Habari za kazi kaka.
Katika kuperuziperuzi nimekutana na maelezo mengi tu yanayoelezea namna ambavyo kiswahili kimekua miongoni mwa lugha zinazolengwa sana kimatumizi katika ulimwengu wa tekinolojia,hasa upande wa teknolojia ya habari na mawasiliano.

Wakati sisi watanzania tukipingana kwa hoja mbalimbali juu ya matumizi ya kiswahili na umuhimu wake katika jamii na taifa letu,wenzetu wakenya wameshajua kuwa kwa sasa kiswahili kinalipa na wamekua wakijitangaza kama wao ndio wenye lugha hiyo ya kiswahili.

Kufuatia kujitangaza huko,sasa hivi wakenya wakishirikiana na makampuni makubwa ya kutengeneza programu za komputa kama vile microsoft, wamekuwa na miradi mingi inayohusu matumizi ya kiswahili katika nyanja hizo.

Hivi jamani  ni kweli sisi watanzania hatuna la kufanya katika hili? Sie tupo wapi mpaka hawa jamaa ndio waonekane wanyeji wa kiswahili,au ndio kama yale ya Kilimanjaro?.

Kibaya zaidi ni kuwa wamekuwa wakichangia katika kukiharibu kiswahili chenyewe kwa kutoa tafsiri na maana za maneno zisizokuwa sahihi na pia kuchanganya matumizi ya herufi katika maneno.

Kitaaluma mimi ni fundi,kutokana na mfumo wetu wa elimu masomo yangu yote yalikuwa kwa lugha ya kiingereza.Nilibahatika kuja Ufaransa kundelea na masomo lakini nilichokuta huku ni kwamba kiingereza hakitumiki kama huko kwetu na unaweza kukuta ni 1/10 wanaoongea kiingereza.Kwa hiyo ilinibidi kujifunza kifaransa na mpaka sasa naendelea na masomo ya ufundi lakini katika lugha hii ya kifaransa.

Kutokana na hilo nimekuwa na tamaa ya kuona kuwa huko kwetu tunatumia lugha ya kwetu katika kutoa taaluma.Naamini hii itachangia kwa kiasi kikubwa kuwa na wahitimu wengi wenye uwelewa mzuri kitaaluma.Nchi nyingi duniani zinatumia lugha za kwao katika kutoa taaluma isipokuwa nchi zile zilizokuwa makoloni ya muingereza au mfaransa. 

Wito wangu kwa wahusika wa taasisi za ukuzaji na uendelezaji wa lugha ya kiswahili : jitahidini kutafuta tafsiri na maana za maneno ili kuweza kuondoa tatizo la kutokupata tafsiri sahihi ya misamiati katika fani mbalimbali mf. utabibu,uhandisi n.k,mimi mwenyewe huwa napata taabu sana kupata tafsiri ya kiswahili kwa misamiati katika fani yangu, lakini sijakata tamaa na natumai polepole tutafanikiwa.

Kitangazeni kiswhili na kutangaza taasisi zetu pia ili kuweza kutambulika nyumbani na kimataifa pia!

Kwa kweli kuna umuhimu mkubwa sana wa watanzania kuanza kuona umuhimu wa lugha hii na hivyo kuitilia maanani na kuweza kufaidika nayo katika kila nyanja.Wakati sie tunakimbilia ugenini, mambo sasa yanageuka nao wanaona neema ipo huku kwetu ila sie hatuioni.


Unaweza kujionea zaidi katika viungo vifuatavyo:


http://www.ushahidi.com
http://habariproject.org/en/
http://perl.kamusiproject.org/cgi-bin/main.cgi
http://techdirt.com/articles/20070925/012311.shtml

fier d'être Tanzanien,
Stan D.M
8 Av du Parc,
31700 Blagnac.
France.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Tatizo tunatumia muda na nguvu nyingi kutafuta nani mchawi,nani anatuonea, n.k Huo muda uliotumia kuandika hapo si ungekuwa tayari unawaza nini la kufanya na wewe uungane na hao Google. Hizo ni private initiative kwa hiyo kama wewe unaona hiyo ni opportunity then why wait, venture in...

    ReplyDelete
  2. annon no.1 umenena sawa kabisa
    yan wee mtoa mada ungesema nini umeanza fanya so far na ikitegemea ni msomi ulieko nje ambapo aya maswala ungefanya tu kwa uhakika,afu wee ndo waishia lalamika,,,
    shida ya watu ndo hii maneno mengi na kuona wakenya wanatunyanganya vitu vyote ilhali sii kweli.wao walichukua initiatives so why dont we??
    me uwa nafundisha wageni kiswahili na siku zote nawasiliana na jamaa mataifa mbalimbali na naitangaza sana lugha hii inatoka kwetu na aswa Zanzibar na kuna madenti kibao wa nje weshakuja kusoma Tz na wanakuja mana nao wanapeana newz izi mtu unazowapa!!

    DUNIA NI USHONDANI,FANYA KITU KWA NCHI YAKO.

    ReplyDelete
  3. Bure unajisumbua na mawazo yako, uku kwetu kiswahili ni ushamba. ukiongea kishahili bila kutia neno la kiingereza hata moja unaonekana mshamba. katika hari ya namna hiyo usitegemee tena kuona watu wakijishughulisha na kiswahili. acha tu watu wa kenya waseme ni chao maana sisi tunakionea aibu. ndio maana hata katika mikutano mikubwa na asilimia kubwa ikiudhuliwa na waswahili wenyewe lugha inayotumika kuiendesha ni kiingereza. bongo tambarare bwana!!!

    ReplyDelete
  4. Nchi ya wajinga.

    ReplyDelete
  5. Bongo tambarareee!sie tulishalala usingizi mzito na hakuna wa kutuamsha.Kama wewe ukishtukia dili ichangamkie kivyako..!!

    Uliwahi kuisikia hii???

    Tanzania Loses Name To Tanning-Salon Chain
    September 3, 2003 | Issue 39•34

    TALLAHASSEE, FL—The country formerly known as the United Republic of Tanzania has lost the use of its name to Tampa-based Tanzania Tanning Salons, the Florida Supreme Court ruled Monday.
    "Any use of my country's name constitutes infringement on the plaintiff's trademark," said Benjamin Mkapa, president of the currently unnamed republic. "We've lost our national identity. This is a very sad day for the people once known as Tanzanians."

    http://www.theonion.com/content/node/29405

    ReplyDelete
  6. Namba 3 nakuunga mkono kabisa. Watanzania tuko washamba sana kwa lugha yetu. Mimi niko hapa USA, ukikutana na Mtanzani ukisalimiana naye kwa Kiswahili yeye anajibu kwa Kiingereza. Unashindwa kueliwa huu ni ulimbukeni gani jamani. Na siku hizi Kiswahili kinalipa sana. Kuna hii Kampuni WWW.FHI.ORG, WWW.RTI.ORG. WWW.CARE.ORG. Kama unajua Kiswahili unameuliwa. Wakenya wanachukuliwa kama vile hawana akili nzuri. Kuna Kampuni nyingi sana wanataka watu wanaojua Kiswahili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...