NINI MAANA HALISI YA TUZO KWA MWANASOKA BORA WA CAF??

MAMBO VIPI KAKA MISUPUNina swali la kizushi kwa wapenzi wenzangu wa SOKAKama Tuzo ya Mwanasoka Bora wa mwaka Africa inayotolewa na CAF inawalenga wanaolisakata Soka Kabumbu hapa barani Africa..
Je ADEBAYOR wa Arsenal alistahili hio Tuzo..?
Na je kama Haiwalengi wa hapa Africa tu..Je, Christian Ronaldo angekuwa anaichezea Simba Sports Club angeweza kuwa na Vigezo vya Kupata Hio tuzo..?
Mdau
KaKa BijO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Viongozi wa hio CAF hamna kitu
    Mdau Bijo hapo zawadi inawalenga waafrica tu hata ukiwa unasakata soka mwezini ila kama mwafrika basi unastahili kupata hio tuzo kulingana na kiwango
    Mdau USA

    ReplyDelete
  2. huo ni wizi mtupu!!!!sababu mimi ni mdau wa arsenal tena damu kabisa ila nimesikitishwa sana labda hao CAF wana vigezo vingine ambavyo sisi hatuvijui kwanza huyu jamaa sasa hv anatukera sana pale arsenal!!!!!bora hata ingekuwa aliachiwa tu akaondoka mwaka jana alipokuwa akitaka kwenda AC millan!!!naihi CAF labda imeshikwa na watu wa togo au west africa!!!mbona wapo watu kama kina Etoi,mama dou niang,eboe,nk wakali kuliko hata huyu adebayor!!!!nadhani kuna ufisadi kwenye shirikisho la soka africa!!!na kwa hali hii soka la afrika litaendelea kudumaa!!!!!!!!!!inauma sana masela!!!sababu wenzetu Ulaya mtu akipewa uchezaji bora yaani huwa tunaona kabisa kwamba ana kiwango kweli na anakuwa amestahili tuzo hiyo ila kwa afrika ni wizi mtupu!!!!

    ReplyDelete
  3. Mdau bijo
    Wewe kama mpenzi wa soka kweli hilo
    Sio swali la kuuliza kabisa .hio ni tuzo inamlenga muafrica tu na sio kina ronaldo..

    ReplyDelete
  4. wewe usilete kampeni za man united hapa

    ReplyDelete
  5. wewe ndio bwana bijo WANTED au..?

    ReplyDelete
  6. Ronaldo kama ni muafrika atapewa hio tuzo kama waafrica tu
    Boniface pawasa

    ReplyDelete
  7. CAF meant for africans

    ReplyDelete
  8. Hio tuzo Adebayor hakustahili ilipaswa apewe Essien wa Chelsea au jamaa wa misri

    ReplyDelete
  9. Adebayor deserved the prize
    He's the best player
    fan of Arsenal

    ReplyDelete
  10. Hii mada niliona ikijadiliwa Supersport juzi Usiku

    ReplyDelete
  11. Wizi Mtupu.......!
    Mdau bijo ladba umekosea kuuliza swali lako na kwa mtazamo wangu nadhani ulitaka kujua kama kweli Adebayor alistahili hiyo tuzo au kwa kuwa anacheza Europaa huku.....ni mtazamo tuu wadau msijenge chuki.
    CAF nao vigezo vyao sijui ni vp,labda kwa kuwa alipachika mabao 30 ktk club yake msimu uliopita,au
    kwa kuwa anachezea chama kubwa arsenal.
    Ila vigezo ni pamoja na;
    1.Mafanikio ya club,
    2.Mafanikio ya timu ya Taifa,
    3.Mchango wako binafsi ktk timu,
    4.Maendeleo/kukua kisoka zaidi na sio kushuka kiwango,
    5.Nidhamu n.k

    Je unajua ni mara ngapi THIERY HENRY kakosa tuzo ya Ulaya na misimu hiyo alikuwa anang'aa ile mbaya??
    Alikuwa mzuri kwenye Club but timu ya Taifa mdebwedooo,
    sasa je Africa ni Wizi mtupu au ni sawa?

    ReplyDelete
  12. ZAWADI IMETOLEWA KUTOKANA NA PERFOMANCE YA SEASON ILIOISHA HILE NA KAMA UNAKUMBUKA ADEBAYOR ALIKUWA KWENYE FORM NZURI NA KUWEZA KUFUWANGIA ARSENAL NA TIMU YA TAIFA MAGOLI MENGI.KWAHIO WAKUBWA MSIJALI INAYOKUJA INAENDA DIRECT KWA ETOO MAANAKE YUKO ON FIRE NAYE HUKO SPIAN MSIMU HUU.

    ReplyDelete
  13. JAMAA MMESAHAU MAMBO YA ADEBAYOR MSIMU ULIOPITA MPAKA AC MILAN NA BARCELONA WAKATAKA KUMWAGA FEDHA KIBAO KWA AJILI YAKE?

