MTanzania mwenzetu kaniuliza swali nami jibu sina, tafadhali mwenye jibu asaidie.

Msaada : Swali kuhusu usajili wa magari ya LHD Tanzania
Anaomba maelezo/maelekezo kuhusiana na utaratibu wa kusajili na kutumia motakaa ambayo usukani na uendeshaji wake vipo upande wa kushoto yaani, LHD. Anauliza hivi:

Je! Gari ambazo ni left hand driving zinaruhusiwa kutumika Tanzania?
Au je, kuna taratibu zozote kuhusu gari hizi?
Mtu unaweza kuiingiza na ikasajiliwa sawa na magari ya right handed ambayo ni common nchini kwetu?
Samahani, nauliza hivi kwa kuwa sielewi na ninatamani kwenda na gari ninayotumia hapa kwenye nchi ambayo uendeshaji wake ni wa Left Hand.
Asante.

Subi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. Wadau, MTanzania anayeomba maelekezo si mimi Subi, bali 'Jina Limehifadhiwa' anayeishi ng'ambo. Ameniandikia kuuliza nami nikaiweka kwenye blogu yangu (bofya hapa kutizama) lakini pia nikaituma huku na kwa bloga wengine ambapo watembeleaji wake ni wengi zaidi.

    ReplyDelete
  2. Sehemu ya kwanza ni mtu kakuuliza, sehemu ya pili ya swali laonyesha ni wewe mwenyewe unauliza.

    Nawakilisha

    ReplyDelete
  3. kwakweli kwa LHD bongo itakusumbua, achana nayo..ipige bei huko huko kisha tafuta ya RHD.....usifanye risky...bongo siasa nyingi sana.....!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. Mbona ziko gari TZ LHD, kuna tofauti gani kwenye uingizaji?

    ReplyDelete
  5. Mtoa Maoni: Anonymous, Tarehe April 23, 2009 8:39 PM,
    Mkanganyiko umetokana uhariri wa ujumbe halisi alofanya Mheshimiwa Mkuu Michuzi mwenyewe kwa kukata maneno ya ujumbe wa awali na kubandika mengine kadiri alivyopenda yeye. Ukitaka unaweza kusoma posti halisi kwenye blogu yangu jinsi nilivyoandika (linki ipo hapo juu).

    ReplyDelete
  6. Mimi ni mdau na huwa nafanya biashara ya kusafirisha magari toka USA ambayo yana usukani kushoto na huwa tunaendeshea kulia.
    Hakuna sheria yoyote Tanzania (siyo kenya) inayokataza magari haya. Huwa hatuulizwi swali lolote kuhusu upande uliko usukani wa gari lako wakati wa kulipia ushuru au hata wakati wa kusajiri. Nipigie kwenye 0001-240-645-2131 nitakupa maelekezo zaidi.
    Matali

    ReplyDelete
  7. Ndugu yangu jilete hiyo motokaa yako hapa bongo lhd zipo nyingi tu na hata kama wanazuia wala usiogope bongo wanataka rushwa tu. vihiace hadi leo zinapeta town wakati zimepingwa marufuku bongo penge yako tu.
    mdau
    kisiju pwani

    ReplyDelete
  8. yes unaweza kutumia sana. mie na uncle zangu magari yetu yote tumenunua marekani na LHD tunayatumia. na yamesagiliwa kama mengine. goodluck

    ReplyDelete
  9. Gari ni Gari tu, utalipia kodi sawa tu na kila gari haijalishi Left hand au Right hand. Na wadau wanaodai Left hand itakusumbuwa bongo hakuna lolote. Kama unajua kuendesha basi, utaendesha tu bila wasix2.

    ReplyDelete
  10. Bongo hakuna kisichowezekana ili mradi ulipe kodi na kuwapa rushwa TRA na Traffic wakati wa kukagua.

