Michuzi na Dada Jiang,poleni na shughuli.
nimeona niwaandikie kwani maswali niliyonao yanaweza tatuliwa vyema na mawazo ya wadau katika blog zenu.
nitashukuru sana mkinisaidia.
kuna utafiti mmoja wa kisayansi unafanyika hapa tanzania,kwa bahati nzuri na mimi nashiriki,nimekumbana na suala moja ambalo (halihusiani na utafiti) lakini katika hisia zangu nimeona ni tatizo hivyo napenda wadau tulifikirie wote.
amini usiamini kuna watoto kati ya umri wa miaka 7 mpaka 15 wameathirika na ukimwi na wanahudhuria mahospitalini kuchukua dawa lakini hawana taarifa kama ni waathirika na hawana elimu yoyote kuhusu ukimwi zaidi ya kusikia maredioni na kwenye TV tena kidogo mno.
je ndugu zangu, ni haki kweli kuendelea kuwaficha au ni bora waambiwe maana tukumbuke ni wanetu,wadogo zetu,na pia tusikatae michezo mingi tu hatarishi inaendelea huko mashuleni na mitaani.
naomba wadau tujadili hili swala.
akhsanteni na kazi njema.
Mdau VA
Just let them know the truth plus give them whole bunch of ushauri nasaha knaaa mean??
ReplyDeleteMachimu
Mdau VA, unaonyesha waziunakiuka maadili ya kazi zako za utafiti kwa kujadili kitu ambacho bado kiko katika utafiti. Kujadili afya za watu kwenye chombo kama hiki ni kudhalilisha haki za watu unaowafanyia utafiti. Kitendo cha kusema kwamba hiki ulichokiandika hapa hakiko katika utafiti ni uongo, kwa kuwa usingejua jambo kama hilo kama usingekuwa katika huo utafiti hata kama utafiti ulikuwa unahusu mambo mengineyo.
ReplyDeleteJaribu kuangalia kwamba hawa ni watoto na wataendelea kutokuja kwani wengi wao wameambukizwa kwa kuzaliwa nao kutoka kwa wazazi wao, au kwa kupewa na wazazi wao waliokuwa wagonjwa na wao wakiwa wanahudumia kwa kutokujua wanaumwa magonjwa ya kuambikiza, au wameupata huku wakijua wanaowahudumia ni wazazi wao na hakuna namna ya kuwaacha serikali au hospitali iwahudumie.
Fikiria kama fedha au misaada ya Bill clinton ya kutokomeza ukimwi au kutoa dawa za kinga kwa bei nafuu hapa TZ, ni nani angewahudumia hata hawa watoto kwa vidonge.
Ndugu yangu VA, haya mambo ya kutoa taarifa za watoto bila ridhaa yao au hospitali huska ni makosa kabisa.Rudi shule ujifunze ethics na client rights.
UMENICHANGANYA NA MADA YAKO HUJAFAFANUA KWAMBA WANAHUDHURIA HOSPITALI KUCHUKUA DAWA GANI NA KAMA WANACHUKUA DAWA YA KUONGEZA IDADI YA SIKU ZA KUISHI MAANA YAKE NI KWAMBA WANAJIFAHAMU NA KAMA HAWAJIFAHAMU NI VIZURI NI VIZURI KWA HAO WATOTO CHINI YA MIAKA13 WASIAMBIWE LAKINI WENGINE WANAWEZA KUAMBIWA BAADA YA KUFAHAMU LEVO YA UELEWA WAO ILI WAWEZE KUCHUKUA TAHADHARI NA MAZINGIRA YASIYOENDANA NA AFYA ZAO.
ReplyDeleteEBWANA DAH KWANZA UMENIGUSA SANA NA HIYO MADA YAKO HAPO KIFUPI NI HIVI HIZI NI ZAMA ZA UKWELI NA UWAZI KWA HIYO TUNAPASWA KUAMBIANA UKWELI KWA KILA KITU MI NAFIKIRI SI ZAMA ZA KUOGOPA KUMWAMBIA UKWELI NA KUMFUNDISHA JINSI YA KUJIKINGA NA HAYO MADHARA NAFIKIRI UMENIELEWA SINA ZAIDI MDAU NGATUNGA TMK.
ReplyDeletemie nathani ni fahari kama watoto wamefikia umri wa kuweza kutambua jambo ni vema wakataarifiwa, hasa kuhusu afya zao. NKOSI from South Africa alikuwa na 11yrs old( kama sijakosea) alipokufa na HIV/AIDS na alikuwa balozi mkubwa africa na dunia kwa ujumla katika kampeni za maradhi haya na aligusa wengi(including me!). Alitambua kwamba alikuwa ni muathirika ingawa sijui taratibu gani walizifanya kumtaarifu.
