anyamaze si ndo matokeo yake kama kasheshe ya EPA na kwanini watu wanyamaze kama ulivyosema "karne ya 21"unajua maana yake? ukweli na uwazi sasa acha watu wakupe ukweli.
    Wewe unaemtetea John Mashaka wewe akisha kununulia lunch hapo city garden unajifanya kumfagilia kwenye kiblog chako cha kishamba mimi mwenyewe binafsi naingia humu kuwaokoa wabongo wenzangu wasije wakapoteshwa na imani yako mbovu.!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  16. Zamani nilikuwa nadhani ndio tabia ya watanzania. Lakini nimegungua wengi ambao hawana zuri la kusema especially kwenye internet maisha yamewashinda, wamejaa frustrations kwahiyo wanataka ku-pull everyone down with them. Kitu ambacho hawajui ni kwamba ndio watazidi kujigandamiza na kuwa insignificant and very unhappy in this world. Laws of attraction. Hamna la kufanya zaidi ya kuwaonea huruma or pray for them.

    ReplyDelete
  17. du haya maoni yako mkuu yamenipunguza speed zangu zengine za kijinga na yamenifundisha kiasi fulani pamoja na ukubwa wangu kweli kila siku unajifundisha jambo jipya ujumbe ulioutoa ni kweli kabisa na nina uhakika umefika kwa wahusika ambao ni sisi wenyewe lakini ubaya wake kila mtu anaona ni mwengine kumbe ndo sisi wenyewe ukisikia tz ni nani ni kila mwananchi wa huko kwahio ndo sie na ni tabia yetu cha kushangaza kila mtz anayo hio tabia mfano enzi hizo tunasoma ukijaribu kuongea eglish ukikosea kidogo utachekwa na hata asiyejua sifuli inaitwa nini kwa english tubadilike watu wangu mie mmoja wapo nisha amua kubadilika

    ReplyDelete
  18. MKUU WA WILAYA YA NANII.... UJUMBE UMEFIKIA WALENGWA, NAFIKIRI SISI WABONGO TUMELAANIWA HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA SASA CHA MPITO, WATANI WETU WA JADI WA NCHI JIRANI WANAPIGA HATUA MBILI MBELE ZA MAENDELEO, SISI WABONGO TUNAPIGA HATUA TATU NYUMA.LAKINI NINA IMANI TUTAFIKA TU, KWANI NAONA SASA HATA MZEE WA "WAUYAGAUYAGA" SIMUONI TENA HAPA.

    ReplyDelete
  19. Michuzi acha uwoga wewe! Unaogopa Mama Sophia atakutumia TAKUKURU!Teh teh teh! Kama sio fisadi hawezi kukufanya chochote usiogope! Wacha wanablogu tujimwage kwa raha zetu as long as hatuchafui hali ya hewa!

    ReplyDelete
  20. Pole Michuzi na asante kwa kukemea, I feel your pain lakini sidhani mambo ni rahisi kama unavyoyaona. Mambo ya watanzania bwana yanavunja moyo sana lakini ni nchi yetu sasa utafanyeje? Maneno maneno yanakuwa ni mengi kuliko actions, watu ni vijiweni majungu na kuharibiana. Watanzania sio watu wa kutakiana mema hata kama una mipangilio ya safari na maendeleo mengine huwezi mwambia mtu maanake atakuharibia. Kumbuka huu ujinga ulianza kwenye miaka ya themanini mwishoni, tisini na elfu mbili ndio ukakomaa kabisa kwa kuingia kwenye internet.
    Inawezekana pia kuwa part ya maendeleo kwa sababu tabia nyingine za waTZ utaziona kwa wamerekani. So we might be evolving going to a different stage.
    Utaona wanawake wa kitanzania hawawataki wanaume wao and vice versa. Kabilas kama za chaga na arusha zinakandiwa kwa meno chocolate, Udini, mzanzibar100%, Angalau tuna amani inakuwa ni maneno ya mdomoni tu.
    Saa nyingine inabidi kuwa na tabia za kizungu kujali yanayokuhusu, akili kichwani nini kinachokufaa na maisha yako. Lakini wewe Michuzi ndio kiungo muhimu kwahiyo linebeke lazima liendelezwe.

