
mzee rashidi mfaume kawawa akipozi na kikosi cha taifa stars cha miaka ya 80 (samahani, sio kilichofanikiwa kwenda nigeria kucheza katika kombe la afrika). kulia kwa mzee kawawa ni kocha jeff hudson, akifuatiwa na kocha msaidizi joel bendera.
wengi wa wachezaji waliounda kikosi hiki walitoka katika mashindano ya shule za sekondari, umiseta. tungekuwa mbali sana endapo mashindano hayo na yale ya shule za msingi, umishumta, isingesimamishwa.
PS: wadu mliochangia naungana nanyi kuwa hiki si kikosi cha nigeria ila ni cha chalenji cup, na kunradhi kwa kuteleza, na asante kwa data za uhakika ambazo nadhani zitanufaisha wengi.
-michuzi
Adidas zanguvu kipindi hiko wachezaji wana Afya ya uhakika, hakukuwa na matatizo kipindi hiko ni nizamu tu na vipimo tosha kapime wachezaji wetu sasa hivi kama hawajakimbizana Kambini. From Pazi.
ReplyDeleteWachezaji wetu wazamani wameshiba inavyotakiwa hata AFRO zao zina Afya sio laini laini nywele zimerutubika wanacheza kwa umoja kwa moyo wa Taifa. mungu awasaidie na wasasahivi wawe na nizamu na ufatiliaji wa kuwatizama wenzao.
ReplyDeleteSALAM! KAKA UMECHEMSHA HAPO. HII NI TIMU YA BARA(TANZANIA BARA)NA HII NI MWAKA 1984WAKIWA BAHARI BEACH HOTEL WALIPOKUWA WAMEWEKA KAMBI KWA AJILI YA KOMBE LA CHALENGE,NCHINI KENYA. NA SIO KIKOSI CHA LAGOS 1980 HATA HIVYO BAADHI YA WACHEZAJI WACHACHE WALISALIA HAPO KATIKA KIKOSI CHA 1980 KUTOKA KULIA KWENDA KUSHOTO. MSATARI WA NYUMA KABISA: OCTAVIA MROPE(MAJIMAJI)HAMISI KINYE(YANGA)WILLY KIANGO(COASTIL UNION)MAREHEMU KIHWELU MUSSA(SIMBA)SALUM CARLOS MWINYIMKUU(PAN AFRICA)AHMED AMASHA(YANGA)MAREHEMU RAPHEL PAUL(PAMBA/SIMBA)MAREHEMU RAJABU RISASI(RTC MWANZA,BIASHARA/PAMBA)GORDIAN MAPANGO(PAN AFRICA)MSATRI WA KATI:(KUSHOTO-KULIA)HUSSEIN NGULUNGU(PAN AFRICA)MAREHEMU LILLA SHOMARI(CDA/SIMBA)PETER TINO(PAN AFRICA/MAJIMAJI)ATUMANI MAULID(SIMBA)ATHUMANI JUMA CHAMA(YANGA)JUMA MHINA(YANGA/PAMBA)ABEID MZIBA(YANGA)ELISHA JOHN(COSTIL UNION/YANGA)NA DOTO RUTA MOKILI(PAN AFRICA/MAJIMAJI)MSTARI WA MBELE(KUSHOTO-KULIA)DR.SIMKUMBUKI JINA JOEL BENDERA KOCHA MSAIDIZI,JEFF ALAIN HUDSON KOCHA MKUU MZEE RASHID KAWAWA NAHODHA CHARLES BONIFACE MKWASA(YANGA)MCHUA MISULI WA TIMU NA MWISHO NI TIMU MENEJA WALIOACHWA