ReplyDeletehili tatizo kubwa sana mimi binafsi ndugu yangu ana binti wake miaka 14 ana tatizo hilo tulikaa nae kutaka kumuelezea huyu mtoto tumeshindwa na anaendelea kutumia dawa na hajui mpka leo ni tatizo kubwa sana ktk familia zetu na pia wapo wengi tu hawatumii dawa sijui mtu utaanzia wapi kuwafahamisha hawa watoto na kukaa kimya pia ni vibaya mie mwenyewe nachanganyikiwa >
ReplyDeleteMimi nafikili mdau hakufanya kosa kuuliza na kuomba maoni. inawezekana pia yupo katika tafiti ili kupata maoni ya watu juu ya suala hili.
ReplyDeletekwangu mimi jambo hili ni gumu na lina pande mbili yaani faida na hasara. kwa upande wa hasara ni kuwa watoto hao ni wadogo sana kiumri na awana uelewa wa kutosha juu ya wao wenyewe ama mambo yanayowazunguka. hivyo, kumuambia kuwa una HIV katika umri wa miaka 7 hadi 10 ni kumchanganya mtoto na kutomtendea haki. pili tunaweza kuharakisha vifo vyao, kwa kuwa katika umri wa namna hiyo, watoto awajui kujithaminisha, yaani kujua yeye ni nani, matokeo ya jambo hilo ni kuwa anaweza kujizuru kwa namna yoyote ile. pia hari ya kumfahamisha inaweza kumletea unyonge mkubwa sana mbele ya wenzie kwa kuwa katika umri huo, ajui siri hivyo anaweza kumwambia mtu yoyote yule, hata mwanafunzi mwenzie na hapo kama ilivyo kawaida ya watoto,wataanza kumtenga.yapo mengi ya kuelezea hapa ila kwa hayo machache yanatosha kuunga mkono hoja yangu.
Ila kwa watoto, kuanzia miaka 14 na kuendelea hawa wanaweza kuambiwa lakini kiutaalam sana na wataalam waliobobea. nasema hivi kwa sababu katika umri huo iwe kwa kijana wa kiume au wa kike ni raisi sana kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi. kwa hiyo ili kuzuia maambukizi mengine kwa watu wengine, basi ni heri kuwaambia, ingawa madhara ni kama yale niliyoyaeleza hapo juu.
kwa kweli jambohili linasikitisha. Ila la msingi mimi ninaona kwa watoto kuanzia miaka 10 na kuendelea wapewe ushauri nasaha na waelezwe hali zao. Kwani kuendelea kuwaficha ni kuzidisha tatizo la ukimwi, kwa maana kuna utafiti ulifanyika na kugundua katika mikoa fulani ya tanzania watoto hasa wa kike wanaanza ngono wakiwa na umri mdogo (9) sasa hamuoni kuendelea kuwaficha itakuwa balaa kwa watoto wenzao au hata kina Fataki?
ReplyDeletesera ya nchi inasema mtoto afikie umri wa miaka 16 ndio aelezwe hali ya uambukizi! huu ni unyanyapaa kwa sababu ufahamu na akili ya mtoto huwa kuanzia umri wa miaka saba anapoanza darasa la kwanza,na iwapo anafahamu akiumwa malaria na kuambiwa na dr kwanini asifahamu ukimwi wakati unafundishwa mashuleni? JAMII KWA UJUMLA BADO TUNA UNYANYAPAA,UKIMWI,LETS CHANGE!
ReplyDeleteMimi naona ni vyema kumtambulisha mtoto kuhusu kuathirika kwake akiwa na umri juu ya miaka 10. Hii ni kutokana na sababu mbili: kwanza watoto katika umri huu haswa wa kike wanaanza kupevuka na kuanzwa na matamaniyo ya kimapenzi hivyo basi kuna uwezekano wa kuanza kujamiiana na kusababisha maambukizo hayo kuenea bila ya wao kujua kuhusu kujamiiana kwa afya ili kuepusha maambukizo zaidi(sexual health). Pili, kwa umri huu watoto hawa watakuwa wamepevuka kiakili na watatafsiri kiakili kuhusu habari hii (They wont panic). Kuwaambia watoto wa miaka 7 kwamba wana ukimwi sio haki kwani wanaweza kuropoka kwa watoto wenzio au wanaweza automatically kujitenga wenyewe toka kwa wenzao kwa kufikilia kwamba wapo tofauti na wengine, au wanaweza fikilia kwamba watoto wengine wanajua kuhusu hali yake na kusababishwa kwa mtoto muadhirika kujitenga. Angalia hii link ina personal stories za watoto waishio na HIV: http://www.avert.org/ypstory.htm ama go to http://ukimwinasisi.blogspot.com/
ReplyDeletebongo bado hatutaki kuamini kuhusu huu ugonjwa. Tunazikawatu kila siku lakini kuongelea huu ugonjwa ni kama taboo.
