

Stori na picha na John Nditi, Morogoro
WANACHAMA wa Taasisi ya Development Entrepreneurship Community Initative (DECI), Tawi la Morogoro jana walimiminika katika Tawi hilo kwa akili ya kujiorodhesha kwa lengo la kurudishiwa fedha zao walizopanda baada ya Serikali kusitisha shughuli za Deci nchini.
Baadhi ya wanachama hao ambao waliwasili katika Tawi hilo alfajiri na mapema baada ya kusoma matangazo yaliyopandikwa katika ofisi hizo wakitakiwa kuanza utaratibu wa kurodhesha majina na vielelezo vyao kwa lengo la kurudishsiwa mbegu zao.
Meneja wa Tawi hilo, Saimon Shenga, aliwatangazia baadhi ya wananchama waliofika katika Tawi hilo kuhusu utaratibu wa kurudishiwa fedha zao ambapo baadhi yao waliafiki na wengine wakiendelea kuhoji mambo kadhaa kuhusiana na faida ya kile walichopanda.
Kwa mujibu wa Meneja huyo , kwamba wanachama watakaoanza kurudishiwa fedha zao ni wale waliopanda mbegu mwezi uliopita baada ya kuorozeshwa wanarudishiwa mbegu zao Aprili 25, mwaka huu na kuendelea hivyo kutokana na muda wa kupanda mbegu zao hizo.
Hata hivyo amewakata wanachama kuwa wa kweli kwa kutoa vielelezo sahihi ili kuweza kuharakisha urudishwaji wa mbegu zao walizopanda bila ya usumbufu wowote.
Kwa mujibu wa Meneja huyo, DECI inawarudishia wanachama waliopanda mbegu kutokana na utaratibu maalumu uliokubwakliwa na Ungonzi wa Deci Taifa.
Akitoa ufafanuzi zaidi wa jambo hilo, Meneja huyo alisema iwapo mwanachama wa Deci aliyepanda mbegu ya kiasi cha sh: 40,000 na kutarajiwa kuvuna sh: 100,000 atakachoweza kurudishiwa ni mbegu yake aliyopanda ya sh; 40,000 tu.
Hata hivyo amewakata Wanachama wa Tawi hilo kuwa watulivu wakati wote wa uhakiki wa majina na viwango walivyopanda mbegu zao kwa ajili ya kuharakaisha na kukamilishwa mapema kwa zoezi hilo.
Nao baadhi ya wanachama waliofika katika Tawi hilo jana asubuhi wakizungumza kwa nyakati tofauti juu suala hilo,walionyesha wasiwasi juu ya mbegu kuweza kurudishiwa kwa wakati kwa vile waliopanda mbegu kwa vipindi tofauti na bila ya kuchukua mavuno yao kwa misingi ya kuongeza mbegu zao katika Tawi la Deci.
“ bado tunahofu juu ya utaratibu wa kurudishwa mbegu zetu…sisi wengine muda wetu wa kuvuna ulipofikia tuliziacha fedha zetu zieongeze mbegu katika Deci …” alisema mwanachama mmoja na kuongeza kuwa.
“ sasa wanasema wataturudisha kiasi tulichopanda kwa mara moja tu hizi nyingine sijui tutazipataje? ” alihoji mwanachama huyo ambaye hakupenda jina lake litajawe
HAKUNA BIASHARA ISIYO NA FAIDA.....ULIYEUZA CHENI BANDIA UKALIPWA FEDHA BANDIA KAKA,NGOMA DROO.
ReplyDeleteJamani kuna minong'ono ya chini kwa chini kuhusu watu waliovuna na baadaye wakadaiwa kutoa mavuno katika watoto wao, anyway hii naiona kama hadithi tu, au watu kutunga ili kuifanya hii kitu ionekane mbaya, lakini kama kuna ushahidi tunaomba watu wautoe
ReplyDeleteWewe wa mwanzo hapo juu uwe na roho ya kibinadamu. Hapana ngoma droo wakati upande mmoja ni matapeli kama walivyo EPA beneficiaries na mwingine ni wanyonge ambao wanaibiwa si lazima kwa tamaa zao, bali wengi kwa upeo mfupi wa kuelewa masuala ya fedha na biashara na pia kwa shida nyingi walizo nazo. Watazame waliosimama hapo - unaweza kuusoma unyonge katika taswira zao.
ReplyDeleteHaya, na wewe wa pili una maana gani kutoa mafao katika miili ya watoto wao?
TAARIFA KUTOKA MBINGUNI KWA WALIOIKOSA DECI
ReplyDeleteWale wote waliopanda mbegu,Mungu atawalipa.Kwani hazina yao wataikuta Mbinguni.
Mimi DECI mlinipenda sana,kwa sababu mnapenda vitu vya mteremko ila SERIKALI amenipenda zaidi, Bwana alitoa Serikali imetwaa.
Tuko wote kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Nimeamini unasanii umekomaa TZ. Hivi kweli watu mnaanzisha biashara yakuzurumu wanyonge?
ReplyDeleteNashangaa wahusika wako jiiii! wakati mwanzoni walijidai kuonesha kutoa maelekezo kwa wateja wao.
Acheni uzushi nyie maDECI lipeni hela za watu pamoja na riba zao. Jasho la mtu haliliwi!
Nakumbuka hili DECI lilivyoanza, kuna rafiki yangu sijui alizipata wapi habari zake akaja kunihubiria jinsi ya upandaji na uvunaji wake,
na kipindi hicho nilikuwa nimepata bingo fulani basi nikamwambia asante kwa maelezo yako ila mimi vijisenti vyangu napenda niwe naviona mtungini ninakohifadhi. Hata bank sipo tayari kupeleka ni wizi mtupu.
Kwani nilihisi kunautata mtupu hakuna kitu cha dezo bongo, tuibiwe kiEPA sio kuwapelekea.
Poleni sana wahanga wa DECI.