NI PAMOJA NA RAJABU RISASI,INNOCENT HAULE, JOHN FAYA,YUSUPH BANA,RAPHAEL PAUL NA MAJERUHI ABDALAH BURHAN NA OMAR HUSSEIN ILIPOFIKA MJINI NAIROBI ILIPATA MATOKEO MABAYA MECHI YA KWANZA DHIDI YA ETHOPIA MATOKE 1-1 GOLI LA TANZANIA LILIFUNGWA NA NAHODHA CHARLES BONIFACE BAADA YA KUNGANISHA KONA ILIOPIGWA NA AMASHA WAHABESHI WAKASAWAZISHA DAKIKA YA MAJERUHI. MECHI ILIOFUATIA ILISHIA KWA SARE YA 0-0 NA HARAMBE STARS KENYA WALIOKUWA MABINGWA WATETEZI NA WALIOKUJA KUTWAA TENA KOMBE HILO(MARA YA TATU MFULULIZO)MECHI HIYO ILIKUMBWA NA BALAA LA KUKUATIKA UMEME,KATIKA UWANJA WA CITY MJINI NAIROBI ILA KUNA TAARIFA KUWA WAKATI UMEME UKIKATIKA MAHMOUD ABBAS KENYA 0NE ALIKUWA AMEDAKA MGUU WA PETER TINO ALIKUWA ANAELEKEA KUFUNGA MECHI ILIOFUATA TUKALALA KWA SUDAN KWA GOLI PEKAA LA NAHODHA .MUSTAPHA NAGGAR TULIPOMAALIZIA MECHI YA KUKAMILISHA RATIBA TUKATOKA SARE TENA NA UGANDA(THE CRANES)1-1 BAO LETU ALIFUNGA ABEID MZIBA AKIMALIZIA GONGA KATI YA CARLOS MWINYIMKUU NA KIANGO WILLY TULIPORUDI TUKAWAKUMBUKA SAANA KINA ZAMOYONI MOGELLA,ADOLPH RISHARD ,NICO NJOHOLE NA JUMA MKAMBI,LAKINI UKIRUDI KATIKA UKWELI WENGI WAO HAWAKUWAANZIA KATIKA UMISETA WALA UMISHUMTA LABDA AMASHA RAPHALE PAUL NA MROPE
ReplyDeleteKAMA NITAKUWA SIJASAHUA, ASANTE KAKA MICHUZI
MDAU
SHEBBE EL JEIZAN
MICHUZI SISI WENGINE TUNAKUHESHIMU SANA KWA KUWA UMETUPITA KIUMRI NA UNAWEZA KURUN BLOG YA JAMII,LAKINI UNATUANGUSHA UNAPOWEKA PICHA ZA KUMBUKUMBU BILA KUWA NA UHAKIKA NA KUPOTOSHA WATU,KUMBUKA YOU CANT CHANGE HISTORY.SASA KUKATA LONG STORY HICHO KIKOSI SIO KILE KILOCHO KWENDA LAGOS,KUNA WACHEZAJI AMBAO WALIKUJA BAADAE KAMA NINAO WAONA HAPO AKINA LILA SHOMARI,AHMED AMASHA,ABEID MZIBA,ATHUMAN JUMA CHAMA JOGOO,CHARLES MKWASA,JOSEPH FUNGO,HAMIS KINYE,MUSSA KIWELO,NA MAKOCHA WAO SIO WALE WALIOKWENDA LAGOS NAKUMBUKA KOCHA WAO ALIKUWA MOHAMMED MSOMALI,NA SIO BENDERA WALA HUDSON,NA BAADHI YA WACHEZAJI WLITUPELEKA NI AKINA EZEKIEL JUJUMAN,PETER TINO,MOHAMMED SALUM (YULE MWARABU WA TANGA),JUMA PONDAMALI,DAUD SALUM,KAJOLE,MOHAMMED TALL,NA HICHO KIKOSI KITAKUWA AIDHA MWAKA 1982 AU 1983,LAKINI SIO 1981 KWA KUWA 1981 KOCHA ALIKUWA MGERMAN RUUD GURTENGOFF,NA 1984 AMASHA ,KINYE,JOGOO WALICHEMSHA WAKAACHA MPIRA.
