JK akiwa katika mkutano na chemba ya biashara na viwanda wa Saudia

JK akitembezwa sehemu mbalimbali katika ziara yake rasmi ya siku tatu huko Saudi Arabia ambayo imehitimishwa leo.
msafara wa JK ukiwa njiani huku bendera zikipepea kila kona

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Michuzi bendera sio bule izo,watu wanapiga hesabu ya badae {LAND}

    ReplyDelete
  2. Mababu zetu walidanganywa na Karl Peters wakadanganyika wakaja kugundua baadaye.Kumbe bado tutaendelea kudanganywa hadi leo na uhuru tuliopata hautatusaidia kitu,Hapo ardhi imezungumziwa sana na wafanyabiashara wa Saudi Arabia na wana nia ya kulima mazao ya mpunga na ngano nchini kwetu kwa ajili ya kulisha watu wao,je sisi tutapata nini? Jamani watanzania angalieni tunakokwenda naona kama tunadanganywa na viongozi wetu tuliowaamini.Kwa nini naamini tunadanganywa,Daily News na Habari leo online imezungumzia uwekezaji kwenye kilimo unaotaka kufanywa na wawekezaji wa Saudia.LAKINI habari nilizosoma kwenye gazeti la ARABIAN NEWS la Saudia Arabia halijazungumzia uwekezaji ila imezungumzia WATAPEWA LEASE YA MIAKA 99 kwa mujibu wa ofisa aliyefuatana na rais Kikwete.Ofisa huyo anaitwa January Makamba,kwa nini daily News na Habari Leo online yametoa maelezo tofauti na magazeti ya Saudi Arabia na Reuters,magazeti yetu na blog kama hii yamejaribu tu kumpamba Kikwete na hiyo medali aliyopewa kama inavyoonekana hapo lakini hayajaeleza kuhusu kupewa ardhi..KWANINI WANAFICHA INA MAANA SI KITU AMBACHO NI HALALI.

    ReplyDelete
  3. Hiyo ni sehemu tu ya habari ambayo mheshimiwa ana mpango wa kugawa ardhi ya Tanzania kwa Saudi Arabia kwa ajili ya kujilimia chakula.Labda na sisi tunaweza pewa ardhi ya kuchimba mafuta kule kwao kwa lease ya miaka 99.



    Saudis eye Tanzanian farmland
    by Sue Thomas,
    Wednesday, 15 April 2009

    zoomFOOD SUPPLIES: Saudis look to Tanzania as possible location for helping feed the kingdom. (Getty Images)Saudi investors have asked Tanzania if they can lease 500,000 hectares of farmland, mainly for rice and wheat farming, as part of a plan to secure food supplies for the desert kingdom, officials said on Wednesday.

    Senior officials from the Saudi capital's chamber of commerce made the request on the sidelines of a meeting with visiting Tanzanian President Jakaya Kikwete.

    "Tanzania is ready to do business with you ... There is 100 million acres (40.5 million hectares) of good arable land," Kikwete told Saudi businessmen.

    Samir Ali Kabbani, head of the chamber's agriculture committee, said: "We had very positive feedback."

    Story continues below ↓
    advertisement


    "He (Kikwete) told us that Tanzanian authorities can lease us plots each of which covers up to 10,000 hectares for a 99-year period," he told Reuters after the meeting.

    The Saudi government has joined private operators to invest in farm projects abroad after a long and costly food sufficiency plan threatened to deplete the desert kingdom's water supplies.

    Saudi businessmen and officials will visit Tanzania in the next few weeks.

    "They can lease the land from the government," January Makamba, an aide to President Kikwete, told Reuters.

    Saudi officials are particularly interested in Tanzania because of its geographic proximity, political stability and the availability of water resources and farmland.

    Several Saudi firms have already started investing in agricultural projects from Indonesia to Ethiopia.

    ReplyDelete
  4. Uranium hiyo.... ningekuwa ni mimi ningetangazia dunia kuwa nchi nzima iko juu ya uranium na hapo hapo utakapoona dunia nzima itakavyotunyenyekea.

