Ndugu zetu watanzania,
Tunasikitika kuwataarifu kwamba Jumuia ya watanzania waishio Kansas City/MO & Kansas City/KS tumepatwa na msiba mzito wa kuondokewa na mtanzania mwenzetu Ndugu Ahabokile Malele, siku ya Jumamosi 03/21/2009.
Tumeunda kamati ambayo inashughulikia hili jambo. Tunaomba msaada wa hiari wa fedha na mawazo ili kuweza kumsafirisha ndugu yetu kwao Mbeya, Tanzania kwa mazishi.
Unaweza kuwasaliana na wanakamati kwa taarifa zaidi:-
1. Mohamed Fundikira (816) 739-5600
2. Fred Mwisomba (913) 999-1862
3. Eric Nyimbo (316) 214-4680
4. Deo Rutabana (816) 812-5495
Pia tumefungua account #355001747541; Jina: Ahabokile Malele Memorial Fund., kwenye Bank of America Ili kuharakisha ukusanyaji wa hii michango.
Gharama zote, mpaka mwili na msindikizaji (Mke) wake kufika Tanzania, ni kiasi kisichopungua US dollar 15,000.00
Maoni, na mawazo yenu wote yanakaribishwa. Tafadhali tunaomba mumtaarifu kila mtanzania ili kuweza kufanikisha lengo letu.
Ahsante
Evans Mambali
Katibu SERA
(816) 606 1604 & (816) 616 0275
e-mail: seraktb@hotmail.com
or katibu.sera@yahoo.com
hakuna mtu aliyetoa maoni tangu jana kwa sababu wengi wetu ni wanafiki, waoga, wajinga, wasiopenda kusema ukweli na mengine kama hayo. mwenyezimungu anisamehe kwani yeye tu ndiye mkamilifu iwapo nitakuwa nimekosea.
ReplyDeletekwa mara ya kwanza tanzia lilipotangazwa hapkuwa na dalili kwamba kunahitajika mchango, mimi nilidhani jamaa ameandaa/ameweka akiba ya safari yake ya mwisho duniani na pia nikadhani anazikwa huko usa na ndio maana watu wakapewa anuani ya nyumbani kwake wakatoe rambirambi kwa mjane.
Hivi nyie mnaobobea huko wakat kipato chenu hakiwatoshi wakati wa matatizo mna mpango gani? nawahusia mpitie upia mipango yenu ya maisha,kwani wengine umechoka sana kimaisha lakini unafuata mkubmo tu hata mnachofanya hakijulikani. wajanja wanaevaluate situation na hii sio kwa ajili ya huyu bwana bali mpo wengi unabeba boxi na kuishia kubugudhi wengine kwa matukio kama haya. kama nilivyoanza kusema nawaomba msamaha wote watakaochukia pamoja na mwenyezimungu, wale ambao mtafaidika tuombeani kheri mwenyezimungu achukue roho zetu sehemu nzuri na bila aibu, amin amin.