
Mzee Nelson Madiba MANDELA anaichoma moto PASSPORT ya KIKABURU ya Afrika Kusini,na anabaki kuwa raia wa asili wa AZANIA yaani Afrika Kusini)
Kuwa na Pasi ya US,Ulaya,uhajemi nk.akumfanyi mtanzania kubadilika heti hasiwe mtanzania au mswahili tufungue macho
Sherehe za Muhungano Zinanukia! Na Uraia wa nchi mbili nao?
Sherehe za kumbu kumbu ya sikuu ya muhungani zinanukia kwa kila mtanzania aliye nje au ndani ya nchi,ni sikukuu ya kumbu kumbu ya kitendo cha kihistoria kilichotuhunganisha watanganyika na wazanzibar ikazaliwa Tanzania nasi tukaitwa watanzania jina au uraia ambao ukienda popote duniani na kujitambulisha hivyo basi utapata heshima ya hali ya juu! kuwa umetoka katika nchi ya waungwana wasio kubali kutawaliwa! pia kugawanywa.
Historia hii inawasuta walio wengi aswa mataifa ya ulaya ya magharibi ambao walijua kuw amuhungano huu hauwezi kudumu!
LAKINI TUJIULIZE SWALI MOJA ? JE PAMOJA NA MATUNDA MENGI YA MAFANIKIO YA MUHUNGANO ? VIPI KIUCHUMI? TUPO UHURU? YAANI SIO TEGEMEZI?TUFANYE NINI? HILI TUSIWE TEGEMEZI LA KUTEGEMEA MISAADA SANA?
Hapa ndipo tuanzie kuzungumuzia swala la URAIA WA NCHI MBILI ambao unataweza kumuruhusu mtanzania kuwa raia wa nchi nyingine bila ya kupoteza uraia wake wa hasili wa tanzania ambao ni wa jamuhuri ya muhungano! kama uwezekano huo hupo basi utakuwa kwa faida ya Tanzania kutumia watanzania wachache walio nje ya nchi kuleta maslahi nyumbani Tanzania kwa faida ya taifa pia kwa familia zao.
Swala hili la urai wa nchi mbili atuwezi kulikwepa na kwa kadri linavyopigiwa MIZENGWE!
ndivyo tutakavyo kuwa nyuma na matokeo ya watanzania tutajikuta tunafungwa bao la kisigino na majirani zetu waliotunguzunguka!!!! kwani nao kwa namna moja au nyingine tumeungana nao japokuwa si kwa jina la JAMUHURI YA MUHUNGANO bali kwa jina la
JUMUHIYA YA AFRIKA MASHARIKI hata pia Kwa muhungano wa jina la SADIC n.k
Wenzetu hao washaanza kula matunda ya uraia wa nchi mbili na kuhakikisha kila manufaa wanapeleka kwao kutoka ughaibuni! wakati watanzania bado tunaliweka swala hili katika mambo ya kisiasa!
Hivi tunachokiogopa ni nini ?aswa katika swala zima la uraia wa nchi mbili?na kulifanya swala zima liwe la mizengwe,na penginepo baadhi ya vyama vya kisiasa watalichukulia ndio MADA YA KAMPENI ZA UCHAGUZI!
Hivi watoto wangapi waliozaliwa nje au ndani ya Tanzania ambao moja ya wazazi wao ni mtanzania !au pengine wazazi wao wote ni watanzania lakini watoto hao kwa kuwa wazazi wao hawana uraia wa nchi mbili kunawafanya watoto hao kukosa uduma fulani muhimu?
Tuchukulie labda wazazi wa mtoto wanaishi ulaya,marekani,Asia,Uhajemi na kungineko!
na mtoto kazaliwa huko ughaibuni na sheria ya huko inasema kama mtoto sio raia wa kujiandikisha awezi kupata uduma za bure za matibabu ya nchi hiyo?itabidi wazazi walipe gharama kubwa kwa kutibiwa mtoto wao kisa mtoto ana uraia wa nchi mbili!
Au mtoto itabidi alipiwe ada ya bei ya juu ya masomo kwa kuwa si raia wa nchi mbilijapokuwa kazaliwa huko ughaibuni na anayo haki ya kuwa raia wa huko! lakini sheria ya jamuhuri ya muhungano haimruhusu! je nani ni mwenye hasara?
