hekaheka za amatus liyumba mahakama ya hakimu mkazi wa kisutu leo ambapo dhamana yake imefutwa na amerudishwa lupango hadi machi 10, 2009 kesi yake itaposikilizwa tena baada ya kushindwa masharti ya dhamana.

mambo ya video ndo yameanza wadau. kaeni mkao wa kula...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Kwa kweli ni fedheha sana, mtu kama ungeridhika na unachopata bila shaka hayo yasingetokea,, sasa hiyo ni moja pili ni ngoma aliyovuna kutoka kwa vimwana mbalimbali,, Pole sana ndugu yangu

    ReplyDelete
  2. Wakina Michuzi kwa kupamba bwana ah ich.Uyo ni Mwizi kama mwizi wa baiskeli Manzese,Ilitakiwa tuanze kumrushia MAWETU ah.

    ReplyDelete
  3. Daah! Bonge la aibu kwa jamaa! Pole zake kwa sana!

    ReplyDelete
  4. SINA UHAKIKA NA SWALA LA KUCHUKUWA VIDEO YA KESI YA MTU AMBAYE HAJAPATIKANA NA KOSA, HICHO KITENDO NI KINYUME NA SHERIA NA HAKI ZA MTU ZA KIMSINGI, JE AKISHINDA KESI HIZO VIDEO SI ZITAKUWA ZIMFUNJIA HAKI ZAKE ZA KIMSINGI, EBU WAULIZE WANASHERIA, NDO MAANA KWA WENZETU HUWA HAIRUHUSIWI KUPIGA PICHA NDANI YA MAHAKAMA WAKATI KESI INAENDELEA

    ReplyDelete
  5. Mamnbo si ndio haya bwana...inabidi sasa order itolewe, wale wote waliopewa red cars wayarudishe mara mmoja. Also mtototo wake aliehuku USA arudishe Lexus ubalozini.. watanzania tupepigwa kikwelikweli, yaani mimi nimeliza mika 15 ndo kwanza namalizia kulipia highlinder, hawa mabinti hawaamiliza miaka miwili wamesha pay off lexus 470 and kai hawafanyi. Nimemaliza kunukuhu machungu yangu

    ReplyDelete
  6. Inasikitisha, Lakini lazima adhabu kali itolewe, ili iwe fundisho kwa wengine. shillingi bilioni zote hizo bila huruma?, Liyumba kwa kweli alikua na roho mbaya saana, na adhabu yake lazima iwe mbaya.

    Lakini na wengine lazima watokee kwa hili, kama wakina Mahalu, etc.

    ReplyDelete
  7. WIZI MTUPU. STILL PICTURE OR MOVE PICTURE .WIZI MTUPU

    ReplyDelete
  8. UZURI WA TANZANIA NI KUWA KIWA KILA RAIA NI MSEMAJI WA SERIKALI, MWANASHERIA NA MWANDISHI WA HABARI! WATANZANIA HUPENDA KUJIPACHIKA MADARAKA YASIYO RASMI.

    ReplyDelete
  9. wewe 3:19 AM, Anonymous: Nani kasema picha zimepigwa mahakamani? Mbona OJ alikuwa anaonyeshwa nje ya mahakama? Unaongea kama vile huyu jamaa ndugu yako au kama vile na wewe una gari nyekundu

    ReplyDelete
  10. Yaani najiona kama niko home thanks kwa hii clip kaka michuzi

    OT- bongo jua watu wamekua weusi utazania wanigeria. Hao afande kulikoni?

    back to the topic. Huyu mtu ajue Payback ni hapa hapa duniani. Hebu ona anavyoingizwa kwenye karandinga nyuma billionaire mzima It is sad lakini ndio ukweli wenyewe. Mimi naona wamuachie tu. Hela kesha zila na kuzirudisha hatarudisha...si unajua bongo yetu...hapo tunazidi kuteketeza hela ya walipa kodi tu....

