mdau akizima moto. wakati hoteli za paradise resort na oceanic bay zikiwaka moto jana, huko bagamoyo hapa dar sehemu za mtoni kijichi nako kulikuwa na balaa la moto ambapo nyumba moja iliteketea kabisa na kuacha familia kadhaa zikiwa hazina pa kuishi. mtu mmoja alijeruhiwa na kukimbizwa hospitali.
gari la faya likiwa limekwama kwenye viambaza vya nyumba katika jitihada za kufikia nyumba inayowaka moto sehemu za mtoni kijichi. wana mipango miji wa dar mpoooooo????
baada ya kupata shida kupenda vichochoro kibao, hatimaye askari wa faya walifanikiwa sehemu ya tukio na kuzima majivu. hawa jamaa siku hizi wana spidi sana tatizo ni jinsi nyumba zetu zilivyojengwa - kwa lugha ingine jinsi nyumba zetu zilivyoachwa kujengwa kiholela. nadhani hili suala inabidi JK alivalie njuga yeye mwenyewe kama alivyofanyia kwenye kuruhusu walipa kodi kufaudu fukwe za bahari bila bugudha. ila siju atafanya kazi ngapi peke yake...







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Hawezi kufanyakazi peke yake kama vile anatunza familia, anatakiwa achague viongozi wanaoweza kufanyakazi yao kwa uadilifu. Kutoa uongozi kwa ushikaji ndio madhara yake, inakuwa vigumu kuwaondoa!!!

    ReplyDelete
  2. Bongo jamani kama tumelaaniwa, vitu hivi havitokei nchi yoyote!!

    ReplyDelete
  3. Bongo jamani kama tumelaaniwa, vitu hivi havitokei nchi yoyote!!

    ReplyDelete
  4. Wabongo tuna vichwa vya mbuzi. haya masuala ya mipango miji yamepigiwa kelele sana kwa miaka mingi lakini hakuna nayesikia wala kujali.
    Serikali za mitaa kama wangekuwa wabunifu, badala ya kusubiri maafisa wa mipango miji kutoka maofisini (wao wanafikiria ufisadi tu) wao wenyewe wangeweza kujiwekea nidhamu katika mitaa yao kuahakikisha wanajiwekea njia ya kupita magari ya kubeba wagonjwa na zimamoto. Wanaweza hata kukubaliana baadhi ya nyumba au sehemu za nyumba zibomolewe (na kuchangiana fidia ya anayebomolewa)kwa manufaa ya wakazi wote wa mtaani au kitongoji.
    Wakimsubiri JK na timu yake, basi hilo wajue kuwa watalipata siku Yesu au Mohammed atakaporejea duniani tena.

    ReplyDelete
  5. Huu ni muda wa wajumbe kufanya kazi yao kamili sio kusubiri ripoti za mke na mume wamegombana nini, Wajumbe na wayu wa kamati za nyumbam itaani wajitahidi wajenge kieneo cha zima moto kila sehemu na Serikali ijue hilo ndio vitu muhimu Hospital karibu Security Pia na vitu kama hivyo vya zima moto. tujitahidi hatuwezi kushindwa bwana Nchi za nje zimeweza sie vipi tushindwe?

    England wameenza kutumia vyoo vya ndani miaka ya 60's mwishoni na 70's wakati huo sie tunavyo ndani maendeleo kwao haya kuanza zamani nchi za kiaarabu utajiri na mafanikio hayajaanza zamani miaka 40 tu nyuma ambayo sio tuna uhuru kwenye miaka ya 40 sasa na kitu.

    Tanzania sie lazima tushikamane tufanye vitendo kwanza ndio baadae kuweka ndani.

    ReplyDelete
  6. Hivi ww anon wa "tumelaaniwa" una akili kweli?
    Hujawahi kusikia Moto ukiharibu mamilioni ya Nyumba katika nchi mbalimbali duniani?
    Marekani kila kukicha unasikia nyumba zinawaka moto.Juzi juzi nchini Australia majumba na misitu viliteketea kwa moto.
    Au mwenzetu bado unaishi mapangoni hufuatilii dunia inavyokwenda.

    ReplyDelete
  7. tumelaaniwa kweli maana sielewi mipango miji wanafanya nini....waaache kazi maana kila mahali makazi holela


    mdau netherlands

    ReplyDelete
  8. "The Buck stop with the President"-Period!.

    Sasa kuanzia Nyerere hadi Kikwete tumedharau sana au tumeshindwa kujua wajibu wa serikali ni nini.

    Jukumu la Serikali Namba moja: "ULINZI NA USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO"

    Kutoka hili serikali iliyoko madarakani kwa kufuata muongozo wa chama kinachounda Serikali inapaswa kuweka sera na kuzisimamia.
    Wakati wa Mwalimu swala la kuweka sera lilikuwa linafanyika lakini usimamiaji ukawa wakati mwingine mbovu na pia ukosekanaji wa viongozi bora walio na uwezo ulichangia. Na pengine Sera nyingine zilikuwa potofu ila kwa kuwa ilikuwa kipindi cha "Zidumu fikra" basi tukafa nazo hivyo hivyo.