    ReplyDelete
  5. JK ANAHITAJI KUJIFUNZA KUWA KILA KIZURI ANACHOKIONA HUKO KIMETOKANA NA MATUMIZI MAZURI YA KODI ZA WANANCHI NA SI VILISHUKA TOKA MBINGUNI. NINAUHAKIKA HAKUONA MASHABIKI WA KICCM (chama kinachotawala) KWANI WATU WAKO BIZEBIZE NA WANAHESHIMU SERIKALI ZAIDI YA VYAMA. NINAOMBA JK ASIMKARIBISHE KIONGOZI WA NCHI HIYO KUTEMBELEA BONGO KWA ITAKUWA KUJITIA AIBU KWA UCHAFU ULIOKITHIRI HUKU.

    ReplyDelete
  6. SIKUFURAHISHWA NA WALA SITAFURAHISHWA KWA SENTENSI HII "......SAUD ARABIA INAWEZA KULETA MAENDELEO TANZANIA...."

    HII KAULI WATANZANIA BILA KUJALI DINI KABILA RANGI NA AINA YOTE YA UBAGUZI TUIKATAE KWA NGUVU ZETU ZOTE.

    NI KWELI WATANZANIA HATUWEZI KUPATA MAENDELEO MPAKA SAUDI ARABIA AU UJEREMANI!!! AU BUSH/OBAMA!! VYANDARUA!!

    VIONGOZI WA AFRICA IKIWEMO TANZANIA BADILIKENI.

    BANA KODI SANA, HIMIZA MATUMIZI BORA YA ARDHI AMBAPO TUTAOPATA MAZAO BORA YA TUTAUZA NA KUPATA MAENDELEO.

    SOMA HII.







    =Mkulima Mbeya amtambia Pinda=

    Mwandishi Wetu, Mbeya Aprili 15, 2009


    Amwambia anajenga nyumba ya hadhi ya Waziri Mkuu kulala

    Ni matokeo ya kilimo cha umwagiliaji


    MRIDI Kidumba ni miongoni mwa wakulima wadogo zaidi ya 200 kwenye mfumo wa umwagiliaji wa Igomelo, Wilaya ya Mbarali, Mbeya, kwa kazi yao wakulima hawa wanathibitisha uwezo wa mkulima mdogo nchini wa kuweza kulisha nchi na kutoa ziada ya kuuza nje iwapo atawezeshwa.

    Katika umri wa miaka 42 sasa, Kidumba anaonyesha ni jinsi gani kilimo cha umwagiliaji kilivyoweza kumbadili kimaisha, kiasi kwamba unapozungumza naye unabaini ni jinsi gani fedha inavyoweza kumjengea mtu moyo wa kujiamini.

    Kidumba alidhihirisha nguvu ya mkulima mdogo katika mapinduzi ya kilimo nchini hivi karibuni pale alipotembelewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati akiwa katika ziara yake maalumu ya siku mbili mkoani Mbeya kukagua shughuli za kilimo.

    Akijibu swali kuhusu mabadiliko aliyoyapata kutokana na kilimo hicho Kidumba alimwambia Waziri Mkuu Pinda:

    “Kilimo kimenisaidia sana kuyabadili maisha yangu. Mwaka jana nilifikisha akiba ya shilingi milioni kumi. Zilikuwa kwenye SACCOS yetu. Nyumbani huwa tunakuwa na matatizo mbali mbali kama vile kuugua, huwa tunahangaika sana, kwa hiyo nilinunua taxi (gari dogo) ipo nyumbani kwa ajili ya kuhudumia familia.

    “Sehemu nyingine ya ile pesa nikanunulia pembejeo kwa ajili ya kilimo cha msimu huu ambapo nimelima mpunga, mahindi, vitunguu na mazao mengine, kwenye akiba sasa zimebaki shilingi milioni moja.

