Wahandisi wa kampuni ya SEACOM Tanzania Limited wakiwa wanafunga kamba ili kuvuta waya ya mawasiliano (fbre optic cable) kutoka ndani ya meli iliyotia nanga bahari ya Hindi ambao utawekwa katika kituo chao kilichopo Kunduchi Jijini Dar
Wafanyakazi ya Kampuni ya SEACOM Tanzania Limited wakiwa wamebeba waya ya mawasiliano (fibre optic cable) kutoka ndani ya meli iliyotia nanga bahari ya Hindi ambao utawekwa katika kituo chao kilichopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam
Mafundi ujenzi wakijenga kituo cha waya ya mawasiliano ( Fibre Optic Cable) cha Kampuni ya SEACOM Tanzania Limited kilichopo Kunduchi Jijini Dar es Salaam. Kampuni hiyo itaanza kutoa huduma hiyo ya kuboresha network nchini mwezi wa sita mwaka huu.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Heloo Michuzi kwa kweli hii habari ni nzuri sana na hasa kwa maendeleo ya watanzania mana hapo sasa mradi ukikamilika gharama za simu na Internet zitapunguwa sana na hapo maendeleo live itakuwa mtandao sio Luxury tena Naomba uwe unatupa Udate zhuo Mradi

    ReplyDelete
  2. Great news for all
    Kili
    BG

    ReplyDelete
  3. Mimi ni mdau wa huku ukerewe, nimefiraishwa sana baada ya kusikia Fibre optic inatandazwa nchini.Hii ina maana internet itakuwa fast pia applications nyingi ambazo sasa zinapatikana kwa shida zitakuwepo murua tu!Huku nchi za nje hizo waya zina-replace miwaya ya simu ya zamani kwa hiyo ina maana bongo tutakuwa hatuko nyuma sana ki mawasiliano na watu wa nje.Uzuri wa fibre optic ni kuwa zenyewe si kama nyaya za kawaida ndani mwake, ila kuna kama kioo cha aina flani ,na nyaya za kawaida zinasafililsha mawasiliano kama electronics zenyewe zinasafilisha kama mwanga(light) hivyo speed inakuwa kali video una-download faster na mengi tu!Lakini ninavyojua `mafisadi`walivyoikalia hiyo nchi basi mafanikio yake yatakuwa hafifu,sababu hata wale ambao inabidi waelimishwe waelewa manufaa ya vitu kama hivyo hawatajua na watazibwa macho.Iwapo kutakuwa na technology kama hii,mambo mengi yanawezekana,sioni sababu ya sehemu nyingi za maofisi,zenye kutengeneza pesa za kutosha hazina hata `database`bado utakuta chumba kizima kimejaa mafaili(halafu eti mara kwa mara unaambiwa yameungua na moto!).Na ofisi nyingi utaabiwa kuna IT department lakini,watu ofisini hawana `information systems`yeyote kazi kuangalia e-mail na kuchat au kucheza karata.Na-hope labda itafika wakati viongozi watafikilia wanaanchi wao na kuleta maendeleo ya kweli,kwani technology kama hizo ni `powerful`ambazo inabidi zilete maendeleo ya kiasi fulani,iwapo technology itapewa ruhusa,wizi utapungua kwani kila kitu kitakuwa kwenye computer,udugu,udini,ukabila vitapungua sababu,technology itahitaji msomi sio kulipachika jitu tu!ambalo baadae linaua kampuni kwa ajili halijasoma na mengi yatapungua.
    ciao.mkeleketwa !!!

    ReplyDelete
  4. je nikitupa nanga ya jahazi langu hapo Kunduchi siwezi kuharibu hiyo 'optic cable' maana naona ka vile imetandazwa juu ya mchanga wa pwani na baharini ka vile inapita ktk ardhi iliyofunikwa na bahari, yaani optic cable haijachimbiwa.

    sije ikawa kama mambo ya Z'bar kukosa umeme toka Tanesco baada ya mvuvi mmoja kutuisha nanga juu ya cable ya umeme na kusababishwa cable ya umeme kuharibiwa.

    nawasilisha wadau
    Mvuvi wa Vina
    Bahari ya Hindi.

    ReplyDelete
  5. Mimi sina matumaini sana kuwa gharama za Internet zitapungua. Sababu hakuna vyombo vya kutetea haki za wateja (wa bidhaa au huduma zozote) katika nchi yetu. Mfano mzuri ni gharama za simu za mkononi. Serikali "INAOMBA" makampuni yapunguze gharama ili Wananchi wengi wamudu. Makampuni nayo yanasema kinachoongeza gharama kwa Wananchi ni kodi inayotozwa na Serikali. Wanatupiana mpira, Wananchi wanazidi kuumia, siku zinakwenda. Sioni kwa nini huduma ya Internet nayo isiwe hivyo, sababu fikra ni zile zile. Kinachobadilika ni technology tu.