ReplyDeleteOCD
HAPANA.Kocha tuliyekwenda naye Lagos alikuwa Mpolish jina lake Slowmir Work. magolikipa walikuwa Athumani Mambosasa, na Juma Pondamali. siwaoni ktk picha hii. pia simuoni nahodha wa timu hiyo Leadgar Tenga.
ReplyDeleteJeff Hudson toka UK amekuja baadaye sana. amekuja hata baada ya Mjerumani Ruud Gutendhof aliyefundisha timu iliyocheza fainali za Challenge DSM.
du wana afya alafu nywele wotee zimetulia hakuna aliyesuka mistari mabutu wala mvaa hereni hata ungewaambia wafanye hivyo wangeshangaa! sasa sijui 20 years baada ya leo wachezaji na WaTz kwa ujumla watakuwa wanaonekanaje hasa ukizingatia by then tutakuwatumeshafika kiwango cha kushiriki World cup!!! hahaa
ReplyDeletemAXIMO NDIO AJUE KUWA TIMU NA MPIRA TULIKUWA NAO.TABIA YAKE YA KUTUDHARAU NA KUSEMA AMEKUJA KUJENGA MSINGI.SIO KWELI KABISA.
ReplyDeleteKOCHA HUYU MBINAFSI SANA ANAJITIA KUWA KAONGEZA KIWANGO CHETU CHA MPIRA.MASIKINI HAJUI TUMEKUWA NA WATU KAMA NICO NJOHOLE,SUNDAY MANARA,ADOLPH WAMECHEZA NJE.PIA FAINALI ZA 1980 NI TOFAUTI NA KOMBE HILI LA CHAN AU MAARUFU KAMA KOMBE LA MAXIMO KWANI HILI HAKIJULIKANI NA FIFA.LILE LA 1980 LINAJULIKANA NA FIFA.
NIMESKITISHWA SANA MAXIMO HAJALETA KOMBE LOLOTE WALA KUTUFIKISHA FAINALI LAKINI ANAONGEZEWA MKATABA.
SITARAJII KUPATA LOLOTE STARS CHINI YA MAXIMO.
Huna uhakika na unachokisema Anonymous18, 2009 9:53,
ReplyDeleteAmasha,chama"Jogoo"Na kinye Sio kweli hawakuchemsha kumbukumbu Zinaonyesha wazi kuwa ahmed amasha alichaguliwa na jopo la Makocha 13 Waliokwenda na timu zao za taifa katika michuano ya Chalenge Nchini uganda 1985 Na kuwa beki wa Kushoto bora wa Michuano,Kipa Efford Chabala(Zambia/Nkana FC)2.Ssemogerere Uganda/KCC )3.Ahmed amasha(Tanzania mainland/Yanga Fc)4.Josephat morilla(AFC Leopard/Kenya)Young Chidzmodzie(Malawi/Bata bullet)Stanley marimo(zimbabwe/Dynamos)Gibby mbesela(Ndola FC/Zambia)Mustapha Nagar(El Hilal/Sudan)clifont Msiya(malawi/)Lucy msiska.Issa Ssekatawa.Willberfoce mulamba na Pia Marehemu Ezekiel Gryson Na mohammed bakar tall hawakumo katika kikosi cha Legos alikuwepo Tenga,leopald taso,jellah salim amir na General Mkambi
MDAU
SHEBBE EL JEIZAN
Kaka Michuzi,hiki sio kikosi chetu "Dream Team"kilichotikisa Afrika mwaka 1978 hadi 81
ReplyDeleteSio kikosi hiki kilichomliza Rais Kaunda uwanja wa Independence pale ambapo ukuta wa Zambia "KK11"wenye mabeki uliokuwa unahesabika kama bora africa chini ya nahondha Mosses Musoreko,Dickson Makwaza,Dick Chama na kiungo bora afrika toka zambia kioindi hicho Hakimu Mwasenge uliposhindwa kuzuia kona ya dakika ya 80 Leopado Tesso Mukebezi na kumkuta Tino Peter tena akiwa amebanwa mno na mabkei 2 wa Zambia lkn akaruka juu zaidi na kuugonga kwa nguvu kwenye nyavu ndogo na kumuacha golikipa wa Zambia Kapambwe Mabenga akiwa hana la kufanya-goli liliitoa Zambia kwenye fainali ya afrika na kuipeleka tz mara ya kwanza na ya mwisho kwenye historia ya soka ya dunia hii inyojumuisha wachezaji wa ndani na nje!
