Mona Lewis

Mbongo Mona Lewis amechaguliwa katika mashindano ya kila mwaka ya The Apprentice ambayo huonyeshwa kwenye kipindi cha BBC kawaida kila Jumatano saa tatu usiku (9pm).


Mona itambidi amuhakikishie Sir Alan Sugar, bosi wa kipindi hicho na tajiri mkubwa hapa UK (Millionnaire) kuwa anakipaji cha kuchaguliwa kuwa The Apprentice na kupata nafasi ya kufanya kazi katika mashirika ya Sir Alan Sugar na kulipwa takriban £100,000 (paundi laki moja) kwa mwaka.


Habari kamili na picha bonyeza link:

Zenjydar Community Association

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. hebu nisaidieni jamani, katika official website ya apprintice inasema kuwa amezaliwa karachi na sasa anaishi uk lakini ni mtanzania! tena alikuwa miss tanzania! haya vipi?

    ReplyDelete
  2. She was miss Tanga miaka ya Tisini.....lol

    Amezaliwa TAnga kasoma Tanga na Arusha haya mengine ni uongo na feki tu.....

    Anyways Congratullations Muna KOJA.

    ReplyDelete
  3. huHUYU MSICHANA NI MTANGA ANAITWA MUNA KOJA AU FATMA KOJA ALIKUA MISS TANGA MWAKA 1996 NA AMESOMA POPATLAL MAMA YAKE KATOKEA KARACHI MUHINDI MWEUSI NA BABA YAKE NI MDIGO WA TANGA NAFIKIRI WALIOWANA NA MAMA YAKE ALIPOKWENDA KUSOMA HUKO KARACHI NA AMEZALIWA TANGA KAKULIA TANGA NDIO AKAOLEWA NA HUYO MZUNGU TANGA MWAKA 2000 NA HAUPENDI USWAHILI HATA KIDOGO NA HATA KUONGEA PIA HUA ANAONGEA KIINGILISHI TU KISWAHILI HAKITAKI...LKN BABA NI MDIGO ORIGINAL

    ReplyDelete
  4. Jamani mmbona mnatuchanganya nimeenda kwenye ma website anaonekana kazaliwa Karachi,Pakistani alafu anaishi Kent,England au Raia wa TAnzania? au Kaishi tu Tanzania ndio mnasema Mtanzania? tujaribu kufahamishiana vizuri kama ana Uraia wa Pakistani au England si Mtanzania kabisaaaaaaaa Tanzania hakuna Uraia miwili. MSije kusema Mtanzania sababu ni Mzee Moja mtanzania.

    Wajanja mnaomjuwa au kama mnajuwa Story zake za kuwa Miss Tanga na Picha mnawezakupeleka Story kwenye magazeti ya Www.thesun.co.uk au mirror.co.uk kwa wale wa hata Tanzania mnaweza kulipwa si chini ya £500.

    ReplyDelete
  5. jamani!tusimbague huyu ni MDANGANYIKA mwenzetu !wanaomjua wanaeleza hapo juu tena kazaliwa
    TANGA-nyika!!??tena wanasisitiza kuwa kiswahili hakipendi!hilo sio kosa katika kukosha udosi wake,
    Tena waswahili hapindi kuongea nao kiswahili! sasa huyu ni mwenzetu !huu UBAGUZI wetu wabongo unatokea
    wapi!wakati huyu binti ni mzawa mwenzetu?na kiswahili akipendi?na sio lazima akipende!pengine anaona akifanani na jinsi alivyo!
    Sasa kwanini abaguliwe????????
    MIE SIMO NAWACHIE WENYE KUSUKUTUA

    ReplyDelete
  6. Ukisoma kiswahili kilichoandikwa hapa unaweza usishangae kwa nini huyo Mtanga au Mdanganyika asikipende. Inaonekana hata kwa wengi wetu kinatuwia kigumu kuandika. Yu wapi mwalimu wangu wa grammar ya kiswahili - angetia bakora kila mmoja hapa.

    ReplyDelete
  7. Jambo la maana hapo ni kuwa Tanzania inatajwa kwa mema,sasa kazaliwa karachi, punjab,makororo,udigo hayana nafasi. wabongo bwana!

    ReplyDelete
  8. kwa hiyo hakuzaliwa karachi? na hakuwa tanzania beuty queen alikuwa tanga beauty queen? well wanaomjuwa na wana proof ni kweli wanaweza kuuza stori zao kwa tabloid papers hapa na kujipatia kilaji. so kama uko hapa uk, huna walakini na paper zako na uko tayari kutokea magazetini kuna takriban £500 zina jina lako wahi haraka!!!!!

    ReplyDelete
  9. 15) MONA LEWIS, 28

    THE Tanzanian beauty queen lives up to her first name and rubs team-mates AND customers up the wrong way in the first task, cleaning cars. The mum of one, a finance manager, now lives in Kent and says: “I work hard and I’m honest.”

    http://www.thesun.co.uk/sol/homepage/showbiz/tv/article2323826.ece?OTC-RSS&ATTR=TV

    Nime Paste Kule www.thesun.co.uk wanajuwa kama kashawahi kuwa Tanzanian Beauty queen. na anasema kwamba yeye mfanyakazi Hodari na Mkweli haya tumuombee mazuri japokuwa Sir Alan sio sana Kuchaguwa wanawake kazini kwake.

