ujenzi unaendelea
ujenzi umesimama

HAPA NI KATIKA MAENEO YA OYSTERBAY TOURE DRIVE. JENGO LA PICHA YA CHINI NI HILI LILILOVUNJWA MNAMO MWAKA 2006 KWA KILICHODAIWA KUKOSEKANA KWA KIBALI CHA MABADILIKO YA MANDHARI KWA KIMOMBO CHANGING OF VIEWS, NA UJENZI WAKE UMESIMAMA.

PICHA YA JENGO LA JUU NI BARABARA HIYO HIYO NA MAHALI HAPO HAPO KIASI CHA MITA300 AMBAPO CHUMA HICHO KINAJITOKEZA KIKIWA KINASHABIHIANA KILA KARIBU KITU NA CHUMA CHENZA KILICHO VUNJWA AWALI, NA UJENZI WAKE UNAENDELEA.

HII IMEKAAJE WADAU??

ASANTE

MDAU OYSTERBAY

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Hicho kilichovunjwa ni kwa sababu hakikukidhi viwango vya uchanganyaji wa zege, chuma na simenti. Ipo hatari kubwa ya jengo la namna hiyo kuanguka na kusababisha maafa makubwa hapo baadae kama ambavyo tumewahi kushuhudia siku za nyuma na kusababisha pia baadhi ya wataalamu wa ujenzi na wasimamizi wake wakifunguliwa mashtaka ya mauaji ya uzembe kazini

    ReplyDelete
  2. KWA KWELI INASHANGAZA NAMPONGEZA MLETA MADA TATIZO LA NCHI YETU NI RUSHWA KUMBUKA KUWA MAENEO YA OYSTERBAY,MASAKI,KUNA SHERIA INAYOSEMA KAMA SIKOSEI MWISHO NI GHOROFA MBILI JENGO LISIZIDI HAPO LAKINI MIMI NAONA HUYO ALIYEVUNJIWA KAONEWA,KUNA MAGHOLOFA MENGI SANA SASA YANAJENGWA HUKO SASA HAO WAMEPATA VIBALI TOFAUTI NA ALIYEVUNJIWA??????????

    ReplyDelete
  3. kama sheria inasema ghorofa mbili basi iyo sheria ni lazima ifuatwe na kila mtu. hiyo sheria kwakweli ni nzuri. hivi hao maofisa wa ardhi au miji wanakua wamelala wakati watu wanajenga hayo maghorofa. hawa maofisa ni vizuri washuulikiwe ama sivyo kesho utasikia watu wamejenga nyumba barabarani na hao maofisa wakajifanya hawaoni. sheria ni sheria na lazima zifuatwe. asante sana michuzi kwa kutuletea picha kama hizi.

    ReplyDelete
  4. haya yalimkumba hata mzee wangu alijenga nyumba arusha akaambiwa anaharaibu mazingira ikavunjwa baada ya mwaka akaja mtu mwingine akajenga palepale

    ReplyDelete
  5. hilo jengo lilivunjwa sio kwasababu ya zege... ni ubinafsi tu wa viongozi fulani fulani ambao mmoja alishabikia sana uvunjwaji wa nyumba hiyo kwasababu nyumba yake iko nyuma ya hilo gorofa aliona atakosa upepo wa baharini! na mwingine pia aliyekuwa katika kufanikisha hilo zowezi ni alikuwa kiongozi wa ngazi ya juu sana.. wote majumba yao yako nyuma ya hilo jengo
    wakadai ati sijui liko karibia sana na barabara sijui litaleta mmomonyoko wa arthi karibia na bahari.. yani wizi mtupu.... amemuwekea fitina mwenye gorofa na yeye mungu akamlipizia... sasa hivi wote wawili wako wapi? MALIPO NI HAPA HAPA DUNIANI!

