Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Kept.John Chiligati akimwonyesha hati miliki ya ardhi ya kimila (certificate of customary right of occupancy) Waziri wa Ardhi wa Namibia Alpheus Naruseb wakati alipotembelea kijiji cha Mitengwe wilayani Kisarawe leo kwa madhumuni ya kujifunza Mipango ya Ardhi inavyoendeshwa nchini. Kulia ni Afisa mipango miji wa Namibia Lelley Nullike akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Namibia Ludwina Shapwa.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Kept.John Chiligati (kulia) na Waziri wa Ardhi wa Namibia Alpheus Naruseb (kushoto) wakikagua jengo la masijala ya ardhi ya kijiji cha Mitengwe wilayani Kisarawe wakati wa ziara yake ya kujifunza mipango ya ardhi kijijini hapo.Picha na Zawadi Msalla wa Maelezo



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. kaka mmepoteza muda wenu cuz mtaondoka na pumu na mafua kutokana vumbi la hayo mafaili hawa watu lini wataanza kukeep data kwenye computer...hii fedhea hadi makao makuu ya wizara karibu zote bado kuna makabrashi kama hayo...vinatia uchungu

    ReplyDelete
  2. Anony wa juu uko very right. Hawa jamaa walikosa nchi nyingine ya kwenda kujifunza? Pole yao kwa kupoteza muda kwa kweli mbona noma?

    Unazungumzia kucomputerize data za Kisarawe lini leo? Hizo ni ndoto kwa sasa. Juzi nimeenda kuomba residence permit idara ya kazi nusura nilie maana mlangoni chini kwenye floor nilikaribishwa na mafile kibao. Hawa jamaa kuomba na kurenew permits ni kitu kimoja kwani hawawezi kutrace back records za nyuma. So unaporenew ni kama vile unaomba upya. Yaani ni aibu mpaka basi na hiyo ni makao makuu ya wizara na ni very sensitive office haiko computerised sembuse huko kisarawe. We have a long way to go.

    ReplyDelete
  3. Mafaili yakiondoka ina maana ulaji tena hakuna. Maana hua unaambiwa makusudi kua faili lako halionekani lakini toa kitu kidogo tuu hata linapoibukia hujui!!!.

    ReplyDelete
  4. Tanzania Tambarare!
    We unaongelea kisarawe??? Airport Dar unapoingia na mzigo wakitaka kukucharge tax zao lazima wafungnue mavijitabu yao kureffer, sasa ikiwa hapo hawajaona umuhimu wamatumizi ya computer itakuwa kisarawe??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...