    “Nina nyumba ya tofali na nimepiga bati, lakini sasa naiona haifanani na mimi. Nimeanza kujenga nyumba nyingine bora zaidi itakayofanana na mimi.”

    Maelezo ya mkulima huyo yalimvutia Waziri Mkuu Pinda, hususan uamuzi wake wa kujenga nyumba nyingine inayofanana na hadhi ya mkulima huyo ya kifedha ya sasa, na ndipo alipomuuliza iwapo nyumba hiyo ataweza kulala kiongozi kama yeye?

    Alijibu Kidumba kwa kujiamini: “Ni nyumba ambayo itakuwa ya hadhi ya kulala hata Waziri Mkuu.”

    Lakini fundisho kubwa lipatikanalo kutoka kwa wakulima hao ni jinsi kilimo cha umwagiliaji kilivyoongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo na kuwawezesha kulima mazao mbali mbali katika kipindi cha mwaka mzima.

    Kidumba anasimulia akibainisha tofauti ya tija kati ya huko walikotoka na waliko sasa akisema: “Nilianza kulima kwenye skimu hiyo mwaka 1986, tulilima kienyeji, hatukuwa na utaalamu wowote, lakini baadaye skimu yetu iliboreshwa, tukapata utalaamu kupitia mabwana shamba, shamba darasa na mzungu mmoja aliyekuja hapa kijijini kwetu.

    “Nimeongeza uzalishaji wa mpunga, sasa navuna gunia kati ya 25 hadi 30 za mpunga kwa ekari moja, huko nyuma nilivuna kati ya gunia saba hadi kumi. Mwaka jana nilivuna gunia 31 katika ekari yangu moja niliyolima, niliuza gunia 15 na kubakiza 16 kwa ajili ya chakula na mbegu.

    “Hapa ni kulima mwaka mzima, tunaita hakuna kulala, mpunga nalima mara moja kwa mwaka, halafu kuna vitunguu nalima mara mbili kwa mwaka, mwaka jana nililima ekari mbili na kuvuna gunia 80 kila ekari, lakini nikienda vizuri navuna hadi gunia 100 kwa ekari.

    “Kwa mfano Julai mwaka jana nilivuna gunia 100 kwa kila ekari, safari ya pili nilivuna gunia 107, na safari ya tatu nilivuna gunia 96, bei ya Januari huwa ni shilingi 50,000 kwa gunia la vitunguu, lakini baada ya Januari huongezeka hadi kufikia shilingi 70,000.”

    Ni wazi basi kipato cha mkulima huyu mdogo kutokana na vitunguu tu si chini ya shilingi milioni 12 kwa uzao mmoja iwapo ataviuza kwa shilingi 60,000 kila gunia na mavuno yakawa wastani wa gunia 100 kwa ekari moja na akalima hizo ekari zake mbili.

    Ongezeko hilo la kipato halijionyeshi kwa mkulima huyu pekee, bali kwa wakulima wote zaidi ya 200 wanachama wa Ushirika wa Umwangiliaji Igomelo kama anavyoelezea Kidumba mwenyewe:

    “Tupo zaidi ya wakulima 200 na tunafanana. Tukinunua pikipiki ni wote. Tunasomesha watoto hadi kwenye sekondari za kulipia, hatutegemei za Serikali pekee.”

    Hiki ni kipato kizuri kwa kiwango chochote kile kwa mwananchi wa kijijini tena kwa zao moja tu kati ya mengi anayolima, ni maelezo ya mkulima huyo mdogo kuhusu mafanikio yake yaliyomsukuma Waziri Mkuu Pinda kutoa tamko la kuwataka Hifadhi ya Kipawa Kipengere kufuta wazo lao la kulichukua eneo hilo akisema ni uwenda wazimu.

    Alihoji Waziri Mkuu Pinda: “Hivi kweli mtu na akili zako unakuja hapa Igomelo na ukasema unachukua mashamba haya kuwa hifadhi, Serikali imewekeza, mlikuwa wapi huko nyuma?”

