Mambo vp Mdau,
Kwanza hongera sana kwa ushindi wa kubahatisha juzi kama walivobahatisha wenzenu Man jana!!

Nakuletea taswirazz ya 'DARAJA LA MUNGU' ambalo linapatikana maeneo ya Kiwira, wilaya ya Rungwe, mkoani Mbeya ambapo jana nilikwenda 'kutalii'. Inasemekana kwamba daraja hilo (Geographical feature) halipatikani sehemu nyingine yoyote duniani!!

Kazi njema
Haidar Chamshama

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Kazi nzuri sana ndugu mdau uliye post hii taswira, ila kuna mengi ambayo ugeweza kutufahamisha, nahamini ni moja kati ya kivutio kikubwa kwa watalii hata sisi wazawa. Sidhani kama sirikali yetu ilisha fikiria kama kuna uwezekano wa kupatikana kwa ajira ya kudumu kwa agalau hata wazawa 10 katika kivutio hiki. Mdau nakuomba ukae chini utupe tahrifa kamili ya mto kiwira na hiyo taswira,kiuchumi na mazingira(geographically).
    keep up the good work.

    ReplyDelete
  2. Hongera saana Chamshama kwa kazi nzuri.Hapo mahala nimefika na juu yake (upstream) kuna maaajabu mawili.
    1 DARAJANI -mto woote unapita katika eneo finyu sana hivyo kusababisha upepo wa ajabu, upepo huo hapo zamani ilifikiriwa kuwa ni mizimu inayomnyonya mtu na kumtumbukiza mtoni hadi kwenye bwawa.

    2 CHUNGU CHA MUNGU-kama nusu kilometa juu(Upstream) kuna chungu kikubwa sana ambamo nusu ya mto hutumbukia humo na kuibukia sehemu nyingine

    Watanzania, watalii karibuni Rungwe

    ReplyDelete
  3. Asante sana mdau uliyepost hii picha. Umenikumbusha 2002 nilipotembelea mkoa wa Mbeya na kujionea vivutio vya utalii vilivyopo. Ungepiga picha na kile chungu hapo pembeni ya hilo daraja ambapo ktk hicho chungu maji yanazunguka.

    ReplyDelete
  4. samahani kaka haidar chamshama ni ndugu wa mahmoody chamshama au vipi maana naoana kila kona mpo ....kama kweli kila la kheri kweli msure kafanya kweli simbaaaa oyeee angali tunafungwa

    ReplyDelete
  5. shukrani mdau, taswira nzuri sana, imependeza. Inafurahisha sana kuona watanzania tukitalli nchini kwetu na kujionea mengi ya kupendeza.

    Ila naomba nirekebishe kauli ya mdau; sio kweli kuwa Tanzania ni sehemu pekee yenye daraja la asili kama hili. Mfano angalia hii hapa:
    Natural Bride, VA

    ReplyDelete
  6. Duh! umenikuna, piga picha na kijungu basi maana kama huamini uwepo wa Mungu basi hapo ndo pa kwenda

    ReplyDelete
  7. R.I.P.Shamsu and Shafin Jadavji...perished here in 1976!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...