
SIKU YA WAJASILIAMALI
IJUMAA TAREHE 3 APRILI 2009
DIAMOND JUBILEE VIP HALL:2:30-11:30 JIONI
KAULI MBIU “PATA MAFANIKIO ENDELEVU”
WAZUNGUMZAJI
- MH. IDDI SIMBA, MWENYEKITI WA PRIDE TANZANIA
- PROF. M. NANGOLI KUTOKA UGANDA
- DR. HAMISI KIBOLA, MKURUGENZI MKUU, DHAMANA YA UWEKEZAJI TANZANIA
- BW. DAVID JAMES, MKURUGENZI MKUU, ACCESS BANK TANZANIA
- BW. RUGE MUTAHABA, MKURUGENZI, CLOUDS MEDIA GROUP NA WENGINE WENGI
Mjasiliamali ni mtu peyote aliye jasiri, mbunifu na mwenye uthubutu wa kuwekeza wazo, pesa au muda alionao katika shuguli itakayompatia tija na mafanikio
Katika kusherehekea siku ya wajasiliamali Tanzania tarehe 3 Aprili 2009, wafanyabiashara wadogo, wakati na wakubwa pamoja na wajasiliamali walioko makazini ambao kila siku wanabuni bidhaa na huduma kwa ajili ya kuendeleza makampuni ikiwa ni pamoja na wakurugenzi wakuu, mameneja masoko, maafisa rasilimali watu bila kusahau wadau wa sekta binafsi watakutana Diamond Jubilee VIP Hall kujadili kuhusu Mitaji, Mikopo, Mgogoro wa fedha duniani, Uwekezaji na Mafanikio katika biashara.
Zaidi ya kukutana na kubadilishana mawazo na wajasiliamali mbalimbali waliofanikiwa katika biashara zao, siku ya wajasiliamali pia itakukutanisha na makampuni, taasisi, mabenki na wadau wengine wanaotoa huduma kwa wajasiliamali ikiwa ni pamoja na mitaji, mikopo na huduma za uwekezaji. Baadhi ya Taasisi hizo ambazo zinafanya kazi na wajasiliamali pamoja na kuendesha programu za kuinua biashara ni pamoja na Tasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, Dhamana ya Uwekezaji Tanzania, Exim Bank, Easy Financy, Mamlaka ya Elimu Tanzania na wengine wengi
Siku ya wajasiliamali 2009 imeandaliwa na East Africa Speakers Bureau na itafunguliwa rasmi na waziri wa viwanda, biashara na masoko Mh. Mary Nagu. Shughuli Itaanza saa mbili na nusu mpaka saa kumi mna moja na nusu ikifuatiwa na cocktail party ambapo washiriki watafahamiana na kubadilishana business cards
Kushiriki nunua kadi yako maalum kwa Tsh 60,000/= kutoka ofisi za Clouds Fm ghorofa ya tano jengo la kitega uchumi, ofisi za meadows promotions zilizopo Haidery Plaza pamoja na Steers Restaurant Millenium Towers.Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0717 653544 au email


Hivi, ni wajasiliamali au 'wajasiriamali?'
ReplyDeleteKiinglio hiko je kimemfikiria mjasilia mali wa hali ya chini au kimembagua maana 60,000 mtaji tosha.
ReplyDeleteHongera kwa kutukumbusha tafsiri kamili ya Mjasiriamali kuwa 'ni mtu yeyote aliye jasiri, mbunifu na mwenye uthubutu wa kuwekeza wazo, pesa na muda alionao katika shughuli itakayompatia tija na mafanikio' katika hali isiyo na uhakika juu ya kuwa atafanikiwa au la.
ReplyDeleteYa mjasiri na mbunifu na mwenye uthubutu wa kuwekeza wazo na pesa na muda alionao katika shughuli itakayompatia tija na mafanikio Mdau uliyosema hayo maneno wala sio uongo kweli kila kichwa imempatia Sh 60,000 kugawana tosha hapo kila siku tutaanzisha viingilio vya hivyo. Mafanikio tosha kwakwe ndomana unaambiwa Mfanyabiashara ambaye Billionea au Millionea hawezi kukusaidia anajisaidia kwa manufaa yake lazima uwe makini unapofanya naye biashara. yeye yupo katika kuzidi kuongeza manufaa yake. Pazi.
ReplyDeleteyaani masponsors wote hao na bado unanitoza 60,000/- kuja kumsikiliza Iddi na Ruge?? Guys be serious acheni utandawizi! Wekeni ka10,000/- application fee na acheni refreshments na vitendea kazi viuzwe na wajasiriamali.
ReplyDeleteKiswahili sahihi ni Mjasiriamali ... (na sio MjasiLiamali)
ReplyDelete