
Mchezaji wa Yanga Mrisho Ngasa akiwa na kocha wa West Ham United Gianfranco Zola wakati wa tizi la timu hiyo ambako Ngasa aliitwa kwa majaribio, lakini habari zinasema hakufanikiwa kupita. Ila sema West Ham wameahidi kumwalika tena Ngasa kwa mazoezi na ziara ya nje ya Uingereza kwenye mechi za wakati wa mapumziko ya Premier League, kwa mujibu wa wakala wake Yusuf Bakhresa. BBC Ulimwengu wa Soka jana jioni ilikuwa na stori yote na pia leo jioni.
kama utaikosa itafute
www.bbcswahili.com
Mdau wa London
HONGERA NGASSA KWA HATUA ULIYOFIKIA
ReplyDeleteNpaenda kutoa hongera kwa Ngassa, Juhudi zake zinalipa.Kwanza kabisa kitendo tu kile cha kuitwa na West Ham United kwa ajili ya mazoezi, na majaribio ni hatua kubwa sana hiyo.Na kizuri zaidi ni West Ham kuona umuhimu wa Ngassa kwa kumtumia hapo kwenye ziara za baadaye.Uwezo wake umemsaidia.Maana kitendo tu cha kufanikiwa kutoka kikosi cha pili cha mazoezi kwenda kujifua na Zola kwenye 1st Eleven kijana umekaza buti.
Naamini hizi mechi mbili za Taifa Stars dhidi ya DRC na New Zealand zitaongeza morali yako.Mambo yatakua sawia ndugu.
Mungu akusaidie ktk njia yako Ngassa.
MAKULILO, Jr.
www.makulilo.blogspot.com
Ngasa nenda college USA, halafu watakudraft kwenye MLS. Wachezaji wa TZ inabidi muanzie kwenye college kwanza, NCAAA. Wana Soccer, tennis, basketball, swimming, riadha, boxing nendeni college za Ulaya na USA kwanza; zipo scholarships kibao kwa wenye vipaji. Pesa baadaye.
ReplyDeleteHongera kijana,
ReplyDeleteMwanzo ni mgumu lakini usikate tama, hapo ulipo tayari ni hatua, huyu anayeongelea "scholarship" hapo anavuta bangi! Kukutana na Zola katika majaribio ni hatua kubwa, piga tizi kijana, ongeza mwili kidogo (piga chuma) maana lazima uwe "aggressive" kama unataka kucheza premier league. Safi sana kijana!!
Kama wadau waliotangulia, napenda kumpongeza sana Ngasa!Binafsi nimefarijika kuona amefikia hatua hii ambayo wachezaji wetu wengi hawajaifikia. Penye nia ipo njia, cha msingi ni kutokata tamaa na kuongeza juhudi katika mazoezi. Naamini nafasi bado ipo, sio lazima iwe kwa West Ham United, inaweza pia kutokea kwa timu yoyote nyingine itakayomwezesha Ngasa kuonekana katika ramani ya kimataifa ya soka. Hongera zake tena Ngasa!
ReplyDeletehttp://mwanasosholojia.blogspot.com
Hongera Ngasa kwa hatua uliyofikia usijali mambo yatakuwa sawa , tunazidi kukuombea
ReplyDeleteKwanza hongera sana Ngasa.
ReplyDeletePili mi nilikuwa naomba hao waliopeleka Ngasa UK, basi wangejaribu kumtafuatia team zingene kama Uholanzi, Ufaransa na France, hata turkey au Belgium. Na uwakika akifanya majaribu kama nchi tatu hivi basi anaweza bahati.
J Mwaikambo, Kampala
Mdau mike John uliyeongelea schplarship ni kweli wanaweza ku-apply vyuo Marekani. Lakini naona huyu Ngassa umri umeshaenda yupo kwenye late 20s au tayari 30s. Inatakiwa vijana chipukizi, si umeona Hashim Thabit?
ReplyDeleteShule, shule, shule kwanza. Ngassa ametemwa sio kwa kutokujua ball bali kwa upeo, mkubali mkatae. Ushauri wangu Ngassa na wengine wenye malengo kama yako waende shule, mzungu bila track record ni kama unampigia mbuzi gitaa, maana anachotaka mzungu sio kucheza leo tu bali muendelezo au 'sustainability'.
ReplyDeleteMawakala wa wachezaji kama Ngassa na kadhalika msiwe mna ng'ang'ania kuwatafutia timu za premier league ya England tu.
ReplyDeleteMfano Kali Ongala, Shaabani Nonda wamepitia na kucheza ktk nchi zingine za ulaya. Hivyo Uhuru Selemani pia akaze buti huko Finland, akionyesha kiwango atapata timu kubwa zaidi.
Hivyo Ngassa ukipata timu iwe ya Israeli(Yakubu- Everton sasa), Cyprus, Greece, Uturuki(Shaaban Nonda-Galatasaray) , Norway(Mikael Obi John-Chelsea sasa)n.k msiziachie nafasi hizo, pia kipato huko ni zaidi ya Yanga/Simba.
Mdau
jijini London.
Huyu ni mtoto wa Halfan Ngasa ambaye alikuwa nachezea Pamba na simba kama ungejua hilo basi ungekuwa unajua Ngasa ana miaka 19 siyo 30. Uzushi mtupu.
ReplyDeleteHongera Ngassa kwa hatua uliyofikia, ongeza juhudi na zingatia mafunzo mambo yatajipa. Athuman China alishapata kuchezea Reading ya Uingereza japo haikuwa kwenye premier league wakati huo. Nonda alicheza bongo kabla ya kwenda Ulaya. Uwezekano wa kucheza ligi za Ulaya upo kabisa.
