Watoto pamoja na mizigo yao wakiwa wamepanda mkokoteni unaokokotwa na ng’ombe majira ya jioni wakitokea Gombani kwenda Macho manne mjini Pemba. Wananchi wengi wa Pemba wamekuwa wakitumia usafiri wa ng’ombe kusafirisha mizigo yao. Picha na mdau Anna Nkinda wa Maelezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Nadhani huo ndio usafiri unaotufaa bongo na sio kile kigali kinachotembea barabarani na baadae kinaruka angani. Hata yale mabasi yanayoua watu kila siku kutokana na carelessness ya madereva nayo naona bongo hayatufai. Kwa kutumia usafiri kama huu hata trafiki hawezi kupata rushwa kama inavyopigiwa kelele kila siku. Hata wale wafanyabiashara wa mafuta wanaotaka kujitajirisha kwa kutumia shida za watanzania hawataweza kutuletea za kuleta. This is the best!! Long live Anna Nkinda wa Maelezo kwa kutuhabarisha na kutukumbusha asili yetu.
    Mdau wa Oslo

    ReplyDelete
  2. Duh...enzi za babu Adamu hapo,at least no pollution,stress,depression,ukimwi n.k.

    ReplyDelete
  3. Tuige hiyo. Sana sana cha kuupgade ni baiskel au punda. Ukifanya research hapo utakuta watoto wenye asthma ni 1% tu compare na miji yenye magari mengi watoto wao 50% wana asthma na magonjwa mengine mengi tu na huduma zenyewe za matibabu ndio hivyo tena.

    ReplyDelete
  4. Mdau nashukuru sana umenikumbusha mbali sana, nilikuwa naendesha gari kama hiyo enzi za Mwaliimmmu. zinatusaidfia sana sisi watu za Pemba/ zanzibar kwa usafiri wa vijijini, zinatumika kama njia ya kujiajiri kwa mmiliki. Pia naomba kuweka Kiswahili sawa sawa, huo sio MKOKOTENI bali inaitwa GARI YA NGOMBE, ni gari kama zilivyo nyengine, engine yake ni ngombe na dereva ni watoto (kwa picha hii)
    Mdau zenj

    ReplyDelete
  5. Duuh!! Michu uminikumbusha hadithi ya zamani kule Pemba ya ng'ombe alikuwa akiitwa "Kipole".. Wapemba wengi wanafahamu hadithi ya Kipole.. (dRU)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...