Mwisho kabisa ninawatakieni heri ya siku kuu ya mhungano na pia tujaribu kuweka AGANO JIPYA KATIKA MUHUNGANO WETU!
NA AGANO HILO NI KULITUPIA JICHO SWALA LA URAIA WA NCHI MBILI NA KWA FAIDA YA NANI?
Mdau Msemakweli
Michu najitolea kuwa editor wako habari inaweza kuwa ni nzuri lakini cha! kiswahili cha aliyetuma kinaweza kukuput off usisome
ReplyDeletekweli lile swala la uraia wa nchi mbili lilimalizikia wapi?atulisikii tena au mpaka wakati wa uchaguzi?
ReplyDeleteHi,kweli sasa wakati umefika kwa watanzania kuweka siasa pembeni na kuangalia ukweli,unajua raia wengi wa bongo walio nje wanaziokoa familia bongo,tuchukulie mfano wa fedha ngapi? wanazituma kwa ndugu zao kupitia Westen Union money transfer? sasa kama wangeweza kuleta maendeleo zaidi kutoka nje!hila kikwazo ni uraia wa nchi mbili?kwa nini bunge lisipitishe sheria? hiyo ya uraia wa nchi 2 kwa faida ya wabongo?
ReplyDeleteminathani hakuna mtoto wa wazazi zaidi ya wawili.ndivyo hivyo katika sheria za nchi.sithania kama kuwa na uraia wa nchhi mbili kutaleta tofauti yoyote au mabadiliko tu kaitka mchakato mnzima.hatuitaji uraia,tunaitaji wazalendo.hao wa nchi mbili hawawezi kamwe kuwa wazalendo.na maana yake uko tayari kufa kwa ajili ya nchi yako,na pia nii utaifaidisha nchi yako kama hulipi tax,au ulitumiki taifa.na pia ni wazi yule anayeishi marekani au uk na kwingineko atapendelea zaidi huko maana bado tanzania hatuwez kulingana na na nchi hizo.hivyo basi,ni wajibu kwa kila mzalendo kurudi nyumbani na kuiendeleza kizazi na nchi yetu kwa ujumla.
ReplyDeletetusiwe na mambo ya kuiga nchi jirani wamefanya nini,tupime nia zetu,maslahi yetu na uzalendo wetu.na kwa mantik hiyo basi,napenda kutoa shukrani kwa Mwl.Jk NYERERE maana hakuangalia nini jirani wanafanya,tulibakia kama sisi watanzania.na ndo kitu ambacho kimetushika kwa pamoja mpaka muda huu.na ukiangalia kwa kina hao majirani zetu wapo wapi?
Mungu Ibariki Tanzania,Mungu ibariki Africa.
mdau-california
I agree. Lugha ya mwandishi inatisha. Wa wapi walimu wa kiswahili? Mrs. Uledi angelia...
ReplyDeleteHuyu jamaa ni hater nini? kwa nini anshambulia watu wenye uraia nchi za magharibi? Hajui ni uhuru wa mtu kuchagua nchi anayotaka kuwa raia: uhuru sawa na wa Mandela.
ReplyDeleteWe jamaa hujui kiswahili kabisa, jamaa anaandika kama mrundi.
