timu zikingia uwanjani na kipute kimeshaanza dakika kumi zilizopita kati ya taifa stars na vancounver white caps wanja jipya la neshno. hadi sasa bao ni 0-0 na wanja liko wazi kwa kile kinachoaminika kwamba mashabiki wote wako vibandani kuangalia gemu letu na mani yu ambalo nasikia refa keshatoa penati ya urongo. lakini el nino kakomboa boa hahhaaa!
na tayari gerrald kichafanza mambo. na bado... ngoja haftaimu iiishe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Kwa kweli inabidi turekebishe lishe tuwajaze upaja wachezaji wetu. Hii noma.

    ReplyDelete
  2. Barclays Cup Premier league England latest news:

    Wanja la Old Trafford jijini Manchester, ManUtd 1 Liverpool 3.
    Vidic wa ManUtd kala kadi nyekundu na mpira bado dakika 14 kuisha.

    Liverpool wanaelekea kuvunja mwiko uliowashinda Inter Milan jumatano ktk wanja la old Trafford.

    ReplyDelete
  3. BWAWA LA MAINI LINAONGOZA HADI SASA KWA 3 HUKU MAN U WAKIWA HOME NA KIFUTIA MACHOZI 1.....Bado dakika tatu mpira uishe....Naona Michuzi full furaha

    MAKULILO Jr,
    www.makulilo.blogspot.com

    ReplyDelete
  4. hahahahahahahaha Bao la Nne sasa, watu weweeeeeee dakika ya 90 Mh Balozi Michuzi Galiiiii kali kinoma...Ngoja nao MAN U wapigwe kama Madrid hapo


    MAKULILO Jr,
    www.makulilo.blogspot.com

    ReplyDelete
  5. Man U wamekunywa goli 4 na mpira umekwisha...

    ReplyDelete
  6. Vipi hapo neshno? Taifa Stars changa imeibuka kidedea? Nani ana listi?

    ReplyDelete
  7. BWAWA LA MAINI OYEEEEEEE HONGERA SANA HN.BAROZI WA ZAINI KWA USHINDI WA 4-1

    ReplyDelete
  8. Wadau mniwie radhi kwa kujirudia: panapo ukweli uongo hujitenga.
    Old Trafford Man U 1 Liverpool 4. Liverpool wamekuwa wageni wabaya na kuwapa kipondo cha mbwa mwizi Man U.

    ReplyDelete
  9. Barclays cup premier league England , matokeo ya mechi iliyo isha hapa Old Traffor jijini Manchester.

    Liverpool leo, imetoa kichapo cha rekodi kwa ManUtd, ambacho Sir Alex Ferguson hajawahi kukipata hapo Old Trafford toka kwa Liverpool FC, baada ya Liverpool kupata magoli 4 dhini ya 1 la ManUTD.

    Bao pekee la ManUTD lilifungwa kwa penalti na Ronaldo dakika ya 21 ya mchezo. Wakati mabao ya Liverpool yalifungwa na Torres dakika ya 28, Gerrard dakika ya 44 kwa penalti, Aurelio kwa free-kick dakika ya 77 na Dossena dakika ya 90 ya mchezo.

    ReplyDelete
  10. Wauzaji wa pombe za kienyeji(mataputapu) wa kule uwanja wa fisi leo watapata hasara kwa sababu wateja wao 95% ni washabiki wa Man United na leo wamejifungia ndani kuogopa kuchekwa.
    Teh!!!!!Teh!!!!!Teh!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  11. Maximo ajifunze kwa liverpool kijana Steven Gerrald ana kesi mtaani.lakini uwanjani anafanya vitu vyake.maximo utasikia nidhamu ndani na nje.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...