    Pamoja na kuwa wakulima hawa wameboreshaji mfumo wao wa umwagiliaji na utalaamu waliopatiwa, yupo mtu muhimu sana kwao ambaye wanasema ndiye aliyewabadili kifikra ambaye wanamwita kwa jina la Daipesa, ambalo kwa hakika ni jina la mradi aliokuwa akiusimamia mzungu huyo.

    Mwenyekiti wa Mfumo huo wa Kilimo cha Umwagiliaji Igomelo, Yohana Mbuna anasimulia: “Alikuja Mzungu mmoja hapa, alianza kwa kutuuliza maswali, nani mwenye simu kati yenu hapa anyooshe kidole?

    “Hakuna aliyenyoosha. Akauliza tena, nani mwenye shilingi 10,000 kati yenu nimuongeze shilingi 90,000? Hakuna aliyekuwa nayo.

    “Ndipo alipotueleza kuwa, watu wa Igomelo, sisi hatujawaletea samaki, tumewaletea nyavu mkavue samaki, tukiwaletea samaki mtakula na kurudi kule kule, tunawaletea mafunzo, leo hii tunamiliki power tillers (matrekta madogo) zetu wenyewe.”

    Uboreshaji wa mfumo huo wa umwagiliaji pamoja na mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na Mradi huo wa Daipesa kupitia utaratibu wa shamba darasa ndio kiini cha mapinduzi hayo ya kilimo kwa wakulima hao wadogo wa Igomelo.

    Mbuna anasema kuwa kabla walikuwa wakitumia mfereji wa asili uliojengwa mwaka 1950 na ilipofika mwaka 2004 mfereji huo uliboreshwa na kugharimu shilingi milioni 300 kutoka Benki ya Dunia, mabadiliko ambayo yaliwezesha kupanuliwa kwa eneo la umwagiliaji kutoka hekta 100 za mfereji wa zamani hadi hekta 312 hivi sasa.

    Mwenyekiti huyo anabainisha ongezeko la tija katika uzalisha mazao mbali mbali kama vile mpunga kutoka tani mbili kwa hekta huko nyuma hadi tani nne, mahindi kutoka tani moja hadi tatu, vitunguu kutoka tani 13 hadi 26 na nyanya kutoka tani tano hadi 35.

    Anasema ongezeko katika tija limeyabadili sana maisha ya wakazi eneo hilo ikiwamo kupunguza kwa kiwango kikubwa tatizo la vijana kukimbilia mijini kutokana na kuwapo shughuli za kilimo hapo kijijini zenye kuwapatia kipato kizuri ikilinganishwa na maisha magumu wanayokabiliana nayo wakimbiliapo mijini.

    Anayataja mabadiliko mengine kuwa ni pamoja na uwezo wa kusomesha watoto hadi elimu ya juu, kufanikiwa kujenga shule yao ya sekondari, ujenzi wa nyumba bora, ununuzi wa zana za kilimo kama vile matrekta madogo na ununuzi wa vyombo vya usafiri kama vile magari na pikipiki.

    Kukua kwa kilimo cha umwagiliaji katika mfumo huo wa Igomelo kunajidhihirisha kwa wasafiri wafikapo katika mji mdogo wa Igawa ambako hukutana na vijana na akina mama wakiuza mahindi ya kuchemsha na karanga, na ni wazi hushangaa kwa sababu ni katika kipindi cha mwaka mzima.

    Ushahidi mwingine ni kukua kwa haraka kwa mji huo wa Igawa ambao katika miaka ya nyuma baada ya usafiri kati ya Mbeya na Dar es Salaam kurahisishwa, ulididimia kiuchumi. Sasa hali ni tofauti, unakua kwa kasi kutokana na kuongezeka kwa tija katika mazao ya kilimo kwenye Skimu hiyo ya Igomelo.

