Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Meja Jenerali Mstaafu Said Kalembo, ( kulia) akifurahia jambo kati yake na Msimamizi wa kituo cha Soko kuu la Morogoro cha kupigia Kura za maoni ya watu wanaotuhumiwa na mauji ya Albino, vikongwe pamoja na dawa za kulevya na Ujambazi, WP Jamila ( katikati). Shoto  ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Mogorogo, Raphael Ndunguru. Hadi viongozi hao wanafika kituoni hapo milango ya saa nne na nusu hakuna kura iliyokuwa imepigwa.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Meja Jenerali Mstaafu Said Kalembo  akimsikiliza Ofisa Mtendaji wa Serikali ya Kijiji cha Gwata, Wilaya ya Morogoro, Salehe Mangala ( kulia) kuhusiana na jinsi ya idadi ya watu 30 hadi kufikia mchana jana  walivyoweza kuitikia wito wa kupiga kura za maoni kwa wauaji wa maalbino, vikongwe na wale wanajihusisha na dawa za kulevya na ujambazi. Kijiji hicho kina jumla ya wakazi 2,110.

Picha na habari na John Nditi, Morogoro
 
WAKAZI  wa Mkoa wa Morogoro wameshindwa kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono Serikali katika zoezi la  kupiga kura za maoni kwa ajili ya kuwafichua wauaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi ( maalbino) , vikongwe, wazalishaji, wauzaji, wasambazaji na watumiaji wa dawa za kulevya na majambazi wa kutumia silaha.
 
Haya  yamebainika katika ziara ya Mkuu wa Mkoa huo, Meja  Jenerali Mstaafu, Said Kalembo  jana  wakati alipovitembelea baadhi ya vituo vya kupingia kura hizo katika Halmashauri mbili za Wilaya ya Morogoro.
 
Ziara hiyo iliyofanyika majira ya saa nne asubuhi ya siku ya upigaji wa kura hizo, akiambatana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Said Mwambungu, katika kituo cha Soko Kuu la Morogoro lenye mkusanyiko mkubwa wa watu hapakutokea mtu hata mmoja kuweza kupiga kura hizo.
 
Hata hivyo katika kituo kilichopo shule ya Msingi  Msamvu, Manispaa ya Morogoro hadi muda huo ni watu sita tu waliweza kujitokeza kupinga kura hizo , ambapo katika kituo cha Kihonda mtu mmoja alikuwa ameshapiga kura hizo.
 
Hata hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, katika vituo vyake viwili watu waliweza kujitokeza hasa  katika kituo cha Gwata,ambapo  idadi ya watu 30 walipiga kura zao za maoni hadi mchana wa siku hiyo.
 
Kituo kingine wambacho kilitembelewa na Mkuu hiyo wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ni  cha Kitongoji cha Kiroka Soweto ambapo idadi ya watu saba walijitokeza kupiga kura hizo za maoni hadi muda huo.
 
Ofisa Mtendaji wa Serikali ya Kijiji cha Gwata, Salehe Mangala, alisema  mafanikio hayo yalichangiwa na viongozi wa serikali ya kijiji na Diwani wa Kata hiyo kuwahamasisha wananchi uhumimu wa upigaji wa kura hizo za maoni.
 
Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji huyo, Kijiji hicho kina jumla ya vitongoji vitano na idadi ya wakazi ni 2,110 na kujitokeza kwao kutaisaidia Serikali kuwabaini waharifu hasa wa ujambazi na dawa za kulevya.
 
Naye Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kihonda, Manispaa ya Morogoro, Winfrida Chausi, alisema kushindwa kujitokeza kwa wingi wa wananchi wa eneo hilo kupiga kura za maoni kumetokana na wengi  wao kwenda katika  shughuli zao za kibinafsi na hivyo kusubiri nyakati za alasiri.
 
Mkuu wa Wilaya hiyo, Said Mwambungu, alisema takwimu za idadi ya  kura hizo za maoni zitatolewa wakati muafaka mara baada zoezi hilo kamilika katika  vituo vyote vya Halmashaui ya Wilaya na Manispaa.
 
Naye Mkuu wa Mkoa huyo, alisema ingawa  idadi ya waliojitokeza kupiga kura hizo za maoni si wengi,  lakini kwa  uchache wao , kura hizo  zitaisaidia Serikali kuweza kufanya uchambuzi na uchunguzi wa kina  kuwabaini wahalifu ili wawezekuchukuliwa hatua za kisheria.
 
Hata hivyo alisikitishwa kwa kuona wakazi wa  Manispaa ya Morogoro  waameshindwa  kujitokeza kutumia nafasi hiyo,  licha ya Mkoa kutokuwa na matukio ya mauaji ya maalbino na vikongwe.
 
Hivyo alisema wananchi hao walikuwa na fursa ya kutumia siku ya zoezi hilo kuweza kuwapingia kura za maoni wa  uharifu wengine wanaowafahamu  hasa wale wa naojihusisha na   dawa za kulevya pamoja na ujambazi wa kutumia silaha.
 
“ Mkoa hauna historia ya mauaji ya maalbino wala vikongwe …lakini tatizo la ujambazi linaweza kuwepo hasa kwa wale wanaotokea Jijini Dar es Salaam na kujificha Mkoani mwetu  hivyo kura zao za maoni zingweza kuisaidia Serikali “ alisema Kalembo
 
Mkoa wa Morogoro katika zoezi hilo ulijumuishwa katika Kanda ya Mashariki wenye Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam, ambapo  vituo 1,959 viliainishwa katika kila Wilaya  na kukadiriwa zaidi ya  watu 927,593 kushiriki zoezi hilo la upigaji kura za maoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. hii imekaa vizuri,inamaanisha kama huyu anapiga kura , alikuw anamhisi mharifu mmoja wapo wa makundi hayo matatu,swali la kujiuliz ani kwamba naye alisubiri hadi itokee chance hii ndo aact, au hapo wanatuzuga. bahati mbaya wanasiasa wanakasumba ya kuchangany ishu serious na siasa. kimtazamo zoezi lote ni kama linapoteza mwelekeo.

    ReplyDelete
  2. HIVI KARIBUNI RAISI ALISIKIKA AKISEMA ANAYO MAJINA YA WATU WANAOKWEPA KULIPA KODI, SIJUI NA YEYE ANASUBIRI SIKU YA KUPIGA KURA ZA WANAOWAFAHAMU WAKWEPA KODI NDIPO AKAWATAJE?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...