Mfalme wa Saudi Arabia Abdullah bin Abdulaziz Al Saud akiwa katika picha ya pamoja na Rais Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kumtunuku nishani ya dhahabu ya kama ishara ya urafiki kati ya Tanzania na Saudi Arabia
Mfame Abdullah bin Aziz Al-Amer wa Saudi Arabia akiwa katika mazungumzo na mgeni wake JK baada ya Dhifa ya kitaifa aliyomuandalia katika makazi yake ya kifalme huko Saudi Arabia(katikati ni mukalimani. picha na mdau Juma Kengele wa Ikulu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Mungu yape nguvu zaidi mawasiliano baina ya nchi mbili hizi na kuimarisha undugu wa dhati

    ReplyDelete
  2. Mola saidia yawe mambo ya heri tu si kututumbukiza katika utumwa "urafiki" wa utenganishi.
    JK kapewa na tuzo ya heshima ya kiarabu kwa utumishi mzuri nao..mh

    aiseee!!

    ReplyDelete
  3. Poor protocols, where is Tanzanian flag?

    ReplyDelete
  4. hi!JK wetu mungu mpe uimara zaidi,
    hapo naulizwa je mzee wa Tz unapenda kinywaji gani?JK wetu anasema hapana ni maji ya kawaida tu,hila anasisitiza uhusiano wa nchi mbili JK hoyeeee!!!!!!!eeeeeee

    ReplyDelete
  5. Hapo JK umecheza, huko ndiko kuna pesa zisizokuwa na riba. Wakikupa mkopo basi itakuwa neema. Unakopa mia unalipa mia si kama IMF.

    ReplyDelete
  6. Mungu tusaidie undungu usiwe wa kuwaumiza Watanzania ,kwa kutumia jina la misaada

    ReplyDelete
  7. Na yeye alibow. Mwenzake Obama alibow mbeye ya huyu King majuzi tu ouch! Na misaada hataki. Huyu itabidi apige magoti tupate shenene

    ReplyDelete
  8. Na bado itawauma saana mmesha anza iko wapi bendera ya tanzania maana ulietoa comment ulikuwa unajuwa hapo ni wapi mpaka ziwekwe bendera zote acha ujinga

    ReplyDelete
  9. JK Usikose kunywa zamzam tena kisimaniiiii,

    ReplyDelete
  10. Wewe Mtoa Maoni Tarehe April 16, 2009 3:26 PM,: Anonymous
    Hayo ni makazi ya kifalme, bendara ya Tanzania itatoka wapi?? Protokali, angalia sio zote zipo sawa. Kwa mfano lazima umwamkie huyu falme kwa kuinama, ila viongozi wengine mnapiga mkono na 'hi' kama Dully Sykes vile.

    ReplyDelete
  11. WASWAHILI HUWA TUNAFIKIRIA MISAADA TU HAKUNA JINGINE KWANINI TUSIJIAMINI TUKATUMIA RASILIMALI ZETU ZA NDANI KUFANYA MAENDELEO.NI AIBU KILA SAFARI ANAYOFANYA RAIS NI KUOMBA OMBA...TUTAJITEGEMEA LINI? HIYO MEDALI ALIYOPEWA RAIS NI NOBEL PRIZE AU? NI KWA AJILI GANI? ACCORDING TO REUTERS,INASEMEKANA JK AMEKUBALI KUWAPA EKARI NUSU MILIONI ILI WASAUDIA WAJE KULIMA NCHINI KWETU KWA AJILI YA KULISHA WATU WAO..JE HUO NI UWEKEZAJI? LABDA WAO WATATUPA ARDHI TUCHIMBE MAFUTA KWA AJILI YA WATU WETU? MNAONAJE WATANZANIA.NILIDHANI INGEKUWA VIZURI KAMA TUNGEWAUZIA MAZAO YA KILIMO AMBAYO WANAYOYAHITAJI KAMA MPUNGA NA NGANO BADALA YA WAO KUJA KULIMA NA KUPEWA LEASE YA MIAKA 99 KAMA ILIVYOELEZWA NA REUTERS JANA.
    INAONEKANA JK NA UJUMBE WAKE NDIO WALIANZA KUUZA IDEA YA KUWAPA ARDHI KWA SABABU ALIWAELEZA KUWA TUNA EKARI MILLIONI 40 AMBAYO HAIJALIMWA.SWALI LANGU NI JE KIZAZI CHETU KITANUFAIKAJE WAKATI ARDHI YETU INAPEWA WASIO RAIA KWA AJILI YA URAFIKI WAO TU(LABDA NDIO MAANA AMEPEWA HUO MKUFU)AU NDIO WATAKAOKUWA MANAMBA BAADAYE ARDHI IKIISHA MAANA NAYO POPULATION YETU INAKUWA.