    Skimu hiyo ya Igomelo inatoa funzo kwa Serikali kwamba hatuna haja leo hii ya kukimbilia kilimo cha mashamba makubwa ambayo yatatumia eneo kubwa la ardhi na kuwatelekeza wananchi zaidi ya asilimia 80 wanaotegemea kilimo.

    Huu ni wakati muafaka wa kuachana na porojo na badala yake kuamua kwa dhati kuwekeza kwa wakulima wadogo kwa kubadili kilimo chao kutoka kile cha kizamani cha jembe la mkono na kuingia kwenye kilimo cha kisasa angalau kwa kuanzia na matrekta madogo, tija itaonekana na tutakuwa tumeingia kwenye mapinduzi ya kweli ya kilimo.

    WATANZANIA TUNAWEZA JANA, TATIZO TUNA VIONGOZI LAINI LAINI SANA.

    ReplyDelete
  7. NAENDELEA,

    NI MWANAMUME GANI ANAWEZA KUACHA NYUMBA YAKE NA KWENDA KUPELEKA MAENDELEO KWA MWANAMUME MWINGINE? AMA ANAFAIDI KITU KATIKA NYUMBA HIYO AMA .....

    ReplyDelete
  8. lease miaka 99 ....no good my friend for our children. kwanini tusilime wenyewe halafu tukawauzia hicho chakula? mikataba mingine tukiingia tutawaumiza watoto wetu. does he know that?

    ReplyDelete
  9. VIONGOZI WETU HAWAKO TAYARI KUTUMIA FEDHA ZA KODI ZA WANANCHI WAO KWA MAENDELEO BALI HUPENDA KUZITUMIA FEDHA HIZO KWA STAREHE ZAO NA KWENDA NJE KUOMBA MISAADA KISHA NAYO HITUMIA KWA STAREHE ZAO PIA NA KUWAACHA WANANCHI HOI, LAKINI YOTE HAYA YANASABABISHWA NA WANANCHI KUTOKUTAKA KUJUA HAKI ZAO BAADA YA KULIPA KODI HII YOTE INATOKANA NA KUTOKUWEPO ELIMU YA URAIA. BAADA YA VIONGOZI KUJUA UDHAIFU WETU WANATUMIA MWANYA WA KUWAPA KANGA, TISHETI, KOFIA NA VITENGE HATA PILAU KWANI WAKISHAPATA HIVYO HUJISIKIA WAMEENDELEA KIMAISHA! UFINYU WA ELIMU. TUNALIPA KODI LAKINI MIJI YETU NI MICHAFU KUPINDUKIA, MITAA HAIPITIKI, ILIYOKUWA NA LAMI WAKATI NA BAADA YA UHURU LEO HII NI TOPE TUPU NASI TUMEBAKI TUKIWASHANGILIA. HEBU TUANGALI KITUO CHA MABASI YA MIKOANI UBUNGO, LICHA YA WANANCHI KULIPA WAINGIAPO HUMO LAKINI HAKUNA PESA ZOZOTE ZINAZOTUMIWA KUKISAFISHA, KUJENGA SEHEMU ZA ABIRIA KUKAA HATA KUTENGENEZA BARABARA ZAKE! LAKINI WANANCHI WANAONA SAWA TU. TUTAENDELEA KUISHI MAISHA DUNI TU HATA MUNGU AKITUMWAGIA ASALI NA MAZIWA WATACHUKUA VIONGOZI WETU NASI TUTABAKI TUKIANGALIA TU KWA UJINGA WETU.

