beyonce akiwa mitaa ya kati mwananyamala
kuna wadau huko ughaibuni wanabishana eti siku Jay Z na Beyonce walipokuja bongo hawakukanyaga uswazi. Hapo ni mwananyamala ambapo anaonekana jigga akimtwika mama ndoo ya maji baada ya kuzindua bomba jipya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. tena hapo mdau kuna picha zingine bibiye Beyonce kavishwa khanga na akacheza nayo ngoma vilevile..........

    ReplyDelete
  2. HAYA SASA ONA, WAKATI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI CCM HUTUAMBIA WATU WOTE DAR WANAPATA MAJI SAFI YA BOMBA NASI HUWA TUNASHANGILIA UONGO HUO, UKWELI WAKAZI WA DAR HUPATA TAABU YA MAJI KAMA WALIVYO WAKAZI WA VIJIJINI, PICHA INADHIHILISHA HILI KWA WANAMUZIKI TOKA NJE KUJA KUTUWEKEA BOMBA LA MAJI YASIYO SALAMA AMBAYO GHARAMA ZAKE NI NDOGO SANA KULIKO KUNUNUA KRETI LA BIA! VIONGOZI TUNAOWACHAGUA NI KWELI WANATUFAA?

    ReplyDelete
  3. michuzi vipi bana,ugaibuni watabisha vipi wakati mawasiliano yako huku.mtu anayeweza bisha ni mtu wa nyumbani kwani mawasiliano zero

    ReplyDelete
  4. and your point is........

    umewahi kusikia PR wewe?

    ReplyDelete
  5. PETER NALITOLELAApril 17, 2009

    MKUU WA NANIHII, MIMI NATUMA ZA RAMBIRAMBI KWA MT. YOHANNA MASHAKA NIKITUMAI HAJAMBO HUKO WOSTRITI MEREKANI. KWANZA MIMI NASHANGAA KINJE ALIFUATA NINI KWENYE HIYO TOUR SASA YEYE NI CELEBRITY WA NINI KUSEMA KWELI? YOHANNA MASHAKA, MIMI NINAKUHITA HUJE HUKU MUZUMBE UNIVESITY TUCHAMBUE MASWALA KWA MAANA ULIMUOGOPA YULE NDUGU YANGU WA OKFODI A.K.A US-BLOGGER. MIMI NAKUSUBIRI NA MADA HADI MADA KWA HIYO NJOO USIOGOPE KAMA KWELI ULIKANYAGA UMANDE. WEE KAMA RAIS MTARAJIWA 2015, SIONI SABABU YA KUTOKUHUDHURIA KWAKO. KAMA NI NAULI BASI NDUGU YANGU US-BLOGGER PEDEJEE ATAKUPA NAULI ILI UJE KWENYE MDAHALO. MIMI NASHANGAA NI KWA NINI HADI LEO WATU WENGI WANAKUABUDU KAMA MUNGU.

    MT. YOHANNA MASHAKA, SASA WEWE KAA MKAO WA KULA KWA MAANA MIMI NA US-BLOGGER VILE VILE TUNAANZA KUANDAA MADA NYETI YA KUWEZA KUKUDHIHIRISHIA KWAMBA KIINGELEZA TUNAKIJUA VIZURI NA NI WASOMI WALIOBOBEA NDUGU YANGU. USITUONE KAMA VILE HATUJASOMA, MUZUMBE UNIVASITI IS GRAET KOLEJ. NA TUNAKUKANYAGA NA UCHAMBUZI WAKO WA WALSTRITI AMBAO NASIKIAGA KWENYE BBC. SISI TUNA DATA NYETI ZAIDI YAKO, PAMOJA NA MSANI MOKES GAMA AMBAYE NI SENENE CHIPUKIZI

    ReplyDelete
  6. Wadau hili ni swali la kizushi tu, hivi Kinje ni celebrity wa nini?

    Asanteni.

    ReplyDelete
  7. Mbona huyo mtoto ni mkubwa sana kubebwa mgongoni?

    ReplyDelete
  8. Unauliza embe kibada? Kinje ni celebrity kwa sababu anamiliki bar maharufu mjini Rose garden..

    ReplyDelete
  9. mi naskia Kinje alitoa vogue sports lilo-mbeba jz na mwandani wake beyonce

    ReplyDelete
  10. Kama kweli Muzumbe ni chuo cua vimeo na vihiyo, Peter Nalitolela ni kimeo kweli.

    yaani amemvaa john mashaka utadhani ni demu anayemtaka mashaka uchumba. Man peter nalitolela get a life. Hacha kumkashifu mwrnzio.

    Mashaka ni matawi ya juu utahifananisha naye wewe bwege? Watu wengine bwana nawashangaa sana. Mashaka chunga kuna manka wanaume mheshimiwa

    ReplyDelete
  11. Mtoto mkubwa!!!! Umemzaa wewe?

    ReplyDelete
  12. Pole sana mdau toka Dodoma pole na vumbi. Ulikuja dar mara na kurudi ndio maana ulisikia majina mawili tu. ROSE GARDEN na KINJE. Ukaunganisha. KINJE HAJAWAHI KUMILIKI BAR HIYO. Ahsanteni

    ReplyDelete
  13. kwani hapo Hood ya Uswazi? Mwananyamala sehemu hiyo hapo si BAA tu na hapo maji bado tabu pengine au wanalipia kujak uchota Gelesha tu. wangeenda MIkoani ndani ndani kusipokuwa na MAJI kabisaaaaaaaaaa wala visima tabu ndio wangesaidia maji sehemu za Dar-es-salaa Vingozi kila kona ni Aibu maji watu kupata kwa tabu.

    ReplyDelete
  14. bongo gym maisha. huhitaji hata kwenda kwenye gym na maisha yetu haya. hebu angalia JZ pamoja na kupiga gym kila siku lakini ndoo inataka kumshinda. mwana mama hajui gym lakini kabeba mtoto mgongoni na anangojea ndoo kichwani. bongo tambarare saaaaaaaaana

    ReplyDelete
  15. afu ndoo yenyewe inayomshidna ni lita 10 tu!!

    angepewa lita 20? au lile dumu la maji??walhahi angeanguka chali!!

    kinamama afrika oyeeeeeee

    ReplyDelete
  16. mimi binafsi huyo beyonce cjamuelewa!kavaa kigauni cha nite wakati mchana jua linapiga la utosini to make matters worse walikuwa wamekwenda uswazi??lo!tuite ushamba au sasa wabongo na ulimbukeni wanaiga tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...