    Mimi nilikuwa naingiza gari toka Japan ilipofika kwenye ukaguzi wa Traffic jamaa wakaniambia nitoe chochote traffic wanipigie muhuri.

    Ukweli ni kwamba magari ya LHD yapo mengi tu bongo sasa kama sheria imeanzishwa 2009 ya kuzuia basi mwenye mpya atoe ila unaingiza na kulipia kama ambavyo magari yoyote yanaingizwa.

    Ushauri: Kazi itakuwa barabarani maana ni lazima uendeshee kushoto kama magari mengine sasa kama unaweza hilo jikoki na mchuma wako, ila kama huwezi usijitafutie pass za mara kwa mara na hasa kama una mpango wa kulitumia jijini Dar.

    ReplyDelete
  11. Nimeona Mercides Benz LHD majuzi nilipokuwa Dar...sidhani kama kuna utaratibu maalumu wa kuingiza magari haya. Kama tuvyojua Tanzania ilivyo hata kama ukiambiwa Full utaratibu ulivyo (on paper), muhusika utakayemkuta Bandarini siku ya kutoa gari lako naye atakupa utaratibu wake...Kaaaziiiii kweli kweli. Sadly, mambo haya ni kama kubahatisha tu...

    ReplyDelete
  12. Ilo unalotamani kulileta bongo ni gari gani ambalo unaona bongo hakuna?kama lhd mbona yako mengi tu kuanzia bima,hummer,benz u name it yapo sasa huko mkoko wako wewe lete tu ili mradi uwe chini ya miaka kumi la sivyo watabonyeza kishenzi kwenye kodi ya uchakavu,na hapo ndio joto ya jiwe utakapo jua bongo sooo.

    ReplyDelete
  13. Dada Subi!
    Bongo hakuna noma wala nini, nyie tu mchecheto wenu.Hapa hata kama usukani uko kwenye matairi, au nyuma ya gari RUKHA!So mambo ya LHD usikonde wala nini

    ReplyDelete
  14. Hey, we can do without LHD in Bongo.

    Au huko uliko wanakuruhusu utumie RHD?

    Sasa kwa nini unataka kutuletea ajali Bongo?

    Uza huo mchuma wako huko huko halafu njoo ujumue kitu kipya cha RHS.

    ReplyDelete
  15. Kwa msaada tu wa haraka haraka, Yes LHD zinasajiliwa kama RHD, mzee wangu anamiliki Dodge Ram ya mmarekani ni LHD.

    ReplyDelete
  16. Aisee Subi Asante kwa kuleta swali la mdau. Hata mimi nasubiri majibu kwa hamu. Labda BTW Blogu yako jaribu kupunguza vitu. Computer zinakataa kusoma. Ukifungua tu unaambiwa "this site may harm your computer". Nafikiri pia hizo add za google nyingi haziruhusu computer zisizo na google fash player na mazagazaga mengine kusoma. Please make it simple wadau tuwe tunakusabahi.
    Wako katika Ujenzi wa Taifa NDUN'GANI NAKAIYO DONGO

    ReplyDelete
  17. Mamaa wa nukta 77 mwelekeze mdau wako atembelee hapa kwani anaweza kuwasiliana na wahusika moja kwa moja.

    ReplyDelete
  18. mimi na-own Bugatti SO hapa dar na ni fresh tu LHD na hausumbuliwi, kwanza wanakuogopa kama gari yako inatisha! karibu!!

    ReplyDelete
  19. Bwana Subi,
    Mimi ni mmoja kati ya watu waliowahi kununua gari LHD, kuisajiri na kuitumia Tanzania, na usajiri ni sawa na magri mengine tu isipokuwa hutaruhusiwa kuisajiri kama Taxi. Kama ni kwa matumizi binafsi haina shida kabisa.
    Mdau, Japani.

    ReplyDelete
  20. Jamaa usiwe na wasi,hapa bongo ni zaidi uijuavyo,hasa tunapoelekea 2010 leta unachoweza bajaj,gutta,toroli... ili mradi uwe tayari kwa kutoa porojo na mlungula.Karibu nyumbani!