    ReplyDelete
  12. We unayesema utumwa hujui utumwa ulifanywa na waarabu wasio waislamu, siku hizi warabu wamesilimu kwa hiyo hakuna utumwa.

    ReplyDelete
  13. Hawa wafalme wa Saudia wako wawili, maana naona majina yanayotofautiana, mara Alsaud mara Al ameir. Mwandishi kumbuka Saudia ina mfalme mmoja tu na wengine ni ma-prince. Au kwa jina la kiswahili mwana mfalme na sio mfalme mwenyewe.

    ReplyDelete
  14. msaada mbona umeshatolewa hiyo tuzo ya dhahabu tosha sana!

    ReplyDelete
  15. SAWA INGAWA HAUJA YALUSHA MAON YANGU LKN ULE NDIO UKWELI WA MAMBO. JK HANA LOLOTE ZAIDI YA MISAADA NA WALA SI MBUNIFU SIJUIN KWA SABABU MKWELE? AMEACHA BANDARI INALIWA NA WATU WACHACHE TU MBUGA , MAZIWA , ARDHI KUUUUUBWASANA. MADINI , MIFUGO,VYOTE HIVI TUNGETUMIA SAWASAWA TUNGEKUWA MBALI SANA. HIYO ARDHI BORA ANGEWAPA WA KEN UG,RWA,BUR , KUMBE ANAWAKATALIA HAWA NA KUWAPA WA SAUD , NIMEAMINI KUMBE SISI WA TZ WANALAANA SIJUI NI NANI ALITULOGA?SIJUI KWA SABABU TULIWAFUKUZA WAISRAEL? NAJARIBU KUTAFUTA MCHAWI SIONI.ANASHINDWA KUBUNI MAENDELEO NDIO MAANA KATIKA MIAKA YOYE 5 ALICHOFANYA NI SAFARI TUUU. MBONA HAENDI ISRAEL? TENA WALE SI WADINI TENA NI WATAALAMU KILA NYANJA. MBONA SERIKALI YETU INA MAHELA MENGI ? NINI LKN MISAADA SI MIZURI INA UTUMWA NDANI YAKE.TZ JITEGEMEEE MWENYEWE WAO WALIPATA WAPI MISAADA KAMA SI KUDHIBITI MAPATO NA KUYAELEKEZA KWENYE MAENDELEO?.MUNGU TUFUNGUE UTASHI SISI WATANZANIA TUWE WABUNIFU HASA VIONGOZI WETU. AMINA