    Awamu ya Mwinyi sera nyingi zilitupwa nje tukawa na sera moja tu ya "RUKSA"
    Katika kufurahia uhuru huu (Unajua tena Ng'ombe wa ndani ukimtoa nje anavyorukaruka) maovu mengi yalijichimbia mizizi, ujenzi wa holela, tukajenga hata kwenye viwanja vya watoto, bustani, makanisa/misikiti. Tukajenga Kiholela.
    Serikali hadi ikawa kama ya Shangazi.

    Akaja Mkapa kwa kweli alijitahidi kurudisha heshima ya serikali na utaratibu ila huku akifanya hivyo akaendelea kuua heshima na muongozo wa chama kwa kukifanya ni cha wote. Hakina msimamo kinakaribisha yeyote kwa imani yeyote matokeo yake Serikali siku hizi inaendeshwa bila muongozo wa Chama ambao ndio makubaliano kati yake na wananchi.
    Hivyo unakuta Chama uko mlala hoi mjumbe, Dewji mjumbe, Kingunge Mjumbe,Mlondon mjumbe, Mmysore mjumbe, Mtexas mjumbe, Mmanchester mjumbe, Rostam mjumbe hivyo muongozo au imani kuu ya chama tawala sasa hivi kwa kweli inaweza kuanishwa na neno moja tu "UFISADI".
    Sasa kwa muongozo huu serikali ikazaa sera ya Richmond, EPA, Kiwira, Radar, "Mtalijua jiji--Giza la Tanesco", kuleni nyasi",ku-kolimba, PHd feki, nk

    Awamu hii ya JMK hata sijaielewa maana inaonekana ni Kama vile "Bora Liende" ili mradi ni kwa kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya.
    Kila nikitembelea maeneo haya tunayoishi, Mwananyamala, tandika, kigogo, Survey, Tandale, manzese nilikuwa nahofia siku Moto utakapotokea na hii ndio hali halisi tunavyoiona sasa.
    Serikali yetu inaona ni vyema kupima viwanja sasa hivi tunafikia Bagamoyo na sasa naona Hata Kigamboni tunaambiwa eti itaendelezwa wakati haya maeneo ndani ya mji hamna kiwanja, hati, maji, wala choo???!! Wakati mwingine ni vigumu kuamini kama katika miaka yetu ya Uhuru karibu 50 sasa hatujawahi kuwa na Vita???!
    Rais wetu anasafiri sana hivyo anaona mengi naamini anajifunza mengi pia lakini bila Yeye kuamka na kuanza kuyaface head-on matatizo yetu ya kila siku sioni ni jinsi gani tutaamka. Yeye Husema anatuhutubia kila mwezi lakini hiyo si sera, Anaita watu Ikuulu anapiga kelele lakini hiyo si sera anakimbia bandarini kusema "Nawajua mafisadi" hiyo si sera.

    Ushauri wangu ni kuwa turudi kwenye utaratibu wa kawaida:
    Chama kitoe muongozo
    Serikali iweke sera na kuzisimamia
    Hakuna njia Rahisi na wala haji mzungu kutusaidia ni sisi wenyewe, tukae tuamue tufanye.
    Mungu Ibariki Tanzania,
    Mungu iokoe Tanzania.
    Mzawa

    ReplyDelete
  9. DAR TAMBARARE. HATA FIRE WANAKWAMA KWENYE VICHOCHORO. MIPANGO MIJI HIYO...TEHETEHETEHEEEE

    ReplyDelete
  10. Huyo kaka jamani, sasa anazima moto kwa maji ya kikombeni au anampasia mtu wa ndani maji ya kunywa? Kweli ana nia ya kuzima moto?

    ReplyDelete
  11. Anon wa March 25, 2009 12:33 AM umeandika fresh sema sikubaliani na wewe kusema "the buck shld stop with the pres". Kwa nini kila kitu mpaka rais? Serikali za mitaa zinafanya kazi gani? town council (halmashauri ya mji) inafanya nini? Ni rais ndo anayekaa na ku-propose how many fire stations zijengwe katika eneo? Those shld be the people who need to be questioned. Kila siku watz tumezoea rais, rais. Huyo rais baba yenu? Ndo maana anakuwa na madaraka makubwa kupita sana. We need to limit his power. Na watu wanahitaji kujua division ya powers Tanzania kusudi wajue ni nani hasa astahiliye kuswaliwa ujinga utokeapo. Lakini hawafundishi haya mambo shule. It should be basic knowledge to every citizen kujua different sectors za govt and their scope of powers. Ujinga mwingi sana bongo...alafu wanataka turudi!!

