HABARI YAKO MICHUZI, 

NAOMBA UNIFIKISHIE HII KWA WADAU.
 
MIMI NI BINTI WAKITANZANIA NAISHI SWEDEN LKN BADO NI MGENI NA HUKU NINAKOISHI NI VIGUMU KUKUTANA NA WATANZANIA WENZANGU NA HIVYO KUJISIKIA MPWEKE.
 
KWA MAANA HIYO NAOMBA KWA WATANZANIA WANAOPENDA KUJUANA(URAFIKI WA KAWAIDA KAMA WA DADA NA DADA AU KAKA NA DADA) NA MIMI WANIANDIKIE WAWE NI WATU WA KATI YA MIAKA 25 KUENDELEA.WANAWAKE KWA WANAUME LKN WASIWE WATU WA MAKUNDI,MASENGENYO.
 
HASA KWA WANAOKAA ÄNGELHOLM, LANDSKRONA,
HÖGANAS,ÅSTORP.KLIPPAN MAANA NI KARIBU KUTEMBELEANA.
 
Email adress.,  
flowermaua@hotmail.com.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. jishughulishe na kujali muda wako, kama una dini tafuta nyumba za ibada, mengineo yatajileta tu taratibu. ukiyatafuta utasononeka bure. ugeni ukiisha hutakuwa hata na muda wa kutaka kujuana, japo si mbaya pia utapata mawazo.pole kila mmoja hupita huko unapoingia ugenini. nakutakia mafanikio kwa kilichokupeleka huko.

    ReplyDelete
  2. dunia ni kijiji na ulaya pako karibu karibu. waweza kutembelewa hata na sisi wa uholanzi au kututembelea.

    ReplyDelete
  3. We mtoto wee huogopi waosha vinywa. Unataka kujuana na watu au unataka kutukanwa kwa masharti yako yasiyo na mchujo. Haya ngoja wenyewe warudi toka kubeba box. Najuuta kukufahamu.

    ReplyDelete
  4. We, we, we, flowermaua, kama jina lako la baruapepe linavyoashiria na ujumbe wako, wewe ni mtu wa makundi na majungu nambari wani. Ningekuwa ninaishi mji unaoishi, ningekukimbia kama ukoma! ni mswahili hasa, tukirejelea ile mada yetu ya uswahili iliyojadiliwa wiki chache zilizopita.

    ReplyDelete
  5. we mtoto Maua Flower kama unatak marafiki nenda kwenye sehemu za dini kama kanisa au Msikiti. vinginevyo mh! jitayarishe kusomeshwa.....chali.

    ReplyDelete
  6. Chukua ushauri wa jamaa aliyekwambia upweke unaisha wenyewe acha ujinga wako! jichanganye na wengine unatoka bongo unatafuta rafiki mbongo what is the difference! chagua kitu cha kufanya, michezo, msikitini etc tafuta your own destiny, legacy! hatuna muda wa kijinga hapa majuu.
    uzoefu wangu mimi "Nilianza kuandika kitabu" nilipokuwa mpweke sasa na earn through, though sikuwa nimepanga iwe kazi yangu.

    ReplyDelete
  7. Ebooooo wewe dada vipi wewe??Wewe huko unadhani upo bongo eheee eti natafuta marafiki hivi kweli unaakili timamu??Alafu unaonekana mambo yako bado hayajawa sawa...Ughaibuni hamna mtu mwenye muda wa kukaa kwenye magenge watu wanapiga kazi kwenda mbele huku hamna kujuana kama wewe mbongo au mtu fulani umekuja huku haijalishi wewe mgeni au sio mgeni fanya kazi dada achana na urafiki usiokuwa na maana!!

    ReplyDelete
  8. Tangu lini dada na kaka wakawa marafiki, ulijifunzia wapi hiyo elimu ya mahusiano?. Wewe kama unatafuta muchumba sema wazi watu wajue, Utakosa bahati hivi hivi kwa kujitia kuringa shingo upande. Na tangu lini urafiki ukaangalia umri. We haya weee! mi sisemi kitu, nasubiri tu nione waosha vinywa watavyokujibu wakimaliza night shift zao. Mswaki wa kwanza utakuwa wewe.

    ReplyDelete
  9. Pole sana Mauwa,hakuna wabongo wabinafsi katika dunia hii kama wabongo wa sweden.kama we ni msomaji wa blog hii nadhani utakuwa unalitambua hilo,au soma hapo chini habari inayomuhusu jamaa anaitwa majuto.utapata ushahidi wa hili,wabongo wa sweden ni wabinafsi kupita kiasi. kila la heri.take care na wabeba box wana cash za kutosha wasije wakakulaghai. Mdau Falujah Iraq

    ReplyDelete
  10. Wewe binti hujapata mtu tayari ushaanza kuleta masharti ya nini. Kama kweli uko mpweke unataka kujuana na watz wenzako ni heri usingeweka masharti, ukishawapata ndio utachuja mwenyewe yupi awe rafiki yako, lakini sasa umeshaanza ubaguzi mapema hivi inaonekana wewe una matatizo (complicated) na inawezakana hata marafiki ulikuwa nao na wamekutosa kwa sabab ya vijitabia vyako. Nakwambia utapata taabu kumpata unayemuhitaji kwa style hii.