    ReplyDelete
  21. Kwa jinsi ninavyoona huyu gari hiyo aiache hukohuko kwani atakuja tusumbua bure kutokana na mazoea. atatuketea taabu huyu kama madereva wengi wanavyoshindwa kukeep left which is the rule of the road here in TZ. Ndugu achana na hilo uza mapema upate bei nzuri kisha agiza gari lingine. Huyu anayetoa website ya TRA anataka kutuambia nini? atueleze ni kipengele gani kinaongelea RHD NA LHD acha kutupotezea muda.

    ReplyDelete
  22. We nguvu yako tulete utakayo, mi nishawahi kuwa nalo halikuwa na usumbufu wowote zaidi ya watu kukutazamatazama tu wanapokuona upo na usukani upande wa kiti cha abiria, Huku bongo hamna noma gari unajiendeshea tuuuuuu barabara yote yako mikasi kibao a.k.a daladala, overtake mpaka kulia utashtukia mendawazimu kesha kuzunguka yuko kwenye sidemirror yako ya kushoto yuko moto juu, akitoka hapo anakeepleft na kwenda kum-bugudhi wa mbele yako na anaekuja mbele yako upande wa kulia kwako ugh!!! nachukia uendeshaji wa baadhi ya wabongo utafkiri uko mombasa kwa watani wetu, ubabe mtupu magari yamejaa makovu kwa uendeshaji wa vurugu lol.

    ReplyDelete
  23. Tanzania wee njoo na chchote kiwe LHS OR RHS, au hata iwe iwavyo, cha muhimu ujue jinsi gani ya kuogea, siunajua kuongea, ndio hukohuko!

    ReplyDelete
  24. AFANDE MIDAKOApril 24, 2009

    Unaweza ukaileta hiyo LHD ukiona inakusumbua kuna vijana kinondoni wanahamisha stelingi kutoka kushoto kwenda kulia

    ReplyDelete
  25. bongo tambararee, we ng'oa huo usukani halafu ubandike upande wa kulia. gear na clutch na brake ziache tu upande wa kushoto, kwani atakusaidia abiria utakaempakiza!wewe right utashikilia usukani, utafika tu uendako, hakuna noma!trafik akikukamata, shs 3,000 zinatosha unapeta tuu

    ReplyDelete
  26. Blogu ya Bro Michuzi kweli kiboko.
    Yaani nkisoma maoni humu huwa nacheka humu hadi basi. Mtu ukiwa na roho ndogo utaishia kugombana na watu bure. Ama kweli penye wengi pana mengi.
    Mtoa Maoni: Anonymous, Tarehe April 24, 2009 3:47 PM: Nitakutafuta unipeleke hospitali kwa kosa la kunisababisha nicheke kushinda kipimo!
    Wadau wooooote, mwenyewe aliyeomba kujua kuhusu suala hili amesoma maoni yenu na kukushukuruni. Yeye kama 'kunguru mwoga' alitaka kufa na shida zake kwa kuepuka kurushiwa madongo hapa maana watu humu ni mitizamo ya kila dizani.
    Hii kweli blogu ya Jamii aka Globu ya Umma!

    ReplyDelete
  27. Japo siwezi kutoa maoni juu ya kukubalika kusajiliwa au la kwa gari LHD naweza kukutahadharisha jambo moja. Uendeshaji wa barabara za Dar umebadilika mno. Ukisimama kwenye taa nyekundu unaweza ukagongwa, ukimwachia mwenda kwa miguu apite kwenye kivuko cha pundamilia unaweza ukagongwa na unaweza kupigwa ovateki kulia au kushoto. Kama ni gari dogo litakusumbua kuendesha mjini maana mashangingi na vipanya vinaongoza kwa kuchomekea magari madogo. Kama una mpango wa kulitumia mikoani haitakuwa na noma.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...