ReplyDeleteNimeshindwa kusoma
ReplyDeleteHakuna cha Uraia wa nchi mbili. Chagua moja, utasuka au kunyoa hakuna mambo ya kuanza kutaka yote.Kwanini utake Uraia wa nchi mbili kama sio tamaa? Huwezi kuwatumikia mabwana wawili, biblia inasema. Hawa mafisadi wanataka kuchukua uraia wa nch nyingine ili wakimbie bongo. Hapana tumeiona kwenye maono, hakuna cha uraia wa nchi mbili
ReplyDeleteSuala si kumkatalia mtanzania anayezaliwa nje ya nchi asiwe raia au yule aliyomba uraia wa nchi nying kuwa tena raia wa Tanzania. Suala ni maslahi na usalama wa nchi. Jiografia imeiweka Tanzania mahali ambapo ukiruhusu uraia wa nchi mbili basi Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda nk wote wanaishia Tanzania. Juzi umeliona suala la ardhi lilivyowatoa macho Wakenya. Ukiwapa uraia watu hawa utaiweka nchi katika hali ipi? Hebu tuweke makini. Tusiweke maslahi binafsi mbele na kuacha maslahi ya taifa ambayo matokeo yake ni kuiingiza nchi katika matatizo makubwa. Na hoja isiwe kwamba tunachelewa kufaidika na uraia wa nchi mbili hasa kwa watanzania walioko nje kwani nchi haijakukataza kurudi nyumbani kwa paspoti ya USA au UK. Na wale ambao wako katika nchi hizo tajiri wasitumie kisingizio cha kupata haki sawa na wazawa wa nchi hizo kwani nchi hizi zinatoa fursa kwa sawa kwa wote na hasa wale ambo wamekaa kipindi kirefu cha kufikia hatua ya kupewa uraia. Hebu tuwe makini na tusiishinikize serikali kwa mambo ambayo yanaweza kutuletea matatizo mbele ya safari kama tukikurupuka na kuwa na uraia wa nchi mbili. Na wala watu wasiseme kuna mtu anawaonea wivu kwa wao kuwa raia wa nchi tajiri, La hasha! Hoja kubwa ni MASLAHI NA USALAMA WA NCHI YETU NA WATU WETU.
ReplyDeleteMdau Msemakweli mada yako nzuri, ila inabidi lugha yako ya asili yaani kiswahili uipige msasa na utafute kamusi(iwe kitabu au internet).
ReplyDeleteNakusaidia baadhi ya maneno, nikianza na yaliyo na kasoro na kufuatwa na neno sahihi:
jumuhiya= jumuia
jamuhuri= jamhuri
muhungano= muungano
akumfanyi= hakumfanyi
heti= eti
hasiwe= asiwe
sikuu= sikukuu
hunganisha= unganisha
aswa= haswa
hili= ili
hasili= asili
atuwezi= hatuwezi
swala= suala
uduma= huduma
uhajemi= uajemi
Mdau
Visiwa vya Papua New-Guinea
Ocenia.
Pamoja na kiswahili kibovu, sioni kama arguments za huyu mleta mada zina mashiko. Mpaka sasa sijaona na wala sijasikia faida zozote zile ambazo hao wanaosema wako nje wameiletea TZ. Sasa wanatushawishi vipi kwamba wakipewa uraia Tanzania itafaidika kupitia wao. Na hata hivyo mpaka sasa sijasikia m-TZ yeyote ambaye amezuiliwa kuwekeza au kuendeleza jambo nyumbani ati kisa ameukana uraia wake au kajilipua huko ughaibuni.
ReplyDeleteKama una mtaji wa kutosha we jitome nyumbani na gamba lako la US au UK fanya mambo yako hakuna wsa kukuzuia, Bongo ni yetu na wabongo sote twaifahamu. Ila usilete UFISADI maana tulio nao unatosha!
Tunatawaliwa na MAFISADI na tumeturia tuli.Heshima hakuna kwa kuombaomba wakati Nchi inajulikana ulimwenguni kwa kua na maliasili nyingi.
ReplyDeleteMichuzi Thanks for posting hii habari ya dual citizenship. Nashindwa kuelewa kwa kweli ni kitu gani kinawafanya wanasiasa wetu washindwe kuoan manufaa ya dual citizenship. It's pathetic. Mimi ombi langu ni kuwa nyinyi waandishi mna power kubwa sana katika profession yenu kwenye kila kitu, kwahiyo please use your profession (nguvu ya kalamu) kuishinikiza serikali kwenye hili jambo na mengine muhimu ya kijamii. Why does it take miaka kuamua the obvious? I was astonished kuona msomi kama Prof. Shivji nae analipinga hili swala labda kwa sababu binafsi!
ReplyDeleteSina imani na uwezo wetu kutengeneza mfumo wa uraia wa nchi mbili utakaosaidia nchi yetu na watu wake. Watungasheria wetu bungeni ndio hao wanaokoteza PhD za 'hamsini hamsini za reo reo' kwenye internet. Itakuwa kama mikataba yetu ya madini, tutapanua wigo wa ufisadi.