    Wateja wa bidhaa na huduma mbalimbali wanatakiwa kuwa na mshikamano la sivyo huu uonevu hautakwisha. Hakuna mfanyabiashara aliye tayari kupunguza faida yake kwa hiari..!!

    ReplyDelete
  6. Mdau wa ukerewe kumbuka kampuni inayotandaza hizo kebo si ya serikali. hivyo....???
    Pili kebo za kuifanya hali ya Tanzania ibadilike ni maelfu ya kilometa hivyo.....??? pengine tuongelee Dar
    Tatu kama huo umeme utaendelea kuwa wa nadra na wa mgao hivyo...??? ni pasenti 23 tu ya watanzania ina huo umeme
    Nne bila kukasirikiana Tanzania bado iko kuzimu katika maswala ya uongozi na uchumi hivyo...??? nilimtumia kafulana ndugu yangu Tz hakukipata kilipotelea posta nasikitika sana.
    Jamaa mmoja kajitutumua kasafirisha kakontena kake Tz. kamefunguliwa Bandarini na alivyotumwa vimeibiwa! jamani sasa fisadi ni nani? mjukuu hadi babu. nchi iko wapi?
    Kili
    BG

    ReplyDelete
  7. Hapa watakao tibua mambo yote we subiri uone,ni TRA tu!Watakuwa wamesha anza kufanya makadirio ya VAT hata kabla Project yenyewe haija anza,utafikiri wao ndio walioleta mitambo!Vinginevyo,kama mradi huu hautaguswa na Kansa ya VAT basi kila nyumba Tanzania itakuwa na Internet!Kitu gani tena Mungu akupe?Hebu wekeni huo ujinga wenu pembeni kwanza,mradi uoneshe mafanikio ndio mtie pua zenu,Nuksi sana nyie!

    ReplyDelete
  8. wow......it sounds good:-)

    mdau netherlands

    ReplyDelete
  9. Kama waya wenyewe unatandikwa kwa stahili hizo za kuvuta kwa mikono kama picha hiyo ya pili inavyoonyesha mpaka uje ufike Kigoma itakuwa miaka mingi ijayo na teknolojia itakuwa imebadilika.

    Hiyo kampuni inayotandika huo waya imeniacha hoi na hii stahili yao ya kutumia watu kama punda wa KU-PULL WIRE.

    ReplyDelete
  10. sorry to bust everyones bubble lakini huu mradi ni wajanja wa nchi hii..gharama hazita shuka hata kidogo! tutaliwa kama tunavyoliwa kwenye mobile phones!! TCRA kwa nguvu za serikali inabidi walibane bunge kutunga sheria mpya itayoleta ushindani wa kweli nchini!

    ReplyDelete
  11. Tatizo ni kuwa,kwa sisi Tanzania bado hatuna wataalamu wa kutosha katika mambo ya Networking,nin ahofu kuwa wdau wakubwa hawatakuwa watanzania then hata hiyo faida haitapatikana katika kiwango chake,
    Maoni yangu ni kuwa serikali iangalie kwa sasa jinsi ya kupromote watu wake kusomea mambo ya netwoking katika level ya expert na sio technician.
    Kwa leo

    ReplyDelete
  12. bunge walete ushindani wa simu?
    wakubali kwanza ushindani wa vyama bila vikwazo vya hapa na pale

    ReplyDelete
  13. kaka mithupu unajua kuna mijitu inaongea kama chiriku! we nani kakwambia optic fibre ni waya? ujinga mtupu...lol

    ReplyDelete
  14. GREATEST NEWS OF THE YEAR IN TZ...!YANI HATA BAADHI YA NCHI TAJIRI HAWANA HIYO TECH.

    ReplyDelete
  15. INTERNET KUWA NA SPEED INATEGEMEA VITU VINGI SI SERVICE PROVIDER TU PIA NA UWEZO WA COMPUTER YAKO SHOULS AS WELL TAKEN INTO CONSIDERATION AS WELL AS SATTELITE POSITIN ABOVE TH COUNTRY

    ReplyDelete
  16. "wakiwa wamebeba waya wa mawasiliano-fibre optic cable"
    sasa wee annon apo juu wabishani?
    siii uo wameshika apo?
    jamani tusomee kuwa consultant wa mambo ayo apo sio mafundi mchundo dah adi ufike mkoa gani sijui sii miaka 10 mbele?hahahahaaaa
    kwa gharama za nchi hii mbona utachoka

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...