    ReplyDelete
  11. WATU MNAPENDA SANA KUSHABIKIA BILA KUJUA NINI KINAENDELEA. YAANI MTU NA AKILI ZAKO UNAAMINI KUWA OVER 200 BILLIONS ZIMEIBWA NA LIYUMBA NA KWEKA PEKE YAO AU KWAMBA TU HAO NI SCAPEGOATS? ACHENI USHABIKI WA KITOTO BE REASONABLE. TUNAKUWA WADAKU KAMA WANAWAKE KUMBE NI WANAUME NA AKILI ZETU. SUBIRINI BWM NAYE ATOKEE HAPO MANAKE YEYE NDO CHANZO.

    ReplyDelete
  12. Kuna mtu alisema jahanamu na pepo viko hapahapa duniani. Mheshimiwa ameishi peponi sana na sasa anaonja jahanamu lakini anayo nafasi ya kurejea peponi kwake. Anyway, hayo yake...Sasa kama video na (I hope na audio) zimeanza, tafadhali tuwekee kidogo kidogo zile za Simba na Yanga za kale kama vile "...wasikilizaji...anaunawa mpira na ni maguu kumi na mbili ya mtu mzima..." - hebu weka ile ya 6-0 (sita bila)...

    ReplyDelete
  13. kwa taarifa mdau hiyo sio karandinga. Siku hizi bongo kuna mabasi ya wafungwa wakati mwingine level seat kuliko hata daladala.

    ReplyDelete
  14. Hizopicha hazijapigwa mahakamani, si umeona jamani alipofika mlangoni mwa mahakama tu picha ikakatwa? kwa sababu Tz hairuhusiwi kurecord proceedings (mwenendo wa kesi) lakini nje ya mahakama unarecord tu.

    ReplyDelete
  15. jamani watanzania wenzangu kwa mtazamo wangu finyu ni kwamba Lyumba sio mwizi paka pale mahakama itapothibitisha hivyo na kuwe na ushahidi wa kutosha. pili watanzania jamani hamuoni kama hiki ni kiini macho, lyumba kusababishia serikarli hasara wakati yeye alikuwa na viongozi wake wa juu. kwa nini sio timu nzima ya BOT na iwe ni Kweka na Lyumba??? tujiulize watanzania. jamaa wanatolewa kafara.

    ReplyDelete
  16. Duh...nimejaribu kujiuliza huyu Liyumba ndio angekuwa Baba yangu sijui kipindi hiki ningekuwa najisikiaje..

    ReplyDelete
  17. hizi kesi za ufisadi saa nyingine zinashangaza. angalia wale wafanya biashara wanaitwa waizi wakati hawa kwenda kwenye hiyo benki na kuiba bali walipewa mikopo. hata kama walikua hawatakiwi kupata hiyo mikopo hatuwezi kusema kwamba waliiba. ukienda kisheria kosa lao ni kutolipa hiyo mikopo on time. watu kama hao mara nyingi inatakiwa benki ichukue mali zao kulipa iyo mikopo na wakishindwa wawapeleke kotini. hawa mafisadi wakiwa na mawakili wataalam na koti zikawa huru wanaweza kushinda hizo kesi zao. hizi kesi zao zifanywe haraka na kuisha kabla pesa zetu za kodi hazijaishia kulipa gharama za kuendesha kesi. washindi kwa hizi kesi watakua mawakili peke yao. hawa mawakili wasipotajirika kwa hizi kesi hawata tajirika tena. THE BALL IS WITH YOU LAWYERS. LET THE GAME BEGIN.

    ReplyDelete
  18. Unauliza ungejiskiaje angekuwa baba yako? Mtenda hutendwa. Ungemfasidi - ukachukua mali yote yeye akingali lupango ukaishia...

    ReplyDelete
  19. wee annon uaesema "ati bongo jua watu weusiii"

    wee ni rangi gani?ata ungekua na rangi ya JK wee rangi gani?

    athari/stress za maisha na ubaguzi zimekusonga uko kwa wabeba boxez.
    ndo nyie kina michael jackson.

    nyambafu...

    ReplyDelete
  20. clip inakata-kata kaa nanihinooo

    ila unajitaidi kip ze gd work bro

    ReplyDelete
  21. khaaaa!!! Watam-balali tu huyo muda si mrefu!!!!

    ReplyDelete
  22. ndugu yetu wamemuonea tu kwa sababu za wanawake lakini twins towels si zipo au akujenga?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...