kuna habari zilitufikia tukiwa hitelini Lusaka kuwa huko Chilabombwe nyumbani kwa kiungo Fred Mitti alizidiwa sana kati ya dimba na Husssein Ngulungu"migulu"watu wenye hasira walivamia nyumba ya wazazi wake kupinga kuzidiwa ujanja na viungo wa tz wasio hata na majina!
Michuzi,hiki sio kikosi cha tz cha mwaka 81 cha lagos,maana hata kocha huyu ni Jeff Hudson,kocha aliyemvumbua Zamoyoni Mogela,kumbuka mwaka 81 kocha alikuwa"white wizard"Slowmir Worke,kocha mtaalamu kupata kutokea barani Afrika anayefundisha soka kutokana na timu ipi mnakwenda kucheza nayo!kwenye kikosi hiki simuoni hata mmoja aliyekuwa first 11 kama vile golikipa Juma pondamali na golikipa wa akiba Athuman Mambosasa,simuoni beki namba 2 aliyeifanya namba hiyo kama mali yake binafsi Leopado Tesso Mukebezi,ila nimemuona Ahmed Amasha lkn sijamuona pia beki zote za kati za mwaka 81 zilizokuja kuitwa kama "viva surulele"ambao ni beki 4 Mohamed Bakar Tall,Jellah Mtagwa na kiungo wa nyuma mkabajiolf Richad
Hapo pia hayupo hata kiungo mchezaji Ezekiel Gryson Jujuman,wala mshambuliaji wa kati Juma Salum Mkambi!
Hiki kikosi hakina hata nusu ya uwezo wa kukifikia kikosi cha 81 kwani kikoso hiki kaka Michuzi kilitutia sana aibu Kenya mwaka 84 kw akushindwa hata kuvuka round ya kwanza hasa pale wakenya akina Bob John Ogolla,Josephat Mulila,Mike weche,Gab Orang,ambrose Ayoyi,Peter Ouma Jakaranda,Jj masiga walitufanya "kama ngoma yao"
Duh!!! kumbe kuna kuzeeka nhee!!!!!
ReplyDeleteMimi nilidhani nitabki kijana siku zote!!! La haullahh!!!!. Kumbe ule wimbo unaosema ''vunja mifupa kama bado meno ipo x2'' haujakoseaaaaa!!!
wadau mimi nilipendezwa sana na majina ya wachezaji wa zamani kama:athumani juma chama,hamasi kinye,abedi mziba,juma pondamali,omari husseni,malota soma,ahmed amasha,piter tino,zamoyoni mogela,hamisi tobias gaga,adolf rishad,mohammed bakari tall,daud salum,juma buruhani,kiwelu mussa,juma mkambi,makumbi juma barwan,hussen masha,yaani haya majina hata watangazaji wa mpira wakiona raha sana kuyatamka.mdau uk
ReplyDeleteMzee Kawawa anaonekana kijana kuliko huyo "kiongongozi mwingine wa chama na serikali" aliyekaa kulia. Sasa sitaki kusikia utani kuwa naye alikuwa mchezaji...