    ReplyDelete
  21. MICHUZI HIYO HOJA YAKO UMEIKOSEA NA INA-BORE NA HAIJAENDA SHULE, MAHALI POPOTE DUNIANI WATU WANAPASHWA KU-ACCOMODATE DIFFRENCES SI KILA KITU UNACHOTAKA WEWE NA MWINGINE ANAKITAKA, KUPINGANA NI KITU CHA KAWAIDA, TUNAENDA SHULE SI KUSOMA TU BALI KUELIMIKA, AMBAKO PIA SI LAZIMA UENDE SHULE KWANI UNAWEZA UKAELIMIKA KUPITIA KWA JAMII INAYOKUZUNGUKA, KUNA TOFAUTI YA KUSOMA NA KUELIMIKA, SASA WEWE UNATAKA KUUNGA MKONO YA SOPHIA SIMBA, KUTOWA RUSHWA ILI ASHINDE, NA HIYO NDO DEMOKRASIA, KAMA ULISIKILIZA MAJIBU YAKE YA MAHOJIANO NA MWANAKIJIJI THEN UTAJUWA NI MTU WA AINA GANI NA KWA NINI WATU WANAMKOSOWA, KWANI NYEYE NANI ASIKOSOLEWE, ANAKOSOLEWA JOJI BUSHI RAIS WA DUNIA NA RAIS WA KWANZA WA AMERIKA MWENYE DEGREE YA MBA NA AMEONGOZA FYONGO KIPINDI CHAKE CHOTE SEMBUSA SOPHIA SIMBA ANAPASHWA UELIMIKA JINSI YA KUISHI NA WATU, ELIMU YA DARASANI TU HAITOSHI MTU KUWA KIONGOZI WA UMMA CHARISMA PIA INATAKIWA, SI SAHIHI KWA MTU KAMA WAZIRI KUTOWA AINA ILE YA MAJIBU NA UKIANGALIA SANA HAKUJIBU MASWALI YOTE KAMA ALIVYOULIZWA NI JAZBA TUPU, AMESOMA LAKINI HAJAELIMIKA ANAPASHWA KUKUBALI TOFAUTI ZA WATU BILA YA HIVYO ATAKUWA KIONGOZI GANI? MIMI SIKUBALIANI NA SOPHIA SIMBA WAKO HUYO KAMA KWELI TUNATAKA KUJENGA NCHI ILIYO NA USAWA, HAKI, UTAWALA BORA NA WA KUFUATA SHERIA NA UKWELI. KAMA MTU KAFANYA KOSA LA KIUTENDAJI NI LAZIMA ASEMWE NA AKUMBUSHWE, HATUTOFIKA TUKIENDELEA NA HUYU MWENZETU, MWISHO NARUDIA TENA USITEGEMEE HAPA DUNIANI KUWA KILA KITU KITAKUWA KAMA WEWE UNAVYOTAKA LAZIMA UKUBALI TOFAUTI TULIZONAZO LA SIVYO UTAMUONA KILA MTU ANAFANYA KINYUME NA WEWE UNAVYOTAKA. NA TUSITEGEMEE KUSIFIWA NA WATU WOTE KILA MTU ANAMTAZAMO WAKE NA TUNAPASHWA KUWASIKILIZA. WATU WAKISEMA MNASEMA ETI NDIVYO WALIVYOFUNDISHWA SEMINARI, HUO NI UDINI.

    ReplyDelete
  22. Siungi mkono tabia ya watu kukandia kila wanachokiona mbele yao lakini napinga hii kauli ya kwamba ni tabia ya watanzania tu.Hii tabia ipo kwa kila taifa, mfano nenda washintonpost.com, thesun.co.uk, bbc.co.uk/606.Katika hizo page fungua news yoyote ambayo ina mtazamo wa kutaka maoni ya wananchi alafu usome watu wanachokiandika.Kuna wengine wanatoa maoni hadi unahisi kama vile wamezaliwa uwanja wa fisi.
    Hata hao watani wa jadi wenyewe ingia kwenye forum za mashada utakuta wnaongea upuuzi tu saa nyingine.

    My point ni kwamba tusichukulie kuwa hii tabia ni ya wabongo wote, ni tabia ya baadhi ya watu ambao wao wameshindwa kutimiza ndoto zao kwa ajili ya ujinga au kushindwa kujipanga kwa hiyo wanapoona watu wengine wako katika kupiga hatua fulani kimaisha wanajaribu kuwakatisha tamaa sio kwa ajili ya wivu bali kwa ajili ya kuhisi "kama mimi nilishindwa yeye ataweza?". Watu kama hawa siku zote usiwasikilize, prove them wrong mwisho wa siku watajiona wajinga.

    Mungu Ibariki Tanzania.
    NAvy.

    ReplyDelete
  23. Kila mtu nakubaliana na wewe nakubaliana na wewe. Yaani inabore na kuonyesha jinsi watu wanavyoogopa kitu. Kwanini unaita watu senene yaani watu wakitoa mawazo yao lazima wakubaliane na wewe? Hapo umechanganya mambo mawili simba na mashaka.

