Wanamuziki wa Mlimani Park Orchestra wakiwa na mratibu wao Juma Mbizo (kati juu, tai nyeupe) baada ya kuongea na waandidhi wa habari Dar.
Uongozi wa Shirika la Maendeleo la Dar (DDC) umesema utawainunulia bendi ya Mlimani Park vyombo vipya vya muziki na kuwakabidhi Machi 1, 2009 siku ambapo ndoa ya bendi hiyo na mmiliki huyo itapovunjwa rasmi.
Kiongozi wa bendi hiyo, Shaaban Dede, amesema hatua hiyo imefikwia baada ya mazungumzo marefu na uongozi wa DDC ambao umeamua kuwatema kwa kile kilichoonekana kuwa mzigo kwa shirika kutikana na ukosefu wa faida.
Wakati huo huo amesema wanamuziki wa iliyokuwa bendi ya muziki wa dansi ya DDC Mlimani Park (Sikinde Ngoma ya Ukae) hawatasambaratika, badala yake wataiendeleza bendi yao.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo) jana, kiongozi wa bendi hiyo Shaaban Dede alisema, bendi hiyo sasa itarejea kwenye jina lake la Mlimani Park iliyokuwa ikitumia mwaka 1978 ilipoanzishwa kabla ya kuchukuliwa na Shirika la Maendeleo Dar es Salaam (DDC).
Bendi hiyo ilichukuliwa na Shirika hilo mwaka 1982 na kuitwa DDC Mlimani Park. Hatua hiyo ya wanamuziki hao imekuja baada ya DDC kuelemewa na kushindwa kuigharamia bendi hiyo na hivyo kuamua kujitoa kuihudumia.
“Biashara yoyote inatangazwa ili iuzike, sasa sisi tulikuwa hatutangazwi tutauzika vipi ndiyo maana imekuwa kama mzigo,” alisema.
“Kwa hiyo sasa tuko wenyewe, hivyo burudani ipo palepale ya Wanasikinde, hatumtegemei mtu, ratiba yetu ya kila siku ipo palepale kila Jumapili tutapiga DDC Kariakoo,”alisema.
Alisema kwa sasa wanajipanga upya na licha ya kuwa na albam zaidi ya 20 wakiwa DDC, lakini wataanza upya na bendi yao ya Mlimani Park na kwamba wanajiandaa kuzindua albam yao ya Supu Umeitia Nazi.
“Mazoezi yetu tunafanya kama kawaida Mlimani Park Klabu na waliosema upinzani na Msondo umekwisha, tunawaambia hapana upo palepale na kama wao wanaitwa Msondo Ngoma basi sisi Mlimani Park,”alisema.
Sikinde ambayo wapenzi wake hupenda kuiita Nginde ni moja ya bendi kongwe za muziki wa dansi nchini, nyingine ni Msondo ambayo imepita katika majina mengi kama Nuta, Juwata, Ottu kwa vile ilikuwa ikimilikiwa na Jumuiya ya Wafanyakazi, kabla ya kutemwa, ambapo sasa wanamuziki hao wanajitegemea wenyewe wakiitwa Msondo Ngoma Music Band.
Kwa sasa Mlimani Park ipo chini ya Mratibu wake Juma Mbizo.
Ikiwa DDC Mlimani Park, ambao wanamuziki wote ndiyo wamiliki wa bendi hiyo. Wanamuziki wanaounda bendi hiyo ni Ally Jamwaka, Shaaban Dede, Hamisi Milambo, Hassan Rehani ‘Bitchuka’, Hassan Kunyata na Ramadhani Mapesa.
Wengine ni Abdallah Hemba, Mjusi Shemboza, Juma Choka, Mbaraka Ousmane na Thomas Mwamwingi. Wengine ni Juma Mkoba, Shaaban Mabuyu, Mwape Ndilima, Mikidadi Abdallah, Steven Maufi, Yusufu Benard, Yasini Rashidi, Karama Regessu, Mustafa Ngosha na Hassan Jeff.
KAZENI BOOT,MNAWEZA MSIWE NA WASIWASI TUPO NYUMA YENU,MNAHISTORIA YA MUZIKI WA TANZANIA TAFUTENI SASA SPONSORS KAMA TBL,VODACOM,NMB MUZIKI WENU UNAUZIKA MSIONGEZE MTU MNAPATA VYOMBO VIPYA NI VIZURI SASA KUJITEGEMEA TUNAWATAKIA KILA LA KHERI NAFIKIRI TUTAWAALIKA KAMPALA FUNGUENI TOVUTI YENU,MTASHINDA TUPO NYUMA YENU
ReplyDeleteMnajifanya nyie mafundi wa kupika supu imekuwaje tena mkatia sumu ya panya ambayo imewamaliza nyie wenyewe au ndo mlikuwa mnataka mpewe na hati za miradi yote ya DDC ? Poleni sana , msijidanganye kwamba eti hamna wasiwasi hiyo ndo salamu ya kwaheri kama mlishindwa kujiendesha mkiwa chini ya milki ( kula kulala ) iweje muweze mkiwa wenyewe wakati hamkuwa na maandalizi yoyote , yetu macho
ReplyDeletemlishaambiwa nyie ni mizigo mkabisha sasa kiko wapi?
