Habari Brother Issa. 
 
Mimi ni mmoja wa wadau wa Blog yako. Haipiti Asubuhi bila ya kufungua na kuona nini kimejiri. Pia hutembelea sites/blog nyengine kwa lengo la kujihabarisha. 
 
Leo katika Website ya BBC, nimepata hii (attachement), naomba sana uwarushie wadau wengine. Ukiweza, nifikishie salamu kwa Jeshi la Polisi Tanzania. Wao wanafanya jitihada gani kuzuia Unyanyasaji wa Raia kutoka Polisi?? (Juzi tuu, pale Buguruni nimemuona Askari wa Trafic anampiga Vibao Dereva wa DalaDala), Ni kweli alifanya Uzembe, lakini jee hii ndio sheria??
 
Mimi ni mmoja ya watu wanaokerwa sana na vitendo viovu vya Polisi Watanzania. "Unyanyasaji, Rushwa na kutokujali sheria za Nchi" Kwa bahati mbaya hapa Tanzania, hakuna mtu anaewakemea. Hivi ni kweli kazi yao haina Maadili?. 
 
Ok, hii imetokea Uingereza na bado mziki unaendelea. Habari kamili
 
Mdau Salim, 
Kitunda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Madereva wa bongo wanaelewa kichapo tu. Sheria zimewashinda na askari wakizi kuwachekea basi wao ndio wanazidi kujiona wajanja.
    Hawa ni kichapo kwenda mbele ndio kitawafanya wafuate sheria.

    ReplyDelete
  2. Ukileta sheria za dunia ya kwanza huku kwetu haitowezekana.

    ReplyDelete
  3. Tanzania hakuna haki za bimadamu ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa,kwa wenzetu ndo kosa kubwa kumpiga raia tanzania wamezidi unyanyasadi kuaznia polisi na wanajeshi bao tupo numa sana kwa haki zetu,sijui JK akiangalia bbc anasemaje kuhusu hili au ndo amepunmzika ikuli hakuna wa kumsusa basi mtajua wenyewe mnaonyanyaswa natamani ningekua kiongozi labda ningebadilisha jambo kuhusu hawa mapolisi wa tz wala rushwa mafisadi.mtu umepotelewa na ndugu yako au kauliwa baso unaanza kuwahonga ili wakusaidie au umeibiwa unawahonga watafute mwizi wakati ni haki yako na unalipa kodi bila hivyo wala husikilizwi,!!!TUTAKUWA HURU LINI WATANZANIA

    ReplyDelete
  4. Anayepiga vibao naye akubali kuzabwa vibao na aliye juu yake ndo atajua utamu au adha ya kupigwa kibao. Tatizo ni hao wenye madaraka kujiona wako juu ya sheria. Kama kila mtu akijichukulia sheria mkononi basi hakutakuwa na haja ya kuwa na vyombo vya dola kama mahakama. Itakuwa ni utaratibu wa nyikani ambapo mwenye nguvu ndo mwenye haki. Huyo dereva wa daladala ana haki ya kumshitaki huyo trafiki kwa unyanyasaji. Hao wanaoshabikia upuuzi huu kuna siku yatawafika ndo watagundua kuwa kunyanyaswa si jambo zuri kwa sasa hawajali na wanasahau msemo MKUKI KWA NGURUWE KWA BINADAMU MCHUNGU.

    ReplyDelete
  5. tunachapwa,,,tunaua basi kazi inaenda bongo

    ReplyDelete
  6. Askari wa Tanzania wote hasa jeshi la polisi wanajiona kuwa wapo juu ya sheria, askari anaamua kumpiga raia au kutukana matusi makubwa ya nguoni; ni wakati umefika sasa sisi wananchi wakawaida tunapopigwa au kutukanwa na askari tuiangalie sheria na tusikubali kuwa wanyonge kwani nao ni watanzania kama sisi uoga wetu ndio unatufanya tuonewe lakini hakuna mwenye sheria ya kumpiga wala kumtukana mtu haswaa hawa askari wa chini chini, mie nafikiri kama kupiga au kutukana ni haki ya polisi basi Kamanda Kova mkono ungekuwa umeshaenda upande kwa kupiga. Alafu hawa wazee wa rusha roho (defenders) mbona wanakuwa wababe kuliko maelezo yaani wakikaa kwenye hizo defender huko nyuma utafikiri wao ndio wenye nchi, wanaleta ubabe kwenye nchi ya amani hebu wajaribu kwenda Darfur kama watajitanua kama wanavyojitanua mitaa ya buguruni na manzese.

    ReplyDelete
  7. KUDUNDANA HAKUTAISHA MAANA HATA POLISI WENYEWE WANADUNDWA VIBAO NA WAKUBWA ZAO KILA KUKICHA,KAMA UNABISHA WAULIZE WATOTO WAO WANAOISHI KOTA WATAKWAMBIA BABA ZAO WANAVYOKUNG'UTWA TENA MBELE YA FAMILIA ZAO.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...