    ReplyDelete
  10. Mimi nimesikitishwa sana na hiyo proposal, kwanini wasiwasaidie wakulima wetu halafu wanunue mazao kutoka kwao? Hiyo itawasaidia wakulima wetu sana. Kwanini viongozi wachache wafanye maamuzi utafikiri nchi ni yao peke yao? Tatizo viongozi wetu hawajadili jambo kwa kina na kuaangalia manufaa na hasara. JK anatumia fedha za walipa kodi kwenda nje ya nchi kukubaliana mikataba ambayo haitawafaidisha wananchi. Ni wakati sasa umefika wananchi tuandamane kupinga jambo hilo. Kuna kila sababu ya kuamini ubinafsi unataka kutekelezwa hapo. Sina uhakikika JK atafaidika nini hapo, sifa ni moja wapo lakini angalia wananchi vijiji wanavyoteseka na umaskini. Hapo nimeshaona opportunity ya masoko ya nje hivyo serikali ingetafuta mkataba wa kuwasaidia wakulima wetu kuwa na nyenzo bora za ukulima wa mpunga na ngano ili kuuza Saudi Arabia. Hii sio nchi ya JK na huyo msaidizi wake. Ni nchi ya watanzania wote na maamuzi yafanywe kuwafaidisha watanzania wote au walio wengi.
    Ni mimi Kiona Mbali

    ReplyDelete
  11. KINACHOKERA KWA WABONGO NI KULALAMIKA PEMBENI TUU. jamani eeehh hatutafika kiivyo chamsingi ni kutake action. Tulaani vikali itafika kipindi tutaambiwa maeneo flani asionekane mtu zaidi ya kiongozi wa serikali. Ardhi hii kwa kifupi ishauzwa, miaka 99 sio mchezo.ukipiga hesabu ni mpaka mwaka 2108. wote tushatangulia mbele ya haki.

    WABONGO AMKENI AMKENI AMKENI eeeehhh.

    ReplyDelete
  12. Huu sio uwekezaji bali ni ufisadi uliokubuhu. Itabidi tumuulize JK amelipwa kiasi gani kufikia uamuzi huu. Wanaharakati hebu tuwaelimishe na kuwahamasisha wananchi tuungane sote na kusimama kidete kupinga Saudi Arabia kumegewa ardhi yetu. Tutakutane katika viwanja vya WASUDIAWASIPEWEARDHIYETU.COM

    ReplyDelete
  13. yani nasema ivi,,,kama Mungu wetu muumba aishivyo sawa wacha aiuze ardhi ya Tanzania miaka 99 then tuone nani mwenye nguvu Mungu vs Rais!!!

    yani nyinyi magazeti nchi hii Tz mnaficha newz tete kama izi???afu makesha kututangazia oooooh tunu tunu ya nini sisi!!!
    it sound too fishy HILI DILI i knew it

    ReplyDelete
  14. Natamani kumzaba kofi JK ili nchi na DUNIA itambuwe anakotaka kutupeleka hata nikifungwa potelea mbali. ujumbe utakuwa umefika,,,hivi kweli JK mtetezi wa wanyonge unakubali hiyo lease ya miaka 99? nakwambia watakuja kuzalisha huo mpunga na sisi tutakuwa watumwa kwa kipato kidogo kwenye hayo mashamba na watatuuzia usio faa kwa pesa nyingi yaani chenga na ulio safi wataenda kula kwao na hivi waarabu wanavyopenda ubwabwa? sasa nani atusaidie hapo? je wanasiasa? wasomi? viongozi wa dini?au sisi wananchi tusimame kidete na kupinga swala hili la wizi wa mali zetu? kama MH Pinda umeona hao wakulima 200 wa igomelo Mbeya wameweza kufanikiwa basi mshauri mwenzako JK hao waarabu walete mapesa then waTanzania tunaweza kisha tutawauzia,,,Nchi kama Japan wameendelea leo hii kwasababu ya kupewa elimu kwanza,,tungekuwa sisi tungetaka msaada wa pesa na tungezimaliza kisha kutizamana lakini wenzetu waliwekeza kwenye elimu,,sasa hao Saud Arabia kama kweli wanataka kutupa maendeleo watupe kwanza elimu ya jinsi ya hicho kilimo cha huo mpunga kisha mambo yote watuachie wenyewe hakika tutafika mbali sana
    MUNGU INUSURU TANZANIA NA JANGA HILI
    MUNGU IBARIKI TANZANIA
    MUNGU WABARIKI VIONGOZI WETU WAWE NA HEKIMA NA BUSARA
    Mdau Kiomboi

    ReplyDelete
  15. Atainunua aridhi hiyo kwa miaka 99 na kuzalisha mpunga na ngano kwa ajili ya watoto wa Saudi Arabia!