    mtoto

    ReplyDelete
  12. Nakubaliana na ann both wa 12:33 NA 3:16. Wote mmeongea vizuri hii inaonyesha ni jinsi gani Tanzania tuna watu wenye akili zao unfortunatley serikali yetu haiwezi kuwatumia. Ni kweli Rais hawezi kufanya kila kitu, lakini ndio hivyo culture ya Bchi inaamini hivyo hata rais mwenyewe anahamini hivyo ndio maana kila kukicha yuko mitaani kufanya kazi za watu aliowachagua mara Bandarini, mara sijui wapi. Sometimes i ask myself why appoint anyone if you can do all the jobs yourslef. Second, as a country we have to hold the president responsible, kama watu uliowaweka hawawezi kufanya kazi wewe kama raisi you have to answer for your people. Kama inakubidi huangaike huku na kule na bado hatuoni sera zozote au chochote kinachofanyika then why are you the president? Put everything aside at the end of the day we all going to hold the president accountable.

    ReplyDelete
  13. Anony wa 3.16 na Wa 11.50 nakubaliana na nyie kabisa kuwa Raisi hawezi kufanya kila kitu, na wala si baba yetu. Na hilo ndio tunalotaka aache ubaba afanye kazi yake anayoisahau kuhakikisha anazo sera na wale aliowateua yeye mwenyewe wanaelewa sera hizo na wanafanya kazi yao.

    Ila ni vizuri ukajifunza na kujiuliza jinsi mfumo wa Serikali unavyofanya kazi na unavyotakiwa kufanya kazi ili uweze kuelewa ni kwa nini Mwanzo ni Raisi na Mwisho ni Raisi.

    Ndio maana marekani wanamkumbuka sana Clinton, Uingereza wanamkumbuka mama Thatcher kwa kuibadilisha nchi, Putin alivyoibadilisha Russia, Au Gobarchev alivyoivunja Urusi. Hawasemi ooh waziri fulani au mkuu wa wilaya hao ni watekelezaji tu.

    Raisi ndio kinara, na ndio CEO wa nchi. Ndio maana unaona kampuni ikiboronga sio Meneja wa Idara anafukuzwa bali ni CEO.
    Na akiwekwa CEO anaefaa mambo yanabadilika lakini watu ni wale wale.

    Sasa jifunzeni kidogo jinsi ya kuendesha "MFUMO" AU "SYSTEM", Captain ndio anaendesha meli sio mabaharia!! Akilipeleka ovyo wote watazama na ndio tatizo tulilonalo Tanzania.

    Sasa akishaweka sera nzuri anatakiwa ateue watu bora(Mawaziri++) na anaowaamini wa kusimamia sera hizo
    na akishawateua anatakiwa ahakikishe wanasimamia sera hizo akishafanya hivyo Wao nao watahakikisha walioko chini yao wanatekeleza wajibu wao hivvyo hivyo hadi katibu kata. Ndivyo mfumo wa serikali unavyotakiwa ufanye kazi.

    Lakini sasa unapoona sasa Rais anawaita watu wa wizara anawachamba, anaita Posta anawachamba, anaenda Bandarini anawachamba, anaenda kukaa na Wa serikali za Mitaa anawachamba ujue kabisa mfumo umekufa maana kutoka Raisi hadi watu hao anaowachamba nguna "Dead wood" katikati na ndio ambayo anatakiwa adili nayo. Kwa maana nyingine huo ndio ubaba wenyewe kuzunguka nchi nzima akichamba watu badala ya kufanya kazi.

    Mzawa!

    ReplyDelete
  14. I like the direction of the discussion.
    Sasa kazi ya Mayor wa mji nini? Mayor si tunamchagua sisi tunapochagua madiwani? Si ina maana yeye yuko directly accountable to wananchi? Mimi nilidhani katika muundo ya mji, hawa madiwani ndo wenye nguvu. Hao ndo wanao-form town council. Na town council inauwezo wa kuweka sheria zake kwa mfano kutoruhusu wamachinga, nk. Wao pia ndo wanahitaji kusimamia jinsi mji ufanyavyo kazi na kuhakikisha hudumu za mji kama kuzomba takataka, maji safi, barabara, na ulinzi wa mali za raia, nk zinafanyika bila taabu.
    Rais ana power, sawa, and accountability comes every 5yrs. Lakini mimi katika kusikiliza kampeni zote za uchaguzi, sijawahi kusikia kitu cha maana chochote kilichosha-semwaga. Hata opposition hawajui jinsi ya ku-attack serikali. Sijawahi kuona wakiweka makosa ya serikali wazi wakati wa uchaguzi.

    Finally, I would propose kile kipindi cha kitimoto kuendelezwa kusudi watu waweze kuletwa na kupigwa maswali ya maana. Kuna watu wengi sana ningependa kuona wanawekwa chini na kupigwa maswali. Na kiwe kinatoka redioni kusudi wananchi wote waweze kusikiliza.

    mtoto

    ReplyDelete
  15. Aah, inabidi apatikane MAGUFULI mwingine kwenye mambo ya Fire ama sivyo Magufuli ahamishiwe kwenye wizara inayoshughulika na majanga baada ya kupambana na wavuvi haramu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...