Mkuu wa Majeshi Jenerali Davies Mwamunyange akijiorodhesha kwenye Kitabu maalum cha Wageni katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania-London.

Mheshimiwa Balozi wa Tanzania Uingereza, Mama Mwanaidi. S. Maajar akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania Jenerali Davies  Mwamunyange.

    Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Mwanaidi. S. Maajar (chini shoto) na Mkuu wa Majeshi Tanzania Jenerali Davies  Mwamunyange. Nyuma toka shoto ni  Capt. CA Ng’habi, Col. P.Mrope, Bwana David Nginilla, BG. PI Mella, Bwana Kiondo, Dada Caroline Chipeta, Bwana, Idrissa Zahran, BG. KG. Msemwa, Bwana Sylvester Ambokile, LT. AP Mutta, na Bwana Othman Mashanga. 

Mkuu wa Majeshi Tanzania, Generali D.A. Mwamunyange, akiongozana na baadhi ya wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama,jana alitembelea Ubalozi wa Tanzania-London na kukaribishwa na kupokelewa na Mwenyeji wake Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mama Mwanaidi. S. Maajar, Mwambata wa Jeshi la Tanzania hapa Ubalozini, Col. P. Mrope na maofisa wengine wa Ubolozini hapo. 

Akiwa kwenye Ofisi hizo za Ubalozi, alielezea kwa kifupi hali halisi ya Ulinzi na Usalama wa nchi yetu ilivyo na muhtasari ya safari yao iliyoanzia nchini Marekani, Canada na hapa Uingereza.  Madhumuni makubwa ni kujifunza na kukuza ushirikiano wa Kiulinzi na Usalama kati ya nchi hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. ziara hizi ni nzuri na naamini zitaleta changamoto kiutendaji ndani ya jeshi letu la wananchi (JWTZ),naamini wakubwa wana upeo na exposure ya kutosha kufanya mambo ya kisasa zaidi.ushirikiano uzidi na wajeshi wetu watoke kwa wingi,iwe mafunzo,ulinzi hata tour!!-itaongeza standard kwa nyanja zote-wakubwa fanyeni iwezekane...!!!
    "mwanakijiji"

    ReplyDelete
  2. Hi,dada Caroline habari za siku nyingi nimie bibi yako wa Kimara email:batamwarwamugila@yahoo.com msalimie Victor pamoja na mjukuu wangu Lulu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...