ReplyDeleteKwanza kwa anony wa 12:15AM hapo juu: SERIKALI YA TANZANIA SIYO MALI YA WAANDISHI WA HABARI, NA WALA HAIPO MADARAKANI KWA RIDHAA YA WAANDISHI WA HABARI. SERIKALI YA TANZANIA NI YA WATANZANIA WOTE. NA NI IMANI YANGU KUWA MAAMUZI YOTE, YATOLEWAYO NA SERIKALI HII NI KWA FAIDA YA WATANZANIA, WALIOPO SASA NA WATAOKUJA. TAFADHALI USITULEE MAMBO YA WEST HAPA.
ReplyDeletePili, najua kinachowasumbua ndugu zangu mliojipatia uraia wa nchi nyingine(na KUUKANA uraia wenu wa asili) ni kutaka kuingia Tanzania FREE OF CHARGE!!Hakuna anayewazuieni kuwatumia ndugu na jamaa zenu vijisenti, wala kuja kuwatembelea,lakini mtakuja kama wajavyo watu wengine wasio watanzania. Kwa kifupi ni kwamba mtalipa kuja KWENU!! MAMBO YA VISA HAYO! nasi mliotuacha tupate angalau ka mchango kenu kwa maendeleo ya nchi yetu. Maana siye tunalipa kodi. Nanukuu toka kwa mchangiaji hapo juu: Tanzania inahitaji WAZALENDO NA SIYO RAIA. Ni mzalendo tu atakayejenga nchi yake na kuwa na uchungu nayo. Namaliza kwa kuwauliza ndugu zangu mnaotaka 'dual citizenship', NI NANI KATI YENU ATAYEKUBALI KUWEPO HAPA TANZANIA MAMBO YAKIBADILIKA NA KUWA KAMA YALIYOTOKEA KENYA BAADA YA UCHAGUZI?
Kuna wengine wanataka kutumia mwanya wa uraia wa nchi mbili kutuharibia amani ili waingie mitini kiurahisi. Majority tutabaki hapa home tunakula kisago wenzetu wachache wapae zao kiulaini baada ya kututibulia. No please tuendelee kusubiri na kutafakari. Tusifanye pupa ktk mambo nyeti haya!
ReplyDeleteMimi ni Mtanzania mwenye pasi mbili. Nimehama Kanada kihalali na nikapewa uraia wao nilipoomba.
ReplyDeleteKama Watanzania wengine wanaoishi nje na pasi mbili, mimi naitumia ya Kanada kwenda nje. Maswala yanapungua katika uwanja wa ndege wa ulaya magharibi na sihitaji viza kwenda nchi za EU na Marekani. Familia nawasaidia Tanzania kama kawaida na sina shida yoyote nikiitumia pasi ya Kanada kwenda likizo Tanzania.
Kwa hivyo, mimi na wengine wengi nje ya Tanzania, sheria za Tanzania za uraia mmoja hazitugusi kabisa. Sana sana, serikali itakosa dola zangu 50 ikiniruhusu kuingia na pasi mbili.
Naomba tubaki kwenye uhalisia.
ReplyDeleteWewe umezaliwa Tanzania, umekulia Tanzania then ukahamia nje na kuchukua uraia wa huko ulikohamia.
Je ndio kusema utashindwa kuja Tanzania na kufanya mambo yako ya kiuwekezaji?
Utashindwa vipi wakati wewe umekulia hapa na unajua kona na vichochoro vyote?
Au unaomba uraia wa nchi mbili ili kukwepa kulipa vijisenti vidogo tu vya VISA ya Tanzania?
Kama kweli unaona ada za VISA ya kuingia Tanzania ni mzigo then how can you argue on grounds za uwekezaji?
Ni wazi kwamba hujui uwekezaji ni nini.
Ingekuwa uraia ni kikwazo kwa uwekezaji basi tusingekuwa na kina Barrick Gold, MovenPick, Kempisky, etc.
