Mkutano wa Kwanza wa Wanajumuiya,
March 1st 2009,
Katika Ukumbi wa Safari,
Saa Kumi Jioni (4:00pm).
Uongozi wa Tanzania Houston Community unapenda kuwaharifu wanajumuiya wa Houston, Texas kwamba kutakuwa na mkutano wa kwanza kabisa wa jumuiya siku ya jumapili, 01/March/2009, Mkutano huu utafanyika katika ukumbi wa Safari uliopo 9651 Bissonnet, Houston , TX 77036 . Muda ni saa kumi jioni (4:00pm) ,
Uongozi utakutana tarehe 28 February 2009 kujalidi ajenda mbali mbali ambazo zitazungumziwa katika kikao cha kwanza. Hivyo basi uongozi wenu unakaribisha maoni na ushauri kutoka kwa wanajumuiya wote.
Uongozi unahaidi kuyatafakari na kuyachambua mapendekezo yote kutoka kwa wana jumuiya
Uongozi,
Tanzania Houston Community
Uongozi,
Tanzania Houston Community
------------------------------------------------------------------------
MISA YA WAFU
Ndugu Wanaumuiya,
Kutakuwa na misa ya kumuombea marehemu Mzee Sylvester Bashasha Jumapili (22/February/2009) saa kumi jioni(4:00pm) nyumbani kwa mfiwa Gerald Bashasha.
Anwani ni:
9001 Kempwood Dr #108,
Ndugu Wanaumuiya,
Kutakuwa na misa ya kumuombea marehemu Mzee Sylvester Bashasha Jumapili (22/February/2009) saa kumi jioni(4:00pm) nyumbani kwa mfiwa Gerald Bashasha.
Anwani ni:
9001 Kempwood Dr #108,
Houston,
TX,
77080
Simu ya mfiwa ni 713 932 6020
Simu ya mfiwa ni 713 932 6020


Way to go Houstonian...... Sio kelelekelele tuu
ReplyDeleteMtoaji wa tangazo la mkutano, nadhani ingekuwa sahihi kutumia neno 'unaahidi' badala ya hilo la 'unahaidi'; nadhani ni typing error ingawaje wakati fulani utakuta mtu alidhamiria kuandika hivyo! Wengine pia kimakosa huandika 'arusi' badala ya 'harusi', 'hahadi' badala ya 'ahadi' 'hamri' badala ya 'amri' nakadhalika; otherwise nawatakieni kila la kheri katika mkutano wenu huko unyamwezi, huku bongo yetu ni macho na masikio! - Ben
ReplyDeleteHengereni sana Watanzania wa Huston kwa kufanya mkutano pasipo kuhusisha uchama kama wale wa London na uCCM wao. Nawatakia kikao chema, tunategemea feedback kwa maadhimio ya kikao. Kila la kheri!
ReplyDeleteTunawatakia Kikao chema. Watanzania USA tunatakiwa kujumuika namna hii bila kubagua chama, dini wala jinsia. Mwaka umeshakwenda karibia mwezi wa tatu sasa hope states nyingine viongozi wa jumuia wanajiandaa kwa vikao vya namna hii. Mambo mengi yanahitaji umoja wetu kuanzia sherehe, misiba na mipangilio mingine ya maendeleo.
ReplyDeleteSamahani naomba nisifikiriwe vibaya kwanza naomba kama itawezekana jumuiya iwe na E-mail yake na sio ya kutumia ya Mwenyekiti ili iwape viongozi wengine uwezo wa kusoma, kwani kwa kutumia Email ya Mwenyekiti inaonekana kama ni jumuiya inamilikiwa na mwenye hiyo E-mail. Samahanini wanajumuiya kama nitakuwa nimekosea naomba msamaha na kama nitakuwa nimegusa panapo husika basi pafanyiwe kazi, Nawatakia mkutano mwema na wenye amani mungu awabariki AMIN.
ReplyDelete"YESU AKASEMA, NIFUATE MIMI, WAACHE WAFU WAZIKE WAFU WAO"- Mathayo: 8:22
ReplyDeleteMzawa