ReplyDeleteWadau mnaosema apitie US na NCAA mmeangalia wasifu wa Ngassa kwamba unaendana na kupewa nafasi ya masomo huko? Vyuo vinaangalia mambo mengi, sio uwezo wa soka tu. Na mnapoangalia elimu msidhani ni physics na commerce tu, soka nayo ni elimu kubwa sana. Mashabiki mkiangalia mechi na Ngassa nina hakika kuna mambo mengi tu tactical yanayoendelea uwanjani ambayo hamtakuwa mkiyaelewa.
pamoja na kumpa hongera Ngassa pia,ningependa kumpa hongera huyu promoter aliyefanyikisha zoezi zima la kumpeleka huyo kijana.ningependa kumpongeza sana.na pia ninapenda kumpa wazo ,ikiwezekana asikimbilie UK tu,aanzie hata sehemu nyingine taratibu tutafika,na pia ajaribu na wengine pia,kwani wakifanyikiwa yeye atakuwa na pesa nyingi pamoja na kututoa tongotongo wabongo.mwisho,wenye umri mdogo na Elimu(kwa mawasiliano ) ni muhimu sana.
ReplyDeletebig up bakhresa!
TANZANIA KIMPIRA HATUJULIKANI KABISA NADHANI STATISTICS HATUJAWAHI KUFIKA KOKOTE KTK MASHINDANO YOYOTE TAKRIBANI MIAKA 30 HIVI NA HAWA HUWA WANAANGALIA HILO HUKU ULAYA KWA KIFUPI TANZANIA HATUNA NAFASI KABISA HUYO NGASA ACHA KUTOKUWA NA ELIMU KAMA MNAVYOSEMA INAYOCHEZA SIYO ELIMU NA WANAO CHEZA HUKU SIO WOTE WANAELIMU SEMA MIKAKATI IANZE KUKUZA SOKA LA BONGO KUANZAIA MASHULENI VIWANJA VYA KUCHEZA MAZOEZI NK. HALAFU HATA MASHULE YA MICHEZO YANGEKUWA YANAFUNGULIWA KWA USHIRIKIANO WA TFF. TFF ITAFUTE NJIA YA KUJIINGIZIA MAPATO KAMA BAHATI NASIBU MADUKA YA VIFAA VYA MICHEZO KUUZA MAJEZI YA TIMU ZA TAIFA NK KAMA HUKU ULAYA LAKINI HUKO MNATEGEMEA MICHANGO YA WAFANYA BIASHARA SOKA HALIWEZI KUKUA MCHEZAJI HAISHI KUKUMBILIA KWA WAFADHIRI KUOMBA PESA AKIPEWA MSHAHARA MZURI NA KUISHI VIZURI ATACHEZA VIZURI KAMA MSHIKO HAKUNA ATACHEZA VIPI WAKATI MAWAZO KIBAO
ReplyDeleteWEWE MDAU WA 2:57 ACHA UZUSHI NA KUWEKA TAARIFA ZA UONGO HAPA. ALIYEKWAMBIA NGASA YUKO KWENYE LATE 20s NI NANI? HUYU DOGO HATA TWENTY HAJAGONGA, NADHANI ANA 18-19. FANYA KARISECHI KADOGO KABLA HUJAKURUPUKA NA KUKOMENTI. NGASA KILA LA KHERI. RATIBA YA MISOSI ULIYOPEWA WESTHAM IFUATILIE KAKA, UTAFANIKIWA INSHA-ALLAH. Mdau Gordon, Dar es salaam
ReplyDeleteDaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaah inaniuma sana,why sasa?mi unajua nlikuwa nshaanza kuhesabu kuanzia agosti nakuwa nachek saaana game za westham nashangaa ghafla zinakuja hizi habari tena aah!Hii imesababishwa na nn tena?sababu inabidi zimwagwe ili kijulikane na kingine kuna timu zinazocheza championship hata ile league 1 vp kwani hakuwezi kupatikana huko timu Bakhresa?fanza mambo kiaina might be akienda na hyo kwamba ashafanya majaribio westham wanaweza fkiria kumcheck check km analipa n naamini dogo anakamua game la uhakika kisera km mie vile!LOL
ReplyDeleteHEBU JAMANI TUACHE HIZO HONGERA, HONGERE FOR WHAT?KWAKUFIKA LONDON HAPO HAPO SOKA IMEISHAKUA HISTURIA HAO JAMAA WANAKIMBIA KUANZA PROCESS ZA WORK PERMIT SO WAMEAMUA KUCHUKUA EU SAWA TUMEONA MANU WALIHANGAIKA ZA WAKINA MANUCHO THOUGH NI KIPAJI KILA MTU ANAJUA HILO NA NYIE MAAGENT WA KIBONGO MUACHE USWAHILI ET ATAITWA LINI BWANA HAWA NDIO WANACHAGULIWA KWA ALIJI YA NEW SEASON AUGUST SO NINACHOWEZA KUKUSHAULI NI ACHENI SAANA KUANGALIA UK KAMA MDAU ALIVYO CHANGIA HAPO JUU ANZENI NA NCHI NYINGINE ZA ULAYA KAMA BELGIUN UGIRIKI NA KWENGINEKO NDIO UNATAFUTIA KASI YA KUJA HUKU COS BY THAT TIME UTAKUA NA EXPERIENCE SABABU HUKU KILA KITU WANATAKA EXPERIENCE ZA KWAO
ReplyDeleteTHANX
mimi naona Ngasa aende kuanzia bonden may be anaweza kuwa mrefu na kupata chance but as i know ngasa kucheza uk itakuwa ngumu kwani wapo akina kally ongalla ni mwingereza tena ni mzuri zaid ya ngasa lkn amweshindwa kupata timu hapo nenda ngazi kwa ngazi kijana
ReplyDelete