Balozi wa Nanihii,
Poleni na moto na faya za kutoka Dar hadi Bwagamoyo. Bongo kweli tambarare, au vipi balozi?
Mie nina shida ya kutaka kujua maana ama tafsiri ya maneno yafuatayo. Hakika yananisumbuaga sana sana mpaka nachanganyikiwa. Yaani we acha tu.
1. Nini tofauti kati ya mgumba na tasa?
2. Nini taftsiri ya maneno 'proof' na 'evidence' kwa kiswahili?
samahani najua uko bize, lakini wewe na wadau wako ambao wengi ni wachambuzi wa mambo kwa kwenda mbele nadhani mtanisaidia.
Natanguliza shukurani
Emma
Mdau wa Belize


Pole sana mkuu wa wilaya kwa kazi ya kuzima majivu!!!!
ReplyDeletekuhusu tasa na mgumba mada hii ilishazungumzwa siki nyingi sana kama we ni mdau mpya nenda
http://issamichuzi.blogspot.com/2008/07/tasa-na-mgumba.html
kuhusu proof ni thibitisha!
evedence ni ushahidi unaoonekana wazi!!!!
asante, Nkya
A.city
1. Nini tofauti kati ya mgumba na tasa?
ReplyDelete2. Nini taftsiri ya maneno 'proof' na 'evidence' kwa kiswahili?
1. Mgumba na Tasa kwa ufahamu wangu yote yana maana moja yaani ni 'noun' inayomaanisha mwanamke au mwanamume asiyezaa japokuwa wakati mwingine kimatumizi haswa ukanda wa Pwani wakati mwingine watu humaanisha mgumba ni yule ambaye bado hajajaaliwa mtoto na tasa ni yule ambaye kwa namna moja au nyingine hawezi kuzaa.
2. Kwa mujibu wa dictionary; 'proof' na 'evidence' kwa kiswahili yote yana maana moja ambayo ni USHAHIDI ila proof wakati mwingine humaanisha UTHIBITISHO wa jambo au kitu fulani kuwa ni kweli su si kweli.
Mdau kwanza napenda kukwambia kuwa swali la kwanza yote mawili ni sawa inategemea unataka kutumia neno lipi kati ya hayo kuwasilisha ujumbe wako. Swali la pili proof ina maana ya uthibitisho wa jambo fulani na evidence ni ushahidi wa kitu au namna fulani.Yategemea na tukio linalohitaji mojawapo ya maneno hayo.
ReplyDeleteTofauti kati ya mgumba na tasa ni katika matumizi tu! ila maana zake ziko sawa.
ReplyDeleteMgumba hutumika kwa binadamu na tasa hutumika kwa viumbe wasio binadamu(wanyama).kumuita binadamu(wakike)tasa ni makosa je ng'ombe nae utamuita mgumba?
Hiyo ya proof na evidence wapo waliojibu sahihi na wengine wamekosea nijuavyo mimi Proof ni HAKIKI/hakikisha/thibitisha na Evidence ni Matokeo ya proof.
Mdau wenu wa Mwanza.
..my two cents:
ReplyDelete1. yote mgumba na tasa yana maana moja ya kiumbe-hai kisichoweza kushika/beba mimba/ujauzito/zaa. Hata hivyo matumizi ya maneno hayo, kwa maoni yangu, yana upendeleo tofauti: tasa ni kwa viumbe hai visivyo binaadamu, k. mf. utasema 'mpapai tasa' si 'mpapai mgumba'...Pia kwa maoni yangu, 'tasa' hutia msisitizo kutowezekana kupata mtoto kwa kiumbe hicho.. Hivyo pia ni mwafaka zaidi kwa matumizi ya binadamu asiye na mwenzi na pia ndo maana watu husema 'alikufa tasa', maana kuna finality uwa kiumbe huyo hataweza tena kupata mtoto. Wakati mgumba ni hali ya kuendelea wakati binaadamu anaishi (aweza kuja pata mtoto - maajabu huwa yapo!- rejea nyimbo ya Mwin'juma Mumini ya jina hilohilo!)na pia ya mwenye kuendelea kujaribu..