    Huwezi ukajiweka public na kutegemea watu wote watakua na mawazo kama yako. Kama mtu hamtukani mtu sio lazima kukubaliana naye kama kutoa mawazo yake ni usenene sijui ina maana gani?

    Obama pamoja na kupata kura zote hizi na kuchagua watu wenye ujuzi kweli lakini bado hawawapitishi tu kama siye wabongo. Angetuletea hao watu bungeni kwetu nadhani wote wangepitishwa bila kuulizwa hata swali na bila kukosolewa kwa vile wamechaguliwa na so and so.

    Huyo Simba ni public servant na watu wana uhuru wakumchambua na kueleza mawazo yao na sioni kwanini unaona big deal watu wakidiscuss kuhusu yeye. Huyo mwingine simjui so I have nothing much to say about him.

    Uoga umetuzidi wabongo na mtu akitoa mawazo yake sio lazima akubaliane na kinachosemwa.

    Kama watu ni rafiki zako na hutaki watu waseme kitu chochote against them basi spare them by not posting them on this community blog.

    Na kama USENENE unaosema ni watu kutoa maoni yao why having a blog? Yaani wote tuwe yes sir, yes sir kama Cuba? Watu wanamawazo tofauti. Nilizania we are better than that? Nini maana ya demokrasia?

    Na ujue kuwa kuna watu wanafanya mambo mazuri kuendezesha ulimwengu na wanachojali ni kusaidia watu na kunawengine wanafanya kitu lakini wanategemea something in return na watu wanaoona mbele it is easy kuspot btn these people na kukosoa basi wengine wanaona ni kurudishana nyuma. Mfano kura za wabunge kila siku wanazozinunua kwa kuwapa watu mikate, sukari na kanga na hivyo vitu watu wasiseme wakiona sio halali?

    ReplyDelete
  24. USENENE??????
    ndo nini michuzi????
    weee unaleta utani na chakula yetu murua kwa kipi asa.
    USENENE NDO NINI FAFANUA,,,and why say usenene

    upesiiii

    ReplyDelete
  25. Huyu the so called Mwanakijiji kilichotuudhi ni kututukana hadharani. Hivi kweli wateja wako wa blog unawatukana kiasi hicho? Kwa kosa gani tulilomkosea? Kutoa maoni kwamba Bi. Simba alikuwa na kiburi, majigambo na lugha ya kukashfu?? Ukweli unabakia palepale lakini kwa nini huyu mwanakijiji atutukane? Kwa kosa lipi? Anatoa hotuba ya kubeza na kutukana wateja wa blog? It is crazy!! Mwambie kwamba next time hatutatembelea tena hilo blog lake. Atabaki analisoma yeye na mke wake. Kwanza yeye mwenyewe alishajilipua huko Marekani halafu leo anatuletea za kuleta hapa. Atuache na Bongo yetu. Viongozi wenye tabia mbaya kama Bi. Simba lazima tuwaseme hadharani. Huo ndio uhuru wa kutoa mawazo. Huwezi ukailazimisha jamii iwe na mtazamo wa aina moja. Yeye alitaka wote tunaochangia tumsifia B. Simba hata kama ameboa. Next time Michuzi kaa kimya usiingilie haya masuala. Maana na wewe umetaka kutuudhi kidogo lakini sio sana unapotuambia tusilete mambo ya Usenene. Tuachie huyu the called Mwanavillage tumshughulie.
    Mdau wa Oslo

    ReplyDelete
  26. Ndio Mzee Ndio Mzee Nyiiingi Humu. Hii Yote Ni Malezi Ya Zidumu Fikra Za Mwenyekiti..... Hata Kama Zinaumiza Zidumu Tu

    ReplyDelete
  27. HUU WAKATI WA UKWELI NA UWAZI KAMA MAMBO YAKO SIO WATU WANAKUCHANA TU.

    MICHUZI TAFADHALI USITULETEE UCCM HAPA.KAMA USHACHUKUA TAKIRIMA KWAAJIRI YA KUMSAFISHA HUYU MAMA HAPA SI MAHALA PAKE FUNGUENI BLOG YA CCM.

    ReplyDelete
  28. Michuzi preach what you do not and believe in.Wacha usenene.Kwenye blogu hii una ubaguzi wa hali ya juu.Unaweka mambo kwa jinsi unavyopenda wewe hivyo ukishabuliwa kuwa na ustahamilivu.Kwenye soka ndio usiseme una timu zako moja ya Dar ingawa unajiita shabiki wa Pan lakini ni uongo mtupu.Bwawa la maini ndio kabisa ikishinda basi kelele kiabo mkipewa kibano hatuoni comments zozote.Badilisha jina tujue ni blogu ya Bwawa la maini au anzisha la Bwawa la maini.Mfano hai CR7 Christiano Ronaldo roho yako ya usenene uliionyesha wazi.Mchezaji kachaguliwa na makocha dunia nzima na makapteni wa timu za taifa wewe unajifanya kuponda.Likikufika wewe ndio unajidai ku preach .Toa boriti kwenye jicho kalo kabla ya kuona kibanzi kwenye jicho la mwenzako.Nawasilisha.