    Gesi inanunuliwa hivyo na kuuzwa popote ulimwenguni kuliko na bei ya juu (pure business); kufanya business sio Taasisi ya Mother Theresa!

    ReplyDelete
  16. WATANZANIA TUAMKE KUMEKUCHA,,,NYIE MLIOKO NJE HUKO KULIKUWA KAMA HUKU NA KWA KUAMKA KWAO NDIO MAANA MNAKIMBILIA NA KUJISAHAU NA KUSAHAU YA KWENU,,,HUU NI UJINGA NA WIZI TENA MBAYA UNAFANYWA NA MTU AMBAYE TEGEMEO LA TAIFA NA WANYONGE LA WALALAHOI,,,HAPO NINI SISI WATANZANIA KWA PAMOJA KUPINGA HUU WIZI LA SIVYO TUTAANGAMIZA KIZAZI CHETU

    ReplyDelete
  17. GEORGE MWIREApril 17, 2009

    NIMESOMA MAONI MENGI HAPA NA KUGUNDUA KUWA UDINI UMETAWALA ZAIDI KULIKO HOJA, HAYA YANGEFANYWA NA NCHI NYINGINE YASINGESEMWA YOTE HAYA.
    TUSIWE WANAFIKI TUWEKE MASLAHI MBELE.

    MJADALA UMEFUNGWA.

    ReplyDelete
  18. JK KAENDA KUTAFUTA WAWEKEZAJI WA MBEGU ZA MITI

    ReplyDelete
  19. Tanzania imefanikiwa kupata msaada wa mbolea ya kinyesi cha ng'ombe kutoka north korea, Serikali itaghalamia usafirishaji tuu.

    ReplyDelete
  20. (US Blogger)

    Mashaka usithubutu kuleta nakala zako mbovu za kuponda uhusiaono wetu na Saudi Arabia-dont even think about it kama ulivyowafanyia wa-China then kwenye interview uraruka na kudai hujui kama bidhaa mbovu hutoka China wakati ulishaandika nakala ya kuwa convict.Ukijaribu utanilazimisha niku 'sniper' kwa kalamu yangu.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  21. (US Blogger)

    Nyinyi munaoshangaa wa-Saudi kuwa offered 99yr lease wacheni nonsense, hiyo ni sheria ya nchi, mbona wazungu wakipewa 99yr lease hamupigi kelele kama kweli kinachowasumbua ni lease?

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  22. nyote mnaempinga JK MNAWAZIMU TZ INA ARDHI KUBWA KIASI HATA SISI WENYEWE HATUITUMII ,WATU WOTE MNAKIMBIRIA DAR MNAACHA ARDHI,SASA AKIWAPA WAHARABU WAITUMIE KWA MAZAO KUNA UBAYA GANI KWANI ITAKUWA BURE? MNAJUWA SISI TUTAFAIDIKA NINI? KWANI HIZO NDEGE ZA SAUDIA ZIKIJA BONGO TU KUCHUKUWA CHAKURA ,TAYARI AIRPORT IMESHAINGIZA PESA,PIA MNAFIKIRI WATA HAJIRI WASAUDIA KWENYE HAYO MASHAMBA YA HEKARI CHUNGU MZIMA HIVO?
    JIULIZENI WATANZANIA WANGAPI WATAFAIDIKA /WATAPATA KAZI KWENYE HAYO MASHAMBA ,MITAMBONI,MPAKA UWANJA WA NDEGE.

    YANI HATA KAMA BURE WAPE TU,WASAIDIENI BINADAMU WENZENU ARDHI MTAIACHA HAPA HAPA DUNIANI,KWANI NYERERE KAONDOKA NA TANZANIA? SI KAIACHA?