NAPINGA HOJA YA URAIA WA NCHI MBILI. CHAGUA MOJA, KUSUKA AMA KUNYOA.
sijasoma iyo newz apo,,ila kutokana na annons apa inaonekana ni mambo ya uraia wa nchi 2,
ReplyDeletesisi kama wa-tz tubakie tu ivivi nini tunakimbilia nchi 2???ulimbukeni wa watu bongo wooote watakimbilia kujisajiri majuu wee bila kuelewa kwanza.
oyaaa nyie mnaotaka KAJILIPUENI UKO-UKO tuu
NO URAIA WA NCHI 2
MIMI NAWASHANGAENI SANA MNAOKAZANIA URAIA
ReplyDeleteMTU ANAISHI POPOTE DUNIANI ILI MLADI ROHO YAKE INAAMANI NA AISHIPO
MAMBO YA URAIYA HAYAMSAIDII MTU HUU ULIKUWA NI UJANJA TU WA WAZUNGU KUWEKA MIPAKA ILI KILA MTU AMILIKI SEHEMU YAKE.
HATA UKIJILIPUA POA TU KWANI HATA YESU ALIKUWA MKIMBIZI SO MINAONA POA TU NA KUTAKA URAIA WA NCH MBILI NI SAWA NA KUCHANGANYIKIWA
Dual citizenship is absolutely necessary for all the right reasons, and if countries like America or Germany allow it...why should Tanzania feel that it knows any better?Ndio maana hatuendelei.
ReplyDeleteKipofu hawezi kumwongoza kipofu mwenzake.Mdau wa Papua New Guinea umeamua kumkosoa mwenzako wakati ww mwenyewe unakosea.
ReplyDeleteKosa Sahihi
Jumuhiya/jumuia Jumuiya
hunganisha/unganisha Huunganisha
Aswa/haswa Hasa
swala/suala Swala
NB:- Uhajemi ni sahihi tofauti ni
kuwa "H" haitamkwi kama
isivyotamkwa ktk HOUR.
Walimu wenu wa kiswahili lazima walifoji vyeti.
Ama ni "Mother Tongue" effect kama ndugu zangu Wahaya wanapenda kuongeza "H" mahali pasipotakiwa.
Wakurya hawana "L" wao ni "R"
Wahangaza hawana "R" wao ni "L"
Wachagga na Wapare wao Vurugu mechi mara "z" ibadilishwa na "S", "Th"
Wamakonde dah
I DON'T BELEAVE IN ANYTHING EXCEPT ACCEPTING ANYTHING NECESSARY FOR MY SURVIVE. I WILL DENY TZA CITIZENSHIP TO GAIN EUROPE,AMERICA OR JAPANISE CITIZENSHIP IF I CAN'T GET BOTH.I'LL HAVE BETTER CHANCE FOR GOOD EDUCATION,SOCIAL SERVICE AND HELPING MY FAMILY IF I AM AMERICAN OR EUROPEAN CITIZEN. TOO MUCH POLITICS! WHY NOT DUAL CITIZENSHIP! HONESTLY I WILL LOOSE NOTHING IF I DENY TZA AND GAIN USA OR EUROPE CITIZEN. MICHUZI YOU NEVER HEARD 'AFADHARI NIZALIWE MBWA ULAYA KULIKOKUA TZA' REALISTIC WE NEED DUAL TO HELP OUR ECONOMY. SEE AMERICA, GERMANY, ENGLAND AND MOST OF EUROPEAN COUNTRIES HAVE DUAL CITIZ AND MAKING PRETTY SAFE, WHAT'S THE FU**** WRONG WITH TZA LEADERS? WE NEED THAT! NO MORE POLITICS ;LETS STEP UP OUR GAME.
ReplyDeleteIT IS WHAT IT IS.
Haters utawajua tu kutokana na maandishi yao. Hawa ni wale wanaotaka kwenda ughaibuni lakini hawawezi ama niwale waliojaribu kwenda kwenye balozi mbalimbali na benki statements na vyeti vya kufoji wakapigwa chini. Hasira zao wanamalizia kwa walio pata mwanya huo. Anony mmoja hapo juu kawapa faida moja kubwa na muhimu sana nayo ni uwezekano wa kusafiri kwenda nchi yeyote bila purukushani za viza ukiwa rai wa mataifa makubwa. Hamjawahi kusafiri hamjui haya mambo kwa hiyo kaeni kimya wenyekujua wawaeleweshe. Wengine wanaleta masuala ya warundi na wanyarwanda kinachoombwa hapa ni kwa ajili ya watanzania na siyo kwamba eti tz ikiruhusu kwa raia wake basi itakuwa imeruhusu na kwa nchi zingine.