    ReplyDelete
  29. Hiyo ndio maana ya jamii, fikra za watu zatofautiana na kila mtu ana haki ya kujieleza na kujieleza sio lazma aunge mkono hata kama sababu ni wivu au kadhalika.Hii sio kwa wabongo tu ila ndo binadamu alivyo.
    Kwa maoni yangu acha jamii ijirekebishe yenyewe bila sensa ya aina yoyote. Na wewe kama mwendeshaji ya blog nakusihi usichukue sides na kama unaogopa kitu au mtu nakushauri ufunge blog ila tu ujue kuwa utawanyima uhondo wengi pamoja na mimi.

    Malisa
    Bulgaria.

    ReplyDelete
  30. Anony wa 11:07,well said.
    Demokrasia jamani!!

    ReplyDelete
  31. Michuzi. Nilidhani kuwa hii blog ya jamii haimlindi mtu. Nashangaa unawalinda Sophia na Mashaka. Mtazamo wako wa usenene unamaanisha kwamba wewe ndio una miliki ukweli. I mean you own the truth and other people don't have the truth.

    Your role in this blog should be a moderator in the quest for truth.

    In real life, No one owns the truth. Instead people make an honest attempt to be truthful. Thats it. You are becoming a totalitarian now.

    Kuwa kemea eti kwakuwa wametoa mawazo yao dhidi ya Mashaka au Sophia unajipa wewe cheo cha anayejua yote kuhusu hao wawili na mengine. Unataka mawazo yanayo pendeza kwakutumia chujio la mlengo wako. Dhana hiyo ni potofu,ila inaonyesha jinsi ulivyo na upendeleo kwao. Kuna kitu kinakufanya uwaone wana merameta. Sikijui ila najiuliza.

    Kwa wanao toa maoni dhidi ya jambo au mtu mwingine yeyote kwenye blog hii, wafanye hivyo kwa ustaarabu bila kuchafua hali ya hewa. Hicho tu ndio kiwe kipimo.

    Kinyume cha hapo Kaka unachezea shilingi shimoni. Unatukwaza wengine hapa.


    Ahsante ni mimi

    Mpezi wa Michuzi Blog ninaejali mwelekeo wa blog hii ya jamii.

    ReplyDelete
  32. MICHUZI UNAWAPIGIA MBUZI GITA.NI KITU KINAITWA STRESS ZA MAISHA WABONGO INAWASUMBUA NA WIVU USIOKUWA NA KIPIMO.
    KAMA UNA FURAHA YA MAISHA YAKO MTU SIONI KWANINI JOHN MASHAKA HAKUKASILISHE KIASI CHA KUMSHAMBULIA KAMA ADUI AU MTU MWINGINE YEYOTE ALIKUWA KARIBU YAKO.
    SHIDA ULIKUWA NAYO KWENYE MAISHA YAKO AU MATATIZO YAKO HUWEZI KUYATATUA KWA KUWASHAMBULIA WATU WENGINE.

    ReplyDelete
  33. Shkamoo Mkuu wa wilaya

    Naona hii ishu imekuwa tabu, pole kaka, kwa tuliomkosoa Mh Simba hatukua na nia mbaya. Binafsi sikua namjua sana hadi wakati wa uchaguzi wa UWT na hasa baada ya mahojiano na Mwanakijiji. 90% ya walioskiliza na ku comment walimkosoa, hivo hata ujitahidi namna gani, haitakuwa rahisi kumsafisha.

    Kwa wale wanaofikiri mtu kumkosoa mtu ni kutokana na frustration, hayo ni maoni yenu, siwezi pinga, atleast umepata cha kujifariji kuhusu wakosoaji.

    Kaka Michuzi, kwa jinsi unavomtetea ndo watu wengi wanaenda kuzisikiliza zile podcast, na utake usitake, wengi wataendelea kukosoa. Kumsaidia, nenda kafanye nae tena mahojiano, arekebishe maneno yake, aaite jembe jembe ila aliite kwa heshima.

    Ushauri: Naomba utujulishe kwa kila post kama kukosoa inaruhusiwa. Hii itatupa uelewa mzuri kama tunaruhusiwa kueleza mawazo tofauti ua tucheke kila mfalme akicheka.

    Samahani kama nimekuchafulieni hewa onesmo (once more).

