Hawa ndio washiriki wa kipindi maarufu cha TBC cha Maisha Plus waliofanikiwa kuingia katika kumi bora, mmoja kati yao ataondoka na kitita cha shilingi milioni kumi Jumapili ya April 26.

Mdau unaweza kuwaoigia kura kadri  uwezavyo na upendavyo. Majina yao na namba ni kama ifuatavyo:

Abdul 32,Maulid 33,Upendo 18 ,MOdesta 37,MOshy 19,Charles 11,Steve 14,Boniface 20,Hamis 23 na Teddy 36.

Kwa wanaotaka kupiga kura kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi wanapiga kwenda namba 15522 na  kwenye mtandao watembelee maishaplus.g5click.com.

Kwa niaba ya timu nzima ya Maisha Plus nawashuru kwa ushiriakiano mliouonyesha tangu mwanzo mpaka sasa. Mungu awabariki sana.

Julieth Kulangwa
0717 551355

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hellow,hongereni sana kwa kutayarisha hiki kipindi.Kama washindi wangekuwa wawili basi Abdul (32)angekuwa wa kwanza na Charles (11) wapili.lakini kwakuwa mshindi ni mmoja tu. naomba Charles apewe hizo mil 10 zake.please. Pendo hafai kabisa kuishi na jamii.mmbeya yeye,mwongeaji yeye.mchonganishi ni yeye kila sifa mbaya anazo yeye.

    ReplyDelete
  2. Naungana na mtoa maoni wa kwanza. Charles anastahili, yaani mpaka niliota kuwa charles ndiye aliyechukua ushindi.

    ReplyDelete
  3. Haaa haa haa ngoja nicheke kimaisha plus mie.Naungana na mtoa maoni wa kwanza na pili,ebwana eeh Charles anatisha apewe hizo mil 10 zake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...