Mrisho Ngasa

TAARIFA TOKA LONDON ZINASEMA MCHEZAJI MRISHO NGASA WA YANGA AMBAYE YUPO HUKO KWA MAJARIBIO NA KLABU YA WEST HAM UNITED AMEONGEZEWA WIKI MOJA YA KUBAKI NA KUFANYA MAZOEZI KATIKA KILE KINACHOONESHA AMEWAKUNA JAMAA.

KWA MUJIBU WA WAKALA WA FIFA ALIEKO BONGO, SAIDI TULI, NGASA HAJASHINDWA KATIKA MAJARIBIO YAKE HAYO AMBAYO PIA YANA WACHEZAJI TAKRIBAN 30 TOKA SEHEMU MBALIMBALI AFRIKA, NA NAFASI ZILIZOPO HAPO WEST HAM NI TATU TU.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. Kila la KHERI Dogo maana mambo yako yanatisha,kwa sisi tunaofahamu SOKA tunakikubali KIPAJI chako.Litakuwa jambo zuri na sisi WATZ tukiwa na mchezaji anayekipiga Uingereza,pia akifanya vizuri italeta Changamoto na Wadau mbalimbali wa SOKA Duniani wataitupia jicho TZ.Mi naamini mlango ukifunguka tutakuwa na wachezaji wengi wanaocheza Ulaya na kwingineko kwani tunao wachezaji wazuri sana.Tatizo bado hatujajulikana KIMATAIFA.Mungu ibariki TZ,mungu libariki SOKA la BONGO lijulikane kimataifa.
    TIKA(THE KOP)
    ST-JEAN
    CANADA

    ReplyDelete
  2. Kila la heri mtu wetu, wadau tunazidi kukuombea ufanikiwe.

    ReplyDelete
  3. Michuzi acha hizo, semeni ukweli. Hii kufichana hali halisi ndiyo inafanya tuzidi kuwa nyuma.

    Inakuwaje wakala anayetambuliwa na FIFA aliyeko Bongo ndiye atoe taarifa wakati Yusuf mwenyewe kakaa kimya?

    Anyway, mmezoea kudanganywa ndiyo mnasikia raha.Kama nyie waandishi kweli si mpige simu West Ham wawaeleze? Too much speculation, wakati story iko wazi...

    ReplyDelete
  4. Kwako mdau wa tatu mwananchi.co.tz wanadai kuongea na Ngassa mwenyewe ambaye anasema kama habari hii inavyosema. Hapo tuseme Ngassa amewapiga fiksi au...

    ReplyDelete
  5. we anony wa 11:43 PM, unapo-question ukweli wa Michu tukueleweje. Kama unaamini waandishi wetu hawako competent unafanya nini hapa kwenye blog hii, maana news zote anazileta Michu na wewe huzisadiki.

    Pili unaposema tunapenda kujidanganya halafu wewe unajiexclude kama sio mbongo, unafikiri wewe hujidanganyi hapo na uasilia wako.

    Acheni hizoo, kama wewe unajua zaidi habari za Ngasa si uziseme sasa.