ReplyDeleteSHEBBE EL JEIZAN, KWAKWELI UNANIACHA HOI KUTAJA MAJINA YA WACHEZAJI MUDA WOTE KWENYE BLOG YA JAMII ITABIDI NIKUTAFUTE MAANA UKO MAKINI MNO KWA KUWAJUA KWELI WEWE ULIKUWA SHABIKI KUBWA LA SOKA WATU KAMA NINYI NI HAZINA YA TAIFA LETU KWA WAPENDA MICHEZO.Swali langu binafsi uko wapi kwa sasa?
ReplyDeleteMdau Msolopogazi USA
Mzee Shebe El Jeizan unadata kweli na wengine mna data nzuri sana pia lakini ukweli unabaki palepale timu ianzie chini kwenye grassroots angalieni wakati wa Yanga Kids kwa hiyo turudishe michezo ya sekondari mfano mzuri Marekani wacheza Basket wote na American Football wanatokea mashuleni!!!Hakuna short cut.
ReplyDeleteNawashukuru Wote,Mimi Nipo Njiani naelekea Z,bar ila Napatikana Kariakoo,DSM Bahati nzuri sijisifu Ila Nimejaaliwa Hazina Kubwa ya Kumbukumbu, Ninazo Sababu Zinazonifanya nibaki Na kumbukumbu za Mchezo huu Sio Tu Katika Soka la Hapa nyumbani ila kote kuna Duniani.
ReplyDeleteKaka zangu watatu Walionitangulia Waliniachiz maktaba Kubwa ya majirida Mbali Mbali ya michezo,Kisha Wao wakatowekea Ughaibuni Majirida niliobahatika kubakia Nayo Enzi hizo 1980 ni Kama,Shoot,Tiger,Roy And The rover Bingwaa,Sports Scene,Mshindi na Mengineyo Napatika katika email chimoahmed@gmail.com
SHEBE EL JEIZAN HATUKUWEZI KWA DATA MAKINI UNAZOTOA. NILIKUWA NASUBIRI UMTAJE NA YULE MZANZIBARI HODARI WA MASHUTI MAKALI- THUWEIN ALLY MAANA NA YEYE NAKUMBUKA ALIKWENDA LAGOS NA NI MMOJA YA WACHEZAJI WALIOIFUNGA ZAMBIA MBELE YA MZEE KAUNDA.
ReplyDeleteNdugu Shebe El Jeizaan, hicho kipaji chako ni vyema ukakitumia vizuri na usiwe unaibuka ghafla na kupotea. Ikiwezekana wasiliana na vyombo vyetu vya habari ili wakuandalie kipindi ili tuweze kukuona na kufaidi hazina kubwa ya kumbukumbu ulizonazo kwa faida ya Taifa zima. Inaonekana hata wimbo wa Taifa unaweza kuuimba usingizini eeeh!!!! Big Up El Jeizaan.
ReplyDeleteNdugu Shebbe je una habari ya yule kocha wetu wa zamani Mohamed Msomali yuko wapi kwa sasa??
ReplyDeleteKUMBU KUMBU YA SIFA ZOTE !!!
ReplyDeleteMdau Shebbe El Jeizan sielewi unajishughulisha na shughuri gani
lakini ni wazi ni mmojawapo wa wazalendo wanaopenda maendeleo ya
TAIFA STARS kufikia kile kiwango
tunachokingojea kwa mda mrefu.
Kumbu kumbu zako zinastahiri sifa zote,ingawaje siwafahamu wachezaji wengi kati ya hao maana msimu wangu
ulikuwa 1970`s enzi za kina Sunday Manara,King Kibaden,Willy Mwaijibe kumalizia 1980 kikosi cha kina Adolf Rishard kilichotupa furaha za
kutuwakilisha GHANA.
Vijana wetu wa Taifa Stars ya sasa
wana kila kitu kiutaalamu kuanzia matayarisho kupitia VIDEO/TV na Media/mtandao katika upande wa michezo,hata hivyo hawajatupa furaha za kufikia kiwango cha kimataifa.