    EMBU WAPENI MSAADA SANYINGINE MWENYEZI MUNGU ATATULIPIA NA MVUA NA NEEMA KEM KEM ZA CHAKULA.

    HAYA TUSEME MMEWAKATALIA.SASA NYIE ARDHI YOTE HIYO YA TZ MTAIFANYIA NINI????????? ???????
    MNABWABWAJA TU WAKATI NCHI YENU MMEIKIMBIA MKO MAJUU.

    NGOJA AWAKATALIE WAHARABU WAENDE KENYA AU UGANDA.
    NYINYI WENYEWE MTASEMA WAKENYA AU WAGANDA WAMEENDELEA KULIKO WATANZANIA.TENA MIAKA 99 EEEH BWANA BONGE LA DILI.
    KUDADEKI JK WAINGIZE MKENGE WAHARABU TUJIRUSHE TZ, WATATUWEKEA MPAKA UMEME MAMBO YA MGAO FINISH!!!!!! !!!!!.
    MANA MASHAMBA YANAITAJI UMEME BWANA AU VYAKULA VITAOZA.
    TENA GODOWN YA VYAKULA IWE DAR ILI UMEME UWE WA KUMWAGA DAR. WAINGIZE MJINI WAHARABU NA BARA BARA WAZITENGENEZI MANA MALORI YA MSOSI YATAPINDUKA BARA BARA ZIKO VERY NARWO .
    MKITAKA LIST NYINGINE NTAWAPA.

    HALO HALOOOOOOOOOOOOO.
    I LOVE JK.

    ReplyDelete
  23. WEW ULIE MALIZIA NA "KIZAZI CHETU" NAKUPA TAHARIFA HICHO KIZAZI NDO KITAKACHO FAIDIKA.MANA ITAKUWA MIAKA 99 YA KUTENGENEZEWA NCHI YETU,NA KAZI ZITAKUWA KEM KEM KWA MIAKA 99 AU YOYOTE ILE WATAKAO INGIA NAYO MKATABA.
    WATZ TUTAKUWA TUNAENDA SAUDIA KAMA TUNAVOENDA DUBAI.PIA MADADA ZETU WATAACHA KUJIUZA KWA WAZUNGU SASA ITAKUWA WAHARABU ALAFU WAHARABU WANAJUWA KUONGA KWA MANA HIYO KIZAZI CHETU KWA UPANDE WA MACHANGU WA VIZAZI VYETU WATAKUWA WAMEULA.

    HII KITU BABU KUBWA KILA MTU ATAFAIDIKA.MASHAMBA YATAITAJI MAGARI ,MABASI KWA AJIRI YA WAKULIMA.
    UCHUMI UTAINUKA KULIKO MAREKANI.AU MNATAKA WAENDE INDIA?
    CAMPUNY ZA KIMAREKANI KIBAO ZIMEAMIA INDIA.
    INDIA INACHUWANA NA WACHINA.
    WABONGO MAZOBA SANA.WOTE MNAONUNGUNIKA HAPA MAZOOOOOOOBAAAAAAAA

    ReplyDelete
  24. MediaViabilityApril 18, 2009

    KWA WOTE WANAOULIZIA LEASE YA MIAKA 99,

    Do you have any Idea Mlimani City wamelease for how long fom UDSM, Nafikiri kuanzia hapo mnaweza kuanzisha debate ya matumiz1 ya ardhi.

    ReplyDelete
  25. mdau wa [anony April 18, 2009 12:53 AM]..wewe kweli umeenda shule tena shule kali sana...

    tena nina uhakika wengi wa hawa wanaolalamikia wameikimbia TZ wameezamia nje kubeba maboksi wakati ardhi ipo kedekede...

    wabongo tumezidi kuabudu wazungu...wangepewa wazungu hii ardhi asingesema mtu neno...ila akiwa mwarabu, muhindi...ooh, wanatuibia...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...