ReplyDeleteWatu kuzungumza tu juu ya huu ugonjwa bongo ni kama unamwelezea mtoto mdogo ambaye hajui kitu mambo makubwa.
Mtu akiwa na cancer ataambiwa kwanini mtoto yeyote asiambiwe ukweli kama ana teminal illness?
DAH AFADHARI MDAU VA UMELETA HII ISHU. NAONA TUNAMGAWANYIKO MKUBWA SANA WA MAWAZO. MIMI NAFIKIRI WATOTO WOTE AMBAO WAMEATHIRIKA WANAPASWA WAFAHAMISHWE HALI ZAO. UKIMWI SIO HATARI HIVYO KAMA WANAJUMUIA MNAVYODHANI. UGONJWA KAMA KISUKARI NI HATARI KULIKO UKIMWI. SASA KWA BAHATI MBAYA UKIZAA MTOTO MWENYE KISUKARI UTAACHAKUMUAMBIA?. UKIACHAKUMUAMBIA NA KUMFUNZA JINSI YA KUFUATA MASHARTI UJUE WEWE NI MUUAJI HUSTAHILI KUSAMEHEWA. NI VYEMA KUMUELEZA MTOTO YANAYOMSIBU WAKATI AKIWA NA UMRI MDOGO KADRI IWEZEKANAVYO ILIAJUE KWAMBA SIO KOSA LAKE NA AMEZALIWA AKIWA NA BAHATI MBAYA. NAJUA KWAMBA WAKUBWA WANASUTWA NA NAFSI ZAO KISHA WANAHAMISHIA MATATIZO YAO KWA WATOTO. LABDA WADAU WENGINE HAMJA ZAA HII YA KUSEMA MTOTO KIWA NA UMRI WA MIAKA 7-10 ANAWEZA KUTENGWA NA WENZIE HIYO SIO KWELI INATEGEMEA NA UELEWA WA HIYO JAMII. PILI AKILI YA MTOTO WA MIAKA 13 INAFANYAKAZI ZAIDI KULIKO HATA HATA MTU MZIMA NA NDIO MAANA WAZAZI WENGI WASIO NA UFAHAMU WA WATOTO WANAPIGA SANA WATOTO WAKIWA KWENYE UMRI HUO. KATIKA UMRI HUO MDOGO MTOTO ANAWEZAKUVUMILIA TAABU NYINGI SANA BILA HATA KUFA. NAONA WENGI HAMLIJUI HILO. UKWELI TUMEUMBWA HIVYO. NARUDIA TENA VIRUSI VYA UKIMWI SIO UGONJWA NA UKIFUATA MASHARTI UNAISHI TUU KAMA KAWAIDA. MSIWAKOSEE HAKI WATOTO WAELEZENI HALI ZAO NA VILEVILE WAELEZWE SIO KOSA LAO. WATAHUDHUNIKA KUSIKIA LAKINI WAPENI MOYO NA NGUVU WATAISHI NA WATAKUA MSAADA KWA JAMII. MADHARA YA KUSUBIRI MPAKA WAFIKIE MIAKA 16 NI MAKUBWA ZAIDI NA NDIO MAANA WANAAMUA WAFE PAMOJA NA WENGI. NI HAYI TUU.
ReplyDeletekwa kweli umeongea jambo zuri sidhani huyo mtu aliyepost wa kwanza alifikiria vizuri kabla hajakupaka matope. TZ ni yetu na vizazi vijavyo ni muhimu katika maendeleo yetu kama taifa
ReplyDeleteSasa mimi nafikiri huko hospitali waunde idara ya counseling ambayo inaweza kuanza kuwafundisha hawa watoto hali halisi waliyonayo na pia kuwaelimisha jinsi ya kujitunza na kuishi bila kuendelea kusambaza virus. Kizazi hicho kitakua na shida kama hakitaelimishwa maana tunaweza kupoteza taifa lijalo kama hatujihadhari. Kama familia inashidwa kujieleza basi hosipitali wafanye sehemu yao
kwa kweli umeongea jambo zuri sidhani huyo mtu aliyepost wa kwanza alifikiria vizuri kabla hajakupaka matope. TZ ni yetu na vizazi vijavyo ni muhimu katika maendeleo yetu kama taifa
ReplyDeleteSasa mimi nafikiri huko hospitali waunde idara ya counseling ambayo inaweza kuanza kuwafundisha hawa watoto hali halisi waliyonayo na pia kuwaelimisha jinsi ya kujitunza na kuishi bila kuendelea kusambaza virus. Kizazi hicho kitakua na shida kama hakitaelimishwa maana tunaweza kupoteza taifa lijalo kama hatujihadhari. Kama familia inashidwa kujieleza basi hosipitali wafanye sehemu yao
Si kumjulisha tu kama ana ukimwi ndio muhimu,Bali kumjulisha yeye yuko radhi kuwa majaribio ya hizo dawa na hatari zake.
