waziri wa habari, utamaduni na michezo, mh. george mkuchika (kati) na jenerali mstaafu mirisho sarakikya (kulia) wakibadilishana haya na yale na rais wa tff sir leodegar chilla tenga baada ya mechi
kama kawa mabango ya wadhamini yalikuwepo kila kona
vodacom walileta kundi kubwa la watoa burudani
kocha marcio maximo kesharejea kutoka likizo yake na hapa anapozi na kamanda wa kanda maalum ya dar afande selemani kova (shoto) na mdogo wake afande kova. hakika afande anastahili sifa kwani mpangilio wa ulinzi ndani na nje ya uwanja ulikuwa msano
maximo akipozi na wapenzi wa kandanda
jua limeshakuchwa, mechi imeisha na kila mtu anarejea kwake. ila mambo ya kupaki kwenye nyasi bado ni kero ambayo ipo katika wanja letu jipya la neshno.

MPIRA UMEMALIZIKA SALAMA SASA HIVI NA MATOKEO NI YANGA 2 NA SIMBA 2.

SIMBA WANAONDOKA UWANJANI WAKIWA BADO WAMESHIKA NAFASI YA PILI KWENYE MSIMAMO WA LIGI NA WANA MICHEZO MIWILI MKONONI AMBAYO YOTE WANATAKIWA KUSHINDA ILI KUJIHAKIKISHIA NAFASI YA KUWAKILISHA NCHI KWENYE MICHUANO YA CAF.

YANGA WANAONDOKA KWA FURAHA KIASI KWANI UBINGWA WALIOKUWA WAMEUCHUKUA KITAMBO HAUJAINGIA DOA KUBWA SANA NA WATATUWAKILISHA KWENYE KOMBE LA KLABU BINGWA LA AFRIKA.

KOCHA WA SIMBA JAMES PHIRI AKIONGELEA MECHI YAO YA LEO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Simbaaaaaa! Simbaaaaaaa! Simbaaaaaaaaaa! Nyie simba, Mzoea punda hapandi farasi! Rudini mchangani ndo kunakowafaa!!!

    Mnyama Mnyama tu na hilo jina tu, nguruwe ninyi!!!!!

    ReplyDelete
  2. michuziiiiiiiii oyeeeeee uko juuu kakaa kwa up date data ongera sana misoupuuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  3. kaka na wewe mbon mnazi wametoka mikono mitupu wapi wakati wapo nafasi ya pili na ligi haijaisha???? acha hizo kaka!!!

    ReplyDelete
  4. Haya Kaka misupu Tupe kwa ufupi Ndani ya 90+ kadha ndani ya dimba la Taifa Mpya nasikia eti Yanga Wamemaliza mechi wakiwa 9 Uwanjani Ni Kweli Usisahau na mi snap Sisi tuliombali na Bongo tuweze kupta Taswira Teh Teh Teh Mbunge Wa nani hino...na balozi wa nanihiii...

    ReplyDelete
  5. Ina maana mnyama hata nafasi ya 2 kakosa?

    ReplyDelete
  6. Asante Kama Michuzi kwa kutuletea Mechi ya Yanga na Simba kwa picha

    More Pics if possible -- RR --- New York

    ReplyDelete
  7. Msalimie Beda Msibe "lUKWANGULE", mwambie salaam zake toka New York, tikiso la Yanga Imara limevunja mzizi wa fitina.
    Asante kwa kutupatia hvbari jinsi mpira ulivyokuwa unaendelea. Jioni hii nalala nikiwa si mteja wa msimbazi. ASANTE SANA

    ReplyDelete
  8. Acha unazi michuzi SIMBA hawajapoteza bado hiyo nafasi kama wakishinda mechi zao mbili zilizo salia kitu ambacho wanaweza. Nilitaka nikupigie debe TFF lakini inaonekana ukiingia madarakani yanga watakuwa mabingwa milele kama CCM inavyodai itatawala milele. Ama kweli rangi ya kijani nuksi kwelikweli.

    ReplyDelete
  9. Sheikh Yahya kakosea utabiri kwahio Simba 2- Yanga 2 kasema itaisha Yanga 2 Simba 1 na kutatokea Red Card. Ndio mpira Mie kama Simba nawapa Hongera Yanga kwa kuweza kutumia muda wenu wa kupewa Dk za nyongeza na kuutumia Vyema. Wacha turudi kusikiliza Kelele za Mtaa wa Congo na Msimbazi na Nyie mkavue Kambale Jangwani. Pazi.