    ReplyDelete
  34. Nashangaa sana kwa Michuzi kuingilia kati suala hili huku akijenga hoja juu ya "usenene." Sikubaliani na Michuzi kwamba kila kitu watu hupinga. SIO KWELI hata kidogo.

    Ninachokubali ni kwamba kuna watu ni wabishi kwa kila hoja, na hilo sio tatizo la wabongo tu kama unavyosema, bali ni tatizo la kibinadamu hasa katika 'makutano' fulani (tuseme for colleagues). Narudia, sio wabongo tu, ni binadamu wote pahala popote.

    Michuzi, siungani na wewe kwamba kila mtu akileta zake za kuleta humu tupige makofi. Ni mara nyingi tu nimekutana na hoja mbali mbali za mwanakijiji kwenye electronic medias na anaungwa mkono. Au wewe hujawahi kuona hilo? Kwa nini kwanza usijiulize mantiki ya yeye kupingwa?

    Nina wasiwasi kwamba umewaza "unidirectionally" balozi. Ungekuna kichwa zaidi ungetambua kwamba suala aliloleta Mwanakijiji ni siasa tupu, ambayo wenge wetu tunajua maana yake (iwe imekusudiwa au matokeo) kisiasa.

    Usitulazimishe kupiga makofi kwenye kila kitu. Kila mtu ana uhuru wake, ilimradi asivunje sheria. Changamoto kwa wote (ukiwamo wewe) ni kwamba upime jambo la kuwaeleza watu na ukubali kukosolewa.

    Please declare your interest in this issue or person(s) Michuzi. Sio bure! Usitulazimishe kupiga makofi hata 'msibani.' Watu wana akili timamu, na kila aliyechangia amechangia kutokana na anavyoona yafaa, na inafaa, ilimradi havunji sheria ya nchi.

    ReplyDelete
  35. Pole sana mwanakijiji. Naona hatuwezi kukulaumu wewe bali yawezekana ikawa ni upeo wako wa kuchambua masuala ndiyo tatizo. Nina wasiwasi na kiwango chako cha elimu na uzoefu wako katika fani ya uandishi wa habari. Sikutegemea mwandishi wa habari aliyeelimika awe na ufinyu wa mawazo kama ulivyojikanyaga kwenye hotuba yako iliyojaa kukemea na kutukana. Nafananisha hotuba yako na zile za enzi za Nyerere wakati wa uhujumu uchumi. Mimi nadhani kwa hotuba kama uliyoitoa kwa mwandishi wa habari anayejua kazi yake asingethubutu hata kidogo. Hotuba iliyojaa mambo ya kisiasa ambayo utafikiri ni mmbunge au kiongozi fulani wa kitaifa anayekemea jambo fulani. Lakini kwa journalist anayeelewa kazi yake asingeliweza kufanya hivyo. Umeongelea mambo mengi sana ambayo hata Bi. Sophia hakuyasema na wala hata watoa hoja hawakuyasema na hata hayahusiani. Nadhani kwa muda mrefu sana ulikuwa na usongo wa kutoa speech ili wakuone cheche zako. Bahati mbaya speech umeitoa kwenye wrong forum. Nadhani unahitaji urudi shule ukajifunze “Analytical journalism” Uwezo wako wa conceptualize na ku-articulate ideas ni mbovu sana. Ulidakia vitu vilivyo nje kabisa ya topic. Lakini pia wewe ulipotoa sehemu ya watu kutoa maoni ulitegemea nini. Kuna positive na negative opinion to the subject under discussion. Kwa hiyo wewe ulitakiwa usikilize maoni yote halafu uchukue maoni hayo kama unataka kumsaidia Bi. Simba basi ungelimpelekea. Yale mazuri angeshukuru na yale mabaya basi angeliona jinsi ya kujirekebisha. Wewe ni referee na mchezaji, itawezekana kweli? Nadhani inabidi ukasome zaidi kuongeza upeo wako wa kuelewa mambo. That is the fact. Nina wasiwasi hata diploma ya journalism kama utakuwa nayo. Maana kwa hali hiyo! Mmmmmmmmmmmm
    Mdau