Mizigo mizigo mizigo hiyooo aaahahaha!!!
ReplyDeleteMizigo mizigo mizigo hiyooo aaahahaha!!!
Mizigo mizigo mizigo hiyooo aaahahahaa!!!
Imekuwaje tena mafundi wa kupika supu mkaitia sumu ?
Bendi ya Mlimani Park sasa kuwa bendi inayo milikiwa na wanamuziki wenyewe ni hatua kubwa sana ya kimaendeleo na wala siyo ya kubezwa.Muziki wa Sikinde ni Mkubwa sana kwa viwango vya kimataifa.Mtaji mkubwa mnao tayari,jina kubwa mmeshalijenga ulimwenguni,albamu chungu nzima za huko nyuma leo ukizisikia utadhani zimetoka jikoni jana!Ninacho waomba tu kina Dedee na Bitchuka kama tulivyopata kuzungumza pamoja hapo DDC KARIAKOO siku ya tamasha lenu la kila jumapili,kwamba,imarisheni kikosi chenu cha kutafuta matangazo ya biashara,cha kutafuta mikataba mikubwa na ya uhakika na makampuni makubwa,kila mwanamuziki lazima awe na akaunti ya benki,kila mwanamuziki awekewe mpango wa kujenga nyumba yake ya kuishi yeye na wanawe,kila mwanamuziki awekewe bima,na kila mtunzi wa awali lazima apewe motisha yake japo kundi zima la sikinde hatimaye litachangia katika kufyatua recording ya mwisho nk.Katika yote msisahau kuwaenzi wanamuziki waanzilishi kama Michael Enock(sasa marehemu)kwa kuwakumbuka wanawe na familia yake kwa hali na mali,wazee walioilea sikinde kwa posho au shukrani ya aina yeyote.Mkumbuke kujiendeleza kimuziki msibakie hapohapo.Mfanye utaratibu wa kuwaalika wanamuziki Nyota kutoka DRC CONGO kuja kuimba nanyi katika baadhi ya matamasha yenu,itawasaidia sana katika kukuza vipaji vyenu na kujenga udugu na urafiki kimataifa.Mengine tutakumbushana huko mbeleni.Hongereni sana wana sikinde.Msisahau kufungua website yenu,italipa kimataifa.Nyie ni Bendi Kubwa ,acha kabisa!
ReplyDeletehuyu mustafa ngosha ndo yule john ngosha?wadau nisaidieni
ReplyDeleteKaribuni nginde ktk ulimwengu wa kujiajiri. Msondo waliwaambia mtoto hakui kwa baba, msione aibu kuomba ushauri kwa baba zenu!!! Sioni jina la Eddo Sanga yupo au amechungulia na kuanza?
ReplyDeleteWakuu kumradhi. Kwenye hayo majina yaliyotajwa kuwa ndio kikosi cha Nginde kwa sasa mbona sioni jina la Husein Jumbe? au bado yuko Msondo?. Kumbukumbu yangu inaniambia kuwa kuna wakati alitoka Msondo akarudi nyumbani Mlimani Park.
ReplyDeleteMdau
Cardiff
JAMANI HICHO NDIO KIKOSI CHA SIKINDE, AU MACHO YANANIDANGANYA? PIA NAOMBA PICHA ZAIDI ZA WANA NGINDE
ReplyDeletesikinde ngoma ya ukaye!!!!!!
ReplyDeletemimi nawafagilia sana, na ninaipenda sikinde kwasbsbu wengi wao wana vipji na nitajaribu kuandaa mipango ili mje hapa AUSTRALIA kuja kufanya maonyesho kama wiki moja nadhani mtakuwa mmemeki sana, unajua sasa hivi mtandao umekuwa mkubwa sana tanzania na duniani hivyo mtaendelea tuu!!!!!
Mdau Australia
mnanionyesha njia ya kwetu, huku mnanisimanga kuwa sina changu tena,wala faida kwenu,Wimbo huo ulitakiwa uwemo kwenye albam ijayo ya sikinde, nyimbo za zamani zitairudisha sikinde kileleni.
ReplyDelete