PENDO MAGALUDA AMETUTOKA
Tumepokea taarifa kutoka kwa Bwana Abel Magaluda kuwa mke wake mpenzi Mrs. Pendo Magaluda amefariki dunia katika hospitali ya Rochester, New York, tarehe 13 Februari 2009 saa mbili na nusu usiku.
Kutoa heshima za mwisho:
Rochester: Jumatatu (16 Februari 2009) - kutakuwa na utaratibu wa kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu Pendo Magaluda kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi jioni.
Mahali: Rochester Memorial Chapel 1210 Cover Road, Rochester Telephone: 585-797-3553
New York: Ubalozi wa Tanzania, New York utaendelea kuwapa taarifa lini na wapi heshima za mwisho zitatolewa kabla ya kusafirisha mwili Tanzania mara mipango ya kusafirisha itakapokamilika.
Michango
Michango ya hali na mali inaombwa ili kuweza kulipia gharama zifuatazo:
(1) tiketi ya kurejea nyumbani Tanzania, Mama Mlezi wa Marehemu (2) gharama za kusafirisha personal effects za Marehemu (3) gharama za funeral home kwa siku mbili hapa New York wakati wa kusubiri safari.
Unaweza kutuma Mchango wako kupitia
HSBC BANK routing
No:022000020.
ACCOUNT NO: 526410230 yenye jina la
MAGOBE MAGALUDA NA PENDO MAGALUDA.
Kwa taarifa zaidi unaweza kuwasiliana wasiliana na
Bwana Abel Magaluda (Mume wa Marehemu) simu namba 1 347 238 9250, pia wafuatao:
Mr. Amos Shindika TEL -1 203 300 4122 na
Mr. William Malecela TEL-1 914 664 1518.
Tunaomba tushirikiane na familia ya Bwana Abel Magaluda katika kipindi hiki kigumu. Tafadhali watangazie na Watanzania wengine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. JAMANI POLENI SANA, MUNGU AWAPENI NGUVU ZA KUHIMILI HALI HIYO. KUFIWA UGENINI NI JAMBO ZITO SANA HASA MASAFA MAREFU KIASI HICHO, POLENI TENA NA MUNGU AWAONGOZENI.

    ReplyDelete
  2. Pendo Ibambasi, kwaheli dada, kalale salama, nakumbuka tulikuwa wote pale chuo kikuu cha dar es salammu mwaka 1993 hadi 1996 bcomm accounting...

    ReplyDelete
  3. Pendo Ibambasi, kwaheli dada, kalale salama, nakumbuka tulikuwa wote pale chuo kikuu cha dar es salammu mwaka 1993 hadi 1996 bcomm accounting...

    ReplyDelete
  4. Mungu wangu kuna kitu sitaki kuamini, kama itawezekana mithupu tunaomba tuwekewe picha ya marehemu ili tuone kama ni mtu tunayemjua maana kuna jina limetajwa hapo "Pendo Ibambasi",kuna mdada tulisoma naye Zanaki A -lEVEL Miaka ya 1990-91 sisi tulikuwa KLF yeye EGM sasa hatuna uhakika kama ni yeye au la?
    mwenye uhakika atusaidie kwa hilo.

    ReplyDelete
  5. Jamani ni huyo huyo Pendo Ibambasi uliyesoma nae Zanaki. Ameacha watoto wadogo sana watatu. Inasikitisha kwa kweli. She was so so nice, so wise jamani. Nimemjua kipindi cha mwisho akiwa anaumwa. Tunamuomba Mungu awafariji wanae na Mume wake mpenzi. Pole saana Mr. Magaluda,umejitahidi sana kumuuguza mkeo. Lakini tunamshukuru Pendo amelala kwa amani, alijiandaa, safari yake ya mwisho imewadia. bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.

    ReplyDelete
  6. Pendo Magaluda ndiye Pendo Ibambasi.

    Asanteni sana kwa maombi na michango.

    ReplyDelete
  7. Pendo Ibambasi ndio Pendo Magaluda. Napenda kuungana na wenzangu kuwapa pole familia ya Magaluda na Ibambasi kwa msiba huu mkubwa na wa kusikitisha sana. Mungu awape nguvu katika kipindi hiki cha machungu,haswa watoto,mume,mama,na wadogo zake.Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.


    Kwa wanaotaka kuwafariji ndugu jamaa na marafiki kwa hapa Dar es salaam msiba upo nyumbani kwakwe Bunju Basihaya,karibu na shule ya Ununio.

    ReplyDelete
  8. Samahani jamani naomba kuuliza ni yule Pendo wa National Board of Accountant and Auditors-NBAA naomba nieleweshwe vizuri

    ReplyDelete
  9. Ndo yule Pendo wa NBAA!Ametutoka MUNGU amlaze mahali pema peponi!Kweli amekwenda tukiwa bado tunamhitaji!
    REST IN PEACE PENDO IBAMBASI MAGALUDA!

    ReplyDelete
  10. Ndiyo, ni yule Pendo Ibambasi Magaluda wa NBAA. Asanteni sana kwa ushirikiano wenu.

    ReplyDelete
  11. Ni yule dada Pendo wa NBAA

    ReplyDelete
  12. Dada Pendo alikuwa mwanamke mchapa kazi na amekuwa mfano bora kwa kina dada wengi tunaomfahamu...Basi tuendelee tu kuiga mfano wake na siku moja tutaonana naye mbinguni. Asanteni sana.

    ReplyDelete
  13. Tunaomba walau picha yake jamani walau turudishe kumbukumbu nyuma ya Zanaki , pia tunaomba tujulishwe utaratibu wa mazishi na updates zote kwa sisi tuliopo bongo tuwawakilishe walio ughaibuni ktk kumsindikiza mwenzetu

    ReplyDelete
  14. Kutakuwa na kikao cha marafiki wa marehemu pale Nyumba ya Sanaa leo tarehe jtano 18/02/2009 kuanzia saa 12 jioni kwa wale mlio Dar mkiweza mnakaribishwa sana.

    ReplyDelete
  15. Shukurani nyingi kwa ubalozi wa NY, Mama Rose Migiro na dada yetu Rose Mkapa kwa ushirikiano wenu na Upendo wenu mlio-onyesha kwa dada yetu Pendo Magaluda Ibambasi.
    Asanteni sana na Mungu awazidishie Baraka zake.

    ReplyDelete
  16. Namkumbuka Pendo alivyokuwa na upendo, huruma, busara na rafiki wa kweli tangu tukiwa Ashira miaka ya 1985, Zanaki na UDSM nikiwa nimemtangulia mwaka mmoja. Alikuwa ni mdogo wangu, ndugu na rafiki. Alimcha Mwenyezi Mungu na kumtumaini hata nyakati za mwisho alipokuwa na maumivu makali. REST IN PEACE PENDO!

    ReplyDelete
  17. Pole kwa mume,watoto,wazazi ndugu jamaa na marafiki wa marehemu Pendo.Naomba Mungu awafariji wakati huu mgumu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...