ReplyDeleteMwingine eti anasema amani itaharibiwa na uraia wa nchi mbili!!! Mwe!!!! tanzania kuna amani gani? Albino anayewindwa kama mnyama anaijua hiyo amani unayozungumzia? Halafu mbona akina manji, rostam na waziri wenu masha wana urai wa zaidi ya nchi moja?
Kwa taarifa yenu America haikubali dual citizenship. Ukipata uraia kama ulikuwa una visa unasurrender passport a kamaulikuwa greencard unairudisha hiyo pia. Ukweli ni kwamba kama ulikuwa na greencard hawakuulizi passport ndio maana watu walio upgrade kupata uraia kutka greencard bado wana passport za nchi zao. Ila America hairuhusu dual citizenship.
ReplyDeleteMdau Minnesota
Wewe anony wa April 25, 2009 1:24 AM kichwa chako ni ugoro mtupu! Nani kakuambia kuwa serikali ya Tanzania ni mali ya waandishi? Waandishi ni watu muhimu kwenye jamii yeyote ile wewe kunguru mkubwa. Angalia keep left ya BOT inavyofanyiwa kazi kwa sababu ya kalamu ya Issa bin wa Michuzi. Yaani nyie ni wale mnaokimbilia kukurupuka bila hata ya kutafakari kilichoandikwa au jambo. Lete hoja ya msingi kupiga issue sio upumbavu. Nafikiri shule hukufanya vizuri wewe umebakia na wivu kike tu.
ReplyDeleteWEWE KICHWA HAPO JUU HII INAMAANA GANI:- Nafikiri shule hukufanya vizuri wewe umebakia na wivu kike tu....Kama umeshindwa kuchangia mada funga bakuli lako hapa hatupo katika kukashifu wanawake...Wivu wa kike??? Inamaana wanaume hawana wivu...Ukome tena ukome kabisaa..Ukichangia mada usipende kuweka ujinsia ndani yake..Changia mada kama ilivyo takiwa...
ReplyDeleteMNAOPINGA URAIA WA NCHI MBILI HAMNA SABABU KUBWA YA MAANA. HIVYO KUSEMA SABABU YA USALAMA MNA MAANISHA NINI? FUJO ZINAZOTOKEA KATIKA NCHI USABABISHWA NA URAIA WA NCHI MBILI? ACHENI WIVU.WATANZANIA WENGI WAPO NJE YA NCHI NA WENGINE NI WASOMI SANA KIASI CHA KUWA WAMEPEWA URAIA WA NCHI HIZO KWA MASLAI YA NCHI HIZO. WALE WASIOJUA NI KUWA KUNA WATANZANIA WATAALAM WA NYUKLIA NA FANI NYINGINE KUBWA WAMELAZIMIKA KUPEWA URAIA WA NJE KWA MASLAI YA NCHI HIZO, HIVYO TUKUWA NA URAIA WA NCHI MBILI WATU KAMA HAO, WANAWEZA KURUDI NCHINI NA KUISAIDIA NCHI. KATIKA DUNIA YA SASA URAIA WA NCHI MBILI AUKWEPEKI.
ReplyDeleteNadhani uraia wa nchi mbili au tatu au moja haumfanyi mtu asiwe Mtanzania au Mzalendo.Nafahamu watanzania wengi ambao wapo nje ya nchi ambao ni wazalendo kuliko hao waliokuwa Tanzania na nafahamu pia watanzania wangapi ambao wapo nje ya nchi wanataka kurudi Tanzania kwa sababu zao binafsi za kuchuma mali ya nchi na kukimbia.
ReplyDeleteKenge
kwahiyo swala la raia kuwa na uraia wa nchi mbili liwe swala la wananchi watanzania kuamua na sio liwe swala la kulazimishwa kila kitu kina faida na hasara zake huo ndio ukweli wenyewe.