ReplyDeleteNyie mnamshabikia VA, mna matatizo vile vile. Huwezi mwambia mtoto wa miaka saba hadi kumi nne kwamba ana ukimwi na unaua ilihali wewe huna dawa za kumfanya aishi miaka ishirini zaidi. Ni sawa na kumwambia kwamba yeye ni marehemu lakini anatembea mzima. Sisi tulio nje ambao ni wazima kiafya bila huo ugonjwa ndio tunaona huu ugonjwa huku sio tishio tena kwa kuwa watu huku wanaweza ishi hata miaka ishirini zaidi toka wapate maambukizi. Kutokana na dawa wanazopewa na matibabu yao kuwa ya juu katika hospitali zao.
ReplyDeleteLakini tukumbuke jinsi amabvyo huu ugonjwa nyumbani unavyoua watu, na stigma za watu nyumbani za kutokupenda kupima kila mwaka, na tabia amabazo tumeziona za waty wengi kuambikiza wenziwe kwa makusudio. Tena wengi kwa kubaka vibinti vya shule za msingi na sekondari au kuvidanganya kwa fedha zao na chips na kuku.
Tumeona mpaka South Afrika Rais mtarajiwa alivyombaka binti na kuoga kwa maji ya moto kwa madai kwamba hawezi kuambukizwa ukimwi au kuambukiza ukimwi.
Unaweza waelimisha watu kama una dawa za kuwatibu.
Mwaka juzi Yale university ya Marekani ilikuwa inafanya utafiti wa ukimwi TZ kwa akina mama wajawazito, na ikasimamisha utafiti. Kwa kuwa walipendekeza kwa serikali na hospitali kwamba kila mgonjwa atakapokuwa akipimwa aelezwe kwamba damu yake itachukuliwa na kupimwa pia ukimwi, na pindi ikibanika anao basi atafahamishwa na kupewa nasaha aidha za kutoa mimba au kuzaa kwa njia ya upasuaji. Serikali ya TZ mwaka huo ilikata pendekezo hilo kwa kuwa walikuwa hawana dawa za kuwapa pindi itakapofahamika kwamba wana ukimwi, na pia iliogopa kwa kuwa watu wengi hasa akina mama wajawazito wasingependa tena kuja hospitalini kuzaaa kwa kuwa idadi kubwa ingekutwa na viusi na kufanya wengi wao kuanza kuogopa kwa kuhofia kwamba jumuiya itawajua kwamba wao ni waathirika.
Utafiti ulivunjwa kwa ethics principles za marekani kwama taasisi zao za utafiti lazima pia zipate haki ( consent) ya mtu anayepimwa na kumweleza matokeo. Kwao ilikuwa ni sawa kwani wanazo njia, fedha na dawa za kuwatinbu wagonjwa wao. Kwa TZ ya mwaka ule ilikuwa sio haki kuawaambia watu kwamba wameambukizwa ukimwi halafu kuwaacha bila msada wa fedha, dawa au ushauri. Ugonjwa huo ulikuwepo kuanzia miaka ya 1984 na leo hii bado dawa hakuna. TZ imeweza angalau kupata dawa miaka ya 2006 za kurefusha maisha ya waliombukizwa na ukimwi na bado ni mapema sana kuwaeleza hawa watoto kwamba wanaumwa ugonjwa usio na kinga na watafariki katika muda amabao sio mrefu.
Sisi tulio wazima tunatakiwa kujua kwamba sio haki kuwatendea lisilo la haki watu wanaostahili haki zao. Hawa ni watoto wape dawa zao na watajua muda wenyewe utakapofika na huenda wakakubaliana na hali halisi wakati huo. Jamii yetu ni tofauti kimaadili na nchi za Western hivyo huwezi sema ni sawa waambie katika umri huo mdogo. Asilimia kubwa ya watoto hawa wathirika ninaamini hawana wazazi kwani wazazi wao wameshafariki na kitendo cha kuwaongezea uchungu mwingine sio jambo la heshima.
Nawasilisha!!!!!!!!
paediatric counselling needed &paediatric trainings to health care providers
ReplyDelete