rais wa Tanzania basketball federation richard kasesela majuzi alimtembelea mpiganaji athumani hamisi hospitalini johanesburg na kumkuta anaendelea vizuri na anatoa salamu kwa wadau wote na kuwataka wazidi kumuombea kwani sasa anaweza kunyanyua mikono yote miwili ila miguu bado kidogo na tayari ameshatoka ICU. mpiganaji athumani, ambaye ni mhariri wa picha wa gazeti la serikali la kiswahili la habarileo aliumia uti wa mgongo katika ajali ya gari sehemu za kibiti, mkoa wa pwani kiasi cha miezi mitatu iliyopita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mungu atakupigania Athumani...sisi huku nyumbani tunaendelea kukuombea utoke kabisa Hospitali mapema urudi nyumbani kuendelea na kazi..pole sana, ugua pole na tunakusubiri kwa hamu nyumbani!! We miss you Brother...come home soon!!

    ReplyDelete
  2. Pole sana mpiganaji Athuman, ila nataka kuuliza misupu mbona wapiganaji wengi wanapoumwa ama kupata ajali wanakwenda kutibiwa nje, ni utaratibu uliowekwa ama hii imekaaje !!!

    ReplyDelete
  3. Hii habari njema! Kweli Mungu yupo. Tunaendelea kukuombea kaka Athumani! GET WELL SOON!

    ReplyDelete
  4. wewe unayeuliza kama watu maarufu kwa nini wanaenda kutibiwa nje.ambua ni usichotambua ni kwamba,athumani ni mtu wa watu,,,amejitolea kwa jali na mali kusaidia watu na kujishusha kwa watu wengine.leo amepata ajali kwa nini wale aliowasaidia wasimchangie walau matibabu?na wewe jitoe kwa moyo mkunjufu uone kama watu watakutupa siku ukiwa na tatizo.it doent matter kama ni tajiri au mlalahoi.maarufu au sio maarufu.kule mbagala kuna mwananchi ameunguliwa na nyumba....maskini hohe hahe..hajulikana hata serikali za mitaa,unajua wananchi walichomfanyia?wamemchangia kumjengea nyumba nyingine,asiekua na pesa ametoa nguvu zake...na hao wananchi si matajiri wengi wao wamechanga elfu 3,au elfu tano lakini kwa upendo wao wamennusuru mwenzao kua homeless so kinachotakiwa ni kujitoa na kuishi vizuri na watu.huo ni uwekezaji tosha maishani

    ReplyDelete
  5. kiuno tena?
    usijali utapona tu mpenzi.

    Jehovah akuponye kwa upesi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...