Ukilinganisha na zamani wachezaji walitumia kipaji cha kuzaliwa pekee na kusoma magazeti siku ya pili yake baada ya mchezohamna TV/VIDEO wala mtandao wa michezo,
lakini wakati wote walitupa furaha.
Kama Maximo na Waalimu wetu nchini wakiondoa mzizi wa fitna na majungu
na kupeana maoni ya kimsingi kwa TAIFA STARS kucheza kwa pamoja ndani na nje ya mchezo,tutapata furaha za ushindi wa kimataifa.
mickey@mail-online.dk
DENMARK
Asanteni Ndugu Zangu, Jibu Kocha mohammed msomali yupo mjini morogoro na anapatikana mtaa Wa Kingo,Baada Ya mara ya mwisho Kuacha kuifundisha Timu ya Moro United(Zaragoza).Kuhusu Thueni Ally Kweli ni Mshambuliaji aliekuwa akisifika kwa kutumia guu lake la Shoto kuachia Mashuti Makali Lakini Mu-unguja huyu pamoja na shaaban Ramadhan"kichwa"(KMKM) Innocent Haule(Miembeni/SSC)Ramadhan Koroshen(KMKM)Saleh Hija(Yanga)hawakuwa wakitumiwa katika timu yetu ya Bara zaidi waliitwa katika timu ya taifa "Taifa Stars"Na Thuwen kweli alikwenda Nigeria 1980 Akiwa na kina: pondamali,Salim Amir,Mohammed salim,kajole,Tenga,Jellah,Mkambi,Tino,Amasha,
ReplyDeleteDaud Salum,Tasso,na Mkambikatika mechi nitakayomkumbuka Zaidi Thueni ni ile Tulipoichapa Kenya"Harambee Stars" 5-0 kuiondoa kwa (Agg 6-3)kinyang'anyiro cha kufuzu mundial espana 82 (Kombe la dunia)alifunga mabao(2)Tino(2)Adolph Rishard(1)Magoli yote,Thuwen Alipiga DONGO mpaka kocha wa Harambee Stars Siku hizo nashon Mulwa alikosa cha Kusingizia mahmomud abbas Alienda nyavuni mara 5
wachezaji kama elisha John,Justin Simfukwe,Said John.
ReplyDeletebaadaye wakaja kina Said MWAMBA KIZOTA.
MTAALAM TUPE VIKOSI VYA SIMBA NA YANGA 1985 KWENDA HADI 1993.
Nani aseme jina Amasha lilitoka wapi?
ReplyDeleteAhmed Abdul "Amasha" Beki Mahiri Wa kushoto au Full beck Left alitokea Tumbaku Tabora akijiunga Na Dar Young Africa 1980 Akiwa Kiungo Mkabaji Lakini Akabadilishwa Nafasi Hiyo Ktk timu ya Taifa Na Kupewa Nafasi Ya Beki Wa Kushoto Na Kocha Wa Zamani Wa Mabingwa Wa Ulaya SV Hamburg ya Ujerumani (Magharibi ) Siku Hizo Rudi Guterndorf Baada ya Kuona Kuna Viungo Wengine Wazuri Wakati Huo Kama Nicodemus Njohole Charles Boniface na Adolph Rishard Jina Halisi La Amasha Linatoka Kwa Kiungo Mahiri Wa Zamani Wa Timu ya Taifa ya Misri The Pharaos, Ahmed Ramadan Amasha
ReplyDeleteyaani me ni mcheza mpira wa sasa ila mtu alienivutia mpaka leo hii watu wananipenda kutokana na ubora wangu ni kutaka kufikia kiwango alichokuwa nacho salum mwinyimkuu carlos,yaan asikwambie mtu ile middle acha haina masihara nampenda na nataka kuwa km yeye siku za usoni.......coz ni babu yangu............salum said mwinyimkuu..
ReplyDelete