Hallow Brother Michuzi, 
mimi naitwa Pascal, niko UK, naomba msaada wako boss wangu, kuna kaka mmoja anaitwa Abdallah nilimwomba aniletee laptop kutoka tanzania, na alikuja huku terehe 05/04/2009 na BA, sasa toka afike huku hajawasiliana nami. Naomba kama inawezekana awasiliane nami kupitia email yangu
pacs98dgs@yahoo.co.uk
au apige/abeep no. 
07529911474
Nashukuru sana boss wangu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Michuzi vitu vengine hata sio vya kuviweka kama kuzalilishana wanadamu jamani tuweni na kitu kinaitwa SUBIRA kitu kitakuja kama hakijaja bahati mbaya kama ulimpa pesa akakuchukulia basi mwenyezimungu ndio analipa sasa huyo mtu ataonekanaje sasa bora hujaweka jina maarufu. Pazi.

    ReplyDelete
  2. Ndugu yangu naskutakia kila la kheri na lap top yako ifike. Nakumbuka kutumiwa lap top kutoka marekani (SONY VAIO) kuja hapa Dar kupitia mtu tuliyejua ni muaminifu. Ni zaidi ya miak mitano tangu mtu huyo afike lakini laptop bado iko njiani.

    ReplyDelete
  3. huyo kakuibia babu!ah mbongo bwana...kaiuza hiyo laptopu hapo kwetu vingunguti!

    ReplyDelete
  4. Uc'take n'cheke mie Yaani wewe uliagiza Laptop kutoka bongo? UK hakuna? ubahili wako umekuponza.

    ReplyDelete
  5. Mambo mawili naomba kuainisha,

    kwanza ndugu yangu ushamkera huyo jamaa, maana watu watakuwa wanamfikria vibaya, wanadhani ni tapeli. hujui sababu zilizomzuia asiwasiliane nawe, labda kawekwa ndani, you never know. wewe unachojuwa ni kuwa amewasili tu, lakini jee umefanya jitihada gani za kujuwa kama aliruhusiwa kuingia uk? tena kama ulimuagiza akuletee laptop, je ulijuwa atakapofikia, wenyeji wake au anuani ya atakapofikia? kama hukufanya hayao ulitegemeaje yeye au wewe kuwasiliana nae?

    2. Kwa nini uko uk unaagiza laptop tanzania? si rahis kununua huku huku?

    ReplyDelete
  6. bwege!!!

    ReplyDelete
  7. MATUKIO YUKEIIIIIIIIApril 20, 2009

    nshafika mzazi
    sasa huku ni kutaka maujiko au kuniaibisha..dah ile hela ndio nliongezea nauli kaka
    anyways naku dipu muda si mrefu tuongee fresh

    ReplyDelete
  8. vipi ilikuwa inapeleka kwa fundi au? kweli tz kuna laptop za kupeleka uk. duh. kaka acha ubahili

    lakini hata hivyo umefanya juhudi gani kumtafuta?

    ReplyDelete
  9. dah ndugu yangu kweli huna subira,ok,nimefika lakini nimeshangazwa sana na uswahili ulioonesha hasa kwa waTanzania wenzetu hapa uingeleza nyumbani na sehemu zingine,sasa nimejua sababu ya wewe kuwekwa zile kopo za maji yalotumika,chupa za bia na soda zilizotumika,chumbani kwako,na hata kutokuwa wa mabadiliko na mambo yako kiujumla,kwanza nilikushangaa uliponiagiza laptop pentium 2 ya laki na 30,nimekuongezea pesa na nimechukua pentium 3,sitokudai na umenikwaza,see u kesho leo nina majukumu fulani.ila kiukweli punguza uswahili!!!!

    ReplyDelete
  10. Acheni ujinga nyie, Mwenye blog kaona la maana kairusha, hilo ni kama tangazo na siku zimeshapita sana, jamaa kaingia nayo mitini tu lazima atafutwe! Kuagizia toka nyumbani si lazima iwe mpya je kama ni yake ya siku nyingi na ina mambo yake muhimu?

    Ila Pasco nawe unanishangaza, utaagizije mtu ambaye hata kumpata ni tabu? Dunia imeharibika hakuna muaminifu tena.

    GJK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...