    ReplyDelete
  36. Kwa jina jingine huu ndio unaitwa UCHAWI..!! Maana yake ni kurudisha wengine nyuma kimaemdeleo. Hatutaki kukubali yanayoendelea tunataka tu-behave kama binadamu wa kale. Mzungu anaposema Binadamu wa kwanza katoka Afrika na alikuwa katika form ya Sokwe sisi tunafurahi kwamba we are the first ancestors..!! Maana yake ni kwamba sisi ni wanyama hatutaki kukubali ukweli na maendeleo tunataka tubaki hivi tulivyo. Yeye alikubali ndio maana kafika huko kote aliko akaangalia nyuma na akaona mtu mweusi ambaye ndio wa kwanza bado yuko vile vile anavaa majani ndio maana wanatuita "Africans Are Monkeys". Sasa badala ya sisi ku-appreciate changes and development around our society tunataka tum-back mtu down..!! Unategemea lini tutaendelea na kufika huko tuliko? Wewe unadhani kwa nini Marekani in early 1800s wali-suggest kurudisha baadhi ya wafungwa Africa(Liberia) baada ya kupitisha sheria ya kuwaacha huru wafungwa? Walidhani kwamba kama watawaacha wabaki watashindwa ku-assimilate na Western Culture ya Civilization na Maendeleo.
    Inaniuma sana ninavyoona Watanzania(WaAfrica) tunakosoana wenyewe kwa wenyewee...

    ReplyDelete
  37. TATIZO SIKUHIZI KILA MBONGO ANAJIDAI ANAJUA, LAKINI UKIANGALIA KIUNDANI WATU WANO FANYA USENENE, WENGI WANA IFRIORITY COMPLEX, YAANI WAMEISHIWA SASA WATAFANYAJE ILI WASIKIKE NDO WANAISHIA KUSEMA MABO YASIO FAA!

    ILA USIJALI NDUGU MASHAKA NADHANI UKIANGALIA WATU WANAO KUUNGA MKONO NI WENGI KULINGANISHA NA HAO SENENE!

    WASIKUTISHE KITU, NAJUA KWAMBA WATU WENYE USENENE MARANYINGI HAWANA MAENDELEO, NA WAMESHASHINDWA KWAHIYO WAKIONA MWENZAO ANAFANYA KITU CHA MAANA ROHO ZINA WAUMA ! KWAHIYO USIJALI NDUGU YANGU.

    ReplyDelete
  38. Hii blog ni ya CCM? Tuelezane tujue huku.

    Wote walioko bongo ndio wanaona ajabu mtu akikosolewa. Njooni huku muone morning meetings zinavyoendeshwa. Hamna cha boss wala nini kukosolewa na kuambiwa ukweli ni jambo la kawaida.

    Au mmekuwa Nixon "if the president does it, it's not illegal. ..."

    ReplyDelete
  39. Hapa kuna watu wa aina mbili. Wanaoishi bongo na wanaoishi nje ya bongo ndio maana mawazo yanatofautiana sana.

    Situkani mtu wala kumkejeli mtu lakini ukweli ni kuwa ukiwa bongo kila kitu ni swaaafi kabisa. Lakini ukishatoka ukaishi nchi nyingine (sio kuja na kutembea tu huku-you will never learn by doing that) ukiishi huku ndio utaona nini tofauti kati ya nchi yetu na nchi unayoishi.

    Watu wa bongo
    a) Wanaridhika kwa kitu kidogo sana.

    b) Njaa nyingi sana kwetu - Chakula tu na zawadi kidogo kila mtu anakupraise na kukupa kura unazotaka Ndio maana mmarekani yeyote nilivyokua mashuleni na sasa makazini ukimpa kitu chochote lazima akuulize "why you are giving this to me" Au "this is too much I cannot accept this". Wanajua na wanaona mbele hamna cha bure suni ya sasa hivi

    c) TZ hawajui kuwa unapokuwa mtumishi wa umma is a priveledge and not a right.

    d)TZ vingozi hawajui kuwa ukiwa mtumishi wa umma unatumikia watu na sio watu wanakutumikie wewe.

    e) Watu wa bongo wanaogopa sana kumkosoa kiongozi hata kama amefanya kosa. Yaani wanasujudu viongozi na kukubaliana nao kwa kila jambo. Halafu tunajidai tunajivunia amani yetu. Amani gani kama tulionayo moyoni ni uoga. Na wengine wanaogopa nikisema ukweli wataniendea Bagamoyo. SO SAD

    e)Watoto wake wakienda shule vizuri nawa jirani ambaye hawaendi shule sio tatizo lake. Kumbe nchi ikiwa na msomi mmoja haimake any difference. Ndio maana wahujumu wakijenga majumba wanaweka na magait makubwa kwa ajili ya guilty. Ili watu wasione jinsi wanavyoenjoy life wakati nyumba ya jirani inaanguka na yeye ni mtumishi wa nchi wala hilo halimuumizi roho yake.

    Tanzania tuna mengi mazuri ya kujivunia lakini pia kuna mabaya mengi sana na yanahitajika kukosolewa na kubadilishwa sana. Na watu wanaojaribu kutoa mawazo yao na kupanua wengine mawazo kwa mtanzania aliye bongo anaona ni whatever you call it (Usenene Ouch. Kuna watu watoto sana wanaochafua hali ya hewa lakini mawazo ya mtu yeyote ni muhimu katika kujenga nchi

    Kweli tutaendelea kama kila kitu lazima tukubaliane?

