safu ya waimbaji ya msondo ngoma. toka shoto ni kifaa kipya salim sultani a.k.a musemba wa minyigu, papa upanga na juma katundu. bendi hii inasifika pia kama chuo cha mafunzo kwani pamoja na ukongwe wake hii ni bendi pekee yenye vija na wengi wanaopiga muziki wa kiutu uzima usioisha utamu. hii ni shoo katika bonanza la michezio na muziki la kila jumapili ambapo msondo hutumbuiza na twanga pepeta bure chini ya udhamini wa kilaji cha kilimanjaro lager
papaa saidi mabera ambaye ndiye kakamata mpini wa 'suti' ya msondo ngoma asilia. toka ajiunge na bendi hii mwaka 1973 wakati huo ikiwa juwata jazz band hadi leo yupo na hajawahi kuhama
salim sultani akiongozwa na kamanda muhidin maalim gurumo
hassani, mtoto wa marehemu TX moshi william, ameachana kabisa na mambo ya bong fleva na kujikita vyema kwenye msondo ngoma, akifuata nyayo za baba yake. kwa kweli anakuja juu kwa kasi sana.
mkongwe shaaban lendi (kati) akiwajibika na wenzie katiba seksheni ya midomo ya bata
shoo ya msondo inaongozwa mama nzawisa ambaye hana mpinzani kwa manjonjo ya jukwaani
mama nzawisa akiwa kazini hataki mchezo
mama nzawisa akistua kijoti
romanus mng'ande a.k.a romario pamoja na kupuliza mdomo wa bata pia ni repa mkali sana

Video za msondo
na
na








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AHSANTE MICHUZI KWA TAARIFA HII YA MSONDO KWELI HAWA JAMAA WANATISHA HASWA WANAMUZIKI WAO WA MUDA MREFU SANA NDIO UZURI WA KUUTAWALA MUZIKI SIO MARA HAPA MARA PALE ALAFU HAKUNA MAFANIKIO PIA WANAOHAMA WANAHAMA KIMASILAHI JAPO SIONGEI HIVYO

    ReplyDelete
  2. Huu siyo Msondo. Msondo umekumbwa na nini? Msondo usiyo na maadili, adabu, heshima wala hadhi ya Msondo siyo Msondo.

    ReplyDelete
  3. mi napenda sana msondo kwa sababu walikuwa wana fanya mabo ya kiutu uzima sana na wanacheza kwa adabu na wanaimba kwa adabu lakini mi nawaona wanataka kushindan na akudo na twanga pepeta , warudi wafanye muziki ule wa zamani sisi wapenzi wao hatukuwapendea hao akina dada walio vaa skin tait na hatupendi

    ReplyDelete
  4. Michuzi, naomba unisaidie jinsi ya kuwa naingia katika web hii ya musiki, kwani sasa kila nikifungua blog yako nateremka na kubofya penye msondo. najua baadae hii linki itapotea, nifanyeje ili hata hapo baadae niwe naingia katika muziki huu? Nimefurahi kuona miziki mingi tuu ya Tz, nimfurahi sana!! Udumu Michuzi! Mkuu wa wilaya!! Mafisadi ZIIIII!! naona na mwakyembe anataka kuingia kwa mafisadi! jamani!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...