JK akikaribishwa na Balosi wetu Uingereza Mh. Mwanaidi Maajar uwanja wa ndege wa Heathrow asubuhi hii baada ya kuwasili jijini London tayari kwa mkutano maalumu kuhusu mtikisiko wa uchumi duniani ulioitishwa na waziri mkuu wa Uingereza Bw. Gordon Brown. JK ni mmoja wa marais wachache sana walioalikwa kwa ajili ya mkutano huo utaofanyika kwenye jengo la Lancaster House. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Eeh Wazee mbona jamaa (Mkwere) ameukamata kihuni mkono wa Mama Balozi..serious?

    ReplyDelete
  2. Mimi nawashangaa hawa akina browns na smiths - huu si mtikisiko wa uchumi wala cho chote bali ni "COWBOY CAPITALISM", na hilo hawataki kuligusia. ndio hayo unaona wametuletea ya mikashfa ya EPA, BOT, nk. na mingi tu iko njiani inakuja alimradi si kazi yetu ni kuiga!!!!!!

    ReplyDelete
  3. We anony 1,Je una wazazi?Au ndo wale waliorithi utamaduni maskini wa kupakaza kila wanacho ona hata kiwe chema?
    Sasa tuwe serious unavyotaka wewe..
    1.Upato wa mkono umegubika sawia kiganja cha Mkono wa huyu mama Balozi,Uhuni uko wapi? Au unahitaji kwenda specsavers?Usije ukajuta kama yule bibi anaye juta kwa nyimbo za Specs.
    2.Wote wamekutanisha mikono ya kulia kusabahiana,sijaona aliyetoa mkono mshazari.Au anony 1,una matatizo binafsi,ki itikadi,au Dini.Kumbuka Kristo yeye alibusu kabisa wenye dhambi kuashiria upendo na wokovu.
    3.Wote ni Viongozi safi,wenye ndoa zao.Itifaki Imezingatiwa makini na wazi.Haya uhuni uko wapi?
    4.Wenzio tunabadilisha Mtazamo wa fikra kuwa mtaguso chanya,Changamoto kuwa nafasi ya marekebisho,matatizo kuwa mafanikio.Huko unakobaki wewe tunasema BURIANI.

    ReplyDelete
  4. BABA,
    MBONA MAPEMA? YULE MTU MWENYE KAZI NGUMU KULIKO WOTE...BARRY OBAMA ATAKUWA OFISINI MPAKA SIKU MOJA KABLA.IWEJE BABA UHARAKISHE WIKI 2 KABLA?? AU UNAWAHI VITI KARIBU NA UBAMA UPATE ZILE TUNAITA KODAK MOMENT??

    MICHUZI...Usibanie hii

    Mdau Maryland

    ReplyDelete
  5. Kaka Michuzi watu kama Anony 1 usiwe unawapa nafasi ku comment maana kwa hilo wanaona they can easily and readly comment and get it published,hilo lina wapoteza zaidi kifikra.TUTAKULAUMU WEWE.Kila sheria (uwazi)ina mipaka yake,Uhuru una majukumu yake.Utamaduni wa kishetani kama wake lazima ufikie kikomo.Anataka kuainisha picha gani hapa hasa kwa familia za Viongozi hawa.Ukimkubali mjinga utajutia matunda yake hasa kwa watoto mnao zaa huko ulaya.
    KAPILA MATAWANA

    ReplyDelete
  6. aah ndio zake huyo halafu anatekenya tekenya kwa chati ..hehehe

    ReplyDelete
  7. Twafurahishwa na ujio wa JK, atakutana na wabongo hata for 5 mins?

    ReplyDelete
  8. ni miongoni mwa maraisi wachache aliyekaribishwa, lakini akapokewa na balozi wake tu bila kuwa na ujumbe mzito wa serikali ya uingereza. bongo akija beckam tu ,atapokewa na mizengo pinda.
    hapa patamu kwelikweli.

    ReplyDelete
  9. Mimi ni Mwanauchumi. Nilikuwa napenda kujua vipi wafanyabiashara wa nje watakuja kwa wingi Tanzania kapa wale waliokimbilia Dubai au Malaysia kama hatuna maji safi, barabara, umeme wa kutosha na mahakama madhubuti.

    Je, kweli hii mikutano inasaidia au tunapoteza fedha zetu bure?

    ReplyDelete
  10. Hey...!!!
    Mimi naona mkono hauna ubaya,ila kipozi cha Balozi kidogo kimekuja juu amekuwa "uingerezated mno" .Check mama Naibu katibu mkuu UN dahaa mavazi yake hadi raha....!!!.

