JK akipokewa na Rais Ahmed Abdallah Sambi wa Umoja wa Visiwa vya Commoros alipowasili uwanja wa ndege wa Hayaya Prince Said Ibrahim International airport jijini Moroni leo kuhudhuria sherehe za ukombozi wa visiwa vya anjouan.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewaasa wanasiasa wa Comoro kuzingatia na kuheshimu makubaliano baina yao ili kulinda na kutunza amani na utulivu kwa manufaa ya wananchi na visiwa vyao.

Rais Kikwete ameyasema katika hotuba yake kwa wananchi wa Comoro  katika ukumbi wa Bunge ikiwa ni siku yake ya kwanza ya ziara ya kiserikali  katika visiwani vya Comoro.

“Wanasiasa wana dhamana ya kulinda wana Comoro, wanasiasa ndiyo chanzo, mkiamua nchi iwe na umoja, amani na utulivu itakua , mkiamua visiwepo nchi itakosa vyote” amesema Rais Kikwete na kuwaasa kuchagua umoja, amani na utulivu.

Amesema siku zote watu wa nje hulaumiwa, lakini nao hushirikiana na watu wa ndani na hivyo wanasiasa wakiacha kushirikiana na watu wa nje dhidi ya maslahi ya nchi amani na utulivu vitadumu.

“Mara nyingine tamaa za madaraka na mali husababisha kuvunjika kwa amani na wananchi ndiyo wahanga wa tama hizi za wanasiasa, heshimuni yale mnayokubaliana kufanya wakati wa mazungumzo, mkikiuka hizo taratibu mlizokubaliana mnaleta matatizo” Rais Kikwete ameongeza na kusema kuwa mkataba wa Fomboni, mkataba ambao umeweka taratibu za mapatano baina ya visiwa vya Comoro ni chanzo na njia nzuri ya maridhiano.

“ Mkataba wa Fomboni  umeweka misingi mizuri ya Demokrasia, kwa kubainisha kuwa viongozi watachaguliwa na wananchi, visiwa vyote vitatu vya Ngazidja, Anjouan na Moheli vina heshima moja na sawa na kwamba viongozi watabadilishana baina ya visiwa”. Amesema Rais Kikwete.

Mapema baada ya kuwasili Rais Kikwete amefanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Muungano wa Visiwa vya Comoro mheshimiwa Ahmed Abdallah Mohamed Sambi katika ikulu ya Comoro na kuelezea nia yao ya kuimarisha ushirikiano na mahusiano ya kibiashara na kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili.

Rais Kikwete ameahidi kufungua ubalozi mdogo visiwani Comoro haraka iwezekano ili kurahisisha mawasiliano  baina ya nchi na wananchi wake.

Katika ziara hii, Tanzania na Comoro zinategemea kutiliana saini mikataba mbalimbali ya kibiashara na kijamii.

Baadaye leo   (25.Machi, 09) Rais Kikwete na ujumbe wake wanatarajia kutembelea kisiwani Anjouan ambapo atapokea Tuzo kufuatia mchango wa Tanzania katika kuvikomboa visiwa vya Anjouan kutoka katika serikali ya Uasi ya Kanal Mohammed Bacar na baadaye kufungua tawi la Exim Bank.

Imetolewa na Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,

Moroni, Comoro

24. Machi, 09


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Well done Mr President for visiting the Comoros, we still have fresh memories that Tanzania contributed much to oust the dictator from Comoro. I would request His Excellency the President to apply the similar pratical swoop on the youngster self made president in Madagascar. We need Democracy in Africa not Demon cracy...Rajoelina should be forced out of the seat for the betterment of the Malagasy nation.
    mupozile@yahoo.com

    ReplyDelete
  2. video of Id amin..

    Ujumbe wake:
    tuwe tunawapenda viongozi..

    inachekesha saaaaaaaaaanaaaaa!
    http://video.google.com/videoplay?docid=4169600956573058582&hl=en

    ReplyDelete
  3. Wadau mnaosema JK anaenda Marekani tu kila siku si mnaona? Habagui nchi.

    ReplyDelete
  4. mambo mengine bwana.

    ReplyDelete
  5. Safi sana Mr President! Ngaridja onana maudu!

    sabs

    ReplyDelete
  6. Ningependa kujua....hii speech ilikua ni ya kingazidja au kifaransa?????maana hao wenzetu ni 'habari za'kwezi kwezi au 'bonjour'

    sab's

    ReplyDelete
  7. kwezi jk habari zaaa salimina

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...