    Ngasa we wish you luck,

    mdau bongoland

    ReplyDelete
  6. Mimi ndiye nachanganyikiwa kabisa ninapoambiwa kuwa Ngasa ameongezewa wiki moja. Naona kama hizi habari ni za uwongo na zile zilizotangazwa na TBC ndizo sahihi kwa sababu zifuatazo.
    Kwanza, yule jamaa liyekuwa anaongea aliyepigiwa na mtangazaji wa TBC alikuwa London na hivyo ana ukweli zaidi.
    Pili, wakati Mrisho Ngasa anondoka, alikuwa akae kule wiki mbili ambazo zilikuwa zinaisha tarehe 28 mwezi wa nne kwa sababu alitakiwa afike kule tarehe 14 na mkataba wa kule ulikuwa wiki mbili. Kwa maana hiyo, yeye kukaa zaidi ni kwa sababu siku zake za majaribio hazijaisha. Kitendo cha kusema kaongezewa wiki moja kinachanganya na hivyo kuna walakini kuwa wiki moja ilitosha kumuondoa kwenye majaribio.
    Wazo langu ni kuwa,
    Ni vema wachezaji wa Tanzania watafutiwe timu kwenye nchi nyingine ili waonekane wakiwa nchi nyingine kuliko Uingereza. Kwa sababu, nchi nyingine hazina ushindani mkubwa kama Uingereza. Naona wachezaji wengi wa kutoka Afrika walianzia kwenye nchi nyingine ndio wakaenda Uingereza. Kwa hiyo, ni vema lugha nyingine zifundishwe kwenye mashule yetu kama. Lugha kama kifarasa na kidachi ni nzuri sana na zitawasaidia wachezaji wetu.
    Waandishi wa magazeti nao wanatakiwa wasitie chumvi nyingi sana na kufanya watu wafikirie mwelekeo usio sahihi. Waliisifia Yanga hapa, kumbe kwa Alhilal ni kama Daudi mbele ya Goliati
    Nawakilisha

    ReplyDelete
  7. We anony wa 9:25 unaposema nchi nyingine hazina ushindani unamaanisha SPAIN,ITALY,GERMANY au?

    ReplyDelete
  8. Jaribu kijana labda utatuweka kwenye ramani kwa mazuri. Huyu ni mtoto wa Khalfan Ngassa?

    ReplyDelete
  9. Ann wa 11.09, ni kwamba ni rahisi sana kupata namba nchi kama nchi kama FRANCE na NETHERLAND kuliko ENGLAND, huenda nimetumia kishwahili cha kutatanisha

    ReplyDelete
  10. Mdau 9:25Am unafikiri hata Ufaransa au Uholanzi ni mteremko? Kwanza lugha haimwongezei mtu kipaji. Fikiria Wabrazil,wanigeria, walivyotapakaa Ulimwenguni,unadhani wanatoka makwao wakijua kirusi,kiarabu,kijerumani,kigiriki nk? Mtu ukiwa na kipaji(soka) na ukiwa na bahati utafanikiwa.
    Vile vile kuna wachezaji wengi duniani wanajaribu bahati zao kila mwaka kama vile Ngassa na wanashindwa kufuzu kupata nafasi za kucheza.Kinachotakiwa ni kum-support Ngassa na kumwombea afanikiwe si kumkatisha tamaa kama jamaa wa tatu toka juu.
    Mungu mbariki Ngassa,Mungu bariki Tanzania.

    ReplyDelete
  11. Ni mapema mno mno kwa Ngasa kuchezea West Ham kwa sasa, ukweli upo wazi na haina haja ya kujadili kitu kama hichi. Sababu zipo wazi kwa wanaofuatilia soka ya kimataifa na si soka tu wengi wetu tumesikia kuhusu safari ya Hasheem Thabet akiitafuta NBA jinsi ilivyokua ndefu ikipitia milolongo mingi katika kuhakikisha anaiva ili kumudu kucheza NBA. Ni wachezaji wachache sana walioweza kucheza uk premier league tena kutokea Africa mfano ni kina Radhi Njaidi au Zaki ambao kwa kumbukumbu zangu wametoke Africa moja kwa moja kwenye Premier.
    Hivyo ushauri wa bure kwa mawakala ni kwamba haya mambo ndio kwanza tunaanza maana hadi kina Tuli nao mawakala siku hizi. basi jaribuni kuwapeleka wachezaji hasa wa chini ya miaka 18 kwenye timu kubwa kama hizi na type ya Ngasa wapelekeni ligi za nchi nyingine kama Scotland hivi, kama alipo Obua wa Uganda, ama second au first division teams in UK,France,Spain nk au ligi nyingine za ulaya kama Ureno, Switzerland nk huko wanaweza kucheza ligi kubwa za nchi kama hizo ila kwa West Ham ambayo hata Waingeleza wenyewe wanaishukuru kwa kuwazalishia vipaji mfano Rio na Anton Ferdinand, Joe Cole, Frank Lampard, Michael Carrick nk
    Ila nampa pongezi Bakresa kwa hatua aliyofikia hadi sasa na ningemshauri aongeze bidii na ufahamu katika suala zima la uwakala.

