Mkurugenzi wa Benchmark Ritah Paulsen (katikati)akiongea na waandishi wa habari kuhusu shindano la kuwasaka nyota Bongo Star Seach(BSS)kwa mkoa wa Dares Salaam zoezi hilo litafanyika jumamosi hadi jumapili katka ukumbi wa World cinema.(kushoto)Meneja udhamini wa Vodacom Emillian Rwejuna na kulia ni Meneja Mawasiliano Nector Foya wa Vodacom Tanzania ambao ni wadhamini wakuu wa Bongo Star Search.
Shindano la kuwasaka nyota wa Bongo Star Search (BSS)kwa mkoa wa Dares Salaam litafanyika jijini Dares salaam Jumamosi na Jumapili wiki hii katika ukumbi wa World Cinema ambapo washiriki 2000 wanategemewa kujitokeza.

Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nector Foya alisema Jijini jana kwamba sasa ni zamu ya Mkoa wa Dar kusaka vijana wenye vipaji vya uimbaji hivyo vijana wa mkoa huu hawana budi kujitokeza kwa wingi.

Alisema shindano hili limeshafanyika katika mikoa mbali mbali ikiwemo Zanzibar na kwamba sasa ni zamu ya vijana wa Dar es Salaam.

“Natoa wito kwa vijana wa Jijini hapa kujitokeza kwa wingi,” alisema.
Alisema mwaka huu Vodacom Tanzania imedhamini kwa mara ya kwanza shindano hilo na kwamba litakuwa bora zaidi.

Alisema mbali na kuonyesha vipaji vyao, vijana pia watajishindia zawadi mbalimbali kutoka kwa Vodacom Tanzania.

“Ni matumaini yetu kwamba baada ya kujisajili kwa wingi washindi wataweza kuingia katika ulimwengu mpya wa muziki na kuweza kujiajiri katika fani hiyo kwa siku za usoni” alisem.

Nae Mkurugenzi wa Benchmark Rita Paulsen alisema anatoa wito kwa vijana kujitokeza kwa wingi ili waweze kujipatia njia pekee ya kuweza kujiendeleza katika maisha ya mziki katika maisha yao yawe bora.

“Tumekuwa tukifanya hivyo kwa kuamini kwamba sekta hii ikitumiwa vizuri inaweza kutoa nafasi nyingi za ajira kwa vijana na hivyo kupunguza wimbi la umasikini” alisema


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Huyo demu wa kulia analipa saana.

    ReplyDelete
  2. To the very Right is Nector Pendaeli Foya-manager wa mawasiliano Tigo...I am so proud of you Nector, you are doing a great job..Keep up the good work.

    Mdau-USA

    ReplyDelete
  3. nawe mdau -usa ebu acha uongo wa kitoto. wewe unajuaje kama foya anafanya kazi nzuri? hizi kampuni za simu hadi cleaner anaitwa meneja usafi!

    ReplyDelete
  4. ni kweli kabisa huyo mdau wa USA hajui anachokisifia coz huyo dada kwa maelezo hapo juu yupo VODA

    ReplyDelete
  5. OI stay corrected anafanya kazi Voda sio Tigo...na hakika najua Mrs Foya ana masters degree so hawezi kuchimbuka kitabu namna hiyo aishie kufanya kazi ya kusafisha...and please wewe hapo juu acha wivu, mwenzako akipata mfurahie na wewe utapata siku moja...Mungu ndo mgawaji acha roho ya kwanini jamani////mmmmm

    Mdau-USA

    ReplyDelete
  6. wivu tuuu
    msione totoz za kike ziko juuu basi udelele ni mitusi tu

    grow up yu "||\\++#&&*

    ReplyDelete
  7. we mdau - usa kwani ukikaa kimya itakuwaje? hujuwi kila fani inaweza kusomewa hata kufikia phd? acha upambe manake kuna kusoma na kuelimika. ndio nyie mnaosema hamrudi tz eti kisa mtakosa vyeo na digrii zenu za kuunga-unga.

    ReplyDelete
  8. Huwezi jua labda Mdau-USA ni bosi wa Voda ndio maana anasifia utendaji wa Foya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...