    ReplyDelete
  10. jamani"! chonde! chonde! huyu ni
    MDANGANYIKA MWENZETU! tusimbague!bali tumfagilie,Kiswahili ataki kabisa kukisikia! sasa jamani hili sio kosa la jinai! kwa nini?mzalendo mwenzetu tumbague???? je ? huu ni uhungwana???
    Tena kafanya jambo la maana kajichanganya kwa kufunga ndoa na MZUNGU kuliko angeolewa na Mnaijeria aka Mpopo!
    sasa mwanadamu hafanyeje???
    huu ubaguzi wetu utatufikisha pabaya?
    mie simo nawachia baraza

    ReplyDelete
  11. wabongo!tunapenda sana kokolo!na vurugu mechi zisizo kuwa na faida!sasa huyu binti wa kitanga Muna au awe maimuna bint koja,au pnegine tumwite Muna Mwana Koja!
    kwanini ? wanyime usingizi watoa maoni,badala ya kufurahia kuwa mwenzetu anatuwakilisha?
    Hivi mnayo habari kuwa Rais wa Khaizai wa Afghan ni raia wa unyamwezini wa kujiandikisha!sasa huyu Muna awe Mdosi,au mwingereza wa kujiandikisha hilimradi amezaliwa na moja ya wazazi wake mtanzania! Udigo bado anao!
    msilete nongwa!mtafute kazi ya kufanya

    ReplyDelete
  12. nawe anon wa March 18, 2009 6:08 PM akili zako zi wapi? unalaumu watu kuwa wabaguzi ilhali wewe mwenyewe umesema neno la kibaguzi pale uliposema Tena kafanya jambo la maana kajichanganya kwa kufunga ndoa na MZUNGU kuliko angeolewa na Mnaijeria aka Mpopo! au hujui nini maana ya ubaguzi?

    ReplyDelete
  13. Kweli kabisaaaaaaaaaa lazima muwe mnatizama mnachoandika, tuwache wanadamu waishi wanavyopenda wao malipo anayelipa ni mola mwenyezimungu basi tuwache kubaguwana, Watanzania na uhakika angekuwa Mkenya kwenye show hiyo tungeanza Mbona watanzania hawajajitokeza tunaanza kulalamika, Haya leo Mtanzania huyo tumeanza Mengine tumuombee mwenzetu afanye vizuri asije kuhaibu kwanjia mbaya.

    Tanzania na tuwache tabia ya kitu kibaya kusema neno Waswahili bwana, Uswahili ndio Mila yetu kama England ndio English Tanzania ndio Swahili land piga uwa sisi waswahili na lazima tufuraikie Uswahili wetu. Kuwa Mswahili si ndio kuwa na Tabia mbaya. Kutoka kwa Pazi.

    ReplyDelete
  14. kuna mdau mmoja amejaribu ila ukweli ni kuwa moona khoja (jina la nyumbani) au fatma khoja jina analotimia shuleni kweli alizaliwa karachi na alikuja akiwa mdogo sana Tanga, na alisoma popatlal sec hadi form 6 alipomaliza form 4 ndio akashiriki miss Tanga na kuwa miss Tanga, baada ya hapo akaenda miss tanzania akafanikiwa kuwa mshindi wa 3 na aliekuwa miss tanzania alikua shose sinare, ndio akahamia Arusha ndio akaolewa na huyo aliekuwa mume wake wakapata mtoto mmoja. nadhani sasa mtakuwa mmepata kumjua kidogo, ila mpaka sasa hivi tunapoongea ni mtanzania na anatumia passport ya bongo.

    ReplyDelete
  15. Pazi waambie bwana umeweka Point kweli na piah uyo aliyelalamika mtu kusema mnaijeria aKa Mpopo umeongea point kwlei pia kufahamisha watu waache hizo tabia jamani tuwe pamoja tusipondane.

    ReplyDelete
  16. Anaonekana kuwa ni demu mzuri na sijui kwa nini hakushinda Miss Tanzania wakati ule; ushindi ulibebwa kwa Shose Sinare. Hata hivyo, yeye ni kati ya wawili wenye elimu ndogo sana kwenye kundi zima la Apprentices. Kwa nini hakujiendeleza kielimu baada ya kuolewa na huyo mtishi? Nilisikia kuwa Shose naye aliolwea na mtishi, na ma-Miss kadhaa waliofuatia nao waliolewa na watishi.

    ReplyDelete
  17. haya walavumbi semeni sasa , maana mnasema kila alioko ulaya mbeba box na huyu mbeba box? chnga mkieni mabox baadae huwa yana lipa mtu kama huyu na hakika alianza na box kwanza.

    ReplyDelete
  18. ni kweli anaitwa fatma khoja au mona khoja mdogo wake anaitwa naima khoja nimesoma nae ni watu wa tanga mpaka baba yao namjua anafanya kazi TRA .

    ReplyDelete
  19. Mona Lewis previously known as Mona Koja nimekuwa naye alikuwa jirani yetu. Mzee Koja alienda Karachi kusoma accounts akakutana na mmrs koja wakaona na Mona akazaliwa Karachi. Alipofikisha miaka 2 wazazi walihamia TZ. Mwaka 96 akawa Miss Tanga and the Runner up wa Miss TZ, at that time Mona alikuwa ana DUALNATIONALITY mpaka alipofikisha miaka 18 akaapishwa na akachagua kuwa MTANZANIA. Na mpaka dakika hii bado ni mtanzania anaishi kwa VIZA ....sasa acheni umbeya na muanze kumsapoti Mtanzania mwenzetu. Angeongea kiswahili peke asingiweza kuchaguliwa kwenye hicho kipindi, msiojua kingereza acheni wivu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...