Bwana Jordan Gama kutoka chama cha Organic Products Tanzania {TOAM},akitoa maelezo kwa mgeni wakati wa Maonyesho.
Maonyesho Makubwa ya Chakula Duniani {IFE09}yanaendela kufanyika hapa London kwenye Ukumbi wa Excel. Madhumuni ya meonyesho hayo ni kuonyesha biadhaa mbalimbali zinazotengenezwa kwa bidhaa zinazotokana na chakula kutoka kwa wakulima na Makampuni mbalimbali duniani kwa lengo la kupata au kutanua soko la bidhaa hizo.
Maonyesho hayo yemakuwa yakifanyika kila baada ya Mwaka mmoja, IFE09 yatakayofata IFE11.
Ni sehemu pekee ambapo watengenezaji/wauzaji wa bidhaa hizo uweza kukutana uso kwa uso na wanunuzi wa kubwa kwa ajiri ya masoko ya jumla.
Tanzania ni Nchi pekee toka Afrika imekuwa ikishiriki maonyesho hayo kwa msimu wa pili sasa ambapo kKituo cha biashara cha Tanzania kilichopo hapa London, kimekuwa kikiandaa maonyesho hayo kwa upande wa Tanzania na kushirikiana na Makampuni kutoka Tanzania.
Mwaka huu 2009, Makampuni sita kutoka Tanzania yamefanikiwa kushiriki na kujitangaza kwenye soko la Kimataifa.
hongera sana kituo cha biashara London,kwa kweli sasa hivi kutangaza Organic products hapa UK ni wakati muafaka kwani hata serikali ya hapa ina kampeni kubwa ya kuwafanya watoto wa hapa UK kutumia vyakula mbadala ya JUNK FOODS kupunguza tatizo la unene(OBESSITY)mwanzo mgumu lakini tuifanye kazi hii kwa pamoja.
ReplyDelete