    Hao watu unaowatetea wanaweza kuwa wazuri kwako personally lakini kwenye macho ya watu labda sio kama wewe unavyowaona. Ukumbuke [kioo cha binadamu ni watu]

    Kama mwaandishi wa habari unatakiwa usiwe bias. Unaonyesha emotion feelings zako kwa watu fulani mbona wengine wakichambuliwa unakua mwepesi kuweka maoni yao bila kusikitika?

    Ina maana ni watu wawili tu humu kwenye blog yako ndio wamechambuliwa sana kiasi cha wewe kusikitisha hivyo na kuita watu SENENE?

    Ukumbuke humu kwenye blog yako mawazo yatatofautiana sana kwa vile hujui umri wao, elimu yao na kazi zao. Kuna watu wakubwa na pia kuna watu wasomi sana sana wamekuamini na kukubali na haipiti week bila kuingia kwenye blog yako. Kama mtu aliyesema hapo juu usichezee shilling kwenye shimo la choo. Wewe fanya kazi yako kama moderator. Najua wewe ni mpiga picha lakini najua watakua wanawapa lecture pia usiwe unaonyesha mawazo yako kuwa unasimama upande gani.

    ReplyDelete
  40. ~~~~~~~~~~USENENE~~~~~~~~~~~~:
    Mkuu wa wilaya nanihiiiii,, naomba uniruhusu kuchangia katika hii mada uliyoianzisha ya usenene ingawa mchango wangu wangu ni maoni binafsi kuhusu hawa wawili, Mashaka na Mh. Sophia Simba.

    Sina haja kumtetea yeyote kati yao, ila nataka kuutetea ukweli wa mambo.Simba simjui zaidi ya kusoma habari zake kwenye vyombo vya habari, na wala Mashaka sijawahi kumuona wala kuongea naye

    SOPHIA:
    Nikianza na Mh. Sophia Simba, kwa upande wangu sioni kosa lake, nadhani kosa au lawama nitambebeza Mwanakijiji ambaye inaonekana Journalism ability yake ni ndogo mno.

    Sidhani huyu ndugu yetu ana elimu ya kutosha katika uandishi wa habari.Hana ujuzi wa kuchambua mambo kwa kina na style yake ni boring

    Mh. Simba amethubutu na sioni kosa lake, isipokuwa kitu kimoja tu. Sophia Simba ameonyesha ujeuri na usomi wake. Hajatoa maelezo ni kiasi gani usomi wake utaisaidia jamii ya kitanzania.Na pia katika maelezo yake amezungumzia baadhi ya mambo ambayo hayana maana yoyote.

    MASHAKA:
    Kuhusu Mashaka, ndugu zangu, napenda kusema kwamba, huyu ni mtoto mdogo mno. Miaka kati ya 29-31 ni umri mdogo sioni hasa sababu ya kumfanisha na waziri Simba.

    Siyo kwamba wadau wanmchukia Mashaka, Hapana, hawamchukii wanachukia maendeleo yake.Majungu wanayomtupia ni majungu ya wivu

    Wivu unakuja pale wanapomuona mwenzao akirudi nyumbani kila mwaka na kufanya vitu vya maana ambavyo wameshindwa wao kuvifanya, ukizingatia kwamba baadhi ya hawa vijana wamekaa marekani uingereza na kwinigineko kwa zaidi ya miaka kumi bila kurudi nyumbani. Maisha waliyonayo huko waliko ni maisha ya kubahatisha.

    Kama mtanzania niliyeishi ughaibuni kwa muda mrefu, natambua vizuri hasira na jadhba vijana wetu walio nazo dhidi ya Mashaka.

    Wengi wetu maishaa tuliyonayo ni maisha ya kubahatisha na kuhenyeka na vikazi ovyo ovyo ambavyo vinafahamika kama ubeba boxi.

    Asilimia kubwa ya vijana wa kitanzania walio majuu, mara nyingi ni wabeba boxi na waosha makalio, kwa hiyo watu wanaposikia kwamba Mashaka kafanya kitu Fulani hapa na pale wanashikwa na wivu bila kufikiria kwamba hapo alipo kafikaje?

    Wengi hawawezi kuamini kijana wa kitanzania tena mtoto mdogo kama Mashaka anaweza kuhajiriwa kama investment banker, tena na shirika kubwa. Hizi kazi hata wazungu wenyewe wanazitafuta kwa muda mrefu na wasizipate kwa hiyo vijana wa kitanzania mara nyingi hawawezi kuamini kwamba mwenzao anawezekana afanye kazi nyeti kama hiyo. Hii ndio chimbuko la Usenene dhidi ya Mashaka.