2. Proof/Evidence: Ithibati/Kidhibiti. Hususan pale 'proof' ikiwa ni matumizi ya jumla wakati 'evidence' ni matumizi ya kisheria..
..still my two cents! - UZENG
Proof ni Uthibitisho; na Evidence ni Kithibiti..yaani kitu au vitu kitakacho/vitakavyo uweka wazi uthibitisho . Nawakilisha, Ben
ReplyDeleteProof = Thibitisho
ReplyDeleteEvidence = Ushahidi
e.g
Proof of the Gauchy Schwartz Inequality Theorem = Thibitisho la Dhana ya Utoulinganifu wa Gauchy Schwartz
Tazama kwamba "Thibitisho" linafaa zaidi kwenye mfano tajwa hapo juu kwani ungesema "Ushahidi wa..." ingemaanisha kuwa unahitaji tu kuonesha mifano ya vectors zinazotosheleza GSI, whereas kwa kusema "Thibitisho la..." inamaana kuwa unaenda kuonesha kutoka kanuni za mwanzo ya jinsi gani mavector kwa ujumla yao yanatosheleza dhana ya GCI.
Hivi mdau huna access na kamusi ya swahili/swahili-english/swahili au ndo kuanzisha hoja humu!Mi nakushauri utafute hizo kamusi ndo utapata uhakika wa maneno yako.Hata majibu yetu yatatokea huko.
ReplyDeleteKwanza namshukuru mungu kwa kunipa uwezo nilio nao kielimu na kutafuta elimu, pili nawashukuru wote ambao umeshachangia awali, na tatu namshukuru aliyeomba msaada. funzo: hatulingani kiutundu wa kutafuta majibu ndio maana yuko huyu na majibu mnayaona. kwa wale weesi ka mimi tumshukuru allah sw kwa kutuwezesha, na wale wazito tusiwakejeli bali tuwafundishe kwani wote ni waja. wote tungeumbwa sawa pasingetosha, aliyefurahi aniombee kheri aliyechukia anisamehe.
ReplyDelete1. MGUMBA ni mwanamke asiyekuwa na uwezo wa kubeba mimba, na TASA ni mwanaume asiyeweza kutengeneza mimba kwa maana ya mbegu zake kutoweza kurutubisha yai.
ReplyDelete2. PROOF ni uthibitisho na EVIDENCE ni ushahidi.
Nyongeza kwenye tasa. Hata namba zipo tasa yaani namba zinazogawanyika bila baki kwa moja na namba yenyewe. Hazizai zaidi ya hapo. Hakuna namba gumba.
ReplyDeleteanon wa March 24, 2009 10:29 AM...i believe the correct spelling is Cauchy sio Gauchy
ReplyDeletemtoto
JAMANI MIMI NAVYOELEWA KUWA
ReplyDeleteMGUMBA NI MWANAMKE YEYOTE AMABYE ANAPATA SIKU ZAKE KAMA KAWAIDA/PERIOD BUT HAWEZI KUTUNGA MIMBA KWA SABABU ZA KIBIOLOGIKIA MAYAI YAKE YANAKUA DHAIFU HAYAWEZI KUTOA MTOTO. PIA ANAWEZA KUWA MWANAUME AMBAYE JOGOO ANAWIKA LAKINI MBEGU ZAKE ZIKO DHAIFU HIVYO HAWEZI KUMUWEZESHA MAMA KUTUNGA MIMBA.
NA
TASA NI MWANAMKE AMBAYE BADO ANAUMRI MDOGO ( YANI AJAFIKIA ULE UMRI WA MINEPOSE) LAKINI HAPATI SIKU ZAKE KABISA YANI "NO DAMU/PERIOD" NA HAWEZI KUTUNGA MIMBA.YANI KWAKIFUPI NI MWANAMKE AMBAYE HAJAVUNJA UNGO MAISHANI MWAKE MWOTE.