    ReplyDelete
  10. good comments from phiri to praise young africans not in terms f football but also the way they adminstrate their club.
    simba needs to follow suit cuz thats the only way to get out of this old fashion leadership and brings in new and modern structure to govern club like simba.
    well done youngs africans.
    mdau lunyasi.

    ReplyDelete
  11. RR hapo juu ni Rakesh Rajani..Michuzi tunaomba ufafanunuzi hizo parking..kwa nini watu wanapaki kwenye nyasi..DESIGN MPYA??

    HATUJAELWA BADO

    ReplyDelete
  12. "How can you be very very very satisfied with Position # 6?" just to make the matter worse, "we are now aiming to number #2" why not #1?, whats wrong with this Coach!?.

    Next time aim for #1,

    The rest was Just fine.

    B.

    ReplyDelete
  13. Mdau B. Kweli ufatilii kabisa Ligi ya Bongo, kocha alikuwa ana maana kuwa tunafuta nafasi ya pili kwaajili ya kombe la CAF sababu bingwa ni Yanga tayari tangu wiki mbili zilizopita......

    Mdau
    Maryland

    ReplyDelete
  14. Anon wa April 20, 2009 1:17 AM mbona unajiaibisha kwa papara? Au ndio security ya kuwa behind a computer unaweza kuongea upuuzi wowote? Mwenzio kasema alipokuja kakuta timu ipo namba 6, sasa hivi wamepanda mpaka namba 2. Na anataka wachukue hiyo namba 2 kwa sababu yanga washakuwa bingwa!

    Kama hujui kingleza satap!

    ReplyDelete
  15. aiseh michuzi
    uwezi kuamimi mimi naangalia ligi ya nigeria yaani nigeria primier league kila weekend, yaaani ligi yetu ni baaaab kubwa kuanzia wachezaji mpaka infrasructure tuko juuu kishenzi, this is my conclusion VODACOM PRIMIER LEAGUE IS ONE OF THE BEST LEAGUES IN AFRICA, WANAIGERIA HAWATUFIKII KABISA ORGANIZATION YETU NI NZURI MNO.

    ReplyDelete
  16. Kwanza mi napongeza timu zote mbili kwa kabumbu safi lililochezwa jana (HASA YANGA). Pili ulinzi ulikuwa wa kawaida tu. Ila mi nna tatizo na jinsi baadhi ya polisi wetu wanavyobehave kwenye sehemu ya watu wengi namna ile. Tatizo langu kubwa ni jinsi wanavyopenda kutumia nguvu kubwa UNNECESSARILY. Jana wakati watu wanatoka uwanjani baada ya mpira kwisha, nlishuhudia askari fulani wakiwaelekeza watu vizuri, ila kulikuwa na huyu mwenye FORCE NUMBER E1275 (mbavu mbili au tatu, Sikuipata vema) yeye akiwa ni ranked ofisa alitakiwa kuonyesha mfano kwa vijana ambao wako plain. Ila sasa huyu jamaa yeye alikuwa haongei, ANARUSHA BAKORA TU!!!! nlimshangaa sana. Wewe E1275 hebu jirekebishe, nyie ndo wachache mnaofanya jeshi la polisi lidharaulike kwa vile watu wanaona vitendo kama ulivyokuwa unafanya wewe jana na wale wapuuzi wachache waliokuwa wanakutetea ni kujidhalilisha na kudhalilisha jeshi. Lazima mjue jinsi na kudeal na washabiki wa soka. MIGUVU YENU HAITASAIDIA SANA.
    mdau,
    Chiggs, DAR

    ReplyDelete
  17. Acha mpira, mimi namfagilia Michuzi kwa Kiingereza kilichotulia. Hivi ndio huwa unatudanganya, eti wewe Kiinglishi iz not richebo? Tena unaongea vizuri mno, sikutarajia. Wewe ni kiboko. Nimekukubali.

    Mdanganyika - USA

    ReplyDelete
  18. NYASI + PARKING OF CARS=???????

    ReplyDelete
  19. mhe imani madega jifunze kuongea kutoka kwa phiri huyu ndio mwana michezo look the way he talk so sweet.

    ReplyDelete
  20. Huyu imani madega mbona haeleweki kiongozi gani huyu wa kuongoza klabu kubwa mbona hana hata chembe ya busara?

    Yani huo msura wake ulivo mchachu ndio na maneno yake yapo hivo hivo ovyooooo. anaoneka ni mtu wa kijiweni sana na ndio maana akakosa busara.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...