    ReplyDelete
  11. "Dear Mr.Gordon Brown!Shikamoo Mzee!Tunajua mna matatizo makubwa sana ya kiuchumi,lakini sisi wenzenu tunakufa jamani,twafwaaaa!Kwanza nasikia mlipata "Mtikisiko"wa uchumi!Bahati nzuri kuta za nyumba hazikupata nyufa,yallaaaa!Baadaye kidogo kupitia Sky News tukasikia eti Uchumi wenu sijui "Uliparaganyika sijui",halafu tena muda haukupita mkapata "mkanganyiko wa mabenki yenu",yaani kwa kweli!Poleni sana,Mr.Brown.Wamenituma ndugu zenu wa Danganyika Republic nije niwape pole nyingi sana,wako nanyi katika maombolezo ya kipindi hichi kigumu sana duniani!Lakini pia wameniomba niwafikishie haka kaujumbe kafupi tu lakini muhimu sana!Eti wanakumbushia zile ahadi zenu mlizotoa huko zamani za "Kamsaaada",wanauliza Mbona Kimya kimezidi wajemeni?Nyinyi ni Wandugu wetu kabisa,si mnakumbuka mlituachiaga watoto wenu mlipokuwa mnatutawala wakati ule!Ile mitoto sasa ni mikubwa kweli na ina akili kama nyinyi baba zenu!Pamoja na hayo matatizo yenu ya 'kusambaratika"na "kuparaganyika"kwa uchumi wenu ,angalau bado mna ka nguvu kidogo wajemeni.Tunakumbushia kale "Kamsaaada"mklikotuahidi,wala hatukuwalizimsha,mlijisemeaga nyinyi wenyewe Haki ya Mungu!Basi kwa hayo machache nawakilisha machozi ya Afrika kuhusu huu 'Mparaganyiko"maana ni wa hatari!Ukijafika kwetu sijui itakuwaje!Si ndio "Tutasambaratika"kabisa wazee!And you know that,we refused to be "Communists"for your sake!and decided to ammend our "Arusha Declaration" which was thrown into Tabata Dumpo!Did you know that!Please,don't force us to retreat to Communism again!We already Capitalists but without "Capital",read my Lips Mr.Gordon Brown!With that,Shikamooni tena Wazee,Karibuni Afrika,Mbu zimepungua siku hizi,No Malaria like colonial days,so enjoy yourself!".Hii ni sehemu ya Kahotuba kalikoibiwa sehemu fulani kakiwa bado hakajafanyiwa "editing"!

    ReplyDelete
  12. HAHAH DUH WACHANGIAJI UMU WENGIE WANAAAKILI KAMA ZA KENGE HASWA (1)

    ReplyDelete
  13. anony 3:23 umenena.

    ReplyDelete
  14. mi naomba kuuliza, hivi viongozi wetu wakienda huko duniani huwa wanakaribishwa na nani hasa? ndo mana huwa hatuoneshwi jinsi wanavyopokelewa, au wakiwa ziarani huko majuu. siri ya haya yote wanayo waandishi wetu!!

    ReplyDelete
  15. hata mimi naunga mkono anonymous no 1 hafai.....mchuzi naomba uwe unachuja maoni

    mdau netherland

    ReplyDelete
  16. Huu mkutano anaoenda JK sijui kama utakuwa na tija kwetu.Kwa sababu utazungumzia jinsi mataifa makubwa yenye nguvu za kiuchumi kama U.S,UK,China,Japan,Italy,France,Russia,Germany na nyinginezo zitakavyoweza kujinasua na credit crunch crisis,itazungumzia mataifa tajiri tu na wala siyo mataifa omba omba kama letu.Hatuna kitu tutakachoenda kueleza huko zaidi ya kuwaambia na sisi tumeathirika kiuchumi kitu ambacho wanakifahamu kabla hata ya mkutano huo kufanyika kwa sababu ya utegemezi wetu.Cha msingi serikali yetu ingetumia muda huu kujipanga upya na kufanya kile ambacho kinawezekana sasa kama kuzingatia ukusanyaji wa kodi,kutengeneza barabara,kuimarisha huduma za afya na kuimarisha elimu kama ilivyopangwa kwenye bajeti yetu ya mwaka.Huo mkutano kwa nchi yetu sio suluhisho tungekazania mambo ya ndani kwanza ili tatizo la crunch likiisha itukute tumesogea hatua moja mbele.

    ReplyDelete
  17. Hivi sisi watu weusi kweli tunaelewa nini tunahitajia katika maisha kuna wakati waengereza walikuwa na msemo mmoja wanaupenda kuongela ni kuwa hata kama itatokwea siku moja wafrika wote wanaoishi katika bara la afika wachukuliwe na kupewa makazi ya liyo bora kwa muda wakati huo huo wazungu wahamie Afrika na kulijenga bara la afrika likimalizwa kujengwa warudishwe wafrika na wazungu warudi kwao basi walisema haitochuwa hata mwaka watarudi kuomba na kutaka wende wakaishi ulaya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...