    ReplyDelete
  14. kumbkeni hiyo tuzo sio kwaajili ya 2009 ni ya 2008 na mwaka jana alikuwa kwenye kiwango kwahiyo hapo hakuna upendeleo jamani. Msiwe kama jamaa wa darajani hapo uk

    ReplyDelete
  15. viongozi wa CAFA hawajui wanacho kifanya pamoja na makocha wa timu za taifa za Afrika,Adebayo hakuna alishofanya kwamwaka 2008,timu yake ya taifa ya tongo haikufanya vizuri kwenye mashindano ya bara la Afrika,timu ya Arsenal licha ya kufunga maboo 24 lakini timu haikuchuku kombe lolote msimu mzima,kuna jamaa wa misir Abu tirika yeye alisaidia timu yake kuchua kombe la afrika akasaidia klabu yake kuchukua kombe la chapion afrika akasaidia tena klabu yake kuchukua kombe la shililkisho alfu viongozi wanasema ndo ameshika nafasi ya pili,kweli tutaendelea kuwa bara la gizi milele kama viongozi wenyewe ndo hao

    ReplyDelete
  16. Kila bara lina vigezo vyake. CAF wanataka mchezaji wa Kiafrika, bila kuzingatia anachezea wapi soka duniani, aliyetoa mchango wa kueleweka katika klabu yake na timu ya taifa. Hawazingatii kwamba timu yake ni nzuri kiasi gani hata kumfanya naye aonekane mzuri. Ningekuwa napiga kura basi kura yangu ingeenda kwa ama Henry Joseph Shindika au Aboutrika. Kwa mfano Aboutrika anachezea timu ambayo haina wachezaji wenye majina makubwa kama Fabregas wala Nasri lakini muziki wake unaeleweka. Misri imechukua ubingwa wa Afrika kwa kutumia wachezaji wa ndani. Kwa upande wa Henry Joseph ndio hivyo Tanzania inatinga ndani ya fainali za CHAN.

    ReplyDelete
  17. Adebayor scored 24 goals in the English Premier League last season. He also scored four goals in three games for Togo in their World Cup qualifiers.

    Aboutrika,amesaidia timu yake ya tafa kuchukua kombe la bara la Afrika,kachuku kombe la vilabu bingwa Afrika na lashilikisho,kweli viongozi wa Afrika hamuazo!!!!!!!!!!!!!Ata binadamu ambaye hajakamilika anajua mchezajibora wa Afrika niAboutrika,Adebayor hajafanya chochote msimu ulio pita kashindwa kuisaidia timu ya taifa ya tongo,Arsenal msimu uliopita haikuchukua kombe lolote!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  18. WADAU,sijui hao CAF wanatangaza mshindi kwa kuteua au kwa upigwaji wa kura.lakini kwa bara la Ulaya mshindi anapatikana kwa kura.na kura hizo hupigwa na wale walio na taaluma na mchezo huo.kuanzia wachezaji,makocha,media na viongozi kadha wa kadha ktk club ama chama cha soka.sasa kama hivyo ndivyo na hao CAF wanavyofanya,sidhani kama ni wa kulaumiwa.
    na kama ni vinginevyo basi wanastahiri lawama.

    ReplyDelete
  19. Nasikitika kuona wengi wameshindwa kuelewa swali. Ukienda UEFA, wanapochagua mwanasoka bora Ulaya, hawaangalii rangi ya ngozi. ndio maana kina Weah waliweza kushinda miaka hiyo. Sasa CAF wao sijui kigezo chao. Mchezaji bora anacheza Ulaya...namna gani hii?? Kama wanataka kukuza kiwango cha mpira barani, njia watumiayo sasa ni ya kipumbavu. Mtu akienda kucheza Ulaya asiwekwe katika mashindano ya kutafuta mchezaji bora Afrika.

    mtoto

    ReplyDelete
  20. JAMAA ANA WAZO ZURI TU, KIFUPI VIONGOZI WANACHEMSHA, TUZO INATAKIWA KUPEWA MCHEZAJI YOYOTE YULE AWE MZUNGU, MHINDI MCHINA, MWAFRIKA LAKINI AWE ANACHEZEA MPIRA WAKE KATIKA BARA LA AFRIKA, IS A SIMPLE AS THAT, HUWEZI KUMPA TUZO MTU ANACHEZA ULAYA, KWANZA NI UNFAIR KUSHINDANISHA WATU KADHAA AMBAO WANACHEZA KATIKA STANRD TOFAUTI, NDO MAANA HATA NCHI ZA AMERIKA YA KUSINI HAZIMPI MCHEZAJI BORA WA MWAKA MCHEZA ALIYOKO ULAYA, HATA BNCHI MOJA MOJA HUWA HAZITOWI MCHEZA WA MWAKA TOKA NJE YA NCHI KWA SABABU ANATAKIWA AWE NCHINI AKICHEZA NA TIMU ZA NYUMBANI. ANGALIENI BRAZIL, ARGENTINA NA HATA NCHI ZA ULAYA MCHEZA AKIWA NJE YA NCHI HAUSUSHWA KATIKA TUZO ZA NDANI YA NCHI

    ReplyDelete
  21. Wadau wengi pamoja na muuliza swali, mnajibu kiupenzi. inawezekana pia amjui vigezo vinavyochukuliwa. kigezo kikubwa ni jinsi ulivyoisaidia nchi yako ya asili kisoka.na kigezo cha pia jinsi ulivyoisaidia klabu yako bila kujali kuwa ni klabu kutoka africa ama ulaya. pia jueni kuwa tunzo hii utolewa kwa mwaka mmoja nyuma.
    Hivyo adebayo ni kwa sababu ya msimu wa 2007/2008 Hakuna ubishi kuwa katika msimu huo mchezaji huyo alitisha kwenye klabu yake ya arsenal.
    Pia ni katika msimu huo aliiwezesha nchi yake kwa mara ya kwanza kucheza fainali za kombe, zitakazo fanyika mwakani uko SA. sasa kipi wadau mnachojiuliza? mbona ni mafanikio makubwa tu. kumbukeni kuwa mara ya kwanza senegal kufuzu kwa kombe la dunia, Rais wao alitangaza siku moja kuwa ya mapumziko kitaifa, yeye mwenyewe alikuwa katika ziara ya kitaifa nje ya nchi yake, lakini alisitisha na kurudi nyumbani. hivyo kufuzu kwa fainali ya kombe la dunia ni jambo kubwa na heshima kwa nchi.
    Mwacheni Adebayo afurahie ushindi wake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...