Mimi nipo nje lakini sifikiria hata kidogo kuishi tena Tanzania kwenye maisha yangu ya baadaye na wala sifikiri kwamba nikipewa uraia wa Tanzania utanisaidia lolote japo nafahamu naweza kusaidia Tanzania kama nchi niliyozaliwa na nimeweza kujenga visima vya maji na Nyumba kwa ndugu zangu lakini hilo halinihalalishi mimi kupewa uraia wa Tanzania.Nimetumikia Serikali ya Tanzania kwa miaka 10 na nikaamua kuhami ughaibuni kwa sababu zangu binafsi sasa sioni haja ya watu kun'gan'gania urai wa nchi mbili ila cha muhimu watu wafahamu hata Hashim Thabeet karibuni tu atapewa uraia wa USA na watu wakumbuke hatakuwa tena Mtanzania na nchi isije ikajivunie alikuwa Mtanzania
WATU WAACHE KUONGOPEA WANZAO KUHUSU DUAL CITIZENSHIP ANGALIA HIYO
ReplyDeleteDual Nationality USA
The concept of dual nationality means that a person is a citizen of two countries at the same time. Each country has its own citizenship laws based on its own policy.Persons may have dual nationality by automatic operation of different laws rather than by choice. For example, a child born in a foreign country to U.S. citizen parents may be both a U.S. citizen and a citizen of the country of birth.
A U.S. citizen may acquire foreign citizenship by marriage, or a person naturalized as a U.S. citizen may not lose the citizenship of the country of birth.U.S. law does not mention dual nationality or require a person to choose one citizenship or another. Also, a person who is automatically granted another citizenship does not risk losing U.S. citizenship. However, a person who acquires a foreign citizenship by applying for it may lose U.S. citizenship. In order to lose U.S. citizenship, the law requires that the person must apply for the foreign citizenship voluntarily, by free choice, and with the intention to give up U.S. citizenship.
Intent can be shown by the person's statements or conduct.The U.S. Government recognizes that dual nationality exists but does not encourage it as a matter of policy because of the problems it may cause. Claims of other countries on dual national U.S. citizens may conflict with U.S. law, and dual nationality may limit U.S. Government efforts to assist citizens abroad. The country where a dual national is located generally has a stronger claim to that person's allegiance.
However, dual nationals owe allegiance to both the United States and the foreign country. They are required to obey the laws of both countries. Either country has the right to enforce its laws, particularly if the person later travels there.Most U.S. citizens, including dual nationals, must use a U.S. passport to enter and leave the United States. Dual nationals may also be required by the foreign country to use its passport to enter and leave that country. Use of the foreign passport does not endanger U.S. citizenship.Most countries permit a person to renounce or otherwise lose citizenship.
Information on losing foreign citizenship can be obtained from the foreign country's embassy and consulates in the United States. Americans can renounce U.S. citizenship in the proper form at U.S. embassies and consulates abroad.
MJUSI,TANDIKA
Anon apr 26,2009 9:48Pm
ReplyDeleteNimeshasikia Marekani inakubali Dual citizenship.Kuna wamarekani kibao wana uraia wa zaidi ya nchi moja.Pia inategemea na nchi unayotoka kama ina dual citizenship..Sio kweli kuwa Marekani hawaruhusu hili jambo
mungu wangu! mjamaa aliyetuma hii stori anajua anachokifanya!!!!!!kwa kuwavuta watu na maoni ya asira!Msema Kweli endelea hivyo hivyo
ReplyDeleteWewe anony wa April 27, 2009 1:44 PM akili zako ni finyu sana. Wewe ndio umeshindwa kuchangia mada na ndio wewe anony wa April 25, 2009 1:24 AM. Wivu kama nini vile, nyooo ibilisi mkubwa wewe. Watu kusema wivu wa kike sio matusi babu wewe ila inakuwa matusi kwa mwanamke kuwa na wivu wa kiume and vice versa. Umeshindwa kujibu hoja unajifanya wewe sasa umekuwa mkufunzi wa BAKITA, kwa nini hukuendelea kutoa hoja za kuitetea argument yako kuwa serikali ya Tanzania sio ya waandishi wa habari, nyooooo! Hata watergate scandal imeibuliwa na wanahabari, ibilisi mkubwa wee unawangia watu tena mchana kweupee hapa kwenye globu yetu ya jamii!
ReplyDelete