    ReplyDelete
  6. HUYO WA KWANZA HAJAVUNJIWA KWASABABABU MAMLAKA ZINAZO HUSIKA HAZIJAMUONA MPAKA SASA WEE MLETA MADA VIPI UNAKUWA KAMA HUIJUI NCHI YETU BWANA? USIJE UKASHANAGAA ATAKAPOANZA KUFANYA FINISHING NDO WATASTUKA NA KUANZA KUIBOMOA BILA KUJALI RASILIMALI ZILZOKWISHAPOTEA HASA UKICHUKIULIA WAKATI MWINGINE NI PESA ZA KIGENI ZIMETUMIKA. LAZIMA JAMANI TUFIKE MAHALA TUKUBALIANE KWAMBA NCHI YETU MAMBO YANAYOFANYIKA NI KICHEKESHO DUNIA NZIMA ETI UJENZI UMEFIKIA MWISHO WATU TULIOWAWEKA MADARAKANI HAWAONI WANASTUKIA MWISHONI KABISA SIJUI KAMA TUTAFIKA. BINAFSI NATAKA NIACHE KABISA KUFUATILIA MAMBO YA KIBONGO MAANA YANANITIA HASIRA SANA KIASI CHA KUKOSA UZALENDO KABISA.

    ReplyDelete
  7. Kama maoni ya wenzangu hapo juu, jengo la kwanza alikuvunjwa kwa sababu ya kushindwa kufikia kiwango, nafikili kulikuwa na jambo lingine nyuma ya panzia.
    Kila klauz fm wanasema, nchi hii ni zaidi tuijuavyo. kuna mambo mengi yanafanyika, lakini pamoja na kuyasikia na kuyaona kwa macho. lengo na madhumuni yake uwa ni zaidi tujuavyo.

    ReplyDelete
  8. Kwanza cha muhimu ni kufahamu tofauti ya haya majengo mawili kabla ya kwenda kwenye sheria. Ujenzi unaoendelea ni Ghorofa 6 na Ujenzi uliosimama ni Ghorofa 8. Sina uhakika vizuri na sheria zilivyo sasa hivi, lakini wakati hilo ghorofa linavunjwa alikuwa na kibali cha ghorofa 4 nne tu, kama sheria ilivyokuwa inasema, lakini akajua kwa ka-utaratibu ketu cha rushwa, ataweza kujanga zaidi, na watampa vibali baadaye, bahati mbaya ikamkalia vibaya. Binafsi nilifurahi ilivyovunjwa kwasababu hawa wenzetu matajiri wa ki-asia hawaheshimu ofisi zetu za serikali kabisa. Lakini sasa mambo yanavyoendelea. sheria zimeendelea kubadilika kuruhusu maghorofa makubwa zaidi, kwahiyo sitashangaa kuona huyo anayejenga ana kibali na huyo aliyesimama akaendelea kujenga muda siyo mrefu. HII NDIYO NCHI YETU

    ReplyDelete
  9. sichokozi ila nauliza tu jee na jengo hili litaitwa kumbukumbu ya nyerere?

    ReplyDelete
  10. Sheria ni Msumeno!Kwani sheria inasema vipi kuhusu ujenzi karibu na fukwe za bahari?Kama ni umbali gani kutoka kingo za bahari basi umbali wa jengo hilo uhakikiwe mara moja.Kama sheria imevunjwa lazima jengo literemke chini.Kama sheria inasema ni jumba la ghorofa mbili ndilo lijengwe,na kama sheria imevunjwa basi jengo hilo lazima literemshwe chini.Hakuna mjadala katika hilo.Awe na kibali feki au hana jengo lazima liondoke mara moja.Watu binafsi wasiruhusiwe kujenga katika fukwe za bahari.Ni hatari kwa usalama wa nchi.Labda itokee ni Hoteli Kubwa Ya Kimataifa ndiyo inayokusudiwa kujengwa,na hata kwa hilo lazima Hoteli hizo zijengwe katika maeneo maalum yaliyotengwa kwa ajili ya madhumuni hayo,na bila shaka ulinzi wa kutosha utakuwa umewekwa katika maeneo hayo.Au kuna lingine?Kama kuna watendaji serikalini na Manispaa waliokula Rushwa lazima watimuliwe mara moja.Nchi yetu sasa iko vitani.Tusiwachekee hawa Mafisadi watatuharibia nchi.Serikali nzima itaonekana haifai kwasababu ya watu wachache.

