
Meneja wa bia ya Kilimanjaro, Oscar Shelukindo alisema, “TBL kupitia kinywaji chake mkipendacho cha Kilimanjaro Premium Lager inayo furaha kubwa kuweka hadharani majina ya wasanii, watayarishaji wa muziki na wanamuziki wenyewe ili Watanzania kote nchini waanze mchakato wa kuwapigia kura ili tupate washindi wa 2009 Kili Music Awards kama tulivyokwisha fanya katika mashindano haya kwa miaka kadhaa iliyopita”.
Meneja huyo wa bia ya Kilimanjaro aliongeza kuwa wanachotakiwa kufanya Watanzania ni kuwachagua wanamuziki na wasanii wanaowavutia watakaokuwa katika makundi 20 kwa kuwapigia kura kupitia namna kadhaa ikiwa ni pamoja na njia ya ujumbe mfupi wa maneno yaani (SMS), kuponi za magazetini na pia kupitia tovuti ya
www.kilitimetz.com
na kwa njia ya barua pepe kwenda:
“Ikumbukwe kuwa dhumuni kuu la Tuzo za Kili Music Awards ni lile lile siku zote ambalo ni kukuza sanaa ya muziki nchini, kuvumbua vipaji vipya kupitia mashindano ya Kanda, kutambua mchango wa wanamuziki wakongwe pamoja na kuwahamasisha Watanzania kupenda na kuthamini muziki na mchango wa wanamuziki wa Kitanzania katika kukuza sanaa hii hapa nchini kwetu na kuhakikisha kuwa muziki wa nje haupati umaarufu kushinda wetu,” aliongeza Oscar Shelukindo.
Sherehe za kuwatunza wanamuziki washindi wa Tuzo za 2009 Kili Music Awads zitafanyika mapema mwezi wa Aprili 2009, ambapo baada ya hapo kutakuwa na ziara maalum ya washindi wa Tuzo za Kili Music Awards na kutumbuiza katika majukwaa ya miji mbalimbali hapa nchini.
Killi time mnafanya vizuri kwa kuendelesha mashinda haya.Kwa maoni yangu kuwa kila mwaka mnachagua vikundi vile vile na watu wale wale mngejalibu kuchanganya hata na Bendi na wasanii wa kutoka mikoani nafiri itakuwa vizuri zaidi.
ReplyDeleteAsante
komba wa Arusha
KIZUNGUMKUTI KTK TUZO ZA KILI CHAANZA
ReplyDeleteNataka kujua kitu kimoja hapo khs ALBUM BORA YA ASILI YA KITANZANIA. Iweje mgomaniaji awe mmoja??Au ndio kizungumkuti hicho kimeshaanza, mambo yale ya upendeleo?Ina maana hakuna mtu bongo nzima mwenye album ya mziki wa kiasili Tanzania??
Kama Dogo Mfaume, mfano ana Album yake, na nyimbo zote ni za kiasili, na ndio maana hata ktk kutafuta wimbo bora wa kiasili Dogo mfaume yumo na wimbo wake.Kwanini album yake isiwekwe hapo?Kuna ushindani gani kama mtu ni mmoja na pekee?
Hivi nyimbo za Taaraba, mambo ya mwambao nao si ni mziki wa asili ya Kitanzania?Au wasemapo huo mziki mpaka awepo mtu mmoja tu inakuaje hapo?Mfano kule Kigoma kuna watu kama vile MAPIGO SABA, Ukienda Dodoma kuna vikundi vingi vina album za nyimbo za asili.Hivi Wanne Star inakuaje hapo kweli hafai?
KILI hizi kasoro muwe nazo makini, hata kama hamna nia mbaya, mnaleta walakini jamani.Haituingii akilini kusema ni mtu au kikundi kimoja Tanzania nzima ndio kina album ya mziki wa asili.
Fanyieni kazi kasoro hizi mapema.Sio mje kuaibika kama mwaka jana mlipotoa zawadi kwa Bushoke kumbe wimbo sio wake, yeye alifanya colabo tu na mkenya, ikaonesha waandaaji ni wazushi, yaani hata hamjui mwenye wimbo ni nani.Kuweni makini, ombeni ushauri kwa watu mbalimbali kwanza kabla ya kuweka mambo hadharani.Fanya mambo ki-Preofessional jamani.
MAKULILO Jr,
http://www.makulilo.blogspot.com
West Virginia, Marekani
Nakubaliana na Makulilo Jr, hapo juu naongezea kuwa kama moja ya madhumuni ni kutambua mchango wa wanamuziki wakongwe ningetegemea wawepo wazee wa msondo au sikinde. Karama wa sikinde ni kijana hawezi kuwa ktk kundi la wakongwe, kwa hiyo kundi hili naona halina mwakilishi!!
ReplyDelete