    ReplyDelete
  12. Kumbukeni kwamba pia kuna kigezo cha FIFA ranking

    ReplyDelete
  13. NCHI ZINGINE KAMA INDIA,BAGLADESH,SIRILANKA,PAKISTANI HATA COMMORO AKUNA USHINDANI.

    ReplyDelete
  14. Anny 1.03. Umenena vema kabisa. Ponezi kwa huyu wakala ni jambo la maana sana. Pia kuanzia chini ni jambo sahihi. Wachache sana wana fly kabla ya kutembea. Ukizingatia ukweli kuwa FIFA ranking yetu iko chini sana ni vigumu kupeleka mchezaji mtanzania moja kwa moja UK tena kwenye ligi Premier league. Wakala angetakiwa ampeleke Ngasa mahali pengine. Wale Wanorway ndio walikuwa sahihi kwa ngasa japo walionekana kudharau taratibu za FIFA tukapoteza bahati yetu.
    Mimi nashauri mawakala wajaribu chini kwanza

    ReplyDelete
  15. Tumuombee dua mtu wetu Ngassa. kila la Kheri Mwana.
    Chamsingi ni kukaza usiogope mtu mpira ndo ule ule tuu. kujiamini ndio silaha yako tosha. acha mcheche.

    Chebby.
    TMK-DSM.

    ReplyDelete
  16. VİJANA WAJE HAPA TURKEY NDO MWANZO MZURİ WA CHİPUKIZİ KAMA HAO KUMBUKA WACHEZAJI WENGİ WA NİGERİA KAMA AKINA OKOCHA,UCHE,AMOKACH PAMOJA NA ANERKA,RİBERY WALITOKEA HAPA UK NINGUMU JAMANIIIIIIIIIIIII

    ReplyDelete
  17. CHOCHOTE KINAWEZEKANA KTK SOKA,WALA HAIJALI UMETOKEA WAPI,KAMA UWEZO UTAWARIDHISHA HAO WEST HAM BASI HUYU DOGO ATAPATA NAFASI,KWANI NANI ALIMDHANIA HASHEM THABIT ANGELIKUWE ALIPOKUWA LEO? KIZURI NI KUWA NGASA TAYARI ATAKUWA AMEJIFUNZA MENGI KUTOKA HAPA WEST HAM,AKIREJEA TU BONGO HATA KAMA HAKUPITA TRILA YAKE,BASI ATAKUWA AMEJIFUNZA MENGI,NA ATAKUWA AMEBADILIKA KISAIKOLOJIA NA HATA ATAKUWA AMESOMA MENGI KUTOKA KWA BAADHI YA WACHEZAJI WALIOKO WEST HAM AMBAO ANAFANYA NAO MAZOEZI,CHAMSINGI KABLA HAJAPOTEZA MALENGO MAWAKALA WAKE WASIMCHELEWESHE KUMTAFUTIA TIMU SEHEMU NYINGINE ABROAD,KWANI HIVI SASA ATAKUWA NA MOTO NA KITU YA KUFANYA VITU VYA UHAKIKA,NA AKIPATA NAFASI NYINGINE BASI ATAWEZA KUJIKOSOA MAKOSA AMBAYO HII MARA YAKE YA MWANZO ATAKUWA KUNA MAKOSA FULANI FULANI ATAKUWA AKIYAFANYA KUTOKANA NA WOGA,KIMSINGI TUMPE SUPORTER HUYU DOGO ILI AITANGAZIE BONGO KTK CHATI YA SOKA DUNIANI,
    KUNA VIJANA WADOGO KUTOKA BUKINA FASO AMBAO WANACHEZEA BUNDESLIGA WANAPIGA MABAO KILA LEO,WAKATI BUKINA FASO WENYEWE TUMEWAPIGISHA KWATA NA KUWAFUNDISHA SOKA MARA MBILI NYUMBNI NA KWAO KTK AFRICA CUP QUALIFICATION YA GHANA,VIJANA TUNAO LAKINI WANAHITAJIA USHIRIKIANO WA PAMOJA WAtz

    ReplyDelete
  18. It's not like we are negative kwa hii endeavour ya Ngasa, lakini hawa jamaa siyo transparent, wababaishaji - kumleta London peke yake siyo hoja. Je wamefuata taratibu zinazotakiwa?