    ReplyDelete
  11. Kubomolewa kwa hilo gorofa jingine na hilo la pili linajengwa ni matokeo ya ufisadi. Yawezekana huyo wa jengo la kwanza hakutoa kitu kidogo kwa viongozi wa manispaa na ndiyo maana jengo likabomolewa. Huyu wa pili anakula nao vizuri. Ndiyo bongo bwana.
    Mdau

    ReplyDelete
  12. HUKO NYUMA NILISHASEMA KUWA NINGELIFURAHI SIKU MOJA KABLA SIJAFA NIKIONA TANZANIA IKIONGOZWA NA MTU ANAYELINGANA KAMA IDD AMINI MAY BE ITASAIDIA KUNYOSHA RUSHWA NA WANAOVUNJA SHERIA.NCHI GANI HATA MIPANGO MIJI HAINA CHA KUCHEKESHA KIKWETE JUZI ANALALAMIKA JANGWANI WANAPAKI MALORI,SASA CITY HAO HAO WALIOWATOA KIDONGO CHEKUNDU NA KUWAPA ENEO LA JANGWANI WANASEMA WAONDOKE MAANA RAISI KASEMA JE WAENDE WAPI???? MMEWATAYARISHIA SEHEMU NYINGINE YA KWENDA?????????

    ReplyDelete
  13. HUKO NYUMA NILISHASEMA KUWA NINGELIFURAHI SIKU MOJA KABLA SIJAFA NIKIONA TANZANIA IKIONGOZWA NA MTU ANAYELINGANA KAMA IDD AMINI MAY BE ITASAIDIA KUNYOSHA RUSHWA NA WANAOVUNJA SHERIA.NCHI GANI HATA MIPANGO MIJI HAINA CHA KUCHEKESHA KIKWETE JUZI ANALALAMIKA JANGWANI WANAPAKI MALORI,SASA CITY HAO HAO WALIOWATOA KIDONGO CHEKUNDU NA KUWAPA ENEO LA JANGWANI WANASEMA WAONDOKE MAANA RAISI KASEMA JE WAENDE WAPI???? MMEWATAYARISHIA SEHEMU NYINGINE YA KWENDA?????????

    ReplyDelete
  14. yani wacha weee bongo na wabongo waliopo home na majuu popote pale nanao changia madaa katika blog hii na waosha vinywa na macho duu hii kali, yani sheria hizo ziliwekwa toka uhuru na bado tu wanasema tuzivuate mbona wabongo havai viatu vya kisikino kaka shayo na vibwenga bwenga shuruali na kuweka afro kila mmoja leo hii ananifanya mniger mniger mzungu mweusi..
    acheni hizo na pia menichekesha muosha kinywa na macho wa thursday feb 19 at 4.33 pm
    sijui jamaa kanywa kidogo au maisha yanamchanganya, wewe kakambia nani watu binafsi wasiruhusiwe kkujenga katiak fukwe za bahari eti KUTAHATARISHA USALAMA WA NCHI..Duu hii kali nakuambia nitapeleka kwenye sitcom ya u.s.a watu wajicheke, bado waafrica tuko nyumba
    unataka serikali ghani ije ijenge na watu wenginewe wa nje waje wajenge siyo wachukuwe uchumi wetu siyooo..

    sisi wenyewe peke yetu tukiwa na moyo mkujufu na imani na uchungu wa nchi yetu basi yote haya hayatotokea na mafisadi wataogopa kuyafanya siyo eti leo kuwalaumu wa asia sijui nani na nani nani kawapa vibali vya kuishi nchini na ni kawapa vibali vya kufanya kazi na business kama si sisi wenyewe, WAVUNJA NJI NA WAJENGA NCHI NI WANA NCHI WENYEWE, kaeni hivyo hivyo mpigiwe ngoma na kujifanya wastaarabu bongo tambarare, kushibisha vitambi vyenu na kupikiwa ubwana na ma pilau katika sherehe za watu kusaka kura zenu na mnawapa kura zenu kiulaini kwa tonge za pilau halafu nchi ikichukuliwa na mafisadi mnakuja juu mlikuwa wapi siku zote..
    bado mmelala siyo..

    michuzi weka comment hii ili nikupe kura yangu mwakana 2015 nasikia unataka kugombea kiti fulani wewe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...