    Bigsam

    ReplyDelete
  11. Kama unatafuta rafiki, yupo hapo chini,anaitwa majuto tena kaweka hadi email yake wasiliana nae,karibu box. Mdau wa Kiruna Uswidi.

    ReplyDelete
  12. mnaosema ngoja wabeba box waamke nimeona hii data leo nikashangaa. kumbe senene wote wako bongo.


    Issamichuzi.blogspot.com users come from these countries:

    * 47.3% Tanzania
    * 16.8% South Korea
    * 13.4% United Kingdom
    * 4.0% Sweden
    * 3.7% United States
    * 3.6% Cameroon
    * 3.2% Netherlands
    * 3.0% Ghana
    * 1.3% India
    * 0.8% Poland
    * 2.9% OTHER


    sasa nyie mwasoma michuzo ya nini tena wakati mko bongo? habari si mwazipata haraka huko? tena kwa internet cafe na kazini

    ReplyDelete
  13. FlowerMaua
    shorty,Tatizo la wabongo maneno mengi badala ya kutatua tatizo......wengi wao wanaishi maisha ya kubahatisha ndio maana wanajidai hawana muda......karibu tuwe marafiki....mimi nipo Norway nahamia Sweden in two weeks time tuwasiliane ;
    fadhiliss@yahoo.co.uk

    ReplyDelete
  14. Naomba nimtete dada ingawa siamini urafiki uanziao kwa e-mail! Kweli mtu anapotua viwanja nakuwa mpweke sana. Hata kama utakuwa na rafiki wa nchi zingine, hakuna raha kukutana na mbongo mwenzako mkapika ugali na dagaa au samaki wa kulumangia na mkatia story. Mwenyeji atakueleza mengi ila ni juu yako kuchagua nini cha maana na nini changanya mdomo. Pia wenyeji wameshafahamu kuwa wapi kuna nini (rea, forex, makanisa na hiyo misikiti mnayoongelea. Naamini uswahili uko kichwani kwa wabongo wengi na hao hao mkija kukutana nao baada ya muda watakuzengua na story za.... ati mbona wafika na kukaa hapa bila kututafuta watanzania wenzio...
    Acheni wivu, dada amefika muombeeni dua mambo yake yanyooke.

    ReplyDelete
  15. michuzi hebu clarify hiyo habari juu,yaani 16.8% ya watazamaji wako are in korea

    ReplyDelete
  16. mdau tottenham haleApril 17, 2009

    mimi ninandugu zangu kama wanne hapo Sweden, sasa siwezi kumwambia dada yangu au kaka yangu kuwa eti kuna dada wakibongo anatafuta rafiki na jina lake anaitwa flower maua. what is that???? jitambulishe jina lako kamili tukufahamu alafu tutakusaidia. dunia kusaidiana siyo kukashifiana.....Mdau tottenham hale- London lakini mwenye ndugu sweden. ongea na michuzi atakupa details zangu.tuwasiliane.

    ReplyDelete
  17. muoshakinywaApril 17, 2009

    ...Ndio unatujulisha kwamba uko sweden, au????????????

    ReplyDelete
  18. heeeeeeeeeeeeeeeee jamani?
    kumbe una mda wa kusogoa uku majuu?
    webcam na chat zitakusaidia tu wee usitafute watu ki-ivyo,,,

    alaaaa grow up baby

    ReplyDelete
  19. mwacheni dada wa watu,mie ninaelewa anachokiongea nyie hiyo si London ambapo utaona African wakipita au makazi,mie ninaishi hapa Poland ,zaidi ya Nigerians hakuna mtu,eti kanisani ,ni wazungu watupu,msifanye mchezo na upweke nyie.

    ReplyDelete
  20. Flower Maua

    Ulaya umefata nini?Ni kweli jichanganye upweke utaisha,ila usijali .mimi na my husband tunakuja huko for our honeymoon in june.Tutakutafuta tukupe company kidogo.Vipi umebadilika au tabia zako ni zilezile za kupenda mabwana za watu?huko watakugeuza kima oooh.Mamdogo jifiche huko huko ni mimi tu na husband ndo tunajua ulipo ,tulia acha papara.Hata soo lako halijaisha ushaanza kujitoa au sala za watu ulizowaingiza mkenge zinaanza kukutokea puani?Tulia.

    Mrs LM

    ReplyDelete
  21. Uswahili sio Ukoma.Lugha unaiongea kila siki lakini unaona aibu kuitwa mswahili. Hongera wewe Mkenya, maana huko kila mtu anaongea lugha yake.

    ReplyDelete
  22. Watanzania je ni kweli ustaarabu umetushinda. Mbona tunakuwa kama watu tusio na akili huyu binti swala lake liko wazi anachotafuta ni ndugu wakutoka nyumbani watu walio nje siku za nyuma walijitenga sana sasa unonao jinsi Tanzanians Association zinavyo anzishwa hiyo ni baada ya kubaini kuwa umoja ni nguvu.Sasa huyu binti anatafuta ndugu nyie mnajibu vitu vya ajabu, hivi wabongo bongo zetu zikoje? ndo maana wabongo wakubwa wameamua KUTU EPA kwa maana wanajua kuwa bongo zetu zinamatatizo.

    ReplyDelete
  23. Hizo data za hapo juu siyo sahii hata kidogo...regrdless of how many TZ's are in Tanzania compared to other countries.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...