    Kwanini wanakaa kimya? Hivi kweli ndugu zangu mnaamini kabisa kwamba kama Ngasa na wakala wake wangekuwa wamefanikisha kazi yao wangekaa kimya wasiwafahamishe watanzania? Usiri huo haufai, kwasababu unatoa fursa kwa watu kuchonga.

    Lakini ngoja niwambie, tumeshapiga simu West Ham several times, jamaa wanasema Ngassa hakufuzu kuingia stage ya pili. Anyway, Jumamosi wanayosema siyo mbali we'll find out. Transparency is free.

    Wenye shauku, pigeni simu West Ham - ulizieni kuzungumza na Roger Cross, yeye ni Chief Scout.


    Ni mimi wa April 21, 2009 11:43 PM

    ReplyDelete
  19. MUNGU ATAKUSAİDİA MTU WETU TUPO PAMOJA NAWE

    ReplyDelete
  20. Baba UbayaApril 22, 2009

    wachezaji wa kibongo kama wakishindwa kupiga soka ktk nchi za Skandinavia yani hizo sehemu zingine za Ulaya itakuwa ngumu.ushindani sawa upo kila mahali lkn kuna baadhi ya nchi ni easy kidogo kuliko sehemu zingine.
    ni busara hao mawakala wakawatafutia timu/majaribio wachezaji wetu ktk nchi zingine za huko Ughaibuni na mambo yakikaa ktk mstari basi wanaweza kuingia nchi kubwa ktk soka
    ama hao mawakala wangewatafutia ulaji ktk timu zilizo madaraja ya chini kidogo na sio all the way to premier league.
    impossible is nothing.juhudi binafsi ktk hayo majaribio na pia kumpigia magoti Mola kunaweza kumsaidia Ngaza kututoa kimasomaso Wabongo.

    Wishing you all the best.

    ReplyDelete
  21. Hivi mozambique na Angola Wapo katika Rank ya FIFA Namba ngapi Na Ngapi?...Chad Je? Liberia? sidhani kama ni kigezo Msipende Kuombeana Mabaya kwa Sabuabu tu katoka Dar Young Africa(YANGA)Inasikitisha watu kuanza Kutupiana maneno ilihali Haitakusaidia Binafsi katika maisha yako kama Akifanikiwa au asifanikiwe Mbona Hasheem thabet Wote Kwa pamoja Watanzania Tunamuombea apate Kufuzu NBA? Soka haina Nchi unayotoka Wala Nini Kumbukeni maneno ya Anthony Yeboah na romario Waliposema kwa nyakati tofauti "There is only one language I speak well the language of football. ... What European club impresses you most with its .....!!!!namalizia kwa Maswali kwa wote Je yule mtia magoli stadi wa klabu ya AS Nantes ya ufaransa aliemaliza Ligue 1 akiwa mfungaji Bora mwaka 1996 Japhet N'doram kutoka chad aliitoka katika nchi iliokatika rank gani wakati huo?sasa hivi 130 au hata George weah wa Liberia wote walipitia Cameroun Moja Kwa moja hadi Ufaransa Hapo Sijakuambia Benjamin mwaruwari wa manchester City asili yake malawi Raia wa Zimbabwe Kila la heri Mrisho mungu atakusaidia upate Ridhki yako usitishwe na vigezo vya rank za FIFA mwaruwari anatoka Zimbabwe wapo nafasi ya 106 Tanzania Ya 101 wapi mbele wapi Nyuma? wapi juu Wapi chini?Sierra leone (110) lakini kina mahammed kalloni wanatandika ngozi Italia Angalia Cha msingi naomba niwafahamishe kuiwa kuna wa Uzbekistan,Kazakhstan,Kyrgistan , Liechtenstein Hata Kutoka Kisiwa cha Foroes wapo wanaocheza madaraja ya chini hata wanaojaribiwa katika vilabu vya Premier angalieni hizo nchi katika rank ya mwisho ya FIFA kabla ya kuanza kuropoka hovyo
    Asante
    Wako
    Ahmed Jeizan(Shebbe)Chimo