    ReplyDelete
  16. sasa we umeanza matusi wakwele mnatukanwa sasa..maendeleo hayaji kwa miaka mitano kama wewe unavyofikiri mataifa yote tajiri yalijitoa mpaka kuua ili maendeleo yapatikane na watu wake walifanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya nchi yao sasa leo watz wapo wanayasubiri kupitia kwa kikwete tafuta maendeleo yatakuja sio kumlaumu kikwete umaskini wako unasababishwa na uvvivu wako wa kufikiri..unalala unamsubuli kikwete akuletee maendeleo huo ni ujinga mlionao watz wengi jitume komaa utaona maendeleo yanakuja bila wasiwasi zaidi ya hapo hata ashuke adam na hawa kwa akili yetu tutajua ndo wamekuja kutuletea maendelo na tutakaa tukiyasubiri..halafu wewe una udini kikwete kila kukicha anaenda marekani, ulaya leo kaenda saudia unaanza kuongea ujinga wa israel,akili yako fupi sana kama unaongelea plan ya kikwete basi ujue sio ya kuonekana papo kwa papo kama unavyofikiri..subiri maendeleo hayaji siku moja

    ReplyDelete
  17. WIZI MTUPU

    ReplyDelete
  18. Tunasoma historia ya kuwa zamani machifu walipewa shanga na vioo mengine wakabadilishana na dhahabu na pembe za ndovu na waarabu, hivyo basi isije ikawa huo mkufu wa dhahabu aliopewa kiongozi wetu akabadilishana kwa kutoa ardhi na maliasili za watz. Hawa viongozi wetu wa siku hizi ubinafsi mbele halafu wao wanataka wananchi wawe wazalendo wakati wao uzalendo ulishawashinda siku nyingi.

    ReplyDelete
  19. YAANI WEE ANNON 9.15 am UMENIGUSA SAANA TRUTH TUPU

    IVI KWANINI HATUENDI ISRAEL??KWANINI HATUNA BALOZI YAKE TZ??
    KWANINI TUOMBE-OMBE MISAADA KWA WATU?TENA KWA KUUZA ARDHI TULIOWAKATALIA WAKENYA??

    NYIE VIONGOZI NENDENI NCHI AMBAZO HAWATAKUWA NA MASHARTI YA KUUMIZA WANANCHI MISHARTI WEEE ADI LAANA TUPU.

    SERIOUSLY MTALIPA HII KUUZA NCHI NYIE NA VIZAZI VYENU VYOOOTE

    ni hayo

    ReplyDelete
  20. AHHA MZEE WA BLING-BLING SUPER MC...YOOOH

    ReplyDelete
  21. waislaeli wamelaniwa na mwenyezi mungu ndo mana hawana ardhi hapa duniani,hivi waislaeli wanatoka nchi gani? wao ni kuvamia tu hawana kwao.
    sasda watamlani nani wakati wao wenyewe wamelaniwa.

    ReplyDelete
  22. Wee Annon 1:40 am unajua unachokiandika au unaandika kwa sababu unatakiwa kuandika??? Aliekuambia Waislaeli(Waisrael) wamelaniwa na mwenyezi Mungu ni nani??? Fanya utatifiti/soma vitabu ujue historia ya Waisrael my friend...

    ReplyDelete
  23. ",,,ailaanie ISRAEL atalaaniwa,aibarikie ISRAEL atabarikiwa"

    kwa ufupi wee annon apo ushalaanika tayari...kasome vitabu na Bible uone history nani hana ardhi pale!!

    JK mamboz,saudia wana dhahabu swaaafi sana nazifagilia sana

    ReplyDelete
  24. Naomba kuliza swali Balozi.

    Marekani, Raisi na mawaziri wake hawaruhusiwi kuchukua zawadi kutoka kwa wageni na viongozi wenzao ili kudhibiti rushwa.

    Je, kuna mdau anajua sheria za Tanzania kuhusu hili swala? Je, JK atachukua hii zawadi ya nishani ya dhahabu au ataizawadia serikali akiachia ngazi ili isionekane kuwa amekula rushwa.

    Pia, kuna mdau aliyesema kuwa kuna dhahabu Saudia. Dhahabu hamna katika jangwa lao ila wananunua katika soko la dunia. Jangwa lao limejaaliwa mafuta na gesi lakini halina dhahabu.

    Mdau wa Tokyo, Japan

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...