    Nimeyasoma mahojiano yake bongo celebrity, daily news and kwingineko lakini nakubali kwamba huyu mtoto ni mnyenyekevu, mwenye huruma, adabu na mpenda nchi yake. Sioni kosa lake, na kama ulivyosema, wanaomchukia waseme wazi amewatendea nini? Na sidhani atakuwepo hata mmoja mwenye la kusema

    Nadhani wazungu ni watu makini sana, hawawezi kumuajiri mtu hivihivi tulivyo sisi watanzania.

    Ili upate kazi katika taasisi za kifedha, ni lazima upitie mchakato mkali sana, kwani ni kazi zenye ushindani mkubwa.

    kwa maana hiyo sina hofu kwamba Mashaka alionyesha umahiri mkubwa hadi wazungu wakamkubali na kumpa nafasi nyeti.

    Nakumbuka katika mjadala wa Afrika mashariki, ni Mashaka na Mokes Gama ndio vijana wa kitanzania walio simama kidete kuitetea nchi yetu ilhali hii mijitu imejikalia midomo wazi.

    Lyatonga
    Washington DC

    ReplyDelete
  41. allow me to contribute my thoughts here. there is a big contrast betwen the two.

    Sophia Simba is a proud arrogant B****ch while Mashaka seems to be very humble!

    How did this comparison come about anyway? Can I know?

    FUBU

    ReplyDelete
  42. TUKITAKA KUELEWA NAMNA YA KUFANYA KAZI KAMA WAANDISHI WA HABARI AU WATOA HABARI (REPORTERS) TUNAWEZA KUJISOMEA HAPA:


    JOURNALISM, ETHICS, AND STANDARDS

    http://en.wikipedia.org/wiki/Journalism_ethics_and_standards

    SOME OF THE POINTS DISCUSSED:

    1) Be cautious about identifying juvenile suspects or victims of sex crimes.

    2) Competing points of view are balanced and fairly characterized.

    Mdau

    ReplyDelete
  43. Saa Zingine "USENENE" unachangiwa na aitha Michuzi mwenye au mtoa hoja,

    We fikiri tu leo tuko 2009, unaanza kutoa Reference za mwaka Jana april, yaani hata katikati bado, waosha vinywa tutaacha kuponda kweli????!!!!!!!, Ulikua wapi muda wote huooooo?????!!!

    Au mtu antoa hoja ya kutafuta mchumba lakini masharti kibaaaaoooooooo, tutaacha kuponda kweli??

    Mimi kama muosha kinywa "original" ukweli hua inaniuma sana kuona hoja kama hizo,

    Na ushauri wangu ni kua watoa hoja wasiogope challenge, ni sehemu ya maisha,

    Wabillah Tawfiq!!!!!!!!

    ReplyDelete
  44. Tuwekane sawa tu, kama alivyoshauri mdau mmoja hapo juu kwamba michuzi declare interest.

    Nionavyo hii blog ni ya CCM. Ichunguze kwa makini, jumlisha tusi la michuzi kwa wabongo kwamba tuna usenene utagundua hii ni blog ya CCM. No operation Sangara humu!

    Ni hayo tu Balozi!

    ReplyDelete
  45. MICHUZI UMESOMA ANONY 17,2009 8:22 YOTE NILIOKUA NAYO KICHWANI KANITOLEA

    ReplyDelete
  46. Bwana michuzi mimi sielewi maana ya Usenene ila nazielewa pumba ninapoziona.
    Sasa kama unapenda hii blogu iwe ni mahala makini haina budi na wewe kuzitizama hizo pumba kabla ya kuzibandika.
    Tunachohitaji ni mtu atoe Hoja yenye nguvu, ili nguvu ya hoja ndio izungumze na sisi tutatoa hoja.
    Lakini ukibandika porojo kama hizo za mwana mashaka ambazo ni kama Insha basi tegemea majibu kama hayo.
    Watu wasitangaze majina yao kwa porojo ili wadau wasifiwe. Na ukiandika pumba inabidi uambiwe ni pumba ili ujitahidi.
    Asante;
    Mzawa

    ReplyDelete
  47. Hawa wabeba MABOX wanafikiri sisi tunaokaa BONGO hatuna exposure ya kutosha???? pole zenu, wakati mnaangaika na MABOX na KUWAOSHA vikongwe sisi tunajivinjari kwenye dunia. sasa hivi dunia ni kijiji kimoja. SHAURI YENU WABEBA MABOX

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...