    ReplyDelete
  22. Michuzi, wafahamishe jamaa waache kubisha bila kufahamu sheria za ajira za Uingereza.

    Sheria yao inayosimamiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani [Home Office], inasema mchezaji ambaye si raia wa nchi za Umoja wa Ulaya [EU], ili afuzu kupata kibali cha kucheza soka England, anatakiwa awe anatoka nchi iliyo katika 70 za FIFA.

    Pia awe amefikisha mechi asilimia 75 ya mechi kwenye timu hiyo ya taifa, mfano Ngasa ni Taifa Stars.

    Hata hivyo, timu husika ikikunwa na kiwango cha mchezaji hata kama hakidi hayo matakwa, inaweza kumuombea kibali maalum Home Office - ambapo kutokana na application inaweza kukubaliwa au kukataliwa. Wapo wengi ambao walipitia mchakato kama huo. Ni sheria za UK, siyo universal!!

    Isipokuwa kwa Ngassa hakufuzu majaribio bahati mbaya, hawataki kuwambia ukweli wa mambo. Lakini soon itakuwa siyo siri tena.

    ReplyDelete
  23. jibu hili sio Swali Tena Benjamin au benjani Mwaruwari anatoka Zimbabwe Katika rank ya FIFA Zimbabwe wapo katika Nafasi ya 106 sasa hapo katika 70 overall iko wapi? Tanzania ni ya 101 au mchangiaji haijui hata Rank ya FIFA ilivyo? Mradi anachangia tu Kusikia ngassa anasaka Maisha katika klabu Cha Premier? iwe siri isiwe siri wenzetu hawaendeshi Vilabu kiswahili-swahili wana Principal zao sio kama sisi cha msingi ni kusubiri inaelekea umekerwa saana na kijana huyu wa kitanzania kujitafutia Riziki yake huko maana naona umekomalia suala la kutofaulu au kufaulu ikiwa siri isiwe siri wewe unakereka na nini?Mbona hatujawona watanzania walio US Wakifuatilia kwa jicho baya kama lako mafanikio ya hasheem thabet? Kaka acha roho mbaya huyo ni mtanzania mwenzetu akifanikiwa yeye ni kwa faida yake na sisi ni kwa faida ya kizazi chetu kijacho katika medani ya soka na tulishaambiwa ni wiki mbili yani tarehe 28 ndio wiki mbili hizo zitafikia tamati sasa wewe tokea juzi tarehe 21,tayari umeshaanza kuua kama Dogo huyo kafeli au kusudio lako tukujuwe kama una beba mabox huko Ughaibuni kazi ngumu ya kubeba mabox unaona Dogo atakuja kujipatia Ulaji huko hamtaki mnataka wabeba mabox,wasafisha vyoo,watunza vikongwe kama wewe? inaelekea ni Mkenya au Mganda una wivu na roho ya kwanini au korosho...MUNGU IBARIKI TANZANIA WABARIKI NA WATU WAKE AKIWEMO NGASSA MRISHO KHALFAN AMEEN.
    shaffiey Issa

    ReplyDelete
  24. Jamani naomba niwafahamisha jambo moja na la muhimu sana.Wachezaji wengi wanaotoka bara jeusi(Afrika)ni wachezaji wazuri sana lakini pindi wanapopata nafasi kuja ulaya kwenye majaribio wengi wao wanachoshindwa ni kutofata au kutoelewa au kushindwa yale mambo anayotakiwa afanye akiwa uwanjani,mbali ya kuwa mchezaji mzuri lakini ndani ya field(uwanja)kuna mambo mengi sana.

    ReplyDelete
  25. Hatahivyo, Ngassa huenda ameshindwa kuonyesha kiwango kinachoridhisha na sio kimo kwani katika ligi mbalimbali za Ulaya kuna wachezaji wenye vimo vifupi lakini wanategemewa na timu zao kama akina Robinho, Roberto Carlos na wengineo.

    * SOURCE: Nipashe

    ReplyDelete
  26. nyie mnajua kila mtu hapa anapiga box na kuosha vyoo na vibibi hapa kuna watu wana mawe kushinda huyo mchezaj wenu alyefeli majaribio muulizen mithupu anajua nyie danganyweni na bakhresa unafkir hapa unakuja kama chooni kucheza mpira

    ReplyDelete
  27. THERE'S LONG WAY TO GO B4 YOU BECOME PREMIER LEAGUE PLAYER. AND QUOTERS COULD BE A MAJOR FACTOR TO SIGN HIM AS WEST HAM PLAYER. LOOK AT ASIANS PLAYERS

    ReplyDelete
  28. Habari za kuaminika zinaniambia ya kuwa karibu jopo lote la makocha wote wa West-ham limekubali sana kiwango cha mchezaji Mrisho Ngasa, na wangependa kumsajili ila kinachozorotesha process ni umbo lake Mrisho, ambalo wanaogopa linaweza kuleta matata pale atakapoanza kucheza ligi kuu. Lakini bado yu ana nafasi ya kusajiliwa, ambapo jawabu litatolewa ijumaa ya LEO...
    Tunamuombea yote mema Mrisho!

    *THE EMPEROR*

    ReplyDelete
  29. nashukuru sana mchangiaji Wa mwisho The Emperor Kwa moyo mzuri na maoni yako ila napenda ni kufahamishe Unajuwa Urefu hali wa Ngassa? na je kimo cha Gianfranco Zola?Je obafemi martin au Pius Ndiefi? msinichekeshe kabisa katika suala la kimo Diego Maradona Hakuwa Mrefu ila alitisha Micheal owen Kadhalika Hakuna kigezo cha Kimo katika soka ...mwisho nakuambia Nyie Wabeba Mabox mtakufa na roho zenu mbaya za wivu na mavi ya wazee mikononi mwenu wajinga nyie unasema tumuulize mithupu usifikiri UK ni Mbinguni nimeishi huko tena kwa bahati karibu kabisa na hapo ulipo uwanja wa Upton Park Kituo cha Kwanza Nimeishi Barking Road naijuwa london kuliko wewe hakuna mbongo mwenye pesa huko wote wabeba mabox tu mshukuruni saana marehmu abdul msomali alikuwa akiwatoa tongo tongo zama zake alipokuwa akija huko masikini nyie

    ReplyDelete
  30. NINACHOZEA KUSEMA NI KUWA NI VYEMA NGASA AKATIWA MOYO BADALA YA KUMVUNJA MFANO TOSHA K KWA HASHIMU THABITI HAPANA SHAKA ATAFIKA MBALI HATA KAMA ATARUDI MARA KUMI ULAYA BADO KWA TAARIFA NILIZONAZO ANANAFASI NYINGINE UFARANSA HIVYO HATA KAMA ATASHIDWA UINGEREZA BASI ATAKACHOKUWA AMEJIFUNZA HUKO ATAKWENDA NACHO LIGE I,LAKINI KWA SIKU ZA USONI NI VYEMA TUKAJIFUNZA KITU KIMOJA KUTUMIA WKT ULIOPO ZAIDI ACHENI FITINA NA ROHO ZA KWANINI BOB K

    ReplyDelete
  31. we unaijua uk gan labda uk ya manzese we umekaa barking ya mmalampaka unasema wabongo hawana mawe labda hapo ulipofikia kwa ndugu zako wabeba box wabongo wana mawe wewe njoon mumchukue mchezaj wenu akacheze